JamiiForums
βœ”
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS MAGUFULI: NIMEMSAMEHE THOBIAS ANDENGENYE. NITAMTAFUTIA KAZI

- Rais Magufuli amesema amemsamehe aliyekuwa Kamishna wa Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye baada ya kumuomba msamaha kwa zaidi ya mara tatu

- Amesema hawezi kumrudisha katika Jeshi hilo ila ataonekana katika kazi nyingine kwani mtu akiomba msamaha na kuonesha kutubu inabidi asamehewe

Soma https://jamii.app/MagufuliDodoma

#JamiiForums #Zimamoto
SERIKALI KUJENGA UWANJA MKUBWA WA NDEGE DODOMA

> Rais Magufuli amesema Uwanja utajengwa Msalato, Dodoma na utafanana ukubwa na Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere (JKNIA)

> Tsh. Billioni 500 imeshapatikana kwa ajili ya mradi huo

Zaidi; https://youtu.be/icRc467P4tE
RAIS MAGUFULI: BAJETI YA KITENGO CHA DAWA ZA ASILI IONGEZWE

> Rais Magufuli amesema tusidharau dawa za kienyeji kwani ndizo zimesaidia kupunguza #COVID19

> Amesema kujifukiza kumesaidia sana na waliotegemea maiti kuokotwa barabarani matarajio yao hayajatimia

Zaidi; https://youtu.be/MaPGpV5NXI8
Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akizindua Jengo la Ofisi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kuwataka Watumishi kuchapa kazi na kuacha kutafuta fedha za bure

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliDodoma
CHAD: MKUU WA MAJESHI AFUKUZWA KAZI BAADA YA KUMKOSOA RAIS

> Ahmat Koussou Moursal amefukuzwa kazi baada ya kuandika barua ya wazi iliyomlaumu Rais kuwasahau rafiki zake waliokuwa wote Jeshini

> Serikali imesema, Kiongozi huyo hatapata fidia

Soma https://jamii.app/ChadGeneral
RAIS MAGUFULI: KAZI HII NI NGUMU, INA MATESO SANA

- Amewaomba Watanzania wamuombee ili asije kuwa na kiburi au jeuri bali awe kiongozi wa kweli asiyebagua

- Pia, akatimize wajibu wake katika kipindi kilichopangwa Kikatiba ili kusudi baada ya hapo awaachie wengine ambapo pia watatimiza wajibu wao

Zaidi; https://youtu.be/sXisHOi1YVU
KENYA: WAKUMBWA NA UGONJWA WA KUIMBA, WADAIWA KULA MAGIMBI YA WIZI

> Wanafamilia hao 8 wana miaka kati 12 hadi 30, wamekumbwa na ugonjwa wa ajabu wa kuimba kwa nguvu

> Mama wa familia, Susan Wangari amedai wamekuwa hivyo baada ya kula Magimbi yanayosadikiwa ni ya wizi

Soma https://jamii.app/KE8Kucheka
#COVID19 KENYA: MAAMBUKIZI YAFIKIA 3,215

> Watu 121 zaidi wamekutwa na #CoronaVirus. 115 kati ya waliotangazwa ni wakenya na 6 ni wageni

> Idadi ya waliopona imefika 1,092. Pia idadi ya vifo imefikia 92

Soma https://jamii.app/3215COVID19KE
#JFCOVID19_Updates
WIZARA YA FEDHA YAPENDEKEZA KUANZISHWA KWA NAMBA MAALUM ZA USAJILI MAGARI

- Imependekeza kufanyika kwa marekebisho ya Sheria ya Usajili wa Magari Sura 124 ili kuanzisha usajili wa magari kwa kutumia namba maalum (mfano T. 777 DDD) kwa ada ya Tsh. 500,000

Soma https://jamii.app/BajetiTZ2020-21
IFAHAMU KESI ILIYOCHUKUA MIAKA ZAIDI YA 50

> Maria Ridulph alipotea Desemba 3, 1957. Mabaki ya mwili wake yaligundulika Aprili 26, 1958

> Kesi iliibuka tena mwaka 2008. Mshukiwa John Tessier alikutwa na hatia akahukumiwa kifungo cha maisha lakini baadaye alionekana hana hatia

Soma https://jamii.app/KesiMiaka50
#JFHistoria
KENYA: POLISI WALIOMBURUZA RAIA WAKAMATWA

> Polisi 3 wamekamatwa kwa tuhuma za kumburuza Mercy Cherono kwa kumfunga kwenye Pikipiki

> OCS David Kiprotich alimshutumu Cherono kuiba mtungi wa gesi, televisheni, laptop na nguo

Soma https://jamii.app/TuhumaPolisiKE
MFAHAMU MUIGIZAJI N!XAU Η‚TOMA

> N!xau Η‚Toma ni mzaliwa wa Namibia kutoka kabila la San. Kabla ya kuigiza, alikuwa hajui chochote kuhusu maisha ya kisasa

> Alilipwa Dola 300 katika filamu ya β€œThe Gods Must Be Crazy” iliyogharimu Dola Milioni 5

Soma https://jamii.app/MfahamuBushman
#JFMaarifa
MAREKANI: CHANJO YA #COVID19 KUJARIBIWA MARA YA TATU NA YA MWISHO

> Mwezi Julai chanjo ya #CoronaVirus iliyogunduliwa na kampuni ya Moderna, itajaribiwa kwa watu 30,000

> Kampuni hiyo haikutoa matokeo ya majaribio yake ya pili

Soma https://jamii.app/ChanjoCoronaMarekani
NEW ZEALAND: SANAMU LA HAMILTON LAONDOLEWA

> Kapteni John Charles Hamilton, ambaye jina lake limepewa mji wa Hamilton, aliongoza mapigano dhidi ya watu wa jamii ya Maori

> Lisingeondolewa na Uongozi, Waandamanaji wangelivunja sanamu hilo

Soma https://jamii.app/SanamuHamilton
#JFLeo
IMF YAIPA RWANDA DOLA MILIONI 111.06 ILI KUPAMBANA NA #COVID19

> IMF imesema Rwanda imeonesha uwazi na uwajibikaji katika kutumia fedha za dharura

> Ukuaji wa uchumi wa Rwanda ulitabiriwa kushuka kutoka 5.1% hadi 2.0%

Soma https://jamii.app/Rwanda-IMFFunds
#JFLeo
MAREKANI: MKUU WA MAJESHI AOMBA RADHI KWA KUAMBATANA NA TRUMP

> Jenerali Mark Milley amesema uwepo wake kwenye ziara ya Rais huyo inaonesha kuwa Jeshi linatumika kisiasa

> Rais Trump alitembelea Kanisa la St. John lililoharibiwa na Waandamanaji baada ya kuwatawanya Waandamanaji hao kwa nguvu

Soma https://jamii.app/GeneraliAombaRadhi
TWITTER YAFUTA AKAUNTI 170,000, ZIKIWEMO ZILIZOTOA MTAZAMO WA UONGO KUHUSU #COVID19

- Imesema imezifuta akaunti hizo zilizokuwa zinahamasisha maandamano Hong Kong, kutoa mtazamo wa uongo kuhusu #COVID19 na kuhusu maandamano ya George Floyd

Soma https://jamii.app/TwitterAkaunti170000