JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KWANINI MARA NYINGI BAADA YA MTU KUSHTAKIWA, POLISI AU WAENDESHA MASHTAKA HUDAI UPELELEZI HAUJAKAMILIKA?

> Hii huweza kutokea kutokana na mazingira ya tuhuma, ushahidi na taarifa za ziada ambazo huweza kupatikana baada ya kesi kufunguliwa ila endapo vipengele vyote vya uhalifu havikukamilika itakuwa ni upotezaji wa muda kumshtaki Mtu na kumpeleka Mahakamani

> Shauri la Jinai likikaa Mahakamani kwa siku 60 bila ushahidi kukamilika, Mahakama italitupilia mbali shauri hilo na Mtuhumiwa kuachiwa huru

Tembelea - https://jamii.app/SheriaKutokamilikaUpelelezi
#JFSheria
ZITTO ADAI BARUA YAKE KWA BENKI YA DUNIA KUHUSU MKOPO WA ELIMU INAPOTOSHWA

> Amesema si lengo lake kuzuia misaada Nchini ila anafanya hivyo ili kuwalinda Watoto wa Kike wanaopata ujauzito wakiwa masomoni kwa madai ya kuwapo kwa ubaguzi katika mfumo rasmi wa elimu Nchini

Soma - https://jamii.app/ZittoBaruaMkopoWB
SPIKA NDUGAI ATAKA BUNGE KUWEKWA KWENYE VIVUTIO VYA WATALII

- Amesema, wao ni namba moja kwa kuangalia Watalii wanaoenda Bungeni hapo ndani ya Mwaka

- Amehoji kama Wizara ya Maliasili inajua kuwa Bunge linongoza katika vivutio kuliko hifadhi yoyote

Soma https://jamii.app/NdugaiBungeUtalii
SONGWE: MAFURIKO YASABABISHA VIFO VYA WATU WANNE

> ACP George Salala amesema wanne wamefariki baada ya kusombwa na mafuriko katika Wilaya za Mbozi na Ileje

> Amewataka wananchi kuwa makini wakati huu ambapo mvua zinaendelea kunyesha

Soma - https://jamii.app/MafurikoVifoSongwe
CHINA: WATANZANIA 85 WANATARAJIWA KUNYONGWA KWA KUJIHUSISHA NA DAWA ZA KULEVYA

> Watanzania 85 wanatarajiwa kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya #DawaZaKulevya

> Aidha, Watanzania 265 wamekamatwa nchini humo kwa kosa hilo hilo na tayari 130 wamehukumiwa

Zaidi, soma - https://jamii.app/WatzKunyongwaDawaKulevya
KOREA KUSINI: MASHABIKI WALIPWA TZS 722,000 BAADA YA RONALDO KUKOSA MECHI

> Mahakama imeagiza waandaaji kuwalipa mashabiki wawili £240

> Wakili adai mashabiki hao walipata Shinikizo la kiakili baada ya kudanganywa #CR7 atakuwepo

Zaidi, soma - https://jamii.app/RonaldoFidiaKorea
MWENDELEZO: Mke wa Waziri Mkuu wa Lesotho amekamatwa na anatarajiwa kushtakiwa kwa kosa la kuhusika na mauaji ya Mke wa kwanza wa Waziri huyo mwaka 2017

- Maesiah Thabane, ambaye alitoroka nchini humo Januari 10, 2020 na kukimbilia Afrika Kusini amerudi nchini humo na kujisalimisha katika Kituo cha Polisi
IRAN: JASUSI WA SHIRIKA LA UPELELEZI MAREKANI (CIA) AHUKUMIWA KIFO

> Amir Rahimpour amehukumiwa kifo baada ya kutoa taarifa kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran

> Hii ni adhabu ya kwanza ya kifo kutolewa kwa kosa hili kwa takriban miaka 20

Soma - https://jamii.app/CIAIranKifo
HISTORIA NA MAISHA YA MZEE DANIEL ARAP MOI

> Alikuwa Rais wa pili wa Kenya aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka 24 kuanzia 1978 hadi 2002. Kifimbo alichotembea nacho kila mahali, ni ishara ya uongozi katika jamii yake ya Kalenjin

> Moi alikuwa miongoni mwa Wakenya wachache walioteuliwa kuwa Wajumbe wa Baraza la Majimbo la Serikali ya Wakoloni wa Kiingereza 1955

> Mwaka 1967, Kenyatta alimteua Moi kuwa Makamu wake na alipofariki 1978 akiwa na miaka 84 ndipo Moi akarithi kiti chake

Fahamu zaidi - https://jamii.app/HistoriaRaisDanielMoi
#JFHistoria
EWURA YATANGAZA KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA

> Imetangaza ongezeko la bei kwa mafuta yanayoingilia Bandari ya Dar kutokana na kushuka kwa thamani ya Tsh dhidi ya Dola ya Marekani na ongezeko la bei katika soko la Dunia

> Lita moja ya Petroli imepanda kwa Tsh 20 huku Dizeli ikiongezeka kwa Tsh 74 na Mafuta ya taa Tsh 44

Soma - https://jamii.app/PetrolDieselPriceRise
FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA HOMA YA MAPAFU (PNEUMONIA) - 2

> Ugonjwa huu unaweza kumpata yeyote lakini kuna makundi ambao yapo katika hatari zaidi

> Watoto chini ya Miaka mitano ni waathirika wakubwa zaidi wa Pneumonia kwasababu Mfumo wao wa kinga mwilini unakuwa bado haujakomaa

