JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
JINSI YA KUPIKA SUPU MCHANGANYIKO NYAMA, FIGO, MAINI NA UDUVI

Mahitaji: Nyama ya ng’ombe 1/2 kilo, Maini 1/2 kilo, Figo 1/2 kilo, Vitunguu viwili vikubwa, Pilipili hoho tatu, Pilipili kali unazoweza kula, Limao, Chumvi, Uduvi kikombe cha chai

Jinsi ya kupika: Osha nyama, figo na maini kata kata weka pembeni. Weka limao na pilipili kukata shombo kwenye nyama kisha chemsha iive

> Nyama ikiiva osha uduvi (pia huitwa duvi, kijino au ushimbu) weka. Baada ya dakika kumi weka figo, pilipili hohoho na vitunguu vilivyokatwa vidogovidogo

> Kwa kuwa maini hayachelewi kuiva yaweke mwisho na yakiiva supu iko tayari. Weka chumvi na limao...
MAHAKAMA NCHINI KENYA YASITISHA USAJILI LAINI KWA ALAMA ZA VIDOLE

> Mahakama Kuu imesitisha mfumo wa usajili wa wananchi kwa Alama za Vidole hadi Sheria ya kulinda taarifa itakapopitishwa

> Pia, imesema kukusanya taarifa za eneo (GPS) na Vinasaba (DNA) ni kinyume na Katiba ya nchi

Soma - https://jamii.app/BanFingerprintRegistration
MOSHI: WATU 20 WAFARIKI KATIKA MAHUBIRI YA MWAMPOSA

- Wamefariki Jana katika Kongamano la Mhubiri Boniface Mwamposa 'Bulldozer' wakati wa harakati za kukanyaga Mafuta ya Upako

- Vifo vinaweza kuongezeka maana hakuna taarifa rasmi za majeruhi

Zaidi, soma https://jamii.app/Watu20Wafariki-Mwamposa
BIASHARA UNAZOWEZA KUFANYA BILA MTAJI

> Kuuza wazo/Mpango wa Biashara. Mpango wako wa biashara utafutie Hakimiliki. Kisha Uza Mpango wako

> Kuwa Mtafiti wa Bidhaa. Mfikishe anayehitaji kitu kwa mwenye nacho, kisha faidi kamisheni

Soma https://jamii.app/BiasharaUjasiliamali
#JFLeo
UPDATE: MWAMPOSA ATAKIWA POLISI KWA MAHOJIANO

- Mchungaji Boniface Mwamposa ‘Bulldozer’ anatafutwa kutokana na vifo vya Watu 20 vilivyotokea katika Kongamano lake

- Polisi imesema imemfuatilia bila mafanikio katika viwanja vya ndege

Zaidi, soma https://jamii.app/MwamposaPolisi
UPDATE: #CoronaVirus vimeua watu 305 huku Watu 14,300 wakiathirika Ulimwenguni kote

- #Virusi hivyo vimethibitika katika Mataifa 25 tangu vigundulike katika Mji wa #Wuhan huko #China

- Mataifa yanaendelea kutoa Watu wao China huku mengine yakisitisha safari za huko
MWAMPOSA (ANAYETAFUTWA NA POLISI) AENDESHA IBADA JIJINI DAR

> Wakati Polisi wakidai kumtafuta bila mafanikio, Mwamposa yupo anaendesha ibada kanisani kwake Kawe jijini Dar huku kukiwa na ulinzi mkali

> Inadaiwa watu wanadhibitiwa kupiga picha bila kibali na inasemekana ibada ya leo itaisha saa 6 kamili mchana
BONIFACE MWAMPOSA ATIWA MBARONI

> Jeshi la Polisi jijini Dar limemtia mbaroni Mwamposa (almaarufu Bulldozer) kufuatia vifo vya watu 20 na majeruhi 16 huko Moshi, Kilimanjaro

> Mwamposa aliwaaga waumini wake mchana huu kuwa anaenda Moshi kuitikia wito wa Polisi

> Waziri Simbachawene amethibitisha kukamatwa kwa Mwamposa
PALESTINA YASITISHA MAHUSIANO YOTE NA MAREKANI NA ISRAEL

> Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas amesitisha mahusiano yote na Marekani na Israel, yakiwemo yanayohusiana na usalama, baada ya kuupinga Mpango wa Amani wa Mashariki ya Kati uliopendekezwa na Rais Donald Trump

Zaidi, soma - https://jamii.app/PlstCutsRelationsIsraelUS
MARA: MWILI WA MWALIMU WAKUTWA KWENYE GARI LAKE UKIWA UMEFUNGWA MIKONO NA MIGUU

> Ni mwili wa Rose Gulinjwa umekutwa ukiwa umefungwa kwa vitambaa mikono, miguu na mdomo

