JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#IjueKatiba: ZIJUE SIFA ZA KUWA MBUNGE NCHINI TANZANIA

#KatibaTanzania, Ibara 67: Awe Raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza miaka 21, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza

- Awe ni Mwanachama na mgombea aliyependekezwa na Chama cha Siasa
KIJANA AMUUA MAMA YAKE WA MIAKA 70

> Mama huyo alimshutumu Kijana wake kula mayai ikiwa hajawahi kuleta chakula hapo nyumbani

> Kijana alirudi na panga akampiga Mama yake na Mpwa wake na kuwaua, na kisha kumjeruhi Dada yake

Zaidi, soma https://jamii.app/AmuuaMamaye
NJOMBE: SHANGAZI AMPIGA MPWA WAKE NA KUMSABABISHIA KIFO

- Apronia Mwinuka (35) mkazi wa Kata ya Makambako anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumpiga na kumsababishia kifo, Elina Mwinuka (18) kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani

Zaidi, soma https://jamii.app/AmuuaBintiKipigoNJM
SHAKA ZULU: MFALME ALIYEANZA KUUA WATU BAADA YA MAMA YAKE KUFARIKI

> Alimpenda Sana Mama yake Mzazi 'Nandi kaBhebhe' kiasi kwamba Mama yake huyo alipofariki Oktoba 1827, Shaka akaanza kufanya mauaji. Aliua zaidi ya watu 7,000 kwa Mwaka Mmoja tu

> Sifa zake nyingine zimetokana na uwezo wa kupanua utawala wake kutoka eneo ndogo la 260 km² kuwa 28,500 km²

Zaidi, soma https://jamii.app/ShakaZulu
#JFHistoria
KATAVI: AGIZO LA RAIS LADAIWA KUTOTEKELEZWA, VIBOKO WANAZIDI KUWA TISHIO KWA WANANCHI

> Oktoba 10, 2019, Rais Magufuli aliiagiza Mamlaka ya Wanyama Pori kuwahamisha viboko katika bwawa la Milala ili kuzuia uharibifu wa mazao na kulinda Usalama wa Wananchi

Zaidi, soma https://jamii.app/KataviViboko
TCRA: JULAI NI MWISHO MAFUNDI SIMU WASIOSOMEA NA KUSAJILIWA

> TCRA imetangaza Julai kuwa mwisho wa mafundi simu wasio na Elimu na Usajili

> Mafundi hao wametakiwa kufanya kazi kwenye Vikundi ili kupata Elimu na Usajili

Zaidi, soma https://jamii.app/TCRAMafundiSimu
RAIS KAGAME ATAKA ASISHURUTISHWE KUFUNGUA MPAKA WAO NA UGANDA

> Rais wa Rwanda amesema, Serikali yake itafungua mpaka na Uganda wakati itakapojisikia kufanya hivyo na wala hakuna Mtu wala Nchi yoyote itakayomshurutisha kufanya hivyo

> Amesema, Mgogoro wa Kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ni kwamba tatizo lililopo ni kubwa kuliko kufungwa kwa mpaka kama inavyoripotiwa

Zaidi, soma https://jamii.app/ZuioRwandaMpakaUganda
WHO KUFANYA KIKAO CHA KUITANGAZA #CORONA KAMA JANGA LA DHARURA DUNIANI

> Shirika la Afya la Ulimwenguni (WHO) limesema, ni muhimu kuitisha mkutano kwa kuwa Virusi hivyo vimekwishasambaa nje ya China, hali inayozidi kutia wasiwasi

> Idadi ya maambukizi imepanda na kufikia 7,700 na watu 170 wamekwishafariki hadi kufikia mapema leo

Soma - https://jamii.app/CoronaEmergencyOutbreak
WAFUNGWA WAWAANIKA VIGOGO WA MADAWA YA KULEVYA

> Wafungwa 130 Raia wa Watanzania katika Magereza ya Hong Kong nchini China, wametaja vigogo wanaojihusisha na biashara ya #DawazaKulevya nchini

> Mamlaka zimeanza kuyafanyia kazi suala hilo

Soma https://jamii.app/VigogoDawaKulevya
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Wazazi na walezi 23 Wilayani Newala, Mtwara wamekamatwa na watafikishwa Mahakamani kwa madai ya kushindwa kuwapeleka watoto wao kujiunga na Masomo ya Kidato cha Kwanza 2020
-
Aidha, siku 4 zilizopita wazazi 50 walikamatwa na Jeshi la Polisi Wilayani Tunduru, Ruvuma kwa kosa la kutowapeleka shuleni watoto wao waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza
FELA KUTI: MUZIKI WAKE ULIVYOSABABISHA KIFO CHA MAMA YAKE

> Wimbo wake wa ZOMBIE, aliowatukana Wanajeshi na Polisi ulipigwa marufuku mwaka 1976

> Mwaka 1977, aliimba wimbo huo, Wanajeshi wakamkata Mama yake na kumtupa ghorofani

