JamiiForums
55.6K subscribers
33.3K photos
1.97K videos
30.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
JEFF BEZOS KUJIUZULU NAFASI YA 'CEO' WA AMAZON

- Bezos (57) ambaye ni Mwanzilishi wa Amazon amesema hatua hiyo itampa muda kuelekeza jitihada ktk biashara nyingine

- Andy Jassy atakaimu nafasi ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo

Soma > https://jamii.app/BezosAmazon
WAKILI NASIMIRE: KATIBA HAIRUHUSU MTU KUPIGWA VIBOKO HADHARANI

> Amewashauri walioathirika kwa vitendo hivyo kwenda Mahakamani kwani vitendo hivyo ni kinyume na Sheria na Katiba

> Amesema Mahakama ndio yenye Mamlaka ya kutoa adhabu hiyo

Soma https://jamii.app/VibokoSheria
WANANCHI WAOMBWA SUBIRA WAKATI SUALA LA VIFURUSHI LIKISHUGHULIKIWA

- Waziri Ndugulile awataka Wananchi kuwa na subira mpaka mwisho wa Mwezi huu

- Pia, amesema Serikali imeanza kushughulikia watoa Lugha za matusi, kashfa na utapeli mitandaoni

Soma https://jamii.app/SerikaliVifurushi
DKT. OTIENO: JIFUKIZENI WALAU MARA MBILI KWA SIKU

> Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Dawa Asili Muhimbili, Dkt. Joseph Otieno amesema nyungu husaidia kama virusi havijaingia ktk damu

> Vikiingia unapaswa kutumia maji ya moto na tangawizi

Soma https://jamii.app/NyunguMara2
MBUNGE AHOJI ONGEZEKO LA WAGONJWA WA AFYA YA AKILI NCHINI

- Mariam Kisangi amehoji utaratibu wa Serikali kuwasaidia

- Naibu Waziri wa Afya amesema Serikali imehakikisha huduma za matibabu zinatolewa kuanzia ngazi ya Hospitali za Rufaa za Mikoa

Soma > https://jamii.app/AfyaYaAkili
MBUNGE APEWA SIKU 7 KUTOA USHAHIDI WA WIZI WA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU 2020

> Naibu Spika, Tulia Ackson amemtaka Felister Njau mmoja kati ya 19 waliofukuzwa CHADEMA kutoa ushahidi kuhusu kukamatwa kwa mabegi 5 ya kura wakati wa Uchaguzi Mkuu 2020

Soma - https://jamii.app/UshahidWiziKura
ZIFAHAMU HAKI TANO ZA MSINGI ZA MTOTO WAKO

- Haki ya Kuishi: Hii inaanza pale mama anapopata ujauzito

- Haki ya Kulindwa: Inahusu kuzuia vitendo viovu wanavyofanyiwa watoto katika hatua za ukuaji wao, kabla na baada ya kuzaliwa

- Haki ya Kushiriki: Ushiriki wa #Mtoto unapatikana pale mtoto anapopewa nafasi kikamilifu katika kutoa mawazo, kushiriki katika maamuzi ya masuala yanayohusu maendeleo yake.

- #Haki ya Kutobaguliwa: Ubaguzi wa Mtoto umegawanyika ktk makundi mbalimbali

Soma > https://jamii.app/Haki5Mtoto
#JamiiForums
LINDI: MTENDAJI AMZABA RAIA MAKOFI KWA KUVUTA SIGARA KITUO CHA AFYA

> Mtendaji wa Kijiji cha Mbwemkuru, Azidu Mwenda amekiri kumpiga Athumani Ndumba kwa kuvuta Sigara katika kituo cha Kitomanga

> Ndumba alienda kituoni hapo kumuona Mkewe

Soma - https://jamii.app/MtendajiMakofi
MANYARA: MWALIMU MKUU AFUKUZWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UDANGANYIFU

- Oscar Waluye anatuhumiwa kufanya udanganyifu ktk Mitihani ya Darasa la 7 iliyofanyika 2020

- Aliwalazimisha Wanafunzi 2 wa Darasa la 6 kufanya Mitihani badala ya Watahiniwa

Soma > https://jamii.app/MwlMahakama
NDUGAI: WALIMU WAONGEZEWE MASOMO YA KUFUNDISHA

