JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MBUNGE ATAKA WABAKAJI WAHASIWE

> Zainabu Katimba, Mbunge Viti Maalimu (CCM), ameshauri kufanyike Marekebisho ya Sheria ili kuongeza adhabu ikiwemo kuhasiwa kwa wale watakaothibitika kwamba wamefanya Kosa la Ubakaji

> Waziri wa Katiba na Sheria asema, adhabu zilizopo sasa ni kali na kama itabidi kuongeza, basi Bunge likae pamoja

Soma - https://jamii.app/AdhabuKuhasiwaWabakaji
DODOMA: MAGARI YAKWAMA KWA ZAIDI YA SAA NANE

> Mvua zimeharibu barabara na kusababisha magari zaidi ya 100 kukwama eneo la Mpunguzi

> Magari ya mizigo yamenasa kwenye matope na kusababisha magari mengine kushindwa kuendelea na safari

Soma - https://jamii.app/MiundombinuBarabaraDOM
FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA HOMA YA MAPAFU (PNEUMONIA) - 1

> Pneumonia ni ugonjwa unaosababishwa na wadudu, virusi, fangasi na bakteria ambazo hushambulia njia ya hewa na mapafu

> Inakadiriwa kuwa, mtoto mmoja hupoteza maisha kila sekunde 20 kutokana na Homa ya Mapafu. Takwimu za WHO zinaonesha kuwa, watoto 808,694 walipoteza maisha kutokana na ugonjwa huu Mwaka 2017

> Watoto wenye umri chini ya miaka mitano wapo kwenye hatari zaidi ya kupata Pneumonia kutokana na kwamba Mfumo wao wa mwili wa kujilinda haujakomaa bado

Zaidi, soma - https://jamii.app/FahamuUgonjwaPneumonia
KUELEKEA UCHAGUZI: VYAMA VYA SIASA VYADAIWA KUANZISHA VIKUNDI VYA UHALIFU

> Mbunge wa Mtwara Mjini (CUF) amedai, baadhi ya viongozi wa Vyama vya Siasa wameanzisha Vikundi vya Uhalifu kwa ajili ya kufanya fujo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020

> Amemueleza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, kwamba ana ushahidi juu ya hilo na kumtaka aende Mtwara kuchukua ushahidi huo

Soma - https://jamii.app/VijanaUhalifuUchaguzi
SERIKALI KUWABANA MAKOCHA NA WACHEZAJI WA KIGENI KULIPA KODI

> Naibu Waziri wa Fedha amesema, Sheria ya Kodi ya Mapato ya 2004, Kifungu cha 7, inaeleza kuwa, anayepata mapato kutokana na ajira ndani ya Tanzania ana wajibu wa kulipa kodi

Soma - https://jamii.app/WageniSerikaliKodi
#WorldCancerDay: FAHAMU HAYA KUHUSU SARATANI

#Saratani ni kundi la #Magonjwa yanayoweza kuanza takriban kwenye kila Kiungo cha mwili seli zinapokua kuliko kawaida bila kudhibitiwa

- Ukuaji huo unaweza kuvamia viungo vingine vya mwili vilivyo pembeni na kilichoathirika

Zaidi, soma https://jamii.app/CancerDay2020
WAWILI WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUSAFIRISHA HEROIN

> Stanley/Sultan Ngowi na Jimmy Mlaki wamekamatwa baada ya kuwekewa mtego

> Kwa mujibu wa Sheria, Mtuhumiwa wa #DawazaKulevya akitiwa hatiani anaweza kupata adhabu ya Kifungo cha Maisha

Zaidi, soma - https://jamii.app/WatuhumiwaHeroin-DSM
#WorldCancerDay: Februari 4 kila mwaka ni siku ya Saratani Duniani. Siku hii hutumika kwa ajili ya kukumbusha kuhusu ugonjwa huo na namna ya kuendelea kujikinga na kuzuia Ugonjwa huo

- Takwimu zilizotolewa hapa ni za mwaka 2018 na ni kwa Mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Zaidi, soma https://jamii.app/CancerDay2020
KILIMO: MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA MFUMO WA UMWAGILIAJI

- Aina ya udongo; Udongo huathiri uhitaji wa maji hivyo Mkulima anapojua aina ya udongo, inakuwa rahisi kufahamu mfumo sahihi wa umwagiliaji ambao anatakiwa kutumia

- Hali ya hewa; Kwa mfano, Mfumo wa Sprinkler sio sahihi kutumika ikiwa sehemu ina upepo mkali, jua na joto. Inashauriwa kutumia mfumo wa matone ikiwa Shamba lipo eneo lenye hali ya joto

Zaidi, tembelea https://jamii.app/KilimoUmwagiliaji
SERIKALI YALIFUNGA KANISA KUTOKANA NA MGOGORO WA WAUMINI NA VIONGOZI

> Serikali ya Wilaya ya Moshi imelifunga kwa muda Kanisa la Evangelist Assembles of God (E.A.G.T) Mawenzi kutokana na uongozi wa juu wa Kanisa hilo kumuondoa Mchungaji Mwanzilishi wa Kanisa, Frank Mushi na kumleta Mchungaji mwingine bila ridhaa ya waumini

> Uongozi wa Kanisa umesema sababu ya kumuondoa Mchungaji huyo ni kutokuwa na Elimu ya Dini (Theology)

Soma - https://jamii.app/KufungwaKanisaMgogoro
UCHAGUZI MKUU MALAWI: Hawa ndio Majaji wa Mahakama ya Kikatiba waliobatilisha matokeo ya Uchaguzi wa Rais hapo jana

> Uchaguzi huo Mkuu ulifanyika Mei 2019 na ulibatilishwa Februari 3, 2020 kutokana na kasoro zilizokuwepo kwenye uchaguzi huo

> Uchaguzi utarudiwa tena ndani ya siku 150 kutokea jana kulingana na matangazo ya Tume ya Uchaguzi
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MAREKANI: SPIKA WA BUNGE ACHANA HOTUBA YA RAIS

- Nancy Pelosi amechana nakala yake ya Hotuba ya Rais Donald Trump baada ya Rais huyo kumaliza kuhutubia

- Rais Trump alitoa hotuba kuhusu ‘State of the Union’ Bungeni mbele ya Wabunge walioipigia makofi hotuba hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/NancyHotubaTrump
SHINYANGA: NYUMBA ZA WALIMU ZAGEUKA DANGURO, ZASABABISHA WANAFUNZI KUPATA UJAUZITO

> Ni majengo ya nyumba za Walimu katika Shule ya Sekondari Mwasele

> Hali hiyo imechochea Wanafunzi kupata ujauzito na kushindwa kuendelea na masomo

Zaidi, soma - https://jamii.app/WanafunziUjauzito-SHY
UPDATE: VIRUSI VYA CORONA VYAENDELEA KUITESA DUNIA

- #coronavirus vimeua Watu 492 Ulimwenguni hadi sasa ikiwa ni ongezeko la Watu 65 ndani ya takriban saa 24

- Wengi waliofariki ni Raia wa #China huku Mji wa #Wuhan ukiongoza

- Zaidi ya Watu 24,500 wameathirika katika Nchi 25
FAO: NZIGE KUENDELEA KUZALIANA ZAIDI BARANI AFRIKA

> Taarifa iliyotolewa inasema janga la Nzige limetoa tishio kubwa kwa usalama wa chakula na maisha ya Watu huku Nzige hao wakiongezeka nchini Ethiopia na Somalia na kuelekea Kusini hadi nchini Kenya

> Ktk kipindi cha kuzaliana mwezi Februari idadi yao itaendelea kuongezeka katika nchi hizo

Soma - https://jamii.app/KuzalianaNzigeAfrika
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KABLA YA KUCHANWA HOTUBA, HIKI NDICHO KILITOKEA

- Awali, Rais Trump hakupokea salamu ya mkono ya Spika Nancy na haijawa wazi kama alipuuza au hakuona

- Baada ya kuchana Hotuba ya Trump, Spika Nancy amesema "Ilikuwa ni jambo la heshima kufanya, ukizingatia mbadala wake"

Zaidi, soma https://jamii.app/NancyHotubaTrump