MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Mamlaka kufuatilia tukio analodai linadalili za ‘kuminywa’ linalohusu Mtoto wa Kiume wa Miaka Minne Mkazi wa Nyakato kulawitiwa na jirani yake na kwamba suala hilo lilipofikishwa Kituo cha Polisi Kirumba kumekuwa na hali ya sintofahamu kuhusu kinachoendelea.
Mdau anadai Mtoto anaishi na bibi yake, alipofanyiwa ukatili huo mara mbili mtuhumiwa alimwambia asiseme kwa kuwa akisema bibi yake ‘atamchapa sana’. Bibi alipoona mjukuu anatembea kwa kuchechemea akamlazimisha kusema nini kimemsibu, ndipo Mtoto akaelezea na kumtaja jirani yao.
Mdau anaongeza kuwa Bibi na Mtoto walipoenda kuripoti Kituo cha Polisi Nyakato walimkuta Mtuhumiwa eneo hilo pia akipiga ‘stori’ na Askari, Mtoto akaonesha aliyemfanyia ukatili yupo eneo hilo, mtuhumiwa akakamatwa lakini baada ya kesi kuhamishiwa Kituo cha Polisi Kirumba ndipo kukatokea ‘sintofahamu’ na haijulikani nini kinachoendelea.
Soma zaidi https://jamii.app/UkatiliNyakato
#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #ChildRights #Accountability

❤2
MWANZA: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuhoji Kiongozi gani wa juu anayemlinda mtuhumiwa wa Ulawiti kwa Mtoto katika Kituo cha Polisi Kirumba, Mkuu wa Mkoa, Said Mtanda ametoa maelekezo kwa Mwananchi huyo kuhusu kipi anachotakiwa kukifanya.
RC Mtanda ameandika “Namshauri huyo aliyedhurumiwa haki yake kufika pia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya au Mkoa, kwa Mwanza kila Jumanne tunakutana na Wananchi wenye changamoto za namna hizo, anaweza kuwa hajasikilizwa na taasisi moja lakini Kiongozi wa Serikali katika Wilaya ya Nyamagana ni Mkuu wa Wilaya amuone, yawezekana hajui. Kama hatasikilizwa aje Ofisi ya Mkuu wa Mkoa siku ya Jumanne.”
Ikumbukwe Mdau alisema Mtu huyo ambaye amemlawiti Mtoto wa Miaka minne eneo la Nyakato, alifikishwa Kituo cha Polisi akahojiwa, Mtoto akatoa maelezo, vipimo vya Hospitali ya Sekou Toure vikaonesha ameingiliwa lakini hakuna kinachoendelea, akidai kuna mazingira ya Mtuhumiwa kulindwa na Kiongozi wa ‘juu’.
Zaidi soma https://jamii.app/RCMtandaUfafanuzi

Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KATAVI: Mwakilishi wa Wafanyabiashara Mjini Mpanda, Aman Mahella amehoji kwanini mikopo kwa Vijana na akinamama hutolewa karibu na Uchaguzi huku ikiambatana na ujumbe wa Kisiasa jambo linaloashiria rushwa?
Akizungumza katika mafunzo ya kupambana na #Rushwa kuelekea #UchaguziMkuu2025, yaliyotolewa na #TAKUKURU, Ijumaa Agosti 15, 2025, Mahella ametoa wito kwa Serikali kuimarisha mifumo ya kudhibiti rushwa ili kuondoa mianya hiyo wakati wa Uchaguzi.
Soma https://jamii.app/RushwaMikopoUchaguzi
#JamiiAfrica #JamiiForums #UtawalaBora #Uwajibikaji #Accountability #Governance

DAR: Mdau wa JamiiForums.com amedai kuna changamoto ya upatikanaji wa kadi zinazotumika kununua tiketi katika usafiri wa Mabasi ya Mwendokasi na kutoa wito hatua zichukuliwe haraka kwa kuwa hali hiyo ni kero na inawakosesha baadhi ya Watu huduma.
Ikumbukwe Julai 26, 2025 Mdau mwingine alidai kuna kero kubwa ya kutopatikana kwa kadi hizo siku za wikiendi, Agosti 6, 2025, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dkt. Athumani Kihamia alisema sio lengo lao kuuza kadi wakati wa Siku za Jumamosi na Jumapili, abiria anaweza kupata kadi kwa siku tano za wiki ambazo ni Jumatatu hadi Ijumaa.
Mjadala zaidi https://jamii.app/TiketiMwendokasi
#JamiiForums #JamiiAfrica #JFHuduma #Accountability #JFMdau2025 #JFUwajibikaji

❤1
Mdau wa JamiiForums.com kupitia jukwaa la Siasa ameibua hoja kuhusu magari yenye plate number za aina ya SSH 25-30 au SSH 2530, akisema kuna magari mengi yenye namba zinazofanana na wengi mtaani wanajiuliza iwapo wamiliki wake ni viongozi au la!
Amehoji iwapo tukio kama ajali au uhalifu likitokea litahusianishwa na gari lipi? Je, hii si aina ya kampeni ya mapema?
Kushiriki mjadala huu https://jamii.app/PlateNumberZaSamia
#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #JFMdau2025 #JFUwajibikaji #Misinformation #Disinformation #MisDis2025 #TaarifaZaUchaguzi2025

