JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MEJA JENERALI KINGU AWASILI TAKUKURU KUHOJIWA

> Kingu aliingia TAKUKURU wakati Lugola akiwa hajatoka ndani

> TAKUKURU inawahoji Lugola, Kingu na wengine kwa kuhusika na mkataba wa zaidi ya Tsh. Trilioni 1

Soma https://jamii.app/KinguTAKUKURU
MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA DUNIANI

Idadi ya Waathirika wa virusi vya Corona nchini Korea Kusini imefikia 11 huku Uingereza ikithibitisha Waathirika Wawili wa kwanza na Ujerumani pia imethibitisha Mgonjwa wake wa tano
UCHUMI WA TANZANIA WADAIWA KUKUA KWA 6.9%

> Kwa takwimu za mpaka Septemba 2019, uchumi wa Tanzania umekua kwa 6.9% huku matarajio yakiwa ni kufikia hadi 7.1%

> Kwa Nchi za SADC Tanzania ni miongoni mwa Nchi ambazo zinaongoza kwa uchumi wake kukua kwa kasi na ni ya pili kwa Afrika Mashariki kwa kutokuwa na rushwa nyuma ya Rwanda

Soma - https://jamii.app/UkuajiUchumiTz2019
MKE AMUUA MUMEWE BAADA YA KUNYWEA POMBE HELA YA PALIZI

> Mwanamke huyo alimpiga mumewe na kipande cha mti kichwani na kufariki akipatiwa matibabu

> Mtuhumiwa alikiri kosa na anashikiliwa na Polisi akisubiri kupelekwa Mahakamani

Soma https://jamii.app/MkeAmuuaMume
MAREKANI YAFURAHISHWA NA TAMKO LA RAIS MAGUFULI KUHUSU UCHAGUZI

- Imesema imetiwa moyo na hakikisho la Rais kuwa Uchaguzi Mkuu wa 2020 utakuwa wa Haki na Uwazi

- Pia, wamefurahishwa na mwaliko wa Rais kwa Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa

Soma https://jamii.app/Marekani-UchaguziTZ
DODOMA: Mapema leo, Spika Ndugai alisema wanamsubiri Zitto Kabwe awaeleze kwanini aliandika barua hiyo kwa Benki ya Dunia

- Alisema, suala hilo limewagusa na kuwakera wengi wasiojua limekujaje
BURUNDI : WANAHABARI WANNE WAHUKUMIWA KWENDA JELA KWA KUVURUGA USALAMA WA TAIFA

> Pia, imewataka kulipa faini ya Tsh. milioni 1.2

> Wanahabari walikamatwa wakiripoti kuhusu mapigano yaliotokea katika Eneo la Buganza

Zaidi, soma https://jamii.app/WanahabariJela
ZINGATIA HAYA KWA WENYE MAGARI YA ‘AUTOMATIC’

> Usiweke ‘Neutral’ mteremkoni au kwenye taa za barabarani na Usiwashe gari na kuanza kuvuta mafuta

> Usiweke ‘Parking’ kabla halijasimama kabisa. Usiendeshe gari kwa kasi kabla injini kupata joto

Zaidi, soma https://jamii.app/MagariAutomatic
PETITION KWA AJILI YA KUPATA SIKU YA WANAWAKE WALEMAVU TANZANIA

> Wanawake wenye ulemavu hukumbana na ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa kingono kuliko wasio na ulemavu

> Ungana nasi kuliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania kutangaza Siku ya Taifa ya Wanawake Wenye Ulemavu

Ingia hapa https://jamii.app/WanawakeWalemavu
JINSI YA KUFUTA HISTORIA YA TOVUTI ULIZOTEMBELEA KWENYE GOOGLE CHROME

> Bofya nukta 3 zilizopo juu kulia > bofya History (unaweza kutumia CTRL+H). Shuka sehemu iliyoandikwa Clear Browsing Data

> Chagua unata kufuta History kuanzia wakati gani na unataka kufuta nini

> Kama unatumia Google Chrome kupitia simu yako bofya nukta 3 upande wa juu wa browser yako kisha > History na ubofye Clear Browsing Data, na mwisho Clear Data