> Spika Ndugai ameitaka Wizara ya Elimu kuangalia namna ya kufanya Walimu wafundishe masomo kuanzia 3

> Asema Walimu wa Sekondari kufundisha somo 1 au 2 husababisha uhaba wa Walimu kwa baadhi ya Masomo

Soma https://jamii.app/MasomoWalimu
SERIKALI YATAKA HAKI KUTENDEKA KWA WANAOFANYIWA UKATILI

- Maafisa Jamii ktk Halmashauri zote watakiwa kushughulikia Ukatili dhidi ya Wanawake, Wanaume, Wazee na Watoto

- Haki za wanaofanyiwa vitendo vya ukatili zimetakiwa kupatikana kwa wakati

Soma > https://jamii.app/HakiUkatili
RUVUMA: RC AKATAA KUKABIDHI MADAWATI YASIYO NA UBORA

> Madawati 50 na meza 10 zilizotakiwa kukabidhiwa ktk Shule ya Msingi Mtakanini yameshindwa kukabidhiwa kutokana na ubovu kabla ya kutumika

> RC Christina Mndeme ameagiza vifaa hivyo virekebishwe

Soma https://jamii.app/RCRuvuma
ARUSHA: KATIBU TAWALA MKOA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI

> Richard Kwitega amefariki dunia leo Februari 3, 2021 baada ya gari lake kugongana uso kwa uso na Basi la Makara maeneo ya Mdori mkoani Manyara

> Kwitega alikuwa anaelekea mkoani Dodoma kikazi

Soma https://jamii.app/KwitegaAfariki
SERIKALI YATAKIWA KUPAMBANA NA RUSHWA NGAZI ZA HALMASHAURI NA WILAYA

- Akiwa Bungeni, Mbunge Kasali Mageni wa Sumve amedai bado kuna changamoto kubwa

- Asema Halmashauri na Wilaya zinapelekewa Fedha nyingi lakini hazitumiki inavyokusudiwa

Soma > https://jamii.app/RushwaHshauri
MBUNGE WA MAKAMBAKO APENDEKEZA RAIS MAGUFULI AONGEZEWE MUDA

> Mbunge Deo Sanga amesema Rais Magufuli amefanya kazi kubwa katika nafasi yake ya Urais

> Ameomba aongezewe muda hata kama asipotaka ili aweze kukamilisha mipango anayoifanya

Soma - https://jamii.app/RaisAongezeweMuda
DAR: WANNE WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA UHUJUMU UCHUMI

- Ktk Shtaka la Kwanza, Wakili wa Serikali amedai Washtakiwa walikutwa na meno 9 ya Simba Januari 13, 2021 eneo la Magomeni Mwembechai

- Pia walikutwa na vipande 32 vya meno ya tembo

Soma > https://jamii.app/4UhujumuUchumi
SERIKALI YAZIONYA HOSPITALI ZINAZOTOZA BEI KUBWA KWA WENYE MATATIZO YA KUPUMUA

> Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Mabula Mchembe amezitaka Hospitali Binafsi zisitumie #COVID19 kupandisha bei kwa kuwa sio kila Tatizo la Kupumua ni #CoronaVirus

Soma https://jamii.app/BeiMagonjwaKupumua

#JFAfya
WANAHABARI WANAWAKE WATAJWA KUPATA CHANGAMOTO YA RUSHWA YA NGONO

> TAKUKURU imesema Wanahabari Wanawake wana changamoto ya Rushwa ya Ngono ambayo ni kinyume na kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007

Soma https://jamii.app/RushwaYaNgono
EWURA YATANGAZA KUPANDA KWA BEI ZA MAFUTA

> EWURA imetangaza kuwa na ongezeko la Tsh. 53 kwa lita kwa mafuta ya Petroli, ongezeko la Tsh. 134 kwa lita ya Dizeli na ongezeko la Tsh. 119 kwa lita ya Mafuta ya Taa kwa watumiaji wa rejareja

Soma https://jamii.app/BeiMafutaFebruari
SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZAPIGWA MARUFUKU MAENEO YA HIFADHI

- Naibu Waziri wa Utalii asema maeneo ya Hifadhi yanatunzwa ili kuwa kivutio na kwa ajili ya kuleta mapato

- Ameeleza kuwa, Serikali imetenga maeneo kwa ajili ya matumizi ya kibinadamu

Soma > https://jamii.app/MarufukuHifadhi