JamiiForums
βœ”
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#CORONAVIRUS-MAREKANI: WAGONJWA WAPYA ZAIDI YA 22,900 WAMERIPOTIWA JANA

- Wagonjwa 22,921 wameripotiwa jana na kwa mujibu wa WHO visa vimefikia 2,654,827

- Vifo 894 vimeripotiwa na jumla ya vifo ni 119,349. Jumla ya waliopona ni 777,350

Soma https://jamii.app/COVID19Updates
#JFCOVID19_Updates
BAJETI 2020/2021: BAADHI YA MAREKEBISHO YA TOZO NA KODI

> Bajeti imependekeza msamaha wa ushuru wa forodha kwa vifaa vya magonjwa ya mlipuko

> Pia, imependekeza kufuta tozo za OSHA za mafunzo ya elimu kwa umma kwani ni jukumu lao kuelimisha jamii

Soma https://jamii.app/2020-21BajetiTZ
UGANDA YATANGAZA WAGONJWA WAPYA 7 WA #COVID19. VISA VYAFIKIA 686

- Wagonjwa wote wapya ni Waganda. Waliopona wafikia 161

- Madereva wa Kenya-8, Tanzania-4, Congo-2, Sudan Kusini-2 na Eritrea-2 wamerudishwa baada ya kukutwa na COVID-19

Soma https://jamii.app/COVID19-686
#JFCOVID19_Updates
MAREKANI: MICROSOFT KUTOUZA TEKNOLOJIA YA UTAMBUZI WA SURA HADI SHERIA MPYA IWEPO

> Hawatawauzia Polisi 'Facial recognition system' hadi itungwe sheria mpya ya kuheshimu haki za binadamu

> Teknolojia iliyopo ina shida kwenye utambuzi wa sura za watu weusi na jinsia zao

Soma https://jamii.app/TeknolojiaUtambuzi
RAIS MUSEVENI: KUNA VIPIMO VYA #COVID19 VILIONEKANA VINA MAAMBUKIZI KIMAKOSA

- Amesema baadhi ya visa Uganda vilithibitishwa kimakosa kutokana na uzembe katika Maabara ya Makerere

- Amesema watu wachache walikuwa wanafanya kazi katika maabara hiyo na huenda walichoka

Soma https://jamii.app/VisaCOVIDMakosaUG
#JFCOVID19_Updates
TAKUKURU YAWASHTAKI WATUMISHI 7 WA TPA KWA WIZI WA ZAIDI YA TSH. BILIONI 8

> Watumishi hao wanatuhumiwa kughushi nyaraka na kutakatisha fedha

> Aidha, TAKUKURU imetangaza donge nono kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa Chrispine Iranque na Arnold H. Temba

Soma https://jamii.app/TAKUKURU7TPA
#CORONSVIRUS-KENYA: JUMLA YA MAAMBUKIZI YAFIKIA 3,305. WALIOPONA WAFIKIA 1,164

- Wizara ya Afya imetangaza wagonjwa wapya 90 wa #COVID19 na Wagonjwa wapya 72 waliopona

- Wagonjwa wapya wote ni Wakenya; Wanaume 62 na Wanawake 28

Soma https://jamii.app/COVID19KE-3305
#JFCOVID19_Updates
BURUNDI: BARAZA LA MAWAZIRI LAAZIMIA KUONGOZA NCHI BADALA YA SPIKA WA BUNGE

> Uamuzi huo ulifikiwa kufuatia mkutano uliyofanywa Alhamisi, Juni 12

> Kikatiba Spika wa Bunge alitakiwa kuapishwa kushikilia wadhifa wa Rais kwa kipindi cha mpito

Soma https://jamii.app/BurundiBarazaMawaziri
#CORONAVIRUS: MUONGOZO KWA WATU WENYE ULEMAVU

> Epuka mikusanyiko na safari zisizo za lazima

> Vifaa vyote vya kukusaidia kufanya shughuli zako za kawaida kama β€˜wheelchair’, fimbo na magongo vitakaswe kila iwezekanapo

Msaidizi wa Mtu Mwenye ulemavu, zingatia yafuatayo ili umlinde dhidi ya #COVID19;

> Nawa mikono yako kwa maji tiririka na sabuni au Sanitizer

> Endapo unamsaidia asiyeona mruhusu akushike nyuma ya kiwiko cha mkono

Soma > https://jamii.app/COVID19VsWalemavu

#IshiNaCOVID19 #COVID19
#MICHEZO: TFF imesema katika mchezo mmoja timu itaruhusiwa kubadili hadi Wachezaji 5 badala ya 3