> Walio na umri wa miaka 65 na kuendelea nao wanaweza kuumwa Homa ya Mapafu kutokana na kinga yao ya mwili kupungua

> Wenye matatizo ya kifua, wanaotumia mashine za kupumulia, wavuta sigara, wanywa pombe na waathirika wa madawa ya kulevya nao wana hatari ya kuumwa

Zaidi, soma - https://jamii.app/VisababishiPneumonia
ULINZI WA TAARIFA NI NINI?: Huu ni mchakato unaohusisha kuzilinda taarifa kwa kuzingatia mahusiano kati ya ukusanywaji wa taarifa na usambazaji katika Ulimwengu wa Teknolojia

> Faragha na #UlinziWaTaarifa hizi ni jambo kubwa wakati wa matumizi ya taarifa: #UlinziWaTaarifa unahusisha mifumo yote ya ulinzi kwa taarifa Binafsi na zile za Taasisi

> Ulinzi wa Taarifa unahusisha usahihi, ulinzi dhidi ya kuharibiwa, kupotea au kupotoshwa. Unahakikisha watu husika ndio wanapata taarifa hizo
BIASHARA YA KUKODISHA: TENGENEZA KIPATO KIRAHISI KWA MAWAZO HAYA
-
Mdau wa Jukwaa la Biashara ametaja biashara ambazo mtu anaweza kufanya hata akiwa na mtaji mdogo
-
Kukodisha Jenereta. Umeme ni nishati muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Mdau amekadiria kuwa ukifanya biashara hii unaweza kuingiza Sh. 30,000 - 50,000 ndani ya saa 12
-
Kukodisha Mashine za Kuchomelea. Mdau anasema unapokodisha mashine hizi, una uhakika wa kupata Sh. 20,000 hadi 40,000 kutegemea na mashine ulizonazo. Ukitengeneza mahusiano mazuri na mafundi, biashara hii inalipa
-
Zaidi, soma - https://jamii.app/KipatoBiashara
#JFBiashara
BUKOBA MJINI: MENEJA WA CHAMA CHA USHIRIKA AJIUA KISA UPOTEVU WA MILIONI 889

> Humphrey Kachecheba (50) amekutwa amefariki katika nyumba ya kulala wageni

> Alifukuzwa kazi na kufunguliwa kesi Mahakamani baada ya fedha hizo kupotea

Soma - https://jamii.app/KifoFedhaBukoba
SEKTA YA KUBEMBELEZA NI YA NANI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME?

> Mdau wa JamiiForums.com anasema kuna wimbi kubwa la wanadada kudai wanaume wa siku hizi hawajui kubembeleza lakini enzi za wazee wetu wanawake ndiyo walikuwa wanafundwa na kufundishwa namna ya kumbembeleza mume

> Anasema Mwanaume sio mtu wa kubembeleza bali ni mtu wa kubembelezwa kwasababu anapitia magumu na kufanya kazi mbalimbali ili mkewe apate mahitaji

Maoni yako ni yapi juu ya Mdau?
Mjadala - https://jamii.app/KubembelezaMeKeMapenzi
#JFMahusiano
ULINZI WA TAARIFA: Je, Katiba ya Tanzania inasemaje kuhusu Ulinzi Wa Taarifa?

> Ibara ya 16.-(1) inaeleza: Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi, maisha binafsi na familia na unyumba wake, heshima na hifadhi ya maskani na mawasiliano yake

> Ibara ya 16, (2): Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa Sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho Haki ya mtu ya faragha, usalama wa nafsi yake, mali na maskani yake, yaweza kuingiliwa bila ya kuathiri Ibara hii
SHIRIKA LA RELI(TRC) LATANGAZA KUSITISHA HUDUMA RELI YA KATI

> TRC kupitia JamiiForums yaeleza kuwa huduma za usafiri wa Treni ya abiria na mizigo umesitishwa kutokana na uharibifu wa njia ya reli uliosababishwa na mafuriko hasa Kilosa hadi Igandu

Soma > https://jamii.app/UsafiriReliKati
UNHCR YAKUMBWA NA PENGO LA MAKAZI KWA AJILI YA WAKIMBIZI DUNIANI

> Kati ya Wakimbizi milioni 1.4 waliohitaji makazi mapya mwaka 2019, 64,000 pekee ndio waliopata makazi ktk maeneo mbalimbali Duniani

> Zaidi ya Watu milioni 70 walipoteza makazi yao 2019 kutokana na vita au mateso, ambapo Watu milioni 30 walikimbia Nchi zao

Soma - https://jamii.app/PengoMakaziWakimbizi
MAREKANI: BUNGE LA SENETI LAMFUTIA MASHTAKA DONALD TRUMP

> Trump alishutumiwa kwa kutumia vibaya madaraka na kuingilia Bunge

> Kura 52-48 zilipigwa kwenye mashtaka ya kutumia madaraka vibaya, na 53-47 kwenye mashtaka ya kuingilia Bunge

Soma - https://jamii.app/TrumpImpeachment
MALAWI: MUTHARIKA AKOSOA MAHAKAMA KWA KUBATILISHA UCHAGUZI, ATANGAZA KUKATA RUFAA

> Rais Peter Mutharika amesema uamuzi uliochukuliwa na Mahakama ya Katiba ni kifo cha Demokrasia nchini humo

> Ametangaza kukata rufaa Mahakama Kuu

Soma - https://jamii.app/UchaguziMalawi