JamiiForums
53.4K subscribers
34.2K photos
2.36K videos
31.2K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AUAWA AKIAMULIA UGOMVI WA WANANDOA

> Mkazi Songea mkoani Ruvuma, Mohammed Hamim, ameuawa kwa kupigwa na kipande cha bomba la chuma kichwani alipokuwa akiamulia ugomvi wa mume na mke ambao ni majirani zake

> Mtuhumiwa anasakwa na Polisi

Soma - https://jamii.app/MauajiUgomviWanandoa
SERIKALI IKO MBIONI KUAJIRI WALIMU 4,900 WA MASOMO YA SAYANSI

> Walimu hao wataenda kuhudumia shule mpya za Sekondari zinazoendelea kujengwa maeneo mbalimbali nchini

> Huu ni mkakati wa kukabiliana na changamoto ya ongezeko la wanafunzi

Soma > https://jamii.app/AjiraWalimu4900
DFID NA ASASI ZA KIRAIA KUSAIDIA SERIKALI KATIKA UWAJIBIKAJI

- Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa(DFID) imezindua mpango wa miaka mitano wa Uwajibikaji Tanzania

- Mpango huo unalenga Kupambana na Rushwa, Mabadiliko ya tabia ya nchi, usawa wa kijinsia na ujumuishwaji wa Wananchi katika maamuzi ya maendeleo

Zaidi, soma https://jamii.app/UwajibikajiTanzania2019
RAIA 13,000 WAYAKIMBIA MAKAZI YAO SUDAN KUSINI

> Ripoti iliyotolewa na Shirika la wakimbizi (UNHCR) inasema, raia zaidi ya 13,000 wameyahama makazi yao kutokana na mapigano ya hivi karibuni Sudan Kusini

> Zaidi ya raia 5,000 wamehamia DRC

Soma - https://jamii.app/RaiaWahamaSudan
FAHAMU KUHUSU KILIMO BORA CHA MAHARAGE

> Katika ekari moja unaweza kupata Kilogramu 600 hadi 1200 za Maharage na ustawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa mita 1000 hadi 2000 kutoka katika usawa wa bahari au pungufu ya mita 1000 au zaidi ya mita 2000 kutoka usawa wa bahari

> Maharage huitaji mvua ya kutosha kipindi cha kabla ya uwekaji maua na kipindi cha ukuaji wa vitumba vya Maharage

Tembelea - https://jamii.app/KilimoMaharage
#JFKilimo
UPINZANI VENEZUELA WAKAMATA KITUO CHA MAFUTA

> Upinzani unaolidhibiti Bunge la Venezuela umeteuwa bodi ya mpito ya kampuni ya mafuta ya Serikali (PDVSA), ikiwa ni jitihada za kiongozi, Juan Guaido kuidhibiti sekta ya uchimbaji wa mafuta

Soma - https://jamii.app/GuaidoSeizeOilProduction
NIGERIA: WATU 7 WAFARIKI DUNIA KWENYE KAMPENI ZA RAIS BUHARI

> Wengine 12 wamejeruhiwa baada ya umati wa Watu kukanyagana wakati wakitoka kwenye uwanja uliofanyika kampeni za Rais Muhammadu Buhari

> 8 bado wamelazwa Hospitali

Zaidi, soma => https://jamii.app/VifoMkutanoBuhari
AFYA: SIDIRIA INAYOWEZA KUGUNDUA SARATANI YA MATITI YAVUMBULIWA

> Sidiria hiyo inaweza kupima viwango vya joto, kuviweka katika programu na kisha kutoa taarifa

> Wanawake wanaohitaji watalazimika kuivaa kwa dakika 60 hadi 90 kwa wiki

Soma > https://jamii.app/SidiriaSaratani
BUSEGA, SIMIYU: WANANCHI WAPIGA KURA YA SIRI ILI KUWATAJA WAUAJI WA WATOTO

> Zoezi hilo limeendeshwa leo kwenye Kata ya Lamadi ambapo kura hiyo imelenga kuwataja watuhumiwa wa mauaji ya Watoto wilayani humo

Zaidi, soma => https://jamii.app/KuraWauajiSimiyu
MFANYAKAZI WA TAZARA AKAMATWA NA TAKUKURU KWA TUHUMA ZA RUSHWA

> Bahati Selemani amekamatwa na TAKUKURU, Mbeya kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Shilingi laki 2 kutoka kwa Mfugaji aliyemkamata akilisha mifugo kwenye hifadhi ya reli