- Imewataka Wachezaji waliokuwa wamalize mikataba yao Mei 31, 2020 waendelee kutumikia klabu zao hadi Julai 31, 2020 ambapo ndio mwisho wa msimu

Soma https://jamii.app/MaboreshoVPL
#JFSports
- Mbunge Yosepher Komba amelalamika kudhalilishwa wakati Mbunge Jackline Msongozi akitoa ushauri kuwa Msajili wa Vyama aingilie kati CHADEMA kuhusu tuhuma zilizopo ikiwemo Wabunge Wanawake kudalilishwa kingono

- Yosepher aliomba kutoa taarifa na kumshauri Jackline awashauri Wabunge wanaolalamika kwenda kwenye vyombo vya Dola ila Jackline alisema Yosepher naye ni mmoja wa wahanga wa masuala hayo

Zaidi, soma https://jamii.app/MbungeNjeKudhalilishwa
POLISI: MBOWE ALIFIKA HOSPITALINI AKIONEKANA KUWA KATIKA HALI YA ULEVI CHAKARI

> Polisi wameeleza kuwa hakuna shahidi yeyote aliyesikia kelele wala kuona Mbowe akishambuliwa

> Mbowe alidai kuvamiwa na watu watatu alipokuwa akiingia nyumbani kwake wakati akitokea kwa mzazi mwenzake, Joyce Mukya, Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA)

Zaidi; https://youtu.be/BD8ixLNrO-s
- Amesema amelelewa CCM na ameomba msamaha kwa yaliyojitokeza huku akimuomba Mungu na yeye awasamehe waliomfanyia maovu

- Aidha, Spika Ndugai amemkaribisha CCM na huku akisema siasa ni elimu kubwa na Chuo Kikuu ni Bunge

Zaidi, soma https://jamii.app/RizikiLulidaCCM
MANYARA: MAAFISA WATATU WA TRA MBARONI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

> TAKUKURU inawashikilia Eva Mtandika, Jackline Manjira na Ephraim Medard kwa tuhuma za rushwa

> Walimtaka mfanyabiashara alipe Tsh. Milioni 1 ili asifikishwe Mahakamani

Soma https://jamii.app/RushwaTRA
KENYA: BENDERA YAPEPEA NUSU MLINGOTI KUOMBOLEZA KIFO CHA RAIS PIERRE NKURUNZIZA

> Rais Uhuru Kenyatta ameagiza Bendera ya Kenya na ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kupepea nusu mlingoti kuanzia Juni 13 hadi siku ya mazishi ya Rais Nkurunziza

Soma https://jamii.app/BenderaKEPierre
RAIS MAGUFULI ATANGAZA SIKU 3 ZA KUOMBOLEZA KIFO CHA RAIS WA BURUNDI, PIERRE NKURUNZIZA

- Ametangaza maombolezo ya Kitaifa ya siku 3 kuanzia kesho, Juni 13 hadi Juni 15

- Katika kipindi hicho, bendera zote zitapeperushwa nusu mlingoti

Soma https://jamii.app/BenderaTZKifoNkurunziza
#JFLeo #Siasa
TAARIFA: TUTAKUWA OFFLINE KWA DAKIKA KADHAA

> Taarifa imetolewa awali kwenye jukwaa juu ya huduma kutopatikana kwa dakika 30 hadi saa 1

> Baada ya muda huo, huduma itarejea sawa

JamiiForums
JAMIIFORUMS: TUMEREJEA HEWANI

> Huduma katika mtandao wetu wa JamiiForums.com zimerejea sawa

> Ni baada ya kusimamishwa kwa takribani dakika 50 kupisha matengenezo muhimu

> Tunawashukuru kwa uvumilivu baada ya huduma kusitishwa kwa muda

/ JamiiForums
MELI YENYE BENDERA YA TANZANIA YADAIWA KUINGIZA SILAHA LIBYA

- Kwa mujibu wa Vyombo vya Habari vya Ugiriki, Juni 10, meli ya mizigo yenye bendera ya Tanzania iliyokuwa imebeba silaha iliingia Libya ikiwa imesindikizwa na meli tatu za Kijeshi za Uturuki

Soma https://jamii.app/MeliTZSilaha
MTAALAM WA AFYA: KUNA UWEZEKANO TIBA YA #COVID19 IKAPATIKANA KABLA YA CHANJO

> Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Aleji na Magonjwa ya Kuambukiza nchini Marekani, Dkt. Anthony Fauci amesema waliweza kuishinda Ebola na nguvu za ushindi huo zitahamishiwa kwa #CoronaVirus

Soma https://jamii.app/TibaChanjoCorona
#JFCOVID19_Updates