JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
FAHAMU HAYA KUHUSU VIRUSI VYA CORONA

- #Coronaviruses vinavyopatikana zaidi kwa Wanyama, mara machache virusi hivyo vinaweza kuambukizwa kutoka kwa Mnyama kwenda kwa Binadamu

- Huwafanya Watu kuugua katika sehemu ya juu ya mfumo wa upumuaji sawa na mafua ya kawaida

Zaidi, soma https://jamii.app/FahamuCoronaVirus
#JFAfya
BRUNO FERNANDES MBIONI KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED

- Sporting Lisbon imekubali kumuuza Bruno (25) kwa Paundi Milioni 68 baada ya dau la kwanza la Paundi Milioni 46.6

- Kiungo huyo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano lakini bado hawajakubaliana masuala binafsi
UNAFAHAMU KWA NAMNA GANI UNAWEZA KUPUNGUZA USAMBAAJI WA CORONA?

- Hakuna Kinga ya #coronavirus kwa sasa, ila usambaaji wake kwa Binadamu unaweza kupunguzwa kwa Kuosha mikono yako mara kwa mara kwa maji na sabuni

- Epuka kugusa macho, mdomo na pua kwa mikono isiyooshwa

Zaidi, soma https://jamii.app/FahamuCoronaVirus
#JFAfya
MWANZA: UKEREWE YALALAMIKIA BEI KUBWA YA UMEME KWA UNIT 1

> Imeelezwa leo Bungeni kuwa, Watumiaji wa umeme katika Wilaya ya Ukerewe wanatumia nishati hiyo kwa gharama ya Tsh. 2,500 kwa Unit moja badala ya Tsh. 100 inayotozwa kwa maeneo mengine

> Serikali imemuagiza Mkuu wa Mkoa huo kufuatilia kuhusu gharama za umeme wanazotozwa Wananchi

Zaidi, soma https://jamii.app/GharamaUmemeUkerewe
SERIKALI YATENGA MAENEO KWA WATAKAOGUNDULIKA KUWA NA #CORONA

> Maeneo hayo ni Mawenzi (Kilimanjaro), Buswelu (Mwanza) na Kigamboni (Dar es Salaam)

> Wizara ya Afya inafanya uchunguzi kwa wasafiri wote kutoka Bara la Asia, kwenye mipaka na wanaoingia nchini kupitia Viwanja wa Ndege vilivyopo Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza

Zaidi, soma https://jamii.app/MaeneoWagonjwaCorona
HUJAOA WALA KUOLEWA: JE, UNAKUTANA NA CHANGAMOTO GANI KATIKA JAMII?

> Mdau kutoka JamiiForums anasema, Jamii zetu za Kiafrika zinafuatilia sana suala za ndoa na kuzaa bila kuelewa kuwa kuna mambo mengi yanayosababisha vijana wachelewe kuoa au kuolewa

> Anasema, kuna watu wanapenda ndoa na wanatamani kupata watoto lakini hawajabahatika kupata wenza wa kuishi nao na kuanzisha familia

Je, wewe unapitia changamoto zipi?

Kwa mjadala zaidi - https://jamii.app/ChangamotoKuoaKuolewa
MIRUMBA, KATAVI: AFISA MTENDAJI AMPA MIMBA BINTI YAKE WA KAMBO WA KIDATO CHA PILI

> Polisi imesema, mtuhumiwa amekamatwa na anaendelea kuhojiwa

> Baba mzazi amesema shauri hilo haliwezi kuisha kwa maelewano nje ya Mahakama

Zaidi, soma https://jamii.app/AfisaMimbaMwanae
ULINZI WA KIDIGITALI: JE, UTAJUAJE KAMA MAZUNGUMZO KUPITIA SIMU YAKO YANAFUATILIWA?

> Fuata njia zofuatazo ili kujua kama kuna mtu anafuatilia mazungumzo kwenye Simu yako. Njia hii inatumika kwenye Simu janja (Smart Phone na zile za kawaida)

> Anza kwa kupiga *#61# kisha bonyeza alama ya kupiga kama italeta majibu “FORWARDED“ basi ujue kuna mtu anafuatilia mazungumzo/ujumbe mfupi wa maneno unazotuma

> Na iwapo itaonyesha neno “NOT FORWARDED” basi tambua kuwa uko salama katika mazungumzo na jumbe fupe unazozituma kupitia simu yako

> Kuondoa au kumzuia mtu asiendelee kufuatilia mazungumzo yako piga ##21# na utaondoa
MTOTO WA MIAKA TISA AANZISHA BIASHARA NDOGO YA KUAJIRI WALEMAVU TU

> Camden Myers ambaye ni Mmarekani Mweusi ameunda kiwanda cha kahawa ambacho kinaajiri Walemavu tu

> Wafanyakazi wa kiwanda chake ni Wanafunzi wa Shule ya Walemavu ya Winston-Salem

Zaidi, soma https://jamii.app/BiasharaWalemavu
#IjueKatiba: ZIJUE SIFA ZA KUWA MBUNGE NCHINI TANZANIA