Soma > https://jamii.app/TAKUKURUVsAfisaTAZARA
CHINA YAIPATIA BURUNDI IKULU MPYA

> Balozi wa China nchini Burundi, na Waziri wa mambo ya nje wa Burundi, wamesaini hati ya makabidhiano ya jengo la Ikulu ya Burundi lililojengwa kwa msaada wa China

> Ipo eneo la Mutimbuzi, Bujumbura

Soma - https://jamii.app/BurundiNewWhiteHouse
TRUMP KUSAINI MUSWADA WA KUGHARAMIA MATUMIZI YA SERIKALI

> Muswada huo utazuia kufungwa tena kwa Serikali Kuu na kuwapa ahueni wafanyakazi takribani 800,000 waliopata kadhia ya kutolipwa mishahara mwezi Desemba

> Aahidi kutangaza hali ya dharura ili kupata pesa za kujenga ukuta

Zaidi, soma https://jamii.app/USFundingBill
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU NIGERIA: MAGUNIA 17 YA KURA ZILIZOPIGWA YAKAMATWA

> Magunia hayo yamekamatwa kwenye Jimbo la Kano na inadaiwa kura zake zimepigwa ili kukipa ushindi chama tawala cha All Progressive Party (APC)

Zaidi, soma => https://jamii.app/NigeriaBallotsScandal
WANASAYANSI ITALIA WATENGENEZA CHANJO YA UKIMWI

> Wanasayansi kutoka nchini Italia wamegundua chanjo dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI ambayo imefanikiwa kupunguza idadi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa huo mwilini kwa asilimia 90

Fahamu zaidi, soma - https://jamii.app/UtafitiChanjoUKIMWI
ZANZIBAR: MWANAUME AMJERUHI MKE WAKE USONI, BAADA YA KUKATAA KUTOA PENZI KINYUME NA MAUMBILE

> Amesema Mume wake alianza kumuomba penzi kinyume na maumbile miezi 3 baada ya ndoa

> Baada ya kukataa Mume wake alianza kumwambia hajui mapenzi

Soma > https://jamii.app/AjeruhiwaMapenziZNZ
AIRBUS KUSITISHA UZALISHAJI WA NDEGE AINA YA A380

> Shirika la Airbus limetangaza kusitisha uzalishaji wa ndege zake aina ya A380 Superjumbo ifikapo 2021 kutokana na kukosekana kwa soko

> Mteja mkuu alikuwa ni Shirika la ndege la Emirates

Soma - https://jamii.app/AirbusSeizeA380
TRUMP KUSAINI MUSWADA WA KUGHARAMIA MATUMIZI YA SERIKALI

> Muswada huo utazuia kufungwa tena kwa Serikali Kuu na kuwapa ahueni wafanyakazi takribani 800,000 waliopata kadhia ya kutolipwa mishahara mwezi Desemba

> Aahidi kutangaza hali ya dharura ili kupata pesa za kujenga ukuta

Soma - https://jamii.app/USFundingBill
KENYA: AFISA WA POLISI AHUKUMIWA KIFO KWA KUMUUA MAHABUSU

> Mahakama Kuu imempa adhabu ya kifo Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Nahashon Mutua kwa kosa la kumuua Mahabusu

> Mutua alimpiga na nondo Martin Koome hadi kufa mwaka 2013

Soma - https://jamii.app/AfisaPolisiAhukumiwaKifoKE
RAIA 13 WA ETHIOPIA WAKAMATWA MWANZA

> Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia raia 13 wa Ethiopia baada ya kukutwa wakiwa wamejificha kwenye shamba la mkazi mmoja wa mtaa wa Nyaburogoya Kata ya Nyegezi

> Walikamatwa Februari 13

Soma - https://jamii.app/WahamiajiEthiopiaWakamatwa
KENYA: MAAFISA WATANO WA POLISI WAKUTWA NA HATIA YA KUMUUA MTOTO

> Maafisa 5 wa Jeshi la Polisi, wamekutwa na hatia ktk kesi ya kumpiga na kitu kizito kichwani mtoto mwenye umri wa miezi 6, Samantha Pendo mwaka 2017 na kumsababishia kifo

Soma - https://jamii.app/Maafisa5HatianiMauajiMtoto
KAMPALA, UGANDA: WANAWAKE WAWILI WAFANYAKAZI WA BENKI WABAKWA NA MAJAMBAZI

> Wanawake hao ni wafanyakazi wa Benki ya Development Finance Company of Uganda(DFCU). Wamebakwa na majambazi waliojaribu kupora fedha katika benki hiyo

Soma > https://jamii.app/KampalaBankRobbery