JamiiForums
55.8K subscribers
33.1K photos
1.94K videos
30.2K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kiungo Mshambuliaji wa zamani wa #RealMadrid, Mesut Ozil anaamini kushuka thamani kwa Mchezo wa #ElClasico kumetokana #FCBarcelona kushuka kiwango, ndio maana kwa sasa mechi pendwa za Soka Duniani ni zinazokutanisha Wababe wa #PremierLeague

Kabla ya kustaafu, Ozil alitumikia klabu kadhaa ambazo ni Schalke 04, Werder Bremen, Real Madrid, Arsenal, Fenerbahce na İstanbul Basaksehir

Je, Mdau ni kweli mechi kubwa za EPL zina thamani kubwa kuliko El Clasico?

#Sports #JamiiForums #JFNukuu #JFQuotes
ENGLAND: Klabu zinazoshiriki Premier League zimeombwa kuunga mkono hoja iliyowasilishwa na Klabu ya Wolverhampton Wanderers inayopendekeza azimio la kupiga Kura ya kufuta Matumizi ya 'VAR' kuanzia Msimu ujao

Pendekezo hilo ambalo linadaiwa kupingwa na Bodi ya Ligi Kuu linatarajiwa kusikilizwa Juni 6, 2024 ambapo imeelezwa Bodi inatambua haki ya Wolves kutoa pendekezo hilo, lakini inadhani kufutwa kwa #VAR kunaweza kusababisha maamuzi mengi yasiyo sahihi

Aidha, baadhi ya Maafisa wa EPL wanadai pendekezo hilo litaathiri Ubora wa Ligi, pia kwa mujibu wa takwimu za Msimu huu zinaonesha kiwango cha maamuzi sahihi ya Uwanjani kimeongezeka kutoka 82% hadi 96% kupitia VAR

Soma https://jamii.app/VARAbolition

#JamiiForums #Sports
MICHEZO: Licha ya #CristianoRonaldo (39) kuelekea mwishoni mwa Maisha yake ya kucheza Soka lakini bado katika suala la malipo yupo juu, akiongoza kuliko Wanamichezo wengine wote ndani ya Miezi 12 iliyopita akiwa anaichezea Al-Nassr ya Saudi Arabia aliyojiunga nayo Januari 2023

Ronaldo analipwa Dola Milioni 260 (Tsh. Bilioni 671.3) ambapo kati ya hizo, Dola 200 (Tsh. Bilioni 516.4) zinatokana na mshahara wa Klabu yake, na Dola Milioni 60 (Tsh. Bilioni 154.9) zinazopatikana nje ya mkataba wa klabu

Soma https://jamii.app/HighestPaid

#Sports #JamiiForums #JFDATA #Michezo