Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mke wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, Dkt. Fatma Mganga, amekanusha kuandika barua iliyosambaa mitandaoni inayodai amejiuzulu nafasi yake ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida kutokana na msiba marehemu mume wake kutopewa heshima stahiki.
Dkt. Mganga ametoa wito kauli hiyo usiku Agosti 9, 2025, akisema barua hiyo imeandikwa na watu wenye nia ovu, ipuuzwe.
Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/FatmaSijaandikaBarua
#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #DigitalRights #Accountability

This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (#CCM) Taifa, Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye ametangaza kuhusu harambee ya kukichangia chama hicho, amesema CCM sio taasisi ya kudhibiti fedha haramu, jibu ambalo limetokana na swali kuwa wataweza vipi kudhibiti fedha hizo wakati wa harambee yao ya kukichangia chama kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Amesema hayo wakati akizungumza na Wanahabari, leo Agosti 11, 2025 katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba.
Soma https://jamii.app/CCMSioSerikali
#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Governance #UchaguziMkuu2025 #Accountability

Kupitia Jukwaa la JamiiForums.com Mdau ameibua changamoto anayodai inawakumba Walimu wa Mbeya DC wanaotaka kujitoa kwenye Chama cha Walimu Tanzania (#CWT) ili kujiunga na vyama vingine vya Wafanyakazi.
Anadai licha ya kujaza fomu za kujitoa, maombi yao yamegomewa kwa kisingizio kuwa Mwaka huu ni wa Uchaguzi na muda mwingine wakienda wanaambiwa “hatuna majibu ya kuwapa” na kuongeza kuwa majibu hayo wanayopewa hayaridhishi na yanakera.
Mdau anaeleza kuwa hali hiyo ni kama kuwalazimisha Walimu kubaki CWT kana kwamba vyama vingine havipo kisheria, akisisitiza Walimu wana haki ya kuchagua chama chochote cha Wafanyakazi.
Soma Zaidi: https://jamii.app/WalimuMbeyaCWT
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #Uwajibikaji #Accountability #JFMdau2025

Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Siasa anauliza, Je, Wasanii maarufu wanaotumbuiza kwenye Majukwaa ya Kisiasa hawawezi kupoteza mwelekeo wa Wapiga Kura kutokana na nguvu yao ya Ushawishi?
Anadai Uwanja wa Kampeni ni mahali pa kutolea Hoja, mijadala, maswali na majibu lakini burudani inawafanya Wapiga Kura wasikie muziki na kusahau matatizo yao, kisha kupiga kura kwa hisia badala ya tafakari.
Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/WasaniiKampeni
#JamiiForums #Accountability #Misinformation #Disinformation #ElectionInformation2025 #MisDis2025 #TaarifaZaUchaguzi2025

❤1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KATAVI: Wakulima wa zao la tumbaku kutoka Chama Cha Msingi Cha Ushirika Cha Wakulima wa Tumbaku Mpanda Kati, Manispaa ya Mpanda wamelalamika kutolipwa fedha zao licha ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kutoa maagizo kuwa kabla ya Sikukuu ya Nanenane Wakulima wote wawe wamelipwa.
Wakulima hao wamefika Ofisi ya Chama hicho kufikisha malalamiko yao ambapo pia wamesema kuna nyongeza ya makato ya fedha ya 3% kinyume na utaratibu wa vikao.
Akijibu madai hayo Meneja wa Chama hicho, Zaituni Tembo amekiri Wakulima hao kutolipwa na kufafanua kuwa makato wanayosema ni makubaliano ya Bima ya Mkopo kutoka Benki ya NMB ambayo waliafikiana katika vikao vya Wakulima tofauti na benki waliyokuwa wakifanya nayo kazi awali.
Zaidi soma https://jamii.app/MpandaKati
#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio #JFEconomy #Accountability

