JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFRIKA KUSINI: WANAHARAKATI WAPANDA BANGI KARIBU NA OFISI YA RAIS CYRIL RAMAPHOSA

Ni Wanaharakati wa Jamii ya Khoisan ambayo hutumia bangi kwa matibabu

Mwaka 2018 waliweka kambi nje ya Ofisi ya Rais kushinikiza lugha yao kutambuliwa

Soma - https://jamii.app/BangiAfrikaKusini

#JFMatukio
RAIS SAMIA: WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI MSIWE NA MIGONGANO SABABU YA SAFARI

Asema mara nyingine Waziri na Manaibu Waziri hugombania safari na maslahi

Amewataka kujua nafasi zao ili kuepusha migogoro, kwani kila mmoja ameteuliwa kwa vigezo tofauti

Soma - https://jamii.app/WaziriSafari

#JFSiasa #Governance
RAIS SAMIA: KAMA HUMPENDI RAIS ALIYEPO, PENDA NCHI YAKO

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Urais sio mtu ni Taasisi. Kutompenda Rais aliyepo Madarakani isiwe kigezo cha kupuuza mambo yote ya Serikali

Awataka wateule wake kuheshimu viapo vyao

Soma - https://jamii.app/PendaNchi

#JFSiasa #Governance
RAIS SAMIA: SERA NYINGI NI ZA ZAMANI, ZIBORESHWE

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Mawaziri waangalie Sera, Sheria na kuziboresha kama zinaonekana kuwa ni za zamani

Vilevile, wasikilize maoni ya Wataalamu na kuwa wabunifu

Soma - https://jamii.app/SeraSheria

#Governance
RAIS SAMIA: MSIAJIRI MARAFIKI NA NDUGU ZENU KATIKA TAASISI

Amesema Ajira za kujuana badala ya kuangalia vigezo na kuoneana muhali zinaua Taasisi za Serikali

Amewataka mawaziri kukemeana kwa heshima kunapotokea kosa na kutoajiri watu kwa kujuana

Soma - https://jamii.app/AjiraUndugu

#Governance
WHO: 85% YA WAAFRIKA HAWAJAPATA CHANJO YA #COVID19

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuna safari ndefu ya kufikia lengo la kutoa chanjo kwa 70% katika kila Nchi kufikia katikati ya mwaka 2022

Nchi 90 hazijafikia lengo la 40%

Soma - https://jamii.app/Asilimia85Afrika

#UVIKO3 #JFAfya
MDAU: MAHITAJI MUHIMU WANAYOHITAJI WATOTO KUTOKA KWA MZAZI/MLEZI

1. Uwepo wako na Umakini: Hili ni hitaji kubwa kwa Watoto. Kumpatia huduma zote Mtoto hakutoshi kama haupo naye karibu kimwili na kihisia

2. Kupendwa kwa dhati: Watoto wanapenda Wazazi wajifunze kuwapenda kwa namna walivyo. Kuzungumza naye kwa lugha ya Upendo huleta utofauti mkubwa

Soma - https://jamii.app/ChildNeeds
#Malezi
MDAU: WANAFUNZI KUBEBA MZIGO MKUBWA WA MADAFTARI SIO 'FASHION'

Anasema kwa muda mrefu sana Watoto wamekuwa wakibeba mzigo mkubwa wa Madaftari wakati wa kwenda Shuleni na kuonekana aliye na begi kubwa na zito ndiye anasoma kwa bidii

Kwa dhana hii tunasababisha Watoto wapate madhara mengi ya kiafya kwasababu ya kubeba mzigo mzito mgongoni. Anashauri kuweka ratiba rafiki kwa Wanafunzi iliyo na masomo machache au ya kujitosheleza

Mjadala - https://jamii.app/ZigoDaftari

#StoriesOfChange #JFElimu
PROF. MKENDA: ELIMU HAIHITAJI MATAMKO BILA KUSIKILIZA WATAALAMU

Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda asema atatumia Wataalamu wa Elimu ili kutoa maamuzi yenye tija ktk Wizara hiyo

Amesema matamko bila maoni ya Wataalamu huwachanganya Wananchi

Soma https://jamii.app/ElimuMatamko

#JFElimu
RIPOTI HRW: MUSTAKABALI WA MADIKTETA UNAZIDI KUFIFIA

Ripoti inasema Watu wengi wamejitokeza kudai Demokrasia ktk Nchi mbalimbali hata ktk hatari ya kukamatwa/kupigwa risasi