Kwa elimu zaidi, fungua > https://jamii.app/BrowsingHistory
MTANZANIA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI AFRIKA KUSINI

> Chanzo tukio hilo ni mgogoro wa kibiashara

> Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Emmanuel Buhohela amesema, hawajapata taarifa za kifo hicho kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini

Zaidi, soma https://jamii.app/MtanzaniaRisasiSauzi
MAREKANI: KATIBU WA MASUALA YA BIASHARA ASEMA VIRUSI VYA CORONA NI FURSA KWAO

> Wilbur Ross asema, mlipuko huo unaweza kuinua uchumi wao. Wizara ya biashara kupitia msemaji wake iliunga mkono matamshi hayo

Zaidi, soma https://jamii.app/CoronaFursaMarekani
JAMII YA PWANI NA UTAMADUNI WA SHEREHE ZA KUMTOA MWALI (BINTI)

> Katika baadhi ya Mikoa na Pwani ya Tanzania, wana utamaduni wa binti kupatiwa Mafunzo Maalumu ambapo huelekezwa kuhusu unyumba, namna ya kukaa na mume, nguo za kuvaa akiwa na mumewe, chakula cha kupika na kadhalika

> Utamaduni huu umekuwa ukilaumiwa na baadhi ya watu kuwa ndio chanzo cha kusitisha masomo kwa wasichana wengi pamoja na mimba za utotoni

Una maoni gani? - https://jamii.app/UtamaduniKumtoaMwali
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda awekewa vikwazo kuingia Marekani

Soma https://jamii.app/MakondaStopUSA
BAADHI YA MAMBO YATAKAYOKUFANYA UWE DEREVA MZURI ZAIDI

> Acha kutumia simu, kugeuka geuka nyuma au maongezi na abiria wako. Usiisogelee sana gari la mbele yako

> Epuka Brake za ghafla. Kuwa mvumilivu kwa uzembe unaofanywa na madereva wengine

Soma https://jamii.app/DerevaMakini
TANZANIA YAPIGWA MARUFUKU KUSHIRIKI BAHATI NASIBU YA VIZA ZA MAREKANI

- Marekani imepiga marufuku Raia wa Tanzania kushiriki katika Bahati Nasibu ya kupata Viza hizo

- Ni saa chache baada ya RC wa Dar, Paul Makonda kuzuiwa kuingia Marekani

Soma https://jamii.app/ZuioWatanzaniaUSA
MAREKANI: BUNGE LA SENETI LASIFU MAKONDA KUZUIWA

- Limesema kuzuiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kuingia nchini humo ni hatua nzuri ya mwanzo katika kuwawajibisha wale wote walio Tanzania wanaohusika na kuizorotesha Demokrasia

Zaidi, soma https://jamii.app/SenetiSifaZuioMakonda
NAMNA YA KUFANYA NGOZI IWE LAINI

> Tumia mafuta ya nazi gm 250 na karoti moja ya wastani. Bandika mafuta ya nazi, weka karoti iliyosagwa. Subiri hadi karoti iwe brown

> Unaweza kuongeza manukato yoyote ikishapoa

Soma https://jamii.app/UremboNgozi
SPIKA NDUGAI: KAMA BUNGE LA MAREKANI LINAMSHUGHULIKIA RAIS TRUMP, NASI TUFANYE HIVYO KWA ZITTO

> Amesema, kama Bunge la Marekani linamshughulikia Rais wa nchi hiyo kwa vitendo vya kukosa uzalendo, kwa nini isiwe hivyo kwa Mbunge Zitto Kabwe aliyeisaliti nchi kwa kitendo chake cha kuandika barua Benki ya Dunia (WB) akitaka Tanzania isipewe mkopo wa Dola milioni 500 kwa ajili ya Sekta ya Elimu?

Soma - https://jamii.app/BungeUsalitiZittoWB
MWANZA: MJAMZITO APEWA KIFUNGO CHA NJE MIEZI MITATU BAADA YA KUJARIBU KUJIUA

> Dementilia Saidia (22), mkazi wa Kijiji cha Usagara alikiri kutaka kujinyonga baada ya kufukuzwa nyumbani na aliyempa ujauzito kumkataa

Soma https://jamii.app/MjamzitoKifungo