Mdau ametoa wito kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (#PSSSF) kufuatilia utendaji wa baadhi ya Watendaji wake wa Tawi la Dodoma akidai anapigwa 'danadana' nyingi bila majibu ya msingi tangu alipoanza kufuatilia madai ya malipo yake ya kupoteza ajira tangu Mwaka 2024.
Anadai awali aliwasilisha malalamiko kupitia JamiiForums.com akasaidiwa na Ofisi ya PSSSF Kinondoni lakini alipotakiwa kwenda Makao Makuu Dodoma huko ndipo shida ilipo, akidai huduma zinaenda polepole na kila hatua inahitaji wahusika wapigiwe simu ndiyo watimize majukumu yao.
Zaidi soma https://jamii.app/UmunguWatu
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability

Mdau ndani ya JamiiForums.com ametoa wito kwa Waziri wa TAMISEMI kuingilia kati madai ya uwepo wa 'uchakachuaji' wa Fedha za Kujikimu kwa Watumishi wa Ajira Mpya Kada mbalimbali, akidai kuna changamoto ya utoaji wa malipo hayo na hata wanapoulizia hawapati majibu mazuri kutoka kwa Wasimamizi.
Soma https://jamii.app/FedhaKujikimuKuzungushwa
#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #JFMdau2025

DODOMA: Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeeleza kwa kutumia mfumo wao wa #TEHAMA kwa sasa Watu wanaweza kuhudumiwa na tawi lao lolote nchi nzima bila kulazimika kwenda Makao Makuu.
Hayo yameelezwa baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai huduma za baadhi ya Watumishi wa Makao Makuu ya #PSSSF si nzuri, akitoa mfano kuwa alihudumiwa vizuri katika Tawi la Kinondoni lakini alipofika Tawi la Dodoma mambo yakabadilika, hivyo akatoa wito kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko kufuatilia suala hilo.
Akijibu hoja ya Mdau, Meneja - Uhusiano na Elimu kwa Wanachama wa PSSSF, Omega Ngole amesema “Tumepokea taarifa hii, tunashukuru, kwa kuwa hatuna mawasiliano ya Mdau huyo, tunapitia kumbukumbu zetu ili kumpatia huduma kwa haraka kama anavyotarajia. Dhamira ya Mfuko wa PSSSF ni kujenga Kesho Bora na si vinginevyo.”
Zaidi soma https://jamii.app/PSSSFUfafanuzi
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #DigitalRights #Accountability #JFHuduma

KATAVI: Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu ameutaka uongozi wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Mpanda Kati kuhakikisha wanawalipa Wakulima waliocheleweshewa malipo yao Agosti 13, 2025.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya JamiiForums.com kuripoti malalamiko ya Wakulima hao mnamo Agosti 11, 2025 ambao walidai licha ya maelekezo ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kutoa maagizo kuwa walipwe kabla ya Sikukuu ya Nanenane 2025 lakini haikuwa hivyo.
Awali Agosti 11, 2025, alipoulizwa kuhusu malipo hayo, Meneja wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Mpanda Kati, Zaituni Tembo alisema “Kimsingi hatujalipa, tulifunga masoko tangu Julai 11, 2025 sababu Kampuni ambayo tunafanya nazo biashara haikutulipa.”
Soma https://jamii.app/WakulimaKulipwa

MAREKANI: Mtanzania Subiro Osmund Mwapinga amekamatwa nchini Ghana, Aprili 8, 2025 baada ya Idara ya Kudhibiti Dawa za Kulevya ya Marekani (DEA) kutoa taarifa kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini humo kuwa anahusika katika mpango wa kusambaza silaha kwa moja ya magenge ya biashara ya Dawa za Kulevya.
Alikamatwa na baadaye kukabidhiwa Marekani mnamo Julai 25, 2025 ambapo Subiro ni miongoni mwa watuhumiwa wanne wa kigeni ambao walikuwa na mpango wa kusambaza silaha zenye thamani ya Tsh. Bilioni 150 (Dola Milioni 58).
Watuhumiwa wengine ni kutoka Kenya na Bulgara, iwapo watapatikana na hatia wanaweza kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha Miaka 10 au kifungo cha Maisha.
Soma zaidi https://jamii.app/MtanzaniaSilahaGenge
#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #JFMatukio