JamiiForums
52.8K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
BUNGENI, DODOMA: Rais Magufuli amesema hayo alipokuwa anahutubia Bunge na kuvunja Bunge la 11, leo Juni 16, 2020

Soma https://jamii.app/KuvunjaBunge11

#JPMBunge11
Rais Magufuli: Kupitia jitihada zilizofanyika ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ambayo nisingependa kuitaja hapa tumetengeneza ajira 6,032,299

- Kati ya hizo, ajira 1,975,723 zimezalisha na sekta rasmi na 4,056,576 zimezalisha na sekta zisizo rasmi

Soma https://jamii.app/KuvunjaBunge11

#JPMBunge11
LEO NI SIKU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

> #SikuYaMtoto hutumika kuwakumbusha Watoto hatua ya kijasiri waliyoichukua wenzao huko Afrika Kusini ktk kulinda haki zao

> Watoto wanaweza kuleta mabadiliko hata wakiwa wadogo

> Maadhimisho ya #SikuYaMtoto wa Afrika kwa mwaka huu 2020 yanafanyika kwa njia ya mtandao. Hii ni kutokana na kuwepo kwa hatari ya maambukizi ya #COVID19

> Kaulimbiu: "Mifumo rafiki ya upatikanaji wa Haki za Watoto, msingi imara wa kulinda haki zao"

Soma > https://jamii.app/SikuYaMtoto

#SikuYaMtoto
SIKU YA MTOTO AFRIKA: WAZAZI WATAKIWA KUDHIBITI MATUMIZI YA SIMU KWA WATOTO

- Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka Wazazi kuwasimamia watoto katika matumizi ya vifaa vya kielektroniki ili kuwaepusha kujiingiza katika vitendo vya ngono na ukatili mwingine mitandaoni

Soma - https://jamii.app/AfricanChildDay
MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA 2020

> Maadhimisho haya yatukumbushe maendeleo ya Taifa letu hayawezi kupiga hatua bila kutilia maanani mahitaji ya watoto

> Kuzingatia mahitaji ya Watoto ni nyenzo ya maendeleo

Zaidi, Soma > https://jamii.app/SikuYaMtoto

#SikuYaMtoto
#COVID19: RAIS MAGUFULI AZUNGUMZIA WABUNGE WALIOONDOKA BUNGENI

- Rais Magufuli wakati anavunja Bunge leo amewapongeza Wananchi kwa kupambana na #CoronaVirus

- Pia, amewapongeza Wabunge kwa kuendelea na Bunge na kusema walioondoka walionesha uoga na kutojiamini

Angalia; https://youtu.be/i8fusZlszcs
CHINA: PROFESA ASHAURI SERIKALI KURUHUSU WANAWAKE KUWA NA MUME ZAIDI YA MMOJA

- Prof. Yew Kwang Ng ameshauri hivyo ili kukabiliana na ukosefu wa uwiano wa idadi ya Wanawake na Wanaume

- Amesema ushindani wa kutafuta Wanawake umekuwa mkali

Soma - https://jamii.app/WanawakeNdoaChina
EWURA YAAGIZWA KUWASAKA WANAOUZA MAFUTA TOFAUTI NA BEI ELEKEZI

- Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametoa siku 7 kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Wakala wa Kuagiza Mafuta kuwasaka wafanyabiashara wanaoficha mafuta au kuuza juu ya bei elekezi

Soma - https://jamii.app/BeiMafuta
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2020: RAIS AWATAHADHARISHA WAGOMBEA

- Rais Magufuli akivunja Bunge amewataka Wagombea kujiepusha na Shetani wa Matusi

- Amewataka wakashindane kwa hoja na kushindanisha ilani zao huku wakijua Serikali iko macho haijalala

Angalia: https://youtu.be/kW4m-cfyU4g
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2020: CUF YASEMA HAITASHIRIKIANA NA CHADEMA, ACT

- Chama hicho kimesema kimejifunza kwa kilichotokea katika Uchaguzi Mkuu wa 2015

- Hata hivyo, CUF imesema ipo tayari kushirikiana na vyama vyingine vyenye nia ya dhati

Soma https://jamii.app/CUFUshirikianoUchaguzi
KOREA KASKAZINI YALIPUA OFISI YAKE YA PAMOJA NA KOREA KUSINI