❤3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Akizungumza na Waandishi wa Habari, Agosti 16, 2025, Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM, Saipulan Ramsey amesema “Chama Cha Mapinduzi hakijatoa kwa Mwanachama yeyote wala Mwananchi yeyote wala kutoa ruksa ya utengenezaji wa Namba za 'SSH 2530'. Ziko mamlaka husika zinazohusika na utoaji wa vibao vya namba za magari.”
Ameongeza “Chama hakina mamlaka ya kutengeneza vibao vya namba za magari, zipo mamlaka husika zinazoshughulika na jukumu hilo. Naomba mamlaka zinazohusika na utoaji wa namba za magari pamoja na usafirishaji zifuatilie yeyote aliyeweka namba hizo awaeleze amezipata wapi.”
Video Credit: Arusha Zone
Soma zaidi https://jamii.app/NambaZaSSH2530
#JamiiAfrica #JamiiForums #UtawalaBora #Uwajibikaji #Accountability #UchaguziMkuu2025

MWANZA: Mkuu wa Mkoa, Said Mtanda, leo Jumatatu Agosti 18, 2025 amefafanua suala la Mtoto Mkazi wa Nyakato, Wilayani Ilemela aliyesemekana kulawitiwa na Steven Ibasa (Baba Claudia), kwa kueleza kuwa suala hilo limefikishwa Mahakamani na kwamba mtuhumiwa amekosa mtu wa kumdhamini, amepelekwa Gerezani Butimba.
Akiwa ofisini kwake, RC Mtanda amewataka Wananchi kuwa na imani na Muhimili wa Mahakama kwakuwa utatenda haki katika suala hilo.
Ikumbukwe, suala hilo liliibuliwa na Mdau wa JamiiForums.com akidai kuna mazingira ya kumlinda Mtuhumiwa huyo ambaye alishikiliwa katika Kituo cha Polisi Nyakato kisha Kituo cha Polisi Kirumba, hivyo akaomba Mamlaka za Juu kuingilia kati ili Haki ipatikane.
Soma zaidi https://jamii.app/SaidMtandaUpdates
#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #ChildRights #Accountability
Akiwa ofisini kwake, RC Mtanda amewataka Wananchi kuwa na imani na Muhimili wa Mahakama kwakuwa utatenda haki katika suala hilo.
Ikumbukwe, suala hilo liliibuliwa na Mdau wa JamiiForums.com akidai kuna mazingira ya kumlinda Mtuhumiwa huyo ambaye alishikiliwa katika Kituo cha Polisi Nyakato kisha Kituo cha Polisi Kirumba, hivyo akaomba Mamlaka za Juu kuingilia kati ili Haki ipatikane.
Soma zaidi https://jamii.app/SaidMtandaUpdates
#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #ChildRights #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Akizungumza Agosti 18, 2025, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime amesema "Tukiona moshi unafuka hatutasubiri moto uwake, tutachukua hatua. Tukiona matamshi ambayo hayastahili, tunajua huku anakoelekea huyu siyo sahihi, lazima tuzuie kabla ya kutokea madhara."
Soma https://jamii.app/MishimeMoshi
#JamiiAfrica #JamiiForums #UtawalaBora #Uwajibikaji #Accountability #UchaguziMkuu2025
Soma https://jamii.app/MishimeMoshi
#JamiiAfrica #JamiiForums #UtawalaBora #Uwajibikaji #Accountability #UchaguziMkuu2025
❤1👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MWANZA: Kulwa Steven Ibasa (37) anayetuhumiwa kumlawiti Mtoto wa Kiume (4), amefikishwa Mahakama ya Ilemela, jana Agosti 18, 2025 na baada ya shauri lake kutajwa alikosa Mtu wa kumdhamini akapelekwa Gerezani Butimba.
Hati ya Mashtaka imesomwa na Wakili wa Serikali, Mwanahawa Changali mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Juma Opudo imeeleza Kesi hiyo Namba 20028/2025, Ibasa ameshtakiwa kwa shtaka la kulawiti, kinyume na Kifungu cha 154(1)(a)(2) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, marejeo ya Mwaka 2023.
Mshtakiwa alikana mashtaka ambapo kesi imepangwa kutajwa tena Septemba 1, 2025 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa upande wa mashahidi.
Ikumbukwe, Agosti 15, 2025, Mdau wa JamiiForums.com alihoji ukimya wa Mamlaka kuhusu tukio hilo, Mkuu wa Mkoa, Saidi Mtanda, akatoa maelekezo suala hilo lifanyiwe kazi ndipo Agosti 18 mtuhumiwa akafikishwa Mahakamani.
Zaidi soma https://jamii.app/NyakatoMatukio

This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza Agosti 18, 2025 kwenye Baraza la Wafanyakazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari ametoa onyo kwa Watumishi wanaovujisha siri za Serikali, akibainisha kuwa ofisi yake itawafuatilia kwa ukaribu na kuchukua hatua za kinidhamu kwani ni kinyume na miongozo, Kanuni na Sheria za nchi, pia kufanya hivyo ni sawa na kujipiga risasi mwenyewe.
Pia, alieleza kusikitishwa na uwepo wa Mawakili wa Serikali wenye tabia za uongo, akisema jambo hilo linaweza kuipunguzia heshima taaluma ya Sheria na kuichafua taswira ya Serikali mbele ya umma.
Soma zaidi https://jamii.app/MwanasheriaSerikali
#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji