JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SPIKA WASTAAFU KUKABIDHIWA MAJOHO YAO WALIOYATUMIA BUNGENI

> Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema maspika watakaokabidhiwa majoho hayo ni Pius Msekwa, Samuel Sitta (Mke wake, Margareth Sitta atapokea kwa niaba) na Anne Makinda

Soma https://jamii.app/SpikaWastaafuJoho
WANAODAHILI WANAFUNZI WANAOTAKA KUSOMA NJE YA NCHI WATAKIWA KUJISAJILI TCU

> TCU imetoa miezi 3 wajisajili waweze kutambulika

> Kuendesha Uwakala bila Usajili ni kinyume cha Kanuni ya 47 (1) (d) na (f) ya Kanuni za Vyuo Vikuu za Mwaka 2013

Soma https://jamii.app/MawakalaVyuoNje
ULINZI WA KIDIGITALI: UTAJUAJE KAMA SIMU YAKO 'ANDROID' IMEINGILIWA NA 'VIRUS'?

> Simu yako inapofanya kazi taratibu kupita kawaida ni dalili moja wapo ya simu yako kuwa imeathiriwa na virusi. Kila Mtu anatarajia simu yake nifanye kazi sawa sawa na kwa haraka

> Simu yako inaposimamisha utendaji (Stucking) mara kwa mara ni dalili nyingine ya kuonesha kuwa simu yako imeingiliwa na virusi.

> Betri ya Simu kuisha kwa haraka hata bila ya simu kufanya kazi kwa muda mrefu. Virusi kuendelea kufanya kazi bila ya ruhusa ya mmiliki wa simu. Hii inasabanisha betri kuwa na kazi kubwa na kuisha haraka

> Kila ukifungua 'Browser' yako unakutana na matangazo mengi ya biashara hata ambayo hakuwahi kufuatilia. Virusi vinaweza kutumika kifanya matangazo ya biashara

> Simu kuwa na Application ambazo hujawahi kuzipakua (Download) ni dalili nyingine kuwa simu yako imeingiliwa na virusi

> Simu kuwa na matumizi makubwa ya Vifurushi vya Intaneti, pia ni dalili ya simu kuwa na virusi. Watu wengi hulalamika Vifurushi kuisha bila ya kutumika sawasawa, wakati mwingine ni kwasababu ya virusi
BENKI YA DUNIA YACHELEWESHA TENA KUTOA MKOPO WA ZAIDI YA TSH. TRILIONI 1 (USD 500m) KWA TANZANIA

> Benki hiyo imeahirisha mchakato wa Kupiga Kura ya 'Ndiyo au Hapana' ili kuikopesha Tanzania mkopo wa masharti nafuu kwa ajili ya kufadhili Elimu

Soma https://jamii.app/BenkiYaDunia
INTER MILAN YAMSAJILI CHRISTIAN ERIKSEN KUTOKA TOTTENHAM

- Mchezaji huyo amesaini Kandarasi inayoisha Juni 2024 kwa ada ya £17.5m na inaaminika atalipwa £6.5m kwa msimu

- Anaenda kuungana na Romelu Lukaku, Alexis Sanchez, Victor Moses na Ashley Young waliotoka Ligi Kuu England
#KatibaTanzania, Ibara ya 11: Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu unaofaa wa kufanikisha utekelezaji wa Haki ya mtu kufanya kazi, kujipatia elimu

- Bila kuathiri Haki hizo, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi kwa jasho lake

#JFLeo #IjueKatiba
UGANDA: WATU WAWILI WAFARIKA BAADA YA NDEGE YA JESHI KUANGUKA

> Watu wawili wamethibitishwa kufa baada ya Ndege ya Jeshi AF 302 iliyokuwa kwenye mafunzo kuanguka katika Mji wa Gomba

Soma https://jamii.app/WafarikiAjaliNdege
ULINZI WA KIDIGITALI: JINSI YA KUONDOA 'VIRUS' KWENYE SIMU YA ANDROID

> 1. Ondoa 'Application' usiyoitambua katika simu yako: Kama simu yako ina 'Application' ambayo huitambui tafadhali iondoe yawezekana imeletwa na kirusi au yenyewe ni kirusi

> Tumia 'Antivirus' kuondoa virusi kwenye simu yako: zipo Antivirus nyingi sana lakini unashauriwa kutumia Antivirus zifuatazo;

Kaspersky, Avast, Norton na AVG. Tafuta moja kati ya hizo kwenye Play Store kisha itumie kujisafisha simu yako. Tumia Antivirus moja usiweke mbili

> 3. 'Reset Factory' kwenye simu yako: kabla kutumia njia hii, hakikisha umehifadhi taarifa zako (picha, nyimbo na vitu vingine) kwa lugha rahisi Hakikisha umefanya backup ya taarifa zako. Reset Factory kwa hatua zifuatazo;

Settings > System > Advanced > Reset options > Erase all data. Utaondoka kila takataka kwenye simu yako na itaanza upya kama simu mpya

> Endelea kujilinda: kila ukitaka kupakua application mpya hakikisha umeipata Playstore au kwenye chanzo kingine cha kuaminika. Hakikisha umeujua undani wa App husika kabla ya kupakua
SERIKALI YAOMBWA KUSAIDIA KUTAFUTA MIILI YA WAVUVI WATATU WALIOZAMA BAHARI KUU SIKU KUMI ZILIZOPITA

> Akiongea na JamiiForums ndugu wa waliozama baharini amesema, wavuvi hao walienda kuvua, siku hiyo bahari ilichafuka ndipo boti yao ikazama

Soma https://jamii.app/WavuviWatatuWapotea
#IjueKatiba: UNAJUA SERIKALI INAPATA WAPI MAMLAKA YAKE?

#KatibaTanzania, Ibara 8: Jamhuri ya Muungano wa #Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya #Demokrasia na #HakiYaKijamii

Wananchi ndio msingi wa Mamlaka yote na Serikali itapata Mamlaka yake yote kutoka kwa Wananchi

#JFLeo
FAHAMU MMEA MKUBWA UNAOKULA NYAMA

> Mmea mkubwa unaokula nyama unajulikana kama 'Montane Pitche' aina ya 'Nepenthes Rajah' ambao una urefu wa sentimita 41

> Mmea huu hutumia maji yake kuwanasa wadudu warukao kama buibui na pia hukamata hata mijusi na vyura
-
Soma https://jamii.app/MtiUnakulaNyama
MFAHAMU MTU ANAYEWEZA KUSOMA KWA HARAKA ZAIDI

> Anne Jones alisoma Kitabu cha Harry Potter chenye jumla ya kurasa 784 kwa muda wa dakika 47

> Aliweza kusoma Maneno 4,200 kwa dakika. Wastani wa kasi ya kawaida ni maneno 220 hadi 300 kwa dakika

Zaidi, soma https://jamii.app/UsomajiWaHaraka
MWENDELEZO: VIRUSI VYA CORONA VYAUA WATU 132

- Pamoja na vifo hivyo, takriban visa 6,000 vya #coronavirus vimethibitishwa Nchini #China

- Hadi sasa kuna zaidi ya visa 70 vilivyothibitishwa katika maeneo 17 nje ya China, vikijumlisha visa 5 vilivyopo #Marekani

#nCoV2019
KANGI LUGOLA KUCHUNGUZWA NA TAKUKURU KWA UFISADI

> Uteuzi wake ulitenguliwa baada ya kuhusishwa na mkataba wa kifisadi wa zaidi ya Tsh. Trilioni 1 wa ununuzi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

> Haruhusiwi kusafiri bila TAKUKURU kuwa na taarifa

Zaidi, soma https://jamii.app/KangiLugolaPCCB
FAMILIA YA MSUYA YAPEWA MIEZI MIWILI KUFANYA MAKUBALIANO YA MIRATHI

> Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, imeielekeza familia hiyo kupeleka mrejesