JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MARA: MWILI WA MWALIMU WAKUTWA KWENYE GARI LAKE UKIWA UMEFUNGWA MIKONO NA MIGUU

> Ni mwili wa Rose Gulinjwa umekutwa ukiwa umefungwa kwa vitambaa mikono, miguu na mdomo

> Pia, Jonathan Burugu (6) amekutwa akiwa hai na alama za kamba shingoni

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuAnyongwa
SEKTA YA AFYA NCHINI KUNUFAIKA NA MKOPO WA USD MILIONI 600

- Mkopo huo wa takriban Tsh. Trilioni 1.4 utatolewa na Taasisi ya Global Fund, Januari 2021

- Utasaidia mapambano dhidi ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria kwa mwaka 2021 hadi 2023

Zaidi, soma https://jamii.app/MkopoAfya-GlobalFund
SERIKALI KUBADILI SHERIA YA JUMUIYA KUTOKANA NA UTITIRI WA VIBANDA IMANI

> Imesema itaangalia namna ya kubadilisha Sheria ya Jumuiya ili kuwe na utaratibu wa utoaji wa huduma za kiroho, hasa kutokana na kuwapo kwa utitiri wa Vibanda Imani

> Ni baada ya watu 20 kufariki na wengine 16 kujeruhiwa kwenye Kongamano la Maombi la 'Bulldozer'

Zaidi, soma https://jamii.app/MabadilikoSheriaJumuiya
DAR: UAPISHO WA VIONGOZI MBALIMBALI

- Rais Magufuli anawaapisha Viongozi wateule katika hafla inayofanyika Ikulu Jijini Dar

- Miongoni mwa wanaoapishwa ni Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama

Fuatilia https://jamii.app/UapishoIkulu-Feb03-2020
UPDATE: #CoronaVirus vimeua watu 362 huku zaidi ya Watu 17,300 wakiathiriwa Ulimwenguni kote

- Vifo hivyo ni zaidi ya vifo vilivyopatikana na mlipuko wa ugonjwa wa 'Severe Acute Respiratory Syndrome (SARS)' uliotokea China mwaka 2003 ambapo Watu 349 walifariki

#SARSvirus
SOMALIA YATANGAZA UVAMIZI WA NZIGE KUWA JANGA LA KITAIFA

> Hatua hii imefikiwa baada ya wadudu hao kuendelea kuharibu mimea na sasa hali inatishia kuwepo kwa uhaha wa chakula

> Inaelezwa kuna wasiwasi kuwa, huenda ikawa vigumu kudhibiti Nzige hao kabla ya msimu wa mavuno mwezi Aprili 2020

Zaidi, soma - https://jamii.app/LocustNationalDisaster
Rais Magufuli amemuapisha Brig. Jen. Suleman Mungiya Mzee kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza. Kabla ya Kiapo alikuwa mbele ya Rais akiwa amevaa mavazi ya JWTZ

- Alibadili Mavazi na kuvaa Mavazi ya Jeshi la Magereza kisha alirejea mbele ya Rais kwa ajili ya kiapo na kuvalishwa Cheo kipya cha Kamishna Jenerali

Fuatilia https://jamii.app/UapishoIkulu-Feb03-2020
RWANDA NA UGANDA ZAKUBALI KUBADILISHANA WAFUNGWA

> Rais Paul Kagame na Rais Yoweri Museveni wamekubali kushirikiana kuimarisha Amani, Utulivu na Ujirani Mwema

> Hatua hii inalenga kupunguza uhasama wa muda mrefu baina ya Mataifa hayo

Soma - https://jamii.app/UG-RWMakubaliano
DKT. ABBAS KUENDELEA KUWA MSEMAJI WA SERIKALI

- Rais Magufuli amesema Dkt. Hassan Abbas aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ataendelea kuwa Msemaji hadi mwingine atakapopatikana

- Amesema, Dkt. Abbas amefanya kazi nzuri kwa kufuata miongozo vizuri

Fuatilia https://jamii.app/UapishoIkulu-Feb03-2020
MAPUNYE: FAHAMU CHANZO, TIBA NA ATHARI ZAKE KWA NGOZI YAKO

> Ni aina ya fangasi inayoshambulia ngozi haswa ngozi ya kichwa na kwa lugha ya kitaalamu huitwa “Tinea capitis”. Ugonjwa huu hushambulia watu wa jinsia na umri wowote, ingawa huonekana zaidi kwa watoto wadogo

> Husambaa kwa kutumia vifaa vya nywele kama chanuo kwa zaidi ya mtu mmoja, Kugusana au Kushirikiana mavazi au kofia na mtu mwenye maambukizi

Zaidi, soma - https://jamii.app/ChanzoTibaMapunye
MICHEZO: Klabu ya Misr Lel Makkasa SC inayocheza Ligi Kuu ya Misri imemteua aliyekuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike kuwa kocha wa Klabu hiyo hadi mwisho wa msimu
-
Amunike alifutwa kazi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), siku chache baada ya Taifa Stars kutolewa hatua ya makundi kwenye Fainali za AFCON 2019
MALAWI: MAHAKAMA KUAMUA MATOKEO YA URAIS LEO

> Katika matokeo ya awali, Peter Mutharika alishinda kwa 38.6%, Lazaro Chakwera alipata 35% na Saulos Chilima alipata 20%

> Walioshindwa walilalamika kuwa Uchaguzi huo ulikuwa na makosa

Zaidi, soma - https://jamii.app/CourtElectionsMalawi
FAHAMU KUHUSU KURA TURUFU

> Kura Turufu (Veto) ni Haki ya kukataza Azimio lisipite wala kutekelezwa hata kama limekubaliwa na wengi. Katika nchi nyingi Rais au Kiongozi wa Taifa kwa manufaa ya Taifa ana Haki ya kukataza maazimio au Sheria zilizokubaliwa na Bunge

> Mataifa 5 yanaweza kutumia Kura Turufu (Veto) katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa: China, Marekani, Ufaransa, Uingereza na Urusi

Zaidi, soma - https://jamii.app/FahamuKuraVeto
SAMATTA AOMBA WATANZANIA KUACHA MANENO YA KASHFA DHIDI YA ASTON VILLA

> Amesema, amesikitishwa na maneno yanayotolewa na Watanzania kwenye kurasa za timu yake

> Adai hafurahishwi na kuomba mashabiki kuacha kashfa na matusi mitandaoni

Zaidi, soma - https://jamii.app/SamattaKashfaMitandao
SINGIDA: MADAKTARI WATUHUMIWA KUWATAKA KIMAPENZI WAGONJWA

> Madaktari wa Hospitali ya Rufaa hasa Madaktari vijana wanadaiwa kuwatongoza wagonjwa wa kike, wanaofika hospitalini hapo kupata huduma

> Inadaiwa, baadhi yao huwabambikizia magonjwa (wanawake hao) huku lengo likiwa kufanikisha matamanio ya ngono jambo linalosababisha baadhi ya wagonjwa kuikimbia hospitali

Soma - https://jamii.app/MadktKutongozaWagonjwaSGD
TANGA: MAHAKAMA ZA MWANZO 26 KATI YA 68 HAZIFANYI KAZI

- Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Amiry Mruma amesema hazifanyi kazi kutokana na uchakavu mkubwa wa majengo yake na hivyo kusababisha sehemu kubwa ya Wananchi kuhangaikia huduma

Zaidi, soma https://jamii.app/MahakamaMwanzoTanga
BUNGENI: MBUNGE ATAKA WAKULIMA WA BANGI WARUHUSIWE KUIUZA

- Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba amemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene kuwaruhusu Wakulima wa bangi kuiuza katika kipindi cha miezi sita

Zaidi, soma https://jamii.app/MbungeAtakaBangiIruhusiwe
MALEZI: MAADILI YA MTOTO NDANI YA FAMILIA NA JAMII

> Mara nyingi jamii imekuwa ikimtupia lawama nyingi sana mama, kwamba ndiye chanzo cha kuporomoka kwa maadili ya mtoto lakini Baba naye anatakiwa kushirikiana na mama kumlea mtoto katika hatua zote muhimu za ukuaji wake kwa kumpatia huduma stahiki

> Mtoto huanza kujifunza maadili kutoka kwa wazazi au walezi wake kwani ndio watu wanaomzunguka kwa karibu zaidi na baadae hujifunza maadili kutoka kwa majirani, shuleni na kwenye nyumba za ibada

Tembelea - https://jamii.app/JukumuMaadiliMtoto
MBOWE ASEMA KUNA HATARI YA NCHI KUTENGWA KIMATAIFA

- Amesema, wamemuandikia mapendekezo Rais Magufuli ya kujikwamua

- Miongoni mwa mapendekezo hayo ni Kufutwa na Kurejewa kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Kuunda Tume ya Maridhiano ya Kitaifa

Zaidi, soma https://jamii.app/MapendekezoMboweRais
MWANAFUNZI NCHINI KENYA AONYESHA DALILI ZA KUWA NA #CORONA
-
Shukri Jamal Mahmood amelazwa katika Chumba Maalumu katika Hospitali ya Rufaa ya Coast General Jijini Mombasa baada ya kuonyesha dalili ya kuambukizwa #CoronaVirus
-
Shukri aliwasili Mombasa kutoka China Januari 30 ambako anasomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Gaunzou