JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UTEUZI: Rais Magufuli amemteua Balozi Wilbert Augustine Ibuge kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje

> Kabla ya uteuzi huo Balozi Ibuge alikuwa Mkuu wa Itifaki(Chief of Protocol) katika Wizara hiyo na amechukua nafasi ya Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe aliyehamishwa Wizara

#JFLeo
RAIS MUSEVENI AZUIA WAGANDA WALIOKO CHINA KURUDI KWASABABU YA #CORONA

> Rais wa Uganda amesema raia wa Uganda walioko China hawatasafirishwa kurudi nchini humo kutokana na kuwa Serikali ya China tayari imeshachukua jitihada mbalimbali katika kupambana na #coronavirus na hivyo Waganda hao wako salama

Soma - https://jamii.app/UgandansEvacuationCorona
SERENGETI: AKUTWA AMEFARIKI AKIWA NA SIMU ILIYOCHOMEKWA KWENYE CHAJI

> Vumilia Kitang'enyi amekutwa ameanguka akiwa na simu mkononi

> Chanzo cha kifo chake kinadaiwa kuwa ni hitilafu katika mfumo wa umeme

Soma - https://jamii.app/UmemeKifoSerengeti
SERIKALI: HAKUNA MBUNGE ALIYEZUIWA KUFANYA MIKUTANO KWENYE ENEO LAKE

> Waziri Mkuu amesema Vyama vya siasa havijazuiliwa kufanya shughuli zake ila umewekwa utaratibu muhimu kwa viongozi waliopata ridhaa kwenye maeneo yao na ratiba za uchaguzi zitatolewa na kueleza lini shughuli za kampeni zitaanza

Soma - https://jamii.app/KanushoUbabeSerikali
ISTANBUL: WATATU WAFARIKI BAADA YA NDEGE KUTELEZA NA KUACHA NJIA

> Ndege ya Shirika la Pegasus imeteleza na kuharibika vibaya wakati ikitua. Majeruhi 179 wamefikishwa Hospitali

> Hali ya hewa inadaiwa kuwa chanzo cha ajali

Soma - https://jamii.app/PlaneSkiddingIstanbul
SIKU YA SHERIA TANZANIA: KINACHOWAVUTIA WAWEKEZAJI SIO KODI BALI MFUMO WA HAKI

> Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amesema tafiti zinaonesha kinachowavutia wawekezaji sio kodi wala misamaha ya kodi bali utengamano uliojikita katika misingi ya Sheria na kuheshimika kwa mfumo mzima wa Haki

> Maadhimisho haya yana kauli mbiu ‘Uwekezaji na biashara wajibu wa Mahakama, wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji’

Soma - https://jamii.app/UwekezajiMfumoHaki
WASANII: Taasisi ya National Association for the Advancement of Colored People (NAACP) inatarajiwa kumpa tuzo ya heshima (President’s Award), mwimbaji na mwanamitindo, Rihanna Fenty kwenye hafla ya utolewaji wa tuzo za 2020, California, Marekani, Februari 23
-
Katika tuzo hizo ambazo zitatolewa kwa msimu wa 51, huwapa heshima hiyo Wasanii au watu maarufu wenye mchango mkubwa kwa jamii au walioanzisha mambo yenye manufaa kwa Jamii
-
Mwaka jana tuzo hiyo ya heshima alipewa rapa, Jay Z
JamiiForums
SERIKALI: HAKUNA MBUNGE ALIYEZUIWA KUFANYA MIKUTANO KWENYE ENEO LAKE > Waziri Mkuu amesema Vyama vya siasa havijazuiliwa kufanya shughuli zake ila umewekwa utaratibu muhimu kwa viongozi waliopata ridhaa kwenye maeneo yao na ratiba za uchaguzi zitatolewa na…
MWENDELEZO: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amesema majibu yanayotolewa na Serikali juu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwamba iko huru kwa mujibu wa Katiba na Sheria, ni majibu mepesi na itakuja kuleta majuto kwa Taifa
-
Ameishauri Serikali kuanzisha mchakato wa upatikanaji wa Tume Huru ya Uchaguzi, pamoja na kuviacha huru vyama vya siasa vya upinzani kufanya shughuli zake za uenezi wa chama
WANAOFANYA DIET HATARINI KUDHOOFIKA KIAKILI NA KUUMWA

> Mtaalamu wa Lishe amesema wengi hawana Elimu sahihi na wameacha vyakula muhimu ambavyo vinahitajika mwilini