> Pia, Jonathan Burugu (6) amekutwa akiwa hai na alama za kamba shingoni

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuAnyongwa
SEKTA YA AFYA NCHINI KUNUFAIKA NA MKOPO WA USD MILIONI 600

- Mkopo huo wa takriban Tsh. Trilioni 1.4 utatolewa na Taasisi ya Global Fund, Januari 2021

- Utasaidia mapambano dhidi ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria kwa mwaka 2021 hadi 2023

Zaidi, soma https://jamii.app/MkopoAfya-GlobalFund
SERIKALI KUBADILI SHERIA YA JUMUIYA KUTOKANA NA UTITIRI WA VIBANDA IMANI

> Imesema itaangalia namna ya kubadilisha Sheria ya Jumuiya ili kuwe na utaratibu wa utoaji wa huduma za kiroho, hasa kutokana na kuwapo kwa utitiri wa Vibanda Imani

> Ni baada ya watu 20 kufariki na wengine 16 kujeruhiwa kwenye Kongamano la Maombi la 'Bulldozer'

Zaidi, soma https://jamii.app/MabadilikoSheriaJumuiya
DAR: UAPISHO WA VIONGOZI MBALIMBALI

- Rais Magufuli anawaapisha Viongozi wateule katika hafla inayofanyika Ikulu Jijini Dar

- Miongoni mwa wanaoapishwa ni Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama

Fuatilia https://jamii.app/UapishoIkulu-Feb03-2020
UPDATE: #CoronaVirus vimeua watu 362 huku zaidi ya Watu 17,300 wakiathiriwa Ulimwenguni kote

- Vifo hivyo ni zaidi ya vifo vilivyopatikana na mlipuko wa ugonjwa wa 'Severe Acute Respiratory Syndrome (SARS)' uliotokea China mwaka 2003 ambapo Watu 349 walifariki

#SARSvirus
SOMALIA YATANGAZA UVAMIZI WA NZIGE KUWA JANGA LA KITAIFA

> Hatua hii imefikiwa baada ya wadudu hao kuendelea kuharibu mimea na sasa hali inatishia kuwepo kwa uhaha wa chakula

> Inaelezwa kuna wasiwasi kuwa, huenda ikawa vigumu kudhibiti Nzige hao kabla ya msimu wa mavuno mwezi Aprili 2020

Zaidi, soma - https://jamii.app/LocustNationalDisaster
Rais Magufuli amemuapisha Brig. Jen. Suleman Mungiya Mzee kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza. Kabla ya Kiapo alikuwa mbele ya Rais akiwa amevaa mavazi ya JWTZ

- Alibadili Mavazi na kuvaa Mavazi ya Jeshi la Magereza kisha alirejea mbele ya Rais kwa ajili ya kiapo na kuvalishwa Cheo kipya cha Kamishna Jenerali

Fuatilia https://jamii.app/UapishoIkulu-Feb03-2020
RWANDA NA UGANDA ZAKUBALI KUBADILISHANA WAFUNGWA

> Rais Paul Kagame na Rais Yoweri Museveni wamekubali kushirikiana kuimarisha Amani, Utulivu na Ujirani Mwema

> Hatua hii inalenga kupunguza uhasama wa muda mrefu baina ya Mataifa hayo

Soma - https://jamii.app/UG-RWMakubaliano
DKT. ABBAS KUENDELEA KUWA MSEMAJI WA SERIKALI

- Rais Magufuli amesema Dkt. Hassan Abbas aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ataendelea kuwa Msemaji hadi mwingine atakapopatikana

- Amesema, Dkt. Abbas amefanya kazi nzuri kwa kufuata miongozo vizuri

Fuatilia https://jamii.app/UapishoIkulu-Feb03-2020
MAPUNYE: FAHAMU CHANZO, TIBA NA ATHARI ZAKE KWA NGOZI YAKO

> Ni aina ya fangasi inayoshambulia ngozi haswa ngozi ya kichwa na kwa lugha ya kitaalamu huitwa “Tinea capitis”. Ugonjwa huu hushambulia watu wa jinsia na umri wowote, ingawa huonekana zaidi kwa watoto wadogo

> Husambaa kwa kutumia vifaa vya nywele kama chanuo kwa zaidi ya mtu mmoja, Kugusana au Kushirikiana mavazi au kofia na mtu mwenye maambukizi

Zaidi, soma - https://jamii.app/ChanzoTibaMapunye
MICHEZO: Klabu ya Misr Lel Makkasa SC inayocheza Ligi Kuu ya Misri imemteua aliyekuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike kuwa kocha wa Klabu hiyo hadi mwisho wa msimu
-
Amunike alifutwa kazi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), siku chache baada ya Taifa Stars kutolewa hatua ya makundi kwenye Fainali za AFCON 2019