JamiiForums
✔
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: TRUMP AWAFUKUZA MAOFISA 2 WALIOTOA USHAHIDI DHIDI YAKE

> Rais Donald Trump aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka amewatimua kazi Mkurugenzi wa masuala ya Ulaya kwenye Baraza la Usalama la Taifa, Alexander Vindman na Balozi wa Marekani kwenye Jumuiya ya Ulaya, Gordon Sondland

Soma - https://jamii.app/TrumpFiresEUAmbassadr
DAR: POLISI WAZUIA MKUTANO WA JOHN MNYIKA

> Jeshi la Polisi limezuia Mkutano wa Mbunge John Mnyika kutokana na ujenzi wa barabara unaoendelea katika eneo ambalo mkutano huo ulitarajiwa kufanyika

Soma - https://jamii.app/MnyikaPolisi-DAR
UNDP: MAENDELEO YA WATANZANIA YAMERUDI NYUMA KWA ASILIMIA 24.9

> Maendeleo ya binadamu nchini kwa mwaka 2018 yalirudi nyuma kutokana na ukuaji wa uchumi kutokuwa jumuishi katika sekta zinazohusisha maisha ya Watanzania wengi

> Uchambuzi umezingatia hali ya kutokuwepo kwa usawa katika mazingira ya kuzaliwa mtoto, kipato, elimu na tofauti kwa wenye mali na wasiokuwa nazo

Soma - https://jamii.app/KushukaMaendeleoWatz2018
THAILAND: MWANAJESHI AWAUA WATU 20

- Jakraphanath Thomma amewaua Watu hao kwa kuwafyatulia risasi kiholela

- Awali, kupitia Facebook aliweka picha ya bastola na risasi akiandika “ni wakati wa kujifurahisha na hakuna mtu anayeweza kuzuia kifo''

Zaidi, soma https://jamii.app/MwanajeshiAuaRaia-THLD
ETHIOPIA: HALI YA HEWA YATAJWA KUWA SABABU YA UVAMIZI WA NZIGE

> Katibu Mkuu wa UN amesema kuna uhusiano kati ya mabadiliko ya hali ya hewa na uvamizi wa nzige Ethiopia

> Kuna wasiwasi kuwa janga hilo linaweza kusababisha baa la njaa

Zaidi, soma - https://jamii.app/NzigeEthiopia
WANYAMA WENGINE WAHAMISHIWA BURIGI-CHATO

- Simba 20 wakiwemo Simba wakubwa 17 wamewasili kwenye Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti

- Simba hao wamesafirishwa kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na miongoni mwao kuna Simba Dume linaoitwa Burigi na Jike linaloitwa Chato
PWANI: WIVU WA MAPENZI: NYUMBA YACHOMWA MOTO NA KUUA FAMILIA YA WATU 6

> Richard Mathias Mkazi wa Buza, Dar na Masasi, Mtwara anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa kuiteketeza kwa moto nyumba ya Regina Mavondo (31) (mpenziwe)

> Waliofariki ni Regina Mavondo, Agnes Taimu (26), Regina Elias (19), Frida Francis (22), Nuru Seleman (4) na Maimuna (3)

Soma - https://jamii.app/WivuVifoFamiliaMoto
KILIMANJARO: NZIGE HUENDA WAKAINGIA TANZANIA

- Afisa Kilimo wa Wilaya ya Mwanga amesema wamepokea taarifa kuwa Nzige wapo Km 50 kufika ulipo mpaka wa Kenya na Tanzania

- Amewataka Wananchi kutoa taarifa mapema waonapo makundi ya Wadudu aina ya Panzi

Zaidi, soma https://jamii.app/TahadhariNzigeTZ
EL SALVADOR: WANAJESHI WAVAMIA BUNGE WAKITAKA MUSWADA WAO UPITISHWE

> Wanajeshi na Maafisa wa Polisi wenye silaha walivamia Bunge, wakitaka kuidhinishwa kwa mkopo wa dola milioni 109 ili kuwanunulia vifaa vya kukabiliana na uhalifu

> Taifa hilo lina viwango vya juu vya mauaji Duniani na Ghasia nyingi hutekelezwa na magenge ya uhalifu

