JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WAZIRI WA KILIMO AKANUSHA UWEPO WA NZIGE TANZANIA

> Amesema hakuna taarifa za kitaalamu kuthibitisha uwepo wa wadudu hao, japokuwa ni kweli wameonekana takriban Kilomita 50 kutoka Mpaka wa Tanzania na Kenya

Soma - https://jamii.app/NzigeTZ
KENYA: MWAJIRIWA ACHARAZWA VIBOKO KWA KUCHELEWA KAZINI

> Raia 4 wa China wamekamatwa na Polisi baada ya video kusambaa katika mitandao ya kijamii ikiwaonesha wakimchapa viboko Mfanyakazi (Mkenya) katika mgahawa jijjni Nairobi kwa madai ya kufika kazini akiwa amechelewa

Soma - https://jamii.app/WhipsReportingLateWork
MWENDELEZO: Watu 4 wagundulika kuambukizwa #coronavirus nchini Uingereza na kufanya idadi ya waathirika wa ugonjwa huo kufikia 8

> Inaelezwa maambukizi ya #coronavirus kwa siku yameongeza na mpaka sasa watu zaidi ya 900 wameshafariki huku vifo vingi vikitokea China

#JFLeo
TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA KUUNGA MKONO UHURU WA KUJIELEZA KWA WASANII

> Mwaka 2020 Tamasha linaunga mkono juhudi za kukuza Muziki unaopigwa mubashara na kukemea unyanyasaji wa kijinsia kwa kaulimbiu ya 'Paza sauti yako, sema hapana kwa unyanyasaji wa kijinsia’

> Tamasha linatarajiwa kuanza Februari 13 hadi 16, 2020

#JFSanaa
ZINGATIA HAYA KWENYE TOVUTI YAKO KUKUZA BIASHARA YAKO

Tumia Search Engine Optimization (SEO) ili tovuti yako kuonekana katika orodha ya mwanzo inapotafutwa

> Shiriki katika Mitandao ya Kijamii. Chapisha viunganishi 'links' za tovuti, blog na miradi ili watu waweze kutambua kitu unafanya

> Weka taarifa mara kwa mara (Updates). Hii hufanya mtembeleaji kuona kuwa tovuti inafanya kazi

Soma https://jamii.app/TovutiBiashara
BAADHI YA VISABABISHI VYA MAMA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI

> Mama akishajifungua kwa upasuaji katika mimba zilizopita anakuwa katika uwezekano mkubwa wa kujifungua kwa upasuaji pindi apatapo mimba nyingine

> Kuwa na vizuizi ndani ya kizazi au katika njia ya uzazi kama vile Uvimbe. Hitilafu katika nyonga ambazo hupelekea mtoto kushindwa kupita. Ulalo mbaya wa mtoto na mtoto kuchoka

Soma zaidi https://jamii.app/UpasuajiMama
KILIMANJARO: RC ATHIBITISHA KUONEKANA KWA NZIGE NA KISHA KUTOWEKA

> Anna Mghwira amesema kundi la Nzige lilionekana jana Wilaya ya Moshi na kisha kutokomea kusikojulikana, na hadi sasa hawajathibitisha mahali walipo

> Wataalamu wako maeneo mbalimbali ili kufanya ukaguzi na kujiridhisha kama kuna eneo ambalo Nzige wameingia

Soma - https://jamii.app/UwepoNzigeTZ
JIFUNZE KUHUSU ‘U.T.I’ SUGU

> Dalili ni pamoja kuhisi mkojo kuchoma au maumivu wakati wa kukojoa, maumivu chini ya mbavu, maumivu chini ya kitovu au kwenye kibofu cha mkojo

> Madhara ni kusababisha ugonjwa wa figo, kuharibika kwa figo hasa kwa watoto wadogo na kuongezeka hatari ya kuzaa watoto njiti kwa wajawazito

> Kujikinga. Jisafishe kwa kupeleka uchafu nyuma baada ya haja kubwa. Kunywa maji mengi, vaa chupi ya pamba, epuka nguo za ndani zinazobana sana, epuka kujisafisha kwa sabuni zenye kemikali. Ikiwa haujatahiriwa osha vizuri uume wako mara kwa mara

Soma https://jamii.app/UTISugu
KINANA, MAKAMBA WAFIKA MBELE YA KAMATI YA MAADILI YA CCM

> Makatibu Wakuu wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yusuf Makamba na Abdulrahaman Kinana leo wamefika mbele ya Kamati ndogo ya Usalama na Maadili katika ofisi ndogo za CCM Lumumba Jijini, Dar

