JamiiForums
52.8K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mtengenezaji maudhui mtandaoni, Warda Mansour akitoa maoni yake kuhusu watumiaji wa mitandao wanaotumia kauli za kejeli ameshauri kuwa kila mtu ana nafasi ya kutumia maudhui kuelimisha lakini ni muhimu kuheshimu maoni ya kila mtu hata kama hukubaliani nae

Tembelea JamiiFoums.com kwa mijadala zaidi

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #KauliZaChuki #StopHateSpeech #DigitalPeace #NoToHateSpeech #ResponsiblePosting #JamiiYenyeUelewa
1
JF MDAU: Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Mahusiano, Mapenzi na Urafiki ameeleza changamoto aliyopitia katika ndoa yake waliyojaliwa na mkewe kupata Watoto wawili ilivyomsababishia kupata maradhi ya Kiharusi (stroke) licha ya kupambana kuwa Kiongozi wa Familia.

Anasema "Mitikisiko ninayokumbana nayo imenipatia stress (msongo wa mawazo) na sasa ninaishi kwa Neema za Mungu baada ya kupigwa stroke (kiharusi). Bado ni Mwanaume kamili lakini nimejirudi na sasa nailinda sana nafsi yangu dhidi ya tamaa za mwili. Mwaka wa nne sasa nimemuweka mbali shemeji na wifi yenu. Sijaachana naye lakini nina amani yupo mbali."

Soma zaidi https://jamii.app/KiharusiNdoa

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #Maisha #JFLifestyle
1
Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Serikali kuingilia kati kiwango cha faini kinachotozwa na kampuni inayoshughulika na ukamataji wa magari maeneo ya Ubungo, akieleza kuwa faini inayosomeka kwenye fomu ni Tsh. elfu 80 bila kuendana na aina ya kosa.

Amedai kuwa kampuni hiyo imekuwa ikikamata magari licha ya magari hayo kuwa tayari yamekaguliwa (scanned), na wakati mwingine wanakamata hata pale ambapo dereva amesimama kwa dharura.

Zaidi soma https://jamii.app/UonevuKwaMadereva

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #JFMdau2025
ARUSHA: Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ametoa ushauri kwa Mamlaka za Jiji kuangalia changamoto ya baadhi ya Maafisa wa Usalama katika Barabara kati ya Soko Kuu na Sokoine, akidai hawatendi haki kwa baadhi ya madereva wanaopita njia hiyo kiasi kwamba wengine wanatengeneza mazingira ya usumbufu ili 'wamalizana pembeni'.

Soma zaidi https://jamii.app/FainiArusha

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #JFMdau2025 #Accountability
👍1
Msajili wa vyama vya siasa nchini amekitaka chama cha ACT Wazalendo kuwasilisha utetezi wao juu ya malalamiko ya Monalisa Ndala - Mwenezi wa ACT
Wazalendo, Mkoa wa Dar es Salaam, dhidi ya uvunjifu wa kanuni za chama hicho kabla ya kupita tarehe 20 Agosti 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 19, 2025 na Sisty Nyahoza imewataka ACT watoe maelezo juu ya kuvunja kanuni ya chama chao kuhusu uteuzi wa mgombea wa urais wa chama hicho Luhaga Mpina.

Aidha, Monalisa ameilalamikia kanuni ya chama inayoeleza sifa za mgombea wa urais anatakiwa awe mwanachama wa chama hicho kwa muda wa mwezi mmoja na kwamba Mpina hajatimiza mwezi tangu ajiunge na chama hicho.

Zaidi https://jamii.app/ACTKujiteteaKesho

#JamiiForums #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025 #JFSiasa
👍1
DODOMA: Mahakama Kuu inatarajiwa kutoa uamuzi wa mapingamizi yaliyowekwa na Chama Cha Mapinduzi (#CCM) dhidi ya Mchungaji Dkt. Godfrey Malisa, ambaye anapinga uhalali wa mchakato uliompitisha Rais Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwania urais kupitia Chama hicho.

Mawakili wa CCM, Fabian Donates na Alex Mgongolwa, leo Agosti 19,2025 wamewasilisha mapingamizi wakidai hatua za kufungua shauri hilo hazikufuatwa, huku wakisisitiza mlalamikaji alipaswa kuandika barua kwa Katibu Mkuu badala ya mwenyekiti wa Chama.

Aidha, wakili wa mlalamikaji, Denis Maringo, amesema taratibu zilizingatiwa kwani Februari, 2025, Dkt. Malisa alimwandikia barua Rais Samia akilalamikia uteuzi wake, ambapo baada ya hoja za pande zote kusikilizwa, Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 22, 2025.

Soma https://jamii.app/MalisaNaCCM

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Governance
SIMIYU: Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina akiwa katika zoezi la kutafuta udhamini mkoani humo Agosti 17, 2025.

Soma Zaidi https://jamii.app/MpinaMagufuli

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSiasa #UchaguziMkuu2025
Unapocheka, haujifurahishi tu bali pia unapunguza msongo wa mawazo, unaimarisha kinga ya mwili na kulinda moyo wako.

Kwa kifupi, kicheko ni afya — basi jitafutie sababu ya kucheka kila siku. 😄

Tembelea JamiiForums.com kushiriki kwenye mijadala mbalimbali yenye tija.

#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
😁1
KATAVI: Mdau wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa Mkazi wa Wilaya ya Mpanda anatoa wito kwa Shirika la Umeme Tanzania (#TANESCO) kushughulikia changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara, akihoji mbona wanapodai madai yao hutumia magari ya matangazo kuzunguka Mtaani kufikisha ujumbe, lakini suala la kukata umeme hutumia makundi ya WhatsApp ambayo Wananchi wengi hawana au hawatumii?

Zaidi soma https://jamii.app/UmemeMpanda

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFHuduma #Accountability #JFMdau2025 #JFUwajibikaji
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Akizungumza Agosti 18, 2025, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, amesema "Uchaguzi wetu kila baada ya Miaka mitano ni jambo muhimu sana kwa Taifa letu, ndiyo kielelezo cha #Demokrasia ya #Tanzania. Nchi hii haijawahi kuahirisha uchaguzi hata mara moja na katika mazingira magumu kuliko sasa. Wanaotaka Uchaguzi uahirishwe hawaelewi historia ya nchi hii."

Zaidi soma https://jamii.app/KabudiUchaguziMkuu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Governance