> Ametoa wito kwa wanaotaka kupungua kupata ushauri kutoka kwa Wataalamu

Soma - https://jamii.app/DietAfya
UMOJA WA ULAYA (EU) WAKUBALI KUTOA BILIONI 132 ZILIZOKUWA ZIMEZUIWA

> EU imeruhusu kutoa msaada huo ambao ulizuiwa kufuatia mgogoro wa Kidiplomasia

> Rais Magufuli amshukuru Balozi wa EU na kuahidi Tanzania itaendelea kuwapa ushirikiano

Soma - https://jamii.app/TZMsaadaEU
MAAMBUKIZI MAPYA YA MALARIA YAPUNGUA KWA ASILIMIA 27

> Maambukizi mapya yamepungua ikilinganishwa na wagonjwa 164 kati ya watu 1000 mwaka 2015 hadi wagonjwa 119 kati ya watu 1000 mwaka 2018

> Vifo vimepungua kwa asilimia 63 kutoka vifo 6,737 mwaka 2015 hadi 2,540 mwaka 2018

Soma - https://jamii.app/KupunguaMaambukiziMalaria
MEMBE: MAHOJIANO NA KAMATI YA MAADILI CCM YAMENIACHA NA FURAHA

> Bernard Membe amesema amefurahi, kwakuwa amepata nafasi ya kutoa mawazo na kujieleza. Adai wamefanya mijadala mikubwa ya kitaifa kuhusu CCM na Tanzania kwa ujumla

Soma - https://jamii.app/MembeMahojianoCCM
HOJA: TATIZO SI KUKOSA SHERIA BALI NI UDHAIFU NA KUKOSA UWAJIBIKAJI WA KUZISIMAMIA

> Mdau ndani ya JamiiForums.com anasema Si kweli kuwa Sheria nyingi ni dhaifu, butu au hakuna "makali" ya Kisheria au hata Kikatiba. Tatizo ni usimamizi mzuri wa Kanuni, Sheria na Katiba kwa ufanisi, kuzingatia haki, kufuata taratibu na zaidi kutimiza wajibu ipasavyo (Kuwajibika)

> Je, inakuwaje tunakuwa na watendaji ambao wanashindwa kusimamia kwa dhati Kanuni na Sheria na badala yake kutoa matamko au kufanya mambo ambayo hupelekea wananchi tunajiuliza kulikoni?

Kwa mjadala zaidi, soma - https://jamii.app/UtekelezajiSheriaKatiba
WABUNGE WAITAKA SERIKALI KUTONG'ANG'ANIA MAITI NDUGU WANAPOSHINDWA KULIPA GHARAMA ZA MATIBABU

> Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amesema Serikali imekuwa ikisema hakuna Mtanzania anayekosa matibabu lakini wanashikilia maiti hospitalini na hatua hii inawanyima Watanzania kufanya ibada kwa ndugu zao wanaofariki kwa kushindwa kulipia gharama za matibabu

> Naibu Waziri wa Afya asema Wananchi wanaokosa fedha za kulipia matitabu wanapaswa kwenda kwenye Dawati la Ustawi wa Jamii linalokuwepo katika kila Hospitali

Soma - https://jamii.app/SerikaliKushikiliaMaiti
CHINA: DAKTARI ALIYETOA TAHADHARI YA KWANZA YA VIRUSI VYA CORONA AFARIKI DUNIA

> Li Wenliang aliyetoa tahadhari kuhusu mlipuko wa #CoronaVirus tangu Desemba 2019 amefariki kutokana na maambukizi hayo

> Alituhumiwa na Mamlaka kwa kusambaza taarifa za uongo

Soma - https://jamii.app/CoronaChina
ZITTO AHOFIA KURUDI TANZANIA KUTOKANA NA VITISHO ALIVYOVIPATA

> Amesema anaichukulia kwa uzito hofu yake kwa kuwa upo mfano wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kupigwa risasi Jijini Dodoma na hadi sasa ameshindwa kurejea nchini kutokana na hofu ya usalama wake

> Zitto kwa sasa yuko Amerika ya Kaskazini kwa shughuli ambazo hajaziweka wazi kwa umma

Soma - https://jamii.app/HofuUsalamaZittoTZ
MAREKANI YAMUUA KIONGOZI WA JUU WA AL-QAEDA

> Qasim al-Raymi ameuawa katika Operesheni ya Kijeshi nchini Yemen

> Trump amesema Marekani na nchi nyingine zipo salama kufuatia kuuawa kwa Kiongozi huyo

Soma - https://jamii.app/Al-RaymiYemen