Madikteta sasa wanatumia njama ya kuchezea matokeo ya Uchaguzi

Soma - https://jamii.app/HRWDictators
#Democracy
SIMBA SC BINGWA KOMBE LA MAPINDUZI

- Klabu ya Simba imefanikiwa kunyakua Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 2022 kwa kuifunga Azam FC goli 1-0

- Simba inachukua Ubingwa huo kwa mara ya 4 huku Azam ikibaki kuwa Klabu iliyochukua Ubingwa huo mara nyingi zaidi (mara 5)

#JFSports
NIGERIA YAREJESHA HUDUMA YA TWITTER BAADA YA MIEZI SITA

Marufuku ya kutumia mtandao wa #Twitter iliwekwa tangu Juni 4, 2021

Twitter ilipigwa marufuku kutokana na madai kwamba ilikuwa ikitumika kwa shughuli ambazo zingehujumu Taifa

Soma - https://jamii.app/TwitterBackNGR
#DigitalRights
DR CONGO: MFALME WA KISIWA CHA IJWI AWARUDISHA WANYARWANDA WALIOKIMBIA CHANJO

Mfalme Roger Ntambuka wa Kisiwa hicho kilichopo Kivu Kaskazini ashawishi Wanyarwanda zaidi ya 100 waliokimbia Chanjo kurudi kwao

Watu hao wamerejea kwao Januari 13, 2022

Soma https://jamii.app/WanyarwandaDRC

#UVIKO3
#COVID19: Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limesema Nchi tajiri zinagawia Nchi masikini chanjo zinazokaribia kuisha muda wake wa matumizi

Mataifa masikini yatajwa kuwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa vya uhifadhi wa chanjo

Soma - https://jamii.app/ChanjoUNICEF

#UVIKO3
ARUSHA: Mahakama ya Hakimu Mkazi imemkuta na kesi ya kujibu aliyekuwa DC wa Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi

Washtakiwa wataanza kujitetea Januari 17 wakiwa na mashahidi wasiozidi 10 na vielelezo kadhaa

Soma - https://jamii.app/SabayaKesiUhujumu

#Accountability
IKULU, CHAMWINO: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amepokea Hati za Mabalozi wa Nchi 4

Mabalozi waliowasilisha Hati zao Ikulu Mkoani Dodoma leo Januari 14, 2022 ni wa Saudi Arabia, Jamhuri ya Korea, Indonesia na Morocco

Soma https://jamii.app/Mabalozi

#Governance
DODOMA: JELA MIAKA MIWILI KWA KUJIFANYA AFISA WA TRA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imemhukumu Mkazi wa Dar es Salaam, Kitareti Mahuti kwa kosa la kutumia kitambulisho bandia cha TRA kuwatapeli watu kwa kuwatishia kuwapa makosa mbalimbali

Soma - https://jamii.app/TapeliJela

#JFMatukio
MOROGORO: WATAKAOSHINDWA KUPELEKA WATOTO SHULE KUKAMATWA

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Alhaji Majdi Mwanga ameandaa mikataba kati ya Wazazi kuhusu kudhibiti tabia za baadhi yao kuwa chanzo cha Wanafunzi kukatisha Masomo na kukosa Haki ya kupata Elimu

Soma - https://jamii.app/WazaziWalezi

#JFElimu
AL-SHABAAB YATISHIA KUSHAMBULIA KENYA

Wapiganaji hao wametuma ujumbe wa kuishambulia #Kenya kama kisasi cha uwepo wa Majeshi yake Nchini Somalia

Watu 13 wameuawa tangu kuanza mwaka 2022. Vifo vimehusishwa na wapiganaji wa Al-Shabaab

Soma - https://jamii.app/KenyaAlShabaab
UGANDA KUHARIBU DOZI ZAIDI 400,000 ZILIZOISHA MUDA

Kasi ndogo ya utoaji Chanjo dhidi ya #COVID19 imesababisha Chanjo za Moderna na #AstraZeneca kuisha muda wa matumizi

Dozi 12,220,106 zimetolewa hadi sasa. Uganda imerekodi Vifo 3,378

Soma - https://jamii.app/DoziLakiNne

#UVIKO3 #JFAfya