JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ULINZI WA KIDIGITALI: NJIA IPI SALAMA ZAIDI YA KUFUNGA 'SCREEN' YA SIMU YAKO?

Moja ya njia inayotumiwa sana ili kuzuia simu yako (smartphone) kutochakata mambo kinyume na matakwa ya mmiliki au kuzuia mtu asiyehusika kuitumia ni kufunga 'screen' ya simu

Ziko njia nyingi za kufunga screen ya simu. Soma maelezo yafuatayo kisha chagua inayokufaa

> SLIDE TO UNLOCK: Hii ni njia rahisi na isiyoshauriwa, kuweka hii ni sawa na kufunga mlango kisha unaweka jiwe dogo ili usifunguliwe. Kamwe usitumie njia hii!

> PIN CODE LOCK: Hizi ni namba sita zinazotumika kufunga screen ya simu yako. Ni njia kongwe zaidi ya ulinzi wa simu ambapo miliki anapaswa kuweka namba 6 zilizopangiliwa bila ya kufuatana na anapaswa kuzikumbuka wakati wote

> PATTERN LOCK: Hii si njia kongwe ya ulinzi wa simu, imetokana na Maendeleo ya Teknolojia. Njia hii imekuwa ikikosolewa sana na wataalam wa #UlinziWaKidigitali. Inaelezwa kuwa ni rahisi kwa mdukuzi kukariri mchoro ama 'pattern'.

> FINGER PRINT LOCK: Njia hii inahusisha matumizi ya alama za vidole vya mmiliki wa simu. Kila anapotaka kuitumia simu yake basi lazima aguse kwa kidole alichosajili ili simu ifunguke. Njia hii ni bora ingawa ina changamoto kadhaa. Mdukuzi anaweza kujaribu vidole vya mhusika awapo usingizini au akiwa kwenye hali ya kulewa

> FACE ID LOCK: Utambulisho wa sura unatumika kufungua screen ya simu. Teknolojia hii kwa kiasi kikubwa ilianza kutumiwa na Kampuni ya Apple. Hii si maarufu na hakuna ushahidi wa wazi kuhusu udukuzi unaoweza kufanywa dhidi ya 'Face ID'

> EYE LOCK: Kila mwanadamu ana jicho la tofauti na mwengine. Utofauti huu ni nyenzo inayotumika katika ulinzi wa simu. Matumizi yake si makubwa ingawa inatajwa kuwa na usalama wa juu

> PASSWORD LOCK: Hii ni njia rahisi na maarufu zaidi. Ni salama na inashauriwa zaidi ingawa mmiliki anapaswa kufuata vigezo vyote vya utengenezaji wa nywila
INDIA: MTANZANIA AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA

> Ejike Celestine amemkamatwa na vidonge 600 vya #DawazaKulevya, zenye uzito wa gm 250

> Dawa zilizokamatwa zina thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 64.3

> Pia, Ejike amekutwa na 'Visa' bandia

Soma https://jamii.app/DawaKulevyaIndia
MWENDELEZO: Shirika la Afya Duniani (WHO) limevitangaza Virusi vipya vya #Corona kuwa Janga la Dharura kutokana na ugonjwa huo kusambaa mataifa mengine kwa kasi huku kukiwa na Mfumo Duni wa Afya
-
Watu takriban 213 wameshafariki kutokana na virusi hivyo nchini China na kumekuwa na visa 98 katika mataifa mengine 18 ingawa hakuna vifo vilivyobainika
DODOMA: LUGOLA AFIKA TAKUKURU KUHOJIWA

- Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amewasili Makao Makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)

- Anakabiliwa na kashfa ya kuingia mkataba wa kifisadi wa Vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini
SERIKALI YAWATAKA WATANZANIA WANAOSOMA CHINA KUTORUDI HUKO

> Serikali imewataka wanafunzi wanaosoma China ambao wako likizo nchini Tanzania, kutorudi China hadi pale zitakapopatikana taarifa za kidiplomasia kuhusiana na ugonjwa wa Corona

> Itakaporidhika na hali inayoendelea China itatoa tamko kwa Watanzania hao kurudi kuendelea na masomo

Soma - https://jamii.app/CoronaWatzMasomoChina
MPANDA: MTOTO WA MWAKA MMOJA NA NDUGUZE WANNE WATELEKEZWA NA BABA YAO

> Mama yao, aliondoka muda mrefu

> Afisa Ustawi wa Jamii alisema, tabia hiyo inakua kwa kasi mwaka 2019 pekee matukio zaidi ya 170 yaliripotiwa Mkoani humo

Soma https://jamii.app/WatotoWatelekezwa
ULINZI WA KIDIGITALI: ZINGATIA YAFUATAYO ILI KUWA SALAMA UNAPOTUMIA SMART TV

> Maendeleo ya Teknolojia yameleta mabadiliko ya Runinga. Kwasasa kuna wimbi kubwa la watu kutoka katika TV za Analogia na kuhamia kwenye Runinga ambazo ni za Kidigitali

> Jamii Forums inakukumbusha kuhusu umuhimu wa kuhakikisha unaendana na Maendeleo ya Teknolojia ukiwa salama wewe na familia yako

Kwa elimu zaidi, soma > https://jamii.app/UlinziSmartTv
BUNGENI: ZITTO ATAKIWA KUFAFANUA KUHUSU BARUA YA KUZUIA MKOPO WA ELIMU

- Spika Ndugai amesema, wanamsubiri Zitto Kabwe awaeleze kwanini aliandika barua hiyo kwa Benki ya Dunia

