JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UCHAGUZI SINGIDA MASHARIKI: MGOMBEA WA CCM APITA BILA KUPINGWA

> Miraji Mtaturu amepita ktk uchaguzi mdogo baada ya wagombea 12 wa upinzani kutorejesha fomu

> Wenye pingamizi wametakiwa kuwasilisha mapingamizi yao kabla ya kesho saa 10 jioni

Soma https://jamii.app/MgombeaUchaguziSingida
#JFLeo
KUFUZU #AFCON2021: TANZANIA KUNDI MOJA NA TUNISIA NA LIBYA

- CAF yatangaza makundi ya kufuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2021 itakayofanyika Cameroon

- Tanzania ipo Kundi J, pamoja na Tunisia, Libya na Equatorial Guinea

Zaidi, soma https://jamii.app/KufuzuAfcon2021
SKYSPORTS: BARCELONA YAWEKA DAU KWA AJILI YA NEYMAR

- Barcelona inadaiwa kuweka dau la £90m na Wachezaji wawili ili imsajili Neymar kutoka PSG

- Inadaiwa imewapa PSG orodha ya Wachezaji 6 wakiwemo Philippe Coutinho, Ousmane Dembele, Ivan Rakitic, Nelson Semedo na Malcom
AFISA MIPANGO MIJI ASIMAMISHWA KAZI KWA KUUZA ARDHI KINYUME NA TARATIBU

- Waziri Lukuvi amemsimamisha kazi Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Manase Nkuli

- Ameghushi nyaraka na kuuza hekari 6000 za ardhi kinyume na taratibu

Zaidi, soma https://jamii.app/AfisaMipangoSengerema
WAKULIMA WA PAMBA KUPEWA VITAMBULISHO

- Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ameiagiza bodi ya Pamba kuviandaa na kuvigawa bure ili kuwatambua wakulima

- Pia, ameahidi Serikali kufidia kiasi cha fedha ili kilo ya pamba inunuliwe kwa Tsh. 1,200

Zaidi, soma https://jamii.app/VitambulishoWakulimaPamba
UKUAJI WA UCHUMI TANZANIA 2018: BENKI YA DUNIA YATOFAUTIANA NA SERIKALI

- Benki ya Dunia inasema uchumi ulikuwa kwa 5.2% tofauti na Serikali iliyosema ulikuwa kwa 7%

- Moja ya sasabu iliyoathiri ukuaji ni kushuka kwa viwango vya uwekezaji

Zaidi, soma https://jamii.app/UchumiTanzania2018-WB
MOSHI: WAZIRI MKUU AAGIZA WALIOKUWA WALINZI WA KITUO CHA MABASI KUKAMATWA

> Ni walinzi waliokuwa lindo eneo la ujenzi wa stendi ya mabasi ya Ngangamfumuni siku ulipotokea wizi wa tani 5 za nondo

> Amesema endapo walinzi hao hawatapatikana, viongozi wa kampuni husika wakamatwe ili waseme walipo wafanyakazi wao

Soma - https://jamii.app/WiziNondoUjenzi
MAREKANI YADAI KUILIPUA NDEGE YA IRAN ISIYOKUWA NA RUBANI

- Imedai ndege hiyo ilikaribia kwa Yadi 1,000 manowari yake ya kivita ktk mlango wa bahari wa Hormuz

- Hata hivyo, Iran imedai hakuna ndege yake yoyote isiyo na rubani iliyoshambuliwa

Zaidi, soma https://jamii.app/NdegeIran-Marekani
MAHAKAMA TANZANIA: HUKUMU YA KIFO HAIPO KINYUME NA KATIBA

> Mahakama Kuu imesema hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa hukumu ya kifo ni kinyume na katiba ya nchi baada ya Watetezi wa haki za binadamu kufungua kesi kutaka adhabu hiyo ifutwe kwani inakiuka haki ya msingi ya kuishi

> Hukumu hiyo haijatekelezwa tangu mwaka 1994 na wafungwa 500 wanakabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha maisha

Soma - https://jamii.app/AdhabuKifoKatiba
SERIKALI: KAMPUNI BINAFSI ZA ULINZI ZINAZOAJIRI WAZEE KUFUTWA

- Waziri Lugola amesema Serikali itazifuta kampuni hizo zinazoajiri Askari vikongwe na wasio na mafunzo

- Amesema vikongwe hao wanasinzia na wanaweza kunyang’anywa silaha na majambazi

Zaidi, soma https://jamii.app/KampuniUlinziWazeeKufutwa
BAADA YA KUHOJIWA BASATA, IRENE UWOYA NA STEVE NYERERE WALIHOJIWA POLISI

