JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UFUGAJI: SABABU ZA KUKU KUPUNGUZA UTAGAJI WA MAYAI (2)

- Upungufu wa virutubisho muhimu katika chakula cha Kuku wa Mayai husababisha kupungua kwa uzalishaji wa mayai

- Kupukutisha Manyoya: Katika kipindi hiki Kuku hupunguza au kusimamisha utagaji kwasababu hutumia Protini nyingi na nguvu kuotesha manyoya mapya

- Mtiririko wa utagaji wa Mayai kwa Kuku unaweza kuathiriwa na Joto katika mazingira. Kwa kawaida Kuku anahitaji Joto lisiwe chini ya 11°C lisiwe zaidi 28°C

Soma - https://jamii.app/MayaiKukuChini
HOJA: ELIMU YA SASA HAISAIDII KUJIAJIRI WALA HAITOI WAHITIMU WENYE SIFA STAHIKI

- Baadhi ya Wadau wanasema Wahitimu wengi hawana uelewa wa kile walichokisomea kutokana na kukariri, Taasisi zinazozalisha Wahitimu kuwa na hali mbaya, Walimu na Mitaala isiyo bora

- Wengine wanasema Wahitimu wenye hali mbaya wengi wao ni waliosoma kozi ambazo hawakuzipenda au walisoma kwa kufuata mkumbo/ushauri wa Watu fulani

- Je, una mtazamo gani kuhusu hili?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/ElimuKujiajiri
UGANDA: MADAKTARI WATAKA CHANJO YA #COVID19 IWE YA HIARI

- Ni baada ya Viongozi kadhaa wa Wilaya kutaka Watumishi wa Afya wapatiwe Chanjo kilazima

- Umoja wa Madaktari umesema Afya ni suala binafsi na kushauri kampeni za kujenga uelewa zifanyike

Soma https://jamii.app/ChanjoUganda
ZANZIBAR: MCHELE TANI 42.5 WATEKETEZWA, UMEONEKANA HAUFAI KUTUMIWA NA BINADAMU

> Mchele huo uliingizwa toka India, umeteketezwa na Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA)

> ZFDA yasema bidhaa zilizoisha muda hupelekea matatizo ya Saratani

Soma https://jamii.app/McheleZnz
YANGA SC YATAMBULISHA KOCHA MPYA KUTOKA TUNISIA

- Uongozi wa Klabu ya Young Africans umemtambulisha rasmi Kocha Mkuu, Mohamed Nasreddine Nabi pamoja na Kocha Msaidizi, Sghir Hammadi kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu

#JFSports
MDAU ASHAURI NJIA ZA KUTUMIA KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAISHA

> Mdau ameshauri kuacha matumizi yasiyo ya lazima kama kutoa ofa. Pia kutonunua kitu kama haujapanga

> Muhimu kuwa na Bima ya Afya, maisha nk. Pia penda kununua vitu kwa bei ya jumla

Zaidi, soma https://jamii.app/UgumuWaMaisha
CHAD: JESHI LAVUNJA SERIKALI. MTOTO WA DEBY KUONGOZA KIPINDI CHA MPITO

Kufuatia kifo cha Rais Idriss Deby, Jeshi litaongoza kwa miezi 18 na Baraza litaongozwa na Mahamat Idriss Deby

> Chad itaomboleza kwa siku 14. Mipaka ya anga na ardhi yafungwa

Soma https://jamii.app/ChadRaisMpito
ZUNGU ATAKA KUWEPO KWA KODI KWENYE MITANDAO YA SIMU

- Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu, amependekeza kuwepo kwa kodi ya Uzalendo itakayokatwa kila siku kupitia Mitandao ya Simu kwa kila Mtanzania ili kuwa chanzo kipya cha mapato kwa Serikali

Soma - https://jamii.app/ZunguKodiMitandao
NAMNA YA KUTAMBUA MWENZA WAKO ANA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)

- Anakuwa Mtu wa kukasirika sana na kukerwa na kila kitu unachofanya. Pia, anaweza kuwa na huzuni wakati mwingi na hii hupelekea Mawasiliano yenu kuanza kudhoofika

- Hutumia muda mwingi kukamilisha kazi ndogo na huwa mzito katika kufanya maamuzi

Soma - https://jamii.app/MawazoHuzuni
#StressAwarenessMonth
HALI YAKO YA MAISHA INAENDANA NA METHALI GANI?

> Wahenga walikuwa na misemo na methali walizotumia kupeana moyo, maonyo au mafunzo

> Kila mtu ana stori ambayo ni tofauti na mwingine. Je maisha yako yanaendana na methali ipi?

Soma https://jamii.app/MaishaMethali
WASANII KUWEKA MAUDHUI YOUTUBE BILA KULIPA ADA YA LESENI TCRA

> Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbas amesema wanatengeneza Kanuni ili wanaorusha maudhui ambayo si Habari wasilipe Leseni

> Amesema kuna tofauti kati ya Habari na Sanaa

Soma https://jamii.app/YouTubeBure
MAREKANI: DEREK CHAUVIN AKUTWA NA HATIA YA KUMUUA GEORGE FLOYD

> Aliyekuwa Afisa wa Polisi Minneapolis ametiwa hatiani kwa kupiga goti shingoni mwa George Floyd na kumsababishia kifo

> Kitendo hicho kimetajwa kuwa kinyume na Mafunzo ya Kipolisi

Soma https://jamii.app/ChauvinVsFloyd
AKAUNTI ZA BENKI ZA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU ZAFUNGULIWA

- Akaunti za Benki za Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) zilifungwa kwa takriban miezi 8 tangu Agosti 2020 kutokana na Uchunguzi wa tuhuma mbalimbali

Soma - https://jamii.app/OpenAccTHRDC
ATHARI ZA MSONGO WA MAWAZO (STRESS) MWILINI

- Huvuruga mzunguko wa usingizi ambapo huweza kuathiri vibaya na kusababisha kukosekana kabisa kwa usingizi

- Huvuruga mfumo wa Chakula Mwilini, Tumbo kujaa gesi, maumivu ya Tumbo, kushindwa kumeng'enya Chakula, kutapika na kichefuchefu

- Athari kwenye tishu za Ubongo ikiwemo kushindwa kutumia mbinu za utambuzi katika kudhibiti wasiwasi na hofu

Soma - https://jamii.app/MawazoHuzuni
SUDAN KUSINI: MAMLAKA YATEKETEZA CHANJO 60,000 ZA ASTRAZENECA

> Sudan Kusini imesema Chanjo ziliwasili zikiwa zimebakiza muda mdogo kabla ya kuisha matumizi

> CDC-Afrika imesema walikuwa na muda wa kutosha kutumia Chanjo kabla hazijapitwa wakati

Soma https://jamii.app/SudanKusiniAstraZeneca
UAE YAFIKIRIA KUZUIA SAFARI KWA AMBAO HAWAJAPATA CHANJO YA #COVID19

- Umoja wa Falme za Kiarabu umeshatoa Dozi Milioni 9.8 huku ikiwa na idadi ya Watu Milioni 10

- Watu wengi wenye umri kuanzia miaka 16 na zaidi wanapewa Chanjo bure

Soma - https://jamii.app/UnvaccinedUAE
TANZANIA YAPOROMOKA KTK KUIMARISHA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

- Ripoti ya 2020 ya Reporters Without Borders (RSF) imeitaja #Tanzania kushika nafasi ya 124 kati ya Nchi 180 Duniani

- Mwaka 2019 ilishika nafasi ya 118 huku 2018 ikiwa 93

Soma https://jamii.app/PressFreedom2021
#PressFreedom