JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KARIAKOO DERBY: SIMBA NA YANGA KUTUNISHIANA MISULI LEO

- Wakati homa ya mchezo wa Watani wa Jadi ikiendelea kupanda, katika mechi 10 zilizopita Simba imefunga magoli 10 kipindi cha pili na katika kipindi cha kwanza imefunga magoli 10

- Yanga nayo imekuwa moto kipindi cha pili kwa kufunga magoli 8 na katika Kipindi cha kwanza imefunga magoli 6

Je, ni Mashabiki wa timu gani kutoka na kicheko leo Taifa?

Fuatilia https://jamii.app/YanayojiriSimbaYanga
IRAQ: MAZISHI YA QASSEM SOLEIMANI YAFANYIKA

> Maelfu ya Raia wa Iraq wamekuwa wakiimba 'Kifo cha Marekani' wakati wa mazishi ya Kamanda, Qassem Soleimani na Mkuu wa Jeshi la Akiba Abu Mahdi al-Muhandis

> Makamanda hao maarufu wameuawa kwa shambulio la anga lililofanywa na Marekani
MWANAHABARI WA DW ADAIWA KULISHWA SUMU

> Deokaji Makomba amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada ya kufikishwa akiwa hajitambui

> Ndani ya Basi la Ally's alipewa vipande vya Biskuti na abiria aliyepandia njiani

Soma > https://jamii.app/DeokajiSumuBasi
MICHEZO: Klabu ya Simba inapata goli la kuongoza dhidi ya Klabu ya Yanga kupitia goli lililofungwa na Meddie Kagere katika dakika ya 42

- Goli la Simba limepatikana kupitia mkwaju wa penati baada ya Meddie Kagere kuchezewa rafu na Beki Kelvin Yondani ndani ya eneo la hatari

Fuatilia https://jamii.app/YanayojiriSimbaYanga
MICHEZO: Klabu ya Simba inapata goli la kuongoza dhidi ya Klabu ya Yanga kupitia goli lililofungwa na Meddie Kagere katika dakika ya 42
-
Goli la pili la Simba inafungwa na Deo Kanda katika dakika ya 47 huku goli la Kwanza la Yanga likifungwa na Balama Mapinduzi katika dakika ya 50
MICHEZO: Klabu ya Simba inapata goli la kuongoza dhidi ya Klabu ya Yanga kupitia goli lililofungwa na Meddie Kagere katika dakika ya 42

- Goli la pili la Simba inafungwa na Deo Kanda katika dakika ya 47 huku goli la Kwanza la Yanga likifungwa na Balama Mapinduzi katika dakika ya 50

- Goli la pili la Yanga limepatikana baada Mohamed Hussein kujifunga katika dakika ya 53
MICHEZO: Simba na Yanga zimeshindwa kutambiana baada ya timu hizo kufungana goli 2-2 katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

- Magoli ya Simba yamefungwa na M. Kagere (42’) na D. Kanda (47’) huku ya Yanga yakifungwa na B. Mapinduzi (50’) na M. Hussein (53’) aliyejifunga
RAIS TRUMP AIPIGA MKWARA NCHI YA IRAN

> Amesema, Marekani imetumia Dola Trilioni 2 kwa ajili ya Vifaa vya Kijeshi

> Ameonya kuwa, iwapo Iran itashambulia kituo chochote cha Kijeshi cha Marekani au Raia yeyote basi hawatasita kuvitumia

Soma > https://jamii.app/TrumpOnyoIran

#JFLeo
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KENYA: Polisi imethibitisha kuwepo kwa shambulio linaloendelea la #AlShabaab katika Kambi ya Jeshi ya Simba

> Kambi hiyo iliyopo Kaunti ya Lamu inatumiwa na Wanajeshi wa Kimarekani na Kenya

> Mashuhuda wanadai kusikia milio mingi ya risasi huku moshi ukitoka eneo hilo
Kambi ya Jeshi ya Simba iliyopo Kaunti ya Lamu inatumiwa na Wanajeshi wa Marekani na Kenya
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
IRAN YAPANDISHA BENDERA NYEKUNDU KUASHIRIA KISASI CHA DAMU

- Imepandisha bendera hiyo juu ya Msikiti Mtakatifu wa Jamkaran uliopo Qom, tukio linaloashiria kisasi cha damu kinakuja

- Inaelezwa hii ni mara ya kwanza kwa Iran kupandisha bendera hiyo kwani hata kwenye vita vya Iran na Iraq bendera hiyo haikupandishwa

Zaidi, soma https://jamii.app/IranBenderaNyekundu
KIGOMA: WATU WANNE WA FAMILIA MOJA WAUAWA

- Watu hao wameuawa kwa kukatwa mapanga na kubomolewa nyumba yao na watu wasiofahamika

- Chanzo cha mauaji hakijafahamika, ila baadhi wanahusisha mauaji hayo na Imani za Kishirikina

Zaidi, soma https://jamii.app/MauajiFamiliaKigoma
MPYA: Rais Trump amesema ameorodhesha maeneo 52 ya Iran watakayoyashambulia kwa nguvu na haraka iwapo ataguswa Mmarekani au eneo lolote la Marekani kama kulipa kisasi

- Jana, Iran yenyewe ilibainisha kuwa imeorodhesha maeneo 35 ya Marekani watakayoshambulia kulipa kisasi

Zaidi, soma https://jamii.app/USA-52SitesIran
UINGEREZA YAUNGANA NA MAREKANI

- Waziri wa Mambo ya Nje ya Uingereza, Dominic Raab amesema wapo ukurasa mmoja na Marekani kuhusu mauaji ya Jenerali Qassem Soleimani

- Amesema ameongea Rais wa Iraq na Waziri Mkuu, pamoja na Ufaransa na Ujerumani, ikiwa lengo ni kurudisha utulivu na kulinda Majeshi na Wananchi wake katika maeneo ya Mashariki ya Kati

Zaidi, soma https://jamii.app/US-UKSamePage
LIBYA: KAMBI YA MAFUNZO YA KIJESHI YASHAMBULIWA, WATU 28 WAFARIKI

- Wanafunzi 28 wa Mafunzo ya Kijeshi wamefariki na wengi kujeruhiwa katika shambulio lililofanywa kwa njia ya anga ambapo wakati wa shambulio Wanafunzi walikuwa kwenye gwaride

Zaidi, soma https://jamii.app/LibyaMilitaryAcademy
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
VIDEO: Sehemu ya Umati wa Watu iliyojitokeza kupokea mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Iran, Jenerali Qassem Soleimani aliyeuawa na Marekani huko Iraq

- Maelfu ya Watu wamejipanga katika mitaa ya Miji ya Ahvaz na Mashhad huko Iran kutoa salamu za Mwisho
MOMBASA, KENYA: MCHUNGAJI AMUUA KWA KISU MKEWE NA YEYE KUJIUA

> Imeelezwa, Mchungaji Elisha Misiko wa Kanisa la Ground For Gods Gospel (3G) Ministries alimshambulia kwa kisu mkewe kisha na yeye kujiua

> Tukio hili limetokea wakati Ibada ya Jumapili ikiendelea

Soma > https://jamii.app/MauajiKanisani