Soma zaidi https://jamii.app/FelaKuti
MICHEZO: Klabu ya Yanga imepinga adhabu iliyopewa na Kamati ambayo iliwafungia wachezaji wake 3 na kutoa onyo kwa kocha Luc Eymael
-
Imesema, haikubaliani na adhabu hizo kwani kuna mambo mengi ya kisheria hayakufuatwa mpaka kuamua kutoa hukumu hiyo ambayo awali walipeleka malalamiko yao kwa Wasimamizi wa Ligi lakini hawakupewa majibu
-
Yanga wameamua kuandika barua TFF, CAF, FIFA, TAKUKURU na Mamlaka nyingine husika kulalamika juu ya hilo
-
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB), alitangaza kuwafungia mechi 3 na faini ya Tsh. 500,000 wachezaji 3 baada ya kugoma kutoka uwanjani katika pambano dhidi ya Mbeya City
KENYA HATARINI KUKUMBWA NA BAA LA NJAA KUTOKANA NA WINGI WA NZIGE

> Nzige hao wamesharipotiwa kufika katika kaunti 13 kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita na wanaendelea kuenea maeneo mengi nchini humo

> Serikali imekiri hali hiyo itasababisha ugumu wa hali ya maisha kwa mwaka 2020 kutokana na athari mbaya kwa Kilimo na Uchumi

Soma - https://jamii.app/NjaaUvamiziNzigeKE
LUGOLA: NITAVUA NGUO KAMA ITATHIBITIKA NILINUNUA SARE HEWA ZA POLISI

> Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), amemtaka Lugola ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kutoa maelezo kuhusu sakata la ufisadi katika ununuzi wa sare za Jeshi la Polisi nchini

> Lugola alimtuhumu Mussa Assad (Aliyekuwa CAG) kupotosha ukweli juu ya ununuzi wa sare hizo

Soma https://jamii.app/UfisadiKangiPAC
JE, NI SAHIHI MAGARI YA ABIRIA KUJAZA MAFUTA ZIKIWA NA ABIRIA NDANI?

> Mdau ndani ya JamiiForums.com anasema, imekuwa kawaida siku zote kuona Daladala na hata Mabasi ya Mikoani yakijaza mafuta huku yakiwa yamepakia abiria ndani ya gari

> Anahoji kuhusu usalama wa maisha ya abiria kwani moto unaweza kutokea. Je, hatuna sheria za kumlinda abiria katika hili?

Kwa mjadala zaidi - https://jamii.app/DaladalaMafutaAbiria
ARUSHA: JESHI LA POLISI LAUA WATU WATANO WANAODHANIWA KUWA MAJAMBAZI SUGU

> Wamekutwa na Shotgun Pump Action 32265, Chinese Pistol, Bastola bandia, risasi 11, simu 2 na pikipiki 3

> Mkuu wa Mkoa aahidi kuwazawadia waliofanikisha zoezi hilo

Soma https://jamii.app/WatanoWauawa
BUNGE LAJADILI SHERIA YA DHAMANA KWA KESI ZA UHUJUMU UCHUMI

> Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani amesema, kwa kuwa kesi za Uhujumu Uchumi hazina dhamana, ipo haja kwa Bunge kutunga Sheria ya marekebisho na kubadilisha pale ambapo itaona panafaa

> Mbunge Sabrina Sungura alihoji sababu ya vijana wengi wakiwemo kina Tito magoti kukutwa na kesi za Uhujumu Uchumi na kukaa mahabusu muda mrefu

Soma - https://jamii.app/DhamanaUhujumuUchumi
WATOTO MILIONI 6.3 WANATARAJIWA KUFARIKI KWA KICHOMI

> Kichomi husababishwa na Bakteria, Virusi au Kuvu hufanya watoto kushindwa kupumua, mapafu yao huwa yamejaa usaa na maji

> Kichomi kilisababisha vifo laki nane mwaka 2019

Soma https://jamii.app/UNICEFKichomi
NIGERIA: UGONJWA WA LASSA UMEUA WATU 41

> Watu 258 wamethibitishwa kuwa na Homa hiyo, wakiwemo wafanyakazi wa Kupambana na Homa hiyo

> Taasisi ya Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza nchini Nigeria, imeanzisha vituo vya dharura vya tiba

Soma https://jamii.app/LassaNigeria
MAONI YAKO NI YAPI KUHUSU MKE KUMSALIMIA MUMEWE 'SHIKAMOO'?

> Kwa desturi, mazungumzo karibia yote huanza kwa salamu. Aina ya salamu hutegemea wakati gani mmekutana na mna mahusiano gani

> "Shikamoo" ni moja kati ya salamu na wengi husema asili yake ni ya kitumwa na ina maana ya 'nipo chini ya miguu yako'. Je, unadhani salamu hii inafaa kutumiwa na wanandoa au wapenzi?

Tembelea - https://jamii.app/SalamuShikamooMeKe
#JFMahusiano