- Wasanii hao walihojiwa kufuatia kitendo alichokifanya Uwoya cha kuwarushia pesa Wanahabari

- Walihojiwa Julai 17 na kuachiwa kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea

Zaidi, soma https://jamii.app/UwoyaStevePolisi
👍1
WAPELELEZI WATAKIWA KUKAMATA WATUHUMIWA WAKISHAKAMILISHA UPELELEZI

> Jaji Mkuu amesema kesi zinatakiwa kufikishwa Mahakama baada ya upelelezi kukamilika lakini kinachofanyika ni tofauti na hali hiyo kusababisha wafungwa kujaa Magereza

> Tangazo lilitolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini mwaka 2012 linawataka wasikamate watu kabla ya upelelezi kukamilika

Soma - https://jamii.app/MudaUpeleleziMahakama
KENYA: POLISI YAKAMATA FEDHA FEKI ZENYE THAMANI YA USD MILIONI 10

- Fedha hizo sawa na Tsh. 23,006,000,000 pamoja na Watuhumiwa watatu wamekamatwa katika eneo la Fedha, Nairobi

- Wamekutwa pia na kemikali inayoaminika ya kutengenezea fedha hizo

Zaidi, soma https://jamii.app/FakeUSDSeized-Nairobi
WANAFUNZI WALIOKUWA WAHAMISHWE SHULE ZA VIPAJI MAALUMU, KUTOHAMISHWA

- Imesitisha kuwahamisha Wanafunzi 48 wa kidato cha 6 waliopata daraja la 3 kwenye mitihani ya muhula wa pili katika shule za vipaji maalumu kwenda shule za kawaida za bweni

Zaidi, soma https://jamii.app/Kidato6VipajiKotohamishwa
MOSHI: WATANO WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUIBA NONDO TANI 5

> Jeshi la polisi limewakamata watu 5 kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa tani 5 za nondo zilizokua zikitumika kwenye mradi wa ujenzi wa stendi kubwa ya mabasi ya Kimataifa

> Hatua ya kukamatwa kwa Watu hao inafuatia agizo lilitolewa jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Soma - https://jamii.app/WiziNondoUjenzi
UFILIPINO: WANAFUNZI 12 WAFARIKI KWENYE AJALI
-
Wanafunzi 12 wa shule ya msingi, wenye umri kati ya miaka 10 na 12, wamefariki baada ya lori walilokuwa wakisafiria kuanguka kwenye mwamba leo mjini Cebu
-
Taarifa inasema wanafunzi hao walikuwa wakisafiri kwenda kuhudhuria tukio ambalo lilikuwa linafanyika katika mji wa Boljoon, karibu na mahali ambapo ajali hiyo ilitokea
MICHEZO: Timu ya Taifa ya Algeria maarufu ‘LesFennecs’ ndio mabingwa wapya wa #AFCON2019 baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Senegal maarufu ‘Teranga Lions’ goli 1-0 kwenye fainali

- Algeria inachukua ubingwa huo ikiwa mara ya mwisho ilikuwa bingwa wa AFCON miaka 29 iliyopita
MHANDISI WA MAJI WILAYA YA SAME ASIMAMISHWA KAZI

- Waziri Mkuu, Majaliwa amemsimamisha kazi Mhandisi Mussa Msangi kwa kushindwa kusimamia mradi wa maji Hedaru

- Pia, amezivunja Jumuiya 3 za maji za Hedaru na kuagiza viongozi wake wahojiwe

Zaidi, soma https://jamii.app/MhandisiMajiSame
MAHAKAMA YAPENDEKEZA MAKOSA YOTE KUWA NA DHAMANA

- Mahakama ya Tanzania imependekeza makosa yote kuwa na dhamana na masharti ya dhamana hizo kulegezwa kwani itasaidia kuondoa msongamano wa Mahabusu kwenye Magereza mbalimbali nchini

Zaidi, soma https://jamii.app/PendekezoMakosaYoteDhamana
UZINDUZI WA TRENI KUTOKA DAR - TANGA - KILIMANJARO WAFANYIKA LEO

> Uzinduzi wa safari mpya ya treni ya mizigo umefanyika leo baada ya safari za treni hiyo kusimama zaidi ya miaka 12 iliyopita

> Uzinduzi huo umefanywa na Waziri Mkuu ambaye ameipokea treni iliyotokea Tanga ikiwa na mabehewa 20. Mpaka sasa Serikali imeshatumia Tsh. Bilioni 5.7 ili kuirudisha njia hiyo

Soma - https://jamii.app/UzinduziTreniDarKLM