JamiiForums
53.4K subscribers
34.2K photos
2.36K videos
31.2K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SHINYANGA: WATU 2 WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIA KWENYE SHIMO LA MACHIMBO YA KOKOTO

> Shimo hilo limejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwenye kijiji cha Kadoto huko Mwalukwa

Zaidi, soma => https://jamii.app/WafarikiShimoKokoto
SLOVENIA: MBUNGE AJIUZULU BAADA YA KUIBA MKATE

> Mbunge Krajcic wa Slovenia amejiuzulu baada ya kuiba mkate maarufu ''sandwich'' katika duka moja kwa madai kuwa wahudumu wa sehemu hiyo walimpuuzia

> Ameomba msamaha na kujutia kufanya hivyo

Soma - https://jamii.app/PmResignsStealingSandwich
AFARIKI KWA KUCHOMWA KISU NA MKEWE

> Mkazi wa Kijiji cha Lugalawa, Wilaya ya Ludewa-Njombe, Osmund Joseph Mwinuka(37) amefariki baada ya kuchomwa Kisu tumboni na mke wake kwa wivu wa Mapenzi

> Kamanda wa Polisi amethibitisha taarifa hiyo

Soma - https://jamii.app/MkeAuaMumeLudewa
KONDOMU ZADAIWA KUADIMIKA WILAYANI MAFINGA

> Kondomu za kike na kiume zimeonekana kupungua mjini hapo huku zilizopo zikielezwa kupanda bei na kuuzwa ghali kuanzia shilingi 1,000 mpaka 3,000

Soma - https://jamii.app/UhabaKondomuMafinga
SERIKALI KURUDISHA KODI KWENYE TAULO ZA KIKE KAMA HAZITASHUKA BEI

> Hii ni kutokana na wauzaji na wasambazaji wa taulo hizo kushindwa kupunguza bei licha ya kodi kuondolewa

> Waziri wa Fedha na wa Viwanda watakiwa kuanza kusimamia

Soma > https://jamii.app/BeiTauloKike
KILIMANJARO: MADUKA ZAIDI YA 150 YAFUNGWA KUPINGA ONGEZEKO LA KODI

> Wafanyabiashara katika kituo kikuu cha mabasi wamefunga maduka yao wakipinga ongezeko la kodi

> Manispaa imewataka walipe kodi ya 400,000/- hadi 450,000/- kwa kila pango

Soma > https://jamii.app/MgomoMadukaMoshi
ARUMERU: SERIKALI ITAWACHUKULIA HATUA ASKARI WANAOSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

> Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola asema watakaobainika kutumia magari ya Jeshi la Polisi kubeba/kusafirisha/kusindikiza #DawaZaKulevya watawajibishwa

Zaidi, soma => https://jamii.app/KangiArumeru
KAGERA: WALIOKUTWA NA HATIA YA KUCHOMA KANISA WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA

> Mahakama imetoa hukumu hiyo kwa Watu watatu iliyowakuta na hatia ya kuchoma moto Kanisa Katoliki Kigango cha Nyarwele, Parokia ya Kimiza

Zaidi, soma => https://jamii.app/KageraKifungoMaisha
MAREKANI: MKE AMUUA MUMEWE ILI AFUNGE NDOA NA MPENZI WAKE

> Mfanyakazi wa gereza, Amy Murray(40) anatuhumiwa kumuua mumewe, Joshua Murray(72) kwa kumtilia sumu kwenye chakula, ili apate nafasi ya kufunga ndoa na mpenzi wake ambaye ni mfungwa

Soma https://jamii.app/WifeKillsHusbandUS
SAA 5 KABLA YA UCHAGUZI NIGERIA: TUME YATANGAZA KUAHIRISHA KWA WIKI MOJA

> Uchaguzi wa Rais na Wabunge umesogezwa mbele hadi Jumamosi tarehe 23 mwezi huu

> Aidha, uchaguzi wa Magavana umepangwa kufanyika tarehe 9 ya mwezi Machi 2019

Soma => https://jamii.app/NigeriaElectionDelayed
WANAWAKE WENYE MIAKA 30+ HATARINI KUUGUA SARATANI