Zaidi, soma https://jamii.app/KinanaMakambaKamatiCCM
JACKIE CHAN KUTOA FEDHA KWA WATAKAOGUNDUA KINGA YA #CORONA

> Nyota wa filamu nchini China, Jackie Chan ametangaza kuwa atatoa zawadi ya Yuan milioni 1 (Zaidi ya Tsh. milioni 300) kwa mtu au kikundi cha watu watakaogundua kinga dhidi ya #coronavirus

> Asema yupo tayari kufanya chochote kuona #coronavirus vikipatiwa tiba au chanzo na kutokomezwa kabisa

#JFLeo
MAREKANI: WANAJESHI WALIOATHIRIKA UBONGO KUTOKANA NA SHAMBULIO LA IRAN WAFIKIA 109

> Idadi iliongezeka kutoka Wanajeshi 64 walioripotiwa hapo awali

> Rais Donald Trump awali alisema hakuna raia wa Marekani waliojeruhiwa katika shambulio hilo

Soma https://jamii.app/WanajeshiMarekani
JAJI WARIOBA: KATIBA NI SHERIA, WAKATI WOWOTE INAWEZA KUFANYIWA MABADILIKO. AKANUSHA MADAI YA KUPIGWA

> Amesema Katiba ndiyo moyo wa Taifa na kwamba haiwezi kuzuiliwa kwasababu ya gharama kwa kuwa hata maoni ya Wananchi yalipokusanywa kwenye Rasimu walitumia gharama kuzunguka nchi nzima

> Katiba ya sasa ina afya lakini mpya itaboresha yale yaliyopo

Soma - https://jamii.app/WariobaKatibaMoyoTaifa
MAREKANI: WANAJESHI WANNE WA CHINA WASHTAKIWA KWA UDUKUZI WA TAARIFA

> Wanajeshi hao ni Wajumbe wa Jeshi la Ukombozi la Wachina (PLA)

> Udukuzi huo uliofanywa katika Kampuni ya Equifax unadaiwa kuwa mkubwa zaidi kuwahi kutokea

Soma - https://jamii.app/ChineseHackers-US
NZIGE WAKIWA NDANI YA ENEO LA 1KM² WANAKULA CHAKULA CHA KUWATOSHA WATU 35,000 KWA SIKU

> Nzige nchini Kenya wapo katika eneo la takriban km 2,400 za mraba wanaweza kula chakula kinachowatosha watu milioni 84 kwa siku

> Uvamizi wa Nzige unaweza kusambaratisha mazao na malisho haraka sana

Soma https://jamii.app/NzigeUwezo
TSH BILIONI 12 ZAPATIKANA KWA MAKOSA YA UHUJUMU UCHUMI

> Zilipatikana baada ya watuhumiwa kuomba radhi na kurejesha kiasi hicho

> Pia zaidi ya Sh bilioni 19 zimepatikana baada ya kutaifisha mali mbalimbali za wafanyabiashara wasio waaminifu

Soma https://jamii.app/BillionUhujumu
UJERUMANI: SAFARI ZA NDEGE ZAFUTWA KUTOKANA NA KIMBUNGA

> Kimbunga Sabine chasababisha safari takriban 500 kufutwa Ujerumani

> Kimbunga hicho ambacho pia kinajulikana kama Kimbunga Ciara kimesababisha vifo vya watu 7 hadi sasa

Soma - https://jamii.app/KimbungaSabine-Germany
CHINA: WANAFUNZI WA TANZANIA WAOMBA WARUDISHWE NCHINI

> Wasema tatizo sio kukosa nauli ila wamezuiwa kutoka ili kudhibiti #CoronaVirus. Wanafunzi hao wamesema hawajaambukizwa

> Kuna utaratibu ambao Serikali inaweza kufuata ili kuwatoa Raia wake

Soma https://jamii.app/WatanzaniaChina
MARAIS WASTAAFU, MKAPA NA KIKWETE KUSHIRIKI MAZISHI YA DANIEL ARAP MOI

> Marais Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete ni miongoni mwa viongozi wakubwa watakaoshiriki mazishi ya Kitaifa ya Rais wa zamani wa Kenya, Daniel Arap Moi

> Pamoja nao ni Rais Uhuru Kenyatta, Paul Kagame viongozi wengine kutoka Mataifa mbalimbali ambapo Moi atazikwa rasmi nyumbani kwake Kabarak, kesho

Soma - https://jamii.app/KikweteMkapaMazishiMoi
#JFLeo