JamiiForums
54K subscribers
34.1K photos
2.26K videos
31K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DODOMA: Baadhi ya majina yaliyopitishwa na Chama Cha Mapunduzi (#CCM) katika kugombea Ubunge ngazi ya awali kwenye chama hicho ni; Innocent Bashungwa - Jimbo la Karagwe Mjini, Damas Ndumbaro - Jimbo la Songea Mjini pamoja na Makame Mbarawa- Jimbo la Mkoani.

Soma Zaidi https://jamii.app/MkekaWagombeaCCM

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio #UchaguziMkuu2025 #Uchaguzi2025 #Democracy
1
DODOMA: Chama Cha Mapinduzi (#CCM), leo Julai 29, 2025 kimetangaza Wanachama wake waliopita kugombea Ubunge hatua ya awali katika Jimbo la Siha ambao ni Godwin Aloyce Mollel, Tumsifu Andree Kweka, Aggrey Mwanri, Petro Kitingala, Meijo Lolionyo Laizer, Humphrey Mosha na Bertha Izack Mlay.

Soma Zaidi https://jamii.app/MkekaWagombeaCCM

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio #UchaguziMkuu2025 #Uchaguzi2025 #Democracy
2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (#INEC) na Vyama vya Siasa, juzi Julai 27, 2025, kuhusu Uchaguzi Mkuu, Mwenyekiti wa INEC, Jaji Jacobs Mwambegele amesema kutakuwa na uwanja sawa wa kisiasa kwa vyama vyote wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025.

Zaidi https://jamii.app/UsawaKampeniVyamaVyote

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #UchaguziMkuu2025
1
1
DAR: Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA, #TunduLissu inaendelea leo Julai 30, 2025, ikiwa ni siku 14 tangu iliposikilizwa mara ya mwisho Julai 15, 2025, ambapo upande wa Jamhuri uliomba ahirisho ukieleza kuwa tayari umewasilisha ombi la kuwakinga mashahidi, ambalo wamesema lipo Mahakama Kuu.

Hata hivyo, wakati akijitetea, Lissu alipinga akiomba Mahakama itumie mamlaka yake kufuta kesi hiyo kutokana na upande wa Jamhuri kuomba ahirisho mara kwa mara, pia, Mwanasiasa huyo ametimiza siku 112 akiwa gerezani.

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho kesi hii kusikilizwa, Mahakama ilitoa uamuzi kwamba licha ya hoja za Lissu, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Franco Kiswaga, aliutaka upande wa Jamhuri kuwa kama una nia ya kuendelea na kesi hiyo, basi hatua zichukuliwe kwa haraka ili shauri hilo liwasilishwe Mahakama Kuu.

Kushiriki Bofya https://jamii.app/KesiLissuUhaini

#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights #JFMatukio #Uchaguzi2025
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) Taifa, #TunduLissu akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati wa mchakato wa kesi ya uhaini inayomkabili leo Julai 30, 2025 amepinga maombi ya upande wa Mawakili wa Serikali kutaka kusogezwa mbele kwa shauri hilo baada ya kuomba ahirisho.

Aidha, mchakato wa kesi hiyo unaendelea ambapo leo ni siku ya 112 tangu Lissu alipokamatwa na kuwekwa gerezani.

Zaidi Bofya https://jamii.app/KesiLissuUhaini

#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights #JFMatukio #Uchaguzi2025
2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga amesema wanamuachia Mungu maneno yaliyotolewa Mahakamani na Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu wakati akitoa hoja za kupinga ombi la ahirisho la kesi ya uhaini lililowasilishwa na upande wa Jamhuri, ambapo Lissu alidai wamekuwa na uzembe wa makusudi.

Lissu ametoa hoja akipinga ahirisho la kesi kama ambavyo upande wa Jamhuri uliomba, akieleza jambo hilo limekuwa la muda mrefu na kuomba Mahakama iwakatalie ombi hilo na isikubali kuendeshwa kwa maelekezo ya upande wa Jamhuri.

Kushiriki Bofya https://jamii.app/KesiLissuUhaini

#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights #JFMatukio #Uchaguzi
1
Tahadhari ya kutokea kwa mawimbi makubwa ya bahari 'Tsunami' imetolewa baada ya kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa Richa 8.8 katika eneo la Bahari ya Pacific Mashariki mwa Mji wa Urusi wa Petropavlovsk-Kamchatsky kwa mujibu wa Shirika la Jiolojia la Marekani (USGS).

Pia, Mamlaka ya Hali ya Hewa Japan imetangaza tahadhari ya Tsumani kwa maeneno mengi ya Pwani ya Mashariki mwa Nchi hiyo ikitoa onyo kwa Wananchi kuepuka maeneno ya Ufukweni kutokana na uwezekano wa mawimbi yenye urefu wa Mita 3.

Aidha, tahadhari pia imetolewa kwa maeneo ya Taiwan, Ufilipino, Visiwa vya Hawaii na Visiwa vya Aleutin vya Alaska kuwa makini na mawimbi hayo.

Soma https://jamii.app/TsunamiTetemekoRussia

#JamiiForums #JamiiAfrica #RussiaEarthquake #NaturalDisasters #ClimateChange
2
MOROGORO: Mdau ndani ya JamiiForums.com anadai jengo lililopaswa kuwa Zahanati ya Kijiji cha Lungongole lipo hapo takriban kwa Miaka mitatu na kwamba Machi 2025 alitembelea ukurasa wa Halmashauri ya Mji Ifakara akaona waliahidi Wakazi wa eneo hilo kuwa kufikia Oktoba 2025 litakuwa limekamilika, lakini haoni dalili hizo.

Amehoji ni kitu gani kinachokwamisha zoezi hilo kukamilika akidai Wanawake wanaoenda kliniki wanatembea hadi kijiji cha jirani kupata huduma muhimu, hivyo ni vizuri ujenzi huo ukakamilika.

Soma https://jamii.app/ZahanatiIfakaraNiGofu

#JamiiForums #JamiiAfrica #ServiceDelivery #Accountability #Uwajibikaji #JFMdau2025
1😁1
Akielezea hali ya kuishi mkoa tofauti na mkewe tangu Mwaka 2017, Mdau aliyejitambulisha kuwa Mwalimu anasema "Nimekosa uhamisho wa kumfuata mwenza wangu, sasa hivi ndani ya ndoa tuna Watoto wawili lakini umbali wetu umesababisha nimepata Mtoto mwingine nje ya ndoa, mke wangu hajui kuhusu hilo, sijui hata nifanye nini!"

Mdau huyo alikuwa akichangia mada ya Julai, 21 2025 ambapo Mwanachama wa JamiiForums.com alieleza changamoto inayowakumba Walimu wanaoomba uhamisho kupitia mfumo wa Kielektroniki wa 'Employee Self Service' (ESS) unaosimamiwa na TAMISEMI, akidai kuna ugumu wa maombi kujibiwa na kwamba mchakato huo unawakatisha tamaa."

Soma Zaidi https://jamii.app/KukosaUhamishoKazini

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #Uwajibikaji #Accountability #JFMdau2025
1