> Breast Cancer Now limefadhili utafiti uliobaini kwamba, Saratani hutambulika mapema kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 35 hadi 39 wanapofanyiwa uchunguzi kila mwaka(mammograms)

Zaidi, soma - https://jamii.app/WomenVsBreastCancer
#JFAfya
MISRI: MCHAKATO WA RAIS ABDEL FATTAH KUKAA MADARAKANI HADI 2034 WAANZA

> Mchakato huo utamuwezesha rais Abdel Fattah al-Sisi kukaa madarakani hata baada ya muhula wake kuisha 2022

> Wabunge 485 kati ya 596 wameunga mkono mabadiliko hayo

Soma => https://jamii.app/MisriRais2034

#JFInternational
KAYA 2,086 ZAKUMBWA NA MAFURIKO MTWARA

> Wananchi wa vitongoji vya Migombani-Mbuyuni na Mchangani wamelazimika kuyahama makazi yao kufuatia kufurika kwa maji ktk Mto Ruvuma

> Kumetokea uharibifu wa zaidi ya Ekari 3,014 za Mpunga na Mahindi

Soma - https://jamii.app/Kaya2086MafurikoMTR
ARUSHA: MKURUGENZI WA KAMPUNI YA OBC AFIKISHWA MAHAKAMANI

> Siku 3 zilizopita Serikali iliagiza kukamatwa kwa ndugu, Isack Mollel(59) Mkurugenzi wa Ortello Business Cooperation, kwa tuhuma za kuajiri Wafanyakazi 10 wa kigeni bila vibali

Soma => https://jamii.app/MkurugenziOBCMahakamani
SERIKALI YAAHIDI KUSHIGHULIKIA SUALA LA KIJANA ALIYEPIGWA RISASI NA POLISI, ARUSHA

> Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola

> Richard Peter, alipigwa risasi na Askari Polisi ktk eneo la Kituo cha Polisi, Usa River

Soma > https://jamii.app/SerikaliVsMauajiArusha
Mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0

> Goli pekee la Simba SC limefungwa na Meddie Kagere kunako dakika ya 71 ya mchezo huo

#JFLeo #JFMichezo
MAREKANI: WATANO WAFARIKI KWENYE MAJIBIZANO YA RISASI

> Watu 5 wameripotiwa kufariki na askari 5 kujeruhiwa ktk makabiliano ya risasi yaliyotokea ktk jimbo la Illinois nchini Marekani

> Aliyeendesha shambulizi hilo naye ameuawa

Soma - https://jamii.app/5KilledGunmanUS
#JFInternational
AKIUA KICHANGA KWA KUJIFUNGULIA KWENYE NDOO ILIYOJAA MAJI

- Polisi mkoani Manyara inamshikilia Ramla Omary(23) kwa kutupa kichanga shimoni baada ya kukiua alipokuwa anajifungua

- Inaelezwa Ramla amefanya hivyo kwa madai kuwa ana maisha magumu

Zaidi, soma https://jamii.app/AjifunguliaNdooMNYR
SIMIYU: MWILI WAOKOTWA UKIWA UMETOLEWA BAADHI YA VIUNGO

- Mwili wa Mmwanamke ambaye jina lake halijafahamika umeokotwa katika kijiji cha Lamadi Wilayani Busega

- Umekutwa katika nyumba chakavu ukiwa umekatwa sehemu za siri na titi la kushoto

Zaidi, soma https://jamii.app/MauajiMwanamkeSMY1
UFARANSA: MAANDAMANO YAFANYIKA KWA MIEZI MITATU MFULULIZO

- Waandamanaji wanaovaa vizibao vya njano na kupinga sera za kiuchumi za Rais Macron waliandamana jana

- Takribani Waandamanaji 41,500 waliandamana ikiwa ni wikiendi ya 14 mfululizo

Zaidi, soma https://jamii.app/MaandamaniVisibaoNjano