JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MJADALA: NI UMRI GANI SAHIHI WA KUACHA KUMCHAPA MTOTO?

Katika Malezi Wazazi hukutana na changamoto nyingi hasa pale Mtoto anapokuwa mtovu wa Nidhamu. Mbinu mbalimbali hutumika ili kumuweka sawa ikiwemo Viboko

Je, ni wakati gani au umri gani wa kuacha kumpiga/kumchapa Mtoto anapokosea?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/KuchapaMtoto

#JFMalezi #Parenthood
MALEZI: ONESHA UMAKINI PALE UNAPOZUNGUMZA NA MTOTO WAKO

Mtoto huumizwa Kisaikolojia pale ambapo utaonesha kutokuwa makini wakati unazungumza naye. Unatakiwa kuhakikisha Macho yako hayatazami kwengine zaidi ya Uso wa Mtoto wako

Msikilize kwa makini na utumie Lugha rahisi kumwelewesha. Wataalamu wa makuzi wanaeleza, Watoto wanaosikilizwa hujengeka na kuwa Watu wazima wanaoheshimu mawazo ya wengine

Soma - https://jamii.app/ListenChild

#JFMalezi #Parenthood
MALEZI: TUNZA AFYA YA MTOTO KWA KUMFUNDISHA USAFI

Usafi wa Kinywa: Mpigishe Mtoto Mswaki kila siku Asubuhi na ikiwezekana kila baada ya kula. Mfundishe namna ya kuswaki vizuri ili kuzuia kuoza kwa Meno na Magonjwa ya Fizi

Usafi wa Mikono: Wafundishe Watoto kunawa Mikono kwa Maji safi na sabuni kila wanapotoka Kucheza, kabla ya Kula, baada ya Kula na baada ya kutoka Maliwato

Soma - https://jamii.app/UsafiWatotoAfya

#JFMalezi #Parenthood
MDAU: WATOTO WENGI SIKU HIZI HAWALELEWI KATIKA MIKONO YA WAZAZI WAO

Anasema kwa Dunia ya sasa Watoto wengi siku hizi hawapati nafasi ya kukua wakiwa katika Mikono ya Wazazi wao. Wengi hupelekwa Shuleni mapema zaidi, wengine wakiwa hawajaweza hata kuongea vizuri

Anasema usimkimbize Mtoto Shuleni mapema akiwa bado haelewi wala hawezi kujisaidia kwa lolote. Mlee kwanza apate ufahamu wa kujitunza

Mjadala - https://jamii.app/ShuleWatoto5
#Malezi #Parenthood
👍1
MALEZI: MAMBO YANAYOWEZA KUATHIRI MAENDELEO YA MTOTO KIMASOMO

1. Matatizo ya Kisaikolojia: Matatizo haya hutokana na kubakwa, kulawitiwa, kupigwa, kunyimwa Chakula

2. Matatizo ya Kifamilia: Kuna Familia ambazo kila siku ni Ugomvi, fujo za Ulevi, au hata Unyanyasaji mwingine kama Utumikishaji wa Watoto pamoja na Mazingira Duni ya kuishi

Soma - https://jamii.app/MasomoWatoto
#Malezi #Parenthood
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Ni muhimu kwa Wazazi kufahamu jinsi ya kuzungumza na Mtoto kwani Mazungumzo haya ni muhimu sana katika ukuaji wa ubongo wao.

#JamiiForums #Malezi #Parenthood
👍11
#MALEZI: Kila Mtu ana mipaka yake binafsi (Personal boundaries) ikiwemo Watoto. Watoto wanapaswa wawe na uwezo wa kutambua mipaka yao wakiwa na rafiki zao wa kike au wa kiume

Wazazi au Walezi wana wajibu wa kuwafundisha Watoto kutambua na kulinda mipaka hii. Mipaka inaweza kuwawezesha Watoto kujifunza kufanya maamuzi binafsi na sahihi, kujieleza, na kuwasiliana vizuri na wengine

Soma https://jamii.app/MipakaBinafsiWatoto

#JamiiForums #Parenting #ParentHood
👍6
Mdau wa JamiiForums.com anasema ni muhimu toka Watoto wakiwa na umri mdogo Baba kuonesha kuwajali na sio kusubiri hadi wakiwa wakubwa

Amesema Wababa wanapaswa kujitahidi kuwa karibu na watoto kwa kuwaletea zawadi, kuwafundisha michezo, kuwatoa out n.k.

Ameshauri akina Baba kujiepusha kuwa yule Baba Mkali ambaye akisafiri, Watoto wanajisikia amani na furaha

Soma https://jamii.app/MaleziYaBaba

#JamiiForums #JFChitChats #Malezi #Maisha #Parenting #ParentHood
👍3
Unamshauri Mdau wetu afanye Maamuzi gani kwenye jambo analopitia?

Mjadala zaidi https://jamii.app/SomeshaWatoto22

#JamiiForums #ChitChats #Malezi #Maisha #Parenting #ParentHood #JFStories
🔥2
#MALEZI: Sera ya Uzazi na Malezi nchini Sweden inawapa Wazazi jumla ya Siku 480 za likizo ya Uzazi na Malezi yenye malipo pale Mtoto anapozaliwa au kuasiliwa. Iwapo kuna Wazazi wawili, kila mmoja anapewa Siku 240

Kwa Watoto waliozaliwa mwaka 2016 au baadaye, kila Mzazi ana siku 90 ambazo haziwezi kuhamishiwa kwa Mzazi mwingine kama hazitatumika. Mzazi mmoja (single parent) anapewa Siku zote 480

Wazazi pia wanaweza kuamua kuhamisha hadi Siku 45 za likizo yao kwa Babu, Bibi au Rafiki wa karibu wa Familia, anayewasaidia kulea. Wanaostahili likizo hii ni wanaolea badala ya kufanya Kazi, Kusoma au kutafuta Kazi

#JamiiForums #NordicWeek #ParentHood #LifeStyle
👍1