JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
FREEMAN MBOWE AHAMISHIWA DAR KUTOKEA DODOMA

- Ametolewa katika hospitali ya DCMC na kusafirishwa kwenda jijini Dar kwa matibabu zaidi

- Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Esther Bulaya amesema wataeleza baadaye ni hospitali gani anakwenda

Soma https://jamii.app/MboweAttack
#JFLeo
NIMR: UTAFITI WA DAWA YA #COVID19 YA MADAGASCAR UNAENDELEA

- Taasisi ya Taifa ya Kupambana na Magonjwa ya Binadamu (NIMR), imesema kuwa inaendelea na utafiti wa dawa ya #CoronaVirus kutoka Madagascar, na utakapokamilika itatolewa kwa Umma

Soma https://jamii.app/UtafitiDawaMDGSR
#JFLeo
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
WAZIRI MKUU MIONGONI MWA VIONGOZI WALIOMJULIA HALI MBOWE

- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemjulia hali Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Hispitali ya Ntyuka Jijini Dodoma kabla Kiongozi huyo kusafirishwa kwenda Dar

- Viongozi wengine waliomjulia hali Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai ni pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson

#JFSiasa #Siasa #JamiiForums
RAIS WA BURUNDI, PIERRE NKURUNZIZA AFARIKI DUNIA

- Amefariki akiwa na miaka 55 na kwa mujibu wa Serikali ya Burundi ni kutokana na Mshtuko wa Moyo

- Hivi karibuni Mke wake, Denise Bucumi alilazwa nchini Kenya kwa matibabu ya #COVID19

Soma https://jamii.app/PierreNkurunzizaAfariki
#JFLeo
KENYA YATANGAZA ONGEZEKO LA WAGONJWA 127 WA #COVID19 AKIWEMO MTOTO WA WIKI 3

- Ni baada ya sampuli 2,247 kupimwa ndani ya saa 24 zilizopita. Idadi ya visa imefikia 2,989

- Wagonjwa 124 ni Wakenya na 3 ni wageni; 84 ni Wanaume na 33 ni Wanawake

Soma https://jamii.app/COVID19KE-2989
#JFCOVID19_Updates
UCHAGUZI 2020: WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA RUSHWA

> Waandishi wa habari wameonywa kutojihusisha na rushwa kwa kutumiwa na Wanasiasa

> Wametakiwa kuzingatia miiko na maadili ya kazi. Kutoa elimu kwa raia ili wachague viongozi sahihi

Soma https://jamii.app/TAKUKURUWaandishi
#JFLeo
TETESI: CHELSEA INATAKA KUMSAJILI KAI HAVERTZ KUTOKA LEVERKUSEN

- Havertz (20) ana magoli 15 na pasi 8 za magoli kwa msimu wa 2019/20 hadi sasa

- Chelsea imemsajili Hakim Ziyech na inadaiwa kuwa kwenye makubaliano ya awali kumsajili Timo Werner wa RB Leipzig

- Aidha, Beki wa kushoto wa Leicester City, Ben Chilwell anaendelea kuwa mchezaji anayehitajika zaidi Stamford Bridge

#JFSports #Sports
JIKINGE DHIDI YA MAAMBUKIZI YA #CORONAVIRUS KWA KUZIJUA SEHEMU HATARISHI KWA WASAFIRI

> Msafiri yuko kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa #COVID19 awapo safarini

> Ni muhimu kwa wasafiri kuzijua njia zote za kujikinga na hatari hiyo

Soma > https://jamii.app/COVID19VsWasafiri

#IshiNaCOVID19
BUNGENI, DODOMA: DAVID SILINDE ATANGAZA KUJIUNGA CCM

> Mbunge huyo wa Jimbo la Momba alijiuzulu nafasi zote baada ya CHADEMA kumtaka kufanya hivyo

> Spika Ndugai amempokea na alimuhamisha ili akae upande wa viti vya Wabunge wa CCM

Soma https://jamii.app/SilindeAhamiaCCM
#JFSiasa
IRINGA: WATU 8 MBARONI KWA KUPOKEA MISHAHARA MIWILI KINYUME NA SHERIA

> TAKUKURU imewafikisha Mahakamani waajiriwa wa Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (RUCU)

> Wanatuhumiwa kufundisha Chuo hicho huku wakiwa ni waajiriwa wa Serikali

Soma https://jamii.app/WiziMilioni500
#JFLeo
MTWARA: KIJANA ATUHUMIWA KUMUUA MZEE KWA PANGA ILI KUIBA KUKU NA SOLA