Soma - https://jamii.app/SoldiersOccupiesCongress
MVUA ZASABABISHA ONGEZEKO LA MAJI ZIWA VICTORIA, WANANCHI WAPEWA TAHADHARI

> Usawa wa maji umefikia 1134.22mamls kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa

> Tahadhari imetolewa kwa wavuvi na watumiaji wa vyombo vya usafiri katika Ziwa hilo

Soma - https://jamii.app/TahadhariZiwaVictoria
MWENDELEZO: Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na #CoronaVirus imefikia 910 na kwa mara ya kwanza raia wa Marekani na Japan, wamepoteza maisha wakiwa ugenini (China)
-
Tume ya Afya ya China imetangaza kuongezeka kwa vifo hivyo Jumapili, idadi ambayo imepita ile ya maambukizi ya #SARS ya mwaka 2002-2003 ambapo watu 774 walifariki
-
Watu wengine 40,710 wameambukizwa #CoronaVirus Duniani, huku China pekee ikiwa na waathirika 40,171
WAAMUZI KUBORONGA KWENYE LIGI: WADAI HAWAJALIPWA MISHAHARA KWA MWAKA 1
-
Mmoja wa waamuzi wanaochezesha mechi za Ligi Kuu Bara msimu huu amefungukia sakata la baadhi ya waamuzi kuonekana wakiboronga kwenye mechi za hivi karibuni na kusema sababu kubwa ni kwamba wana msongo wa mawazo kutokana na kutolipwa mishahara
-
Inadaiwa mara ya mwisho Waamuzi kulipwa mishahara ilikuwa ni Januari 2019 na hadi leo hawajalipwa tena
TANZANIA YAOMBA AMANI AFRIKA ILI KUPUNGUZA TATIZO LA WAKIMBIZI

> Makamu wa Rais aomba Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kutatua migogoro ili kuipunguzia Tanzania changamoto ya wakimbizi

> Amesema machafuko yanachelewesha maendeleo

Soma - https://jamii.app/WakimbiziTanzania
FAHAMU KUHUSU HATIMILIKI YA SHAMBA/KIWANJA

> Ni nyaraka ya Kisheria inayoonesha mmiliki wa kipande cha ardhi, ramani na ukubwa wa eneo husika

> Zinatolewa na Wizara ya Ardhi kupitia Halmashauri/Manispaa husika baada ya eneo kupimwa

Soma https://jamii.app/HatiMiliki
AU: MPANGO WA AMANI KUTOKA KWA RAIS TRUMP HAUFUATI SHERIA

> Umoja wa Afrika umelaani pendekezo hilo na kusema haufuati Sheria, uliandaliwa bila kushauriana na Jumuiya ya Kimataifa na kwamba unazikandamiza Haki za Wapalestina

Soma - https://jamii.app/AUAgainstTrumpPeaceTreaty
AFRIKA: WATU MILIONI 239 WAKABILIWA NA NJAA

> Kamishna wa Kilimo wa Umoja wa Afrika Josefa Sacko amesema kuna haja ya kuwa na mbinu mpya za kukabiliana na changamoto za njaa na umasikini

> Pia kupunguza migogoro inayoendelea ili watu wajikite kwenye uzalishaji na kutatua tatizo la chakula

Soma https://jamii.app/NjaaAfrikaFAO
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifutia usajili vyuo 10 kikiwamo Times School of Journalism (TSJ), kwa kutokidhi vigezo vya kutoa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza hilo

> Limevitaka vyuo hivyo kuwahamisha wanafunzi wote kwenda vyuo vingine vilivyosajiliwa

> Vyuo vilivyofutwa ni ERA Training College - Bukoba (REG/TLF/095), Azania College of Management - Dar (REG/BMG/021), Time School of Journalism - Dar (REG/PWF/013), Clever College - Dar (REG/BTP/205P) na Aces College of Economic Science - Zanzibar (REG/BPT/081P)
SUMAYE AREJEA RASMI CCM

> Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye leo Februari 10, 2020 ametangaza kurudi Chama cha Mapinduzi (CCM)

> Disemba 4, 2019 alitangaza kuachana na CHADEMA huku akidai alikosea kudhani kuna demokrasia ndani ya chama hicho

Soma https://jamii.app/SumayeCCM