- Amesema, hilo limewagusa na kuwakera wengi wasiojua limekujaje

Soma https://jamii.app/ZittoAsubiriwaBungeni
JEFF BEZOS APATA TSH. TRILIONI 29.9 NDANI YA DAKIKA 15

> Mkurugenzi Mtendaji wa Amazon amekuwa tajiri mkubwa Duniani baada ya kumpita Bill Gates

> Amepata utajiri zaidi, baada ya hisa za Amazon kupanda na kufikia $2100 sawa na Tsh. 4,840,000

Soma https://jamii.app/AmazonMkurugenzi
NJIA ZINAZOWEZA KUKUSAIDIA KUITAWALA HASIRA (ANGER) YAKO

> Kama upo mazingira fulani na ukaudhiwa na hasira kali ikakushika, ondoka kwa dakika chache eneo hilo ili ubongo upate nafasi ya kutafakari upya

> Fikiria kabla ya kuzungumza: Ukiwa na hasira, ni rahisi kuzungumza maneno makali ambayo yanaweza yakashusha utu wako au wa yule unayemwambia

> Usilimbikize matukio: Kusamehe matukio yaliyopita na kuyasahau ni njia inayopunguza uzito wa tukio jipya. Ukisamehe utakuwa umejisaidia mwenyewe na waliokukosea

Fahamu zaidi - https://jamii.app/NjiaKudhibitiHasira
WAZIRI WA FEDHA ADAIWA KULISABABISHIA TAIFA HASARA YA TSH. MIL 80 KILA SIKU

> Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA) amedai, Waziri Philip Mpango ameshindwa kuruhusu Shirika la Nyumba (NHC), kumalizia miradi yake 4 ya ujenzi wa nyumba na Serikali imelazimika kuwalipa wakandarasi 4 kila mmoja Tsh. milioni 20 kwa siku

Soma - https://jamii.app/DktMpangoHasaraMil80
MEJA JENERALI KINGU AWASILI TAKUKURU KUHOJIWA

> Kingu aliingia TAKUKURU wakati Lugola akiwa hajatoka ndani

> TAKUKURU inawahoji Lugola, Kingu na wengine kwa kuhusika na mkataba wa zaidi ya Tsh. Trilioni 1

Soma https://jamii.app/KinguTAKUKURU
MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA DUNIANI

Idadi ya Waathirika wa virusi vya Corona nchini Korea Kusini imefikia 11 huku Uingereza ikithibitisha Waathirika Wawili wa kwanza na Ujerumani pia imethibitisha Mgonjwa wake wa tano
UCHUMI WA TANZANIA WADAIWA KUKUA KWA 6.9%

> Kwa takwimu za mpaka Septemba 2019, uchumi wa Tanzania umekua kwa 6.9% huku matarajio yakiwa ni kufikia hadi 7.1%

> Kwa Nchi za SADC Tanzania ni miongoni mwa Nchi ambazo zinaongoza kwa uchumi wake kukua kwa kasi na ni ya pili kwa Afrika Mashariki kwa kutokuwa na rushwa nyuma ya Rwanda

Soma - https://jamii.app/UkuajiUchumiTz2019
MKE AMUUA MUMEWE BAADA YA KUNYWEA POMBE HELA YA PALIZI

> Mwanamke huyo alimpiga mumewe na kipande cha mti kichwani na kufariki akipatiwa matibabu

> Mtuhumiwa alikiri kosa na anashikiliwa na Polisi akisubiri kupelekwa Mahakamani

Soma https://jamii.app/MkeAmuuaMume
MAREKANI YAFURAHISHWA NA TAMKO LA RAIS MAGUFULI KUHUSU UCHAGUZI

- Imesema imetiwa moyo na hakikisho la Rais kuwa Uchaguzi Mkuu wa 2020 utakuwa wa Haki na Uwazi

- Pia, wamefurahishwa na mwaliko wa Rais kwa Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa

Soma https://jamii.app/Marekani-UchaguziTZ
DODOMA: Mapema leo, Spika Ndugai alisema wanamsubiri Zitto Kabwe awaeleze kwanini aliandika barua hiyo kwa Benki ya Dunia

- Alisema, suala hilo limewagusa na kuwakera wengi wasiojua limekujaje
BURUNDI : WANAHABARI WANNE WAHUKUMIWA KWENDA JELA KWA KUVURUGA USALAMA WA TAIFA

> Pia, imewataka kulipa faini ya Tsh. milioni 1.2

> Wanahabari walikamatwa wakiripoti kuhusu mapigano yaliotokea katika Eneo la Buganza

Zaidi, soma https://jamii.app/WanahabariJela
ZINGATIA HAYA KWA WENYE MAGARI YA ‘AUTOMATIC’

> Usiweke ‘Neutral’ mteremkoni au kwenye taa za barabarani na Usiwashe gari na kuanza kuvuta mafuta

> Usiweke ‘Parking’ kabla halijasimama kabisa. Usiendeshe gari kwa kasi kabla injini kupata joto

Zaidi, soma https://jamii.app/MagariAutomatic
PETITION KWA AJILI YA KUPATA SIKU YA WANAWAKE WALEMAVU TANZANIA

> Wanawake wenye ulemavu hukumbana na ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa kingono kuliko wasio na ulemavu

> Ungana nasi kuliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania kutangaza Siku ya Taifa ya Wanawake Wenye Ulemavu

Ingia hapa https://jamii.app/WanawakeWalemavu