> Mukhsin Selemani(24) anatuhumiwa kumuua Hassan Mtipa (67) ktk tukio la wizi nyumbani kwa marehemu

> Polisi wamesema baada ya kukamatwa, mtuhumiwa alikiri kuiba na kufanya mauaji

Soma https://jamii.app/WiziMauajiMtwara
#JFLeo
CHINA: DAWA YA #COVID19 KUJARIBIWA KWA MWANADAMU

> Dawa hiyo inayoitwa JS016, itajaribiwa kama haina madhara kwa mwanadamu

> Pia, dawa hiyo inachunguzwa kama inaweza kutumika yenyewe au itahitaji uwepo wa dawa nyingine

Soma https://jamii.app/ChinaDawaCOVID19
#JFCOVID19_Updates
UN: WATU MILIONI 49 WANAWEZA KUINGIA KWENYE UMASIKINI ULIOKITHIRI

> Umaskini uliokithiri utaongezeka kutokana na athari za #COVID19

> Pia, idadi ya watu watakao kuwa na upungufu wa chakula au ukosefu wa lishe bora itaongezeka haraka

Soma https://jamii.app/UmasikiniUliokithiri
#JFLeo
UBELGIJI: SANAMU YA MFALME LEOPOLD II YAONDOLEWA ANTWERP

> Mfalme Leopold II anajulikana kwa kuwa na utawala wa chuma na katika utawala wake aliwaua takriban raia wa Congo milioni 10

> Alitawala kuanzia mwaka 1885 hadi mwaka 1908

Soma https://jamii.app/SanamuLeopoldII
#JFLeo
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA: WABUNGE 69 WA CHADEMA KUHOJIWA TAKUKURU

- TAKUKURU inawahoji Wabunge 69, Wanachama na waliokuwa Wanachama wa CHADEMA

- Baadhi ya Wabunge walidai kukatwa fedha kwenye mishahara yao bila kujua matumizi yake

Soma https://jamii.app/CHADEMA-TAKUKURU
UINGEREZA: MUME WA MALKIA ELIZABETH II, MWANAMFALME PHILIP ATIMIZA MIAKA 99

- Philip, amemuoa Malkia wa Uingereza, Elizabeth II (94) kwa zaidi ya miongo 7 iliyopita

- Kutokana na #COVID19, amejifungia na Mkewe katika nyumba ya Kifalme ya Windsor hivyo Wanafamilia wengine watatuma salamu kwa njia ya simu

Soma https://jamii.app/PrincePhilip99
#JFLeo
DKT. MOLLEL ASEMA WANASHUGHULIKIA TATIZO LA MADEREVA NAMANGA

- Amefanya ziara katika mpaka wa Tanzania na Kenya, Namanga na kuzungumza na madereva wa malori

- Madereva wamedai kuombwa Ksh. 2,000 (Tsh. 43,443) na Maafisa wa Kenya ili kuandikiwa hawana #COVID19

Soma https://jamii.app/MollelNamanga
#JFLeo
MOROGORO: TAKUKURU INAMCHUNGUZA MBUNGE DKT. CHRISTINE

- Mbunge wa Viti Maalum(CCM), Dkt. Christine Ishengoma anachunguzwa akituhumiwa kugawa rushwa kwa wapiga kura

- Pia, aliyewahi kuwa Meya wa Morogoro, Amir Nondo amefikishwa Mahakamani kwa makosa ya uhujumu uchumi

Soma https://jamii.app/IshengomaTAKUKURU
MOROGORO: HEKARI 100 ZA BANGI ZABAINIKA, VIONGOZI WA VIJIJI WATAKIWA KURIPOTI POLISI

> Polisi wamehoji Viongozi walikuwa wapi wakati shughuli hizo zikiendelea

> Afisa Mtendaji asema umbali kutoka makazi ya watu ni sababu ya kutogundua mashamba hayo mapema

Soma https://jamii.app/BangiHeka100
BURUNDI: SPIKA KUONGOZA NCHI HADI NDAYISHIMIYE ATAKAPOAPISHWA

> Kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo, Spika wa Bunge ataongoza hadi aliyeshinda Urais atakapoapishwa

> #Burundi imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku 7 kufuatia kifo cha Rais Pierre

Soma https://jamii.app/BurundiSpikaRais