#KatibaTanzania, Ibara 67: Awe Raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza miaka 21, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza

- Awe ni Mwanachama na mgombea aliyependekezwa na Chama cha Siasa
KIJANA AMUUA MAMA YAKE WA MIAKA 70

> Mama huyo alimshutumu Kijana wake kula mayai ikiwa hajawahi kuleta chakula hapo nyumbani

> Kijana alirudi na panga akampiga Mama yake na Mpwa wake na kuwaua, na kisha kumjeruhi Dada yake

Zaidi, soma https://jamii.app/AmuuaMamaye
NJOMBE: SHANGAZI AMPIGA MPWA WAKE NA KUMSABABISHIA KIFO

- Apronia Mwinuka (35) mkazi wa Kata ya Makambako anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumpiga na kumsababishia kifo, Elina Mwinuka (18) kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani

Zaidi, soma https://jamii.app/AmuuaBintiKipigoNJM
SHAKA ZULU: MFALME ALIYEANZA KUUA WATU BAADA YA MAMA YAKE KUFARIKI

> Alimpenda Sana Mama yake Mzazi 'Nandi kaBhebhe' kiasi kwamba Mama yake huyo alipofariki Oktoba 1827, Shaka akaanza kufanya mauaji. Aliua zaidi ya watu 7,000 kwa Mwaka Mmoja tu

> Sifa zake nyingine zimetokana na uwezo wa kupanua utawala wake kutoka eneo ndogo la 260 km² kuwa 28,500 km²

Zaidi, soma https://jamii.app/ShakaZulu
#JFHistoria
KATAVI: AGIZO LA RAIS LADAIWA KUTOTEKELEZWA, VIBOKO WANAZIDI KUWA TISHIO KWA WANANCHI

> Oktoba 10, 2019, Rais Magufuli aliiagiza Mamlaka ya Wanyama Pori kuwahamisha viboko katika bwawa la Milala ili kuzuia uharibifu wa mazao na kulinda Usalama wa Wananchi

Zaidi, soma https://jamii.app/KataviViboko
TCRA: JULAI NI MWISHO MAFUNDI SIMU WASIOSOMEA NA KUSAJILIWA

> TCRA imetangaza Julai kuwa mwisho wa mafundi simu wasio na Elimu na Usajili

> Mafundi hao wametakiwa kufanya kazi kwenye Vikundi ili kupata Elimu na Usajili

Zaidi, soma https://jamii.app/TCRAMafundiSimu
RAIS KAGAME ATAKA ASISHURUTISHWE KUFUNGUA MPAKA WAO NA UGANDA

> Rais wa Rwanda amesema, Serikali yake itafungua mpaka na Uganda wakati itakapojisikia kufanya hivyo na wala hakuna Mtu wala Nchi yoyote itakayomshurutisha kufanya hivyo

> Amesema, Mgogoro wa Kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ni kwamba tatizo lililopo ni kubwa kuliko kufungwa kwa mpaka kama inavyoripotiwa

Zaidi, soma https://jamii.app/ZuioRwandaMpakaUganda
WHO KUFANYA KIKAO CHA KUITANGAZA #CORONA KAMA JANGA LA DHARURA DUNIANI

> Shirika la Afya la Ulimwenguni (WHO) limesema, ni muhimu kuitisha mkutano kwa kuwa Virusi hivyo vimekwishasambaa nje ya China, hali inayozidi kutia wasiwasi

> Idadi ya maambukizi imepanda na kufikia 7,700 na watu 170 wamekwishafariki hadi kufikia mapema leo

Soma - https://jamii.app/CoronaEmergencyOutbreak
WAFUNGWA WAWAANIKA VIGOGO WA MADAWA YA KULEVYA

> Wafungwa 130 Raia wa Watanzania katika Magereza ya Hong Kong nchini China, wametaja vigogo wanaojihusisha na biashara ya #DawazaKulevya nchini

> Mamlaka zimeanza kuyafanyia kazi suala hilo

Soma https://jamii.app/VigogoDawaKulevya
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Wazazi na walezi 23 Wilayani Newala, Mtwara wamekamatwa na watafikishwa Mahakamani kwa madai ya kushindwa kuwapeleka watoto wao kujiunga na Masomo ya Kidato cha Kwanza 2020
-
Aidha, siku 4 zilizopita wazazi 50 walikamatwa na Jeshi la Polisi Wilayani Tunduru, Ruvuma kwa kosa la kutowapeleka shuleni watoto wao waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza
FELA KUTI: MUZIKI WAKE ULIVYOSABABISHA KIFO CHA MAMA YAKE

> Wimbo wake wa ZOMBIE, aliowatukana Wanajeshi na Polisi ulipigwa marufuku mwaka 1976

> Mwaka 1977, aliimba wimbo huo, Wanajeshi wakamkata Mama yake na kumtupa ghorofani

Soma zaidi https://jamii.app/FelaKuti