- Ni baada ya kutishia kuchukua hatua za kijeshi mpakani mwa nchi hizo

- Korea Kusini imeonya itajibu shambulio hilo ikiwa Korea Kaskazini itaendelea kusababisha mvutano zaidi kati yao

Soma https://jamii.app/MvutanoKorea
MWANZA: BABA AMUUA MWANAYE KWA KUPOTEZA TSH. 500

- Anthony Lyala anatuhumiwa kumpiga mwanaye wa miaka 8 hadi kufa kwa madai ya kupoteza Shilingi 500

- Mwenyekiti wa Kijiji amesema mtuhumiwa amekuwa akijihusisha na matukio mengi ya ukatili

Soma - https://jamii.app/BabaAmuuaMtoto
ALIYEKUWA RAIS WA MGODI WA BULYANHULU NA WENZAKE, WAHUKUMIWA KULIPA BILIONI 1.5

- Deodatus Mwanyika na wenzake 2 wamekutwa na hatia ya kukwepa kodi

- Mbali na faini hiyo, Mahakama imewataka kulipa Milioni 1.5 au kutumikia kifungo cha miezi 4

Soma https://jamii.app/HukumuDeoMwanyika
NACTE YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI WA WANAFUNZI

> Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limefungua dirisha la udahili wa wanafunzi katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi zote na litafungwa Septemba 15, 2020

> Septemba 22 hadi 29 majina ya waliochaguliwa yatawasilishwa NACTE kwa ajili ya uhakiki

Soma - https://jamii.app/UdahiliNACTE
KENYA: VISA VIPYA 133 VYA #COVID19 VYATHIBITISHWA, MAAMBUKIZI YAFIKIA 3,860

- Vimethibitishwa baada ya sampuli 3,860 kufanyiwa vipimo

- Jumla ya wagonjwa waliopona ni 1,326 na vifo vimeongezeka hadi 105 baada ya kifo 1 kurekodiwa

Soma - https://jamii.app/Corona3860-KE
#JFCOVID19_Updates
MAALIM SEIF: HOTUBA YA RAIS MAGUFULI IMESAHAU MAMBO YA MSINGI KAMA DEMOKRASIA

> Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif amesema Rais Magufuli ameongea vitu vingi wakati akifunga Bunge ila amesahau masuala ya msingi kama #Demokrasia, #HakiZaBinadamu, Tume Huru ya Uchaguzi na Uchumi imara kwa kila Mtanzania

Angalia - https://youtu.be/FPsbvCcNS_4
#CORONAVIRUS BRAZIL: VISA ZAIDI YA 34,000 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24

- Visa vipya 34,918 vimeripotiwa na jumla ya maambukizi nchini humo ni 923,834

- Vifo vya #CoronaVirus vimeongezeka hadi 45, 456 na wagonjwa 464,774 wamepona

Soma https://jamii.app/COVID19Updates
#JFCOVID19_Updates
RAIS MAGUFULI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS

- Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Magufuli amechukua fomu ya kugombea Urais ktk Uchaguzi Mkuu ujao kwa muhula wa pili

- Amekabidhiwa fomu katika Makao Makuu ya CCM-Dodoma na Katibu Mkuu, Dkt. Bashiru Ally

Angalia - https://youtu.be/4f3GB_Jc968
#JFLeo
WIZARA YA ELIMU YATANGAZA RATIBA YA MITIHANI KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

- Darasa la 7 wataanza mitihani ya taifa Oktoba 7-8, Kidato cha 2 Novemba 9-20, Kidato cha 4 wataanza Novemba 23

- Darasa la 4 watafanya mitihani Novemba 25 -26

Soma - https://jamii.app/RatibaMitihaniTaifa
#CORONAVIRUS BEIJING: VISA VIPYA 31 VYAREKODIWA. SHULE NA VYUO VYAFUNGWA. MICHEZO YAZUIWA

- Baadhi ya safari za ndege na treni zimepigwa marufuku hadi Julai 9

- Wananchi waliopo maeneo ya hatari wamezuiwa kusafiri nje ya Mji

Soma https://jamii.app/CoronaOutbreakBeijing
#JFCOVID19_Updates