JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MFAHAMU ANAYESHIKILIA REKODI YA KUCHA NDEFU DUNIANI

> Ayana Williams anashikilia Rekodi Hii baada ya kukaa miaka 23 bila kukata kucha zake na kucha yake ndefu zaidi ina urefu wa Sentimita 68

> Hata kuvua nguo yake ni kazi ngumu kutokana na urefu wa kucha zake, amekiri hilo

Zaidi, soma https://jamii.app/KuchaNdefu
IRAN YABADILI MAWAZO YA KUTUMA 'BLACK BOX' UKRAINE

- Awali, ilisema itatuma ili Maafisa wa Marekani, Canada na Ufaransa wakafanyie kazi

- Siku moja baadaye, imesema bado haijaamua kutuma na sasa wanajaribu kupata Data zilizomo ndani

Zaidi, soma https://jamii.app/IranUkraine-BlackBox
DODOMA: MABASI YAPIGWA MARUFUKU KURUHUSU ABIRIA KUJISAIDIA HOVYO

> Hairuhusiwi kujisaidia sehemu isiyo Rasmi na Faini ya kosa hilo ni 200,000 au kifungo cha miezi 6 au vyote kwa pamoja

> Kitendo hicho kimetajwa kuchangia kuchafua mazingira

Zaidi, soma - https://jamii.app/MabasiUsafiMazingira
AFISA ELIMU MBARONI KWA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA ZA MADAWATI

> Stephano Ndabazi anatuhumiwa kuiba Tsh. 24,334,920 Aprili, mwaka 2016

> Alitenda kosa hilo akiwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mpwayungu Wilaya ya Chamwino, Mkoani Dodoma

Zaidi, soma zaidi https://jamii.app/AfisaWizi
SERIKALI KUJENGA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA ZIWA WILAYANI CHATO

> Sababu za kujenga hospitali hiyo ni kuwa, tafiti zinaonesha kuna wagonjwa wengi Kanda ya Ziwa, pia Mikoa ya Kanda ya Ziwa ina watu zaidi milioni 15

Zaidi, soma zaidi https://jamii.app/NeemaChato
EDINSON CAVANI AWASILISHA MAOMBI YA UHAMISHO

- Mkurugenzi wa Michezo wa Paris Saint-Germain, Leonardo amesema Mshambuliaji huyo ameomba kuondoka mwezi huu

- Cavani (33), anahusishwa kutakiwa katika klabu za Atletico Madrid, Manchester United na Tottenham Hotspurs
MAHAKAMA YAWATAKA WADHAMINI WAMPELEKE LISSU KABLA HAIJATOA MAAMUZI MENGINE

> Wakili wa Serikali, amesema jukumu la mdhamini ni kuhakikisha mshtakiwa anafika Mahakamani

> Mdhamini alisema wameandika barua kwa Freeman Mbowe ili Lissu arejee

Zaidi, soma https://jamii.app/WadhaminiLissu
KATIBA: UTEUZI WA NAIBU SPIKA BUNGENI

> Ibara ya 85-(1): Kutakuwa na Naibu Spika ambaye atachaguliwa na wajumbe kutoka miongoni mwa Wabunge

> (2) Waziri, Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine itakayotajwa na Sheria ya Bunge hataweza kuwa Naibu wa Spika

#Katiba
KILIMO CHA MAPARACHICHI CHAMFANYA KIJANA MWENYE ELIMU YA DARASA LA SABA KUSHIKA MAMILIONI

> Steven Mlimbila ameajiri zaidi ya vijana 40

> Mwaka jana alikuwa Mkulima Bora katika maonyesho ya Nanenane kwa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini

> Mafanikio yake kiuchumi yamekuwa gumzo kwa vijana wengi wakiwamo Madereva Bodaboda ambao wamedhamiria kuingia shambani

Zaidi, tembelea https://jamii.app/MaparachichiKilimo
MALAYSIA KURUDISHA MAKONTENA 110 YA TAKA KATIKA NCHI HUSIKA

> Waziri Yeo Bee Yin amesema wanaotaka kuifanya nchi hiyo dampo waendelee kuota

> Nchi hiyo ipo katika harakati za kuachana na matumizi ya plastiki ili kutunza mazingira

Zaidi, soma - https://jamii.app/TakaMazingiraMalaysia
MWANZA: WATUMISHI WA TANESA WANYANG'ANYWA MAJENGO

- TAKUKURU imechukua majengo 4 yenye thamani ya Tsh. milioni 420 yaliyojengwa na Uholanzi na kukabidhiwa Serikali

- Imesema, baada ya mradi kuisha Watumishi walijimilikisha kinyemela majengo hayo

Zaidi, soma https://jamii.app/TAKUKURU-MajengoTANESA
ZAIDI YA WATOTO MILIONI 3 HAWAHUDHURII MASOMO KUTOKANA NA UGUMU WA MAISHA

> Sudan imeorodheshwa kama mojawapo ya mataifa masikini zaidi duniani

> Watoto hawawezi kuendelea na masomo kutokana na hali ngumu ya maisha

Zaidi, soma https://jamii.app/SudanAjiraWatoto
ELIMU KATIBA: SEKRETARIATI YA BUNGE

- Ibara ya 88.-(1) inasema Kutakuwa na Sekretariati ya Bunge itakayokuwa na nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali kwa idadi atakayoagiza Rais

- (2) Sekretariati ya Bunge itakuwa na watumishi kwa idadi na ngazi za utumishi itakavyoamuliwa mara kwa mara na Tume ya Utumishi inayohusika baada ya kushauriana na Katibu wa Bunge
IRAQ: KIONGOZI WA ISLAMIC STATE AKAMATWA

> Abu Abdul Bari amekamatwa na kubebwa na Lori kutokana na uzito wake wa kilo 250. Iraq imethibitisha kukamatwa kwa Kiongozi huyo

> Bari ni Mufti wa Kundi la IS na Mtaalamu wa Sheria za Dini

Zaidi, soma zaidi https://jamii.app/KiongoziIS
ULINZI WA KIDIGITALI: JINSI YA KUWA SALAMA UNAPOKUWA MTANDAONI

> Usifungue Link au Email kutoka kwa mtu usiyemfahamu

> Wadukuzi huambatanisha na jumbe za kuvutia. Endapo utafungua kiunganishi hicho unamruhusu mdukuzi aingilie mawasiliano yako

> Tumia Password (Nywila) iliyo Bora Zaidi

Soma > https://jamii.app/SafeBrowsing
JamiiForums kupitia Jukwaa lake la Ajira na Tenda linakupa nafasi mdau wetu kuweza kupata nafasi mbalimbali za Kazi iwe ni Serikali, katika Mashirika ya Ndani au hata ya Kimataifa

- Kujua nafasi mbalimbali za Kazi na Tenda zilizotangazwa Nchini au Nchi za Nje kwa ajili ya Raia wa Tanzania, tembelea Jukwaa hilo, fungua https://jamii.app/JukwaaTendaAjira
RSF YATAKA UCHUNGUZI WA KINA KUHUSU MAUAJI YA WAANDISHI 3

> REPORTERS WITHOUT BORDERS (RSF) yadai uhakiki wa ushahidi uliotolewa katika uchunguzi wa mwanzo

> Waandishi watatu wa Urusi waliuawa na watu wasiojulikana Jamhuri ya Afrika ya Kati

Zaidi, soma https://jamii.app/RSFWaandishi
MICHEZO: Klabu ya Aston Villa @AVFCOfficial ya nchini England yatangaza rasmi kumsajili Mbwana Samatta kutoka Klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji

> Samatta amesaini kandarasi kuitumikia Klabu hiyo kwa muda wa miaka 4 na nusu

#JFSports #KaribuSamatta
SHINYANGA: MBARONI KWA KUTOZA WATU FEDHA ILI WASAJILI LAINI

- Afisa wa NIDA, Haruna Mushi na Wakala wa Usajili Laini, Victor Vicent wanatuhumiwa kutoza Wananchi Tsh. 30,000 ili wawape Namba za NIDA na kusajili laini zao kwa Alama za Vidole

Zaidi, soma https://jamii.app/WakalaAfisaNIDA-Mbaroni
ADHABU YA KOSA: Kwa mujibu wa Sheria ya Kuzia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007, Kifungu cha 34 (1) kinasema Mtu huyo atakuwa ametenda Kosa na atawajibika kwa kulipa faini isiyozidi Tsh. Milioni 10 au kwenda Jela kwa Kifungo kisichozidi miaka 7 au vyote kwa pamoja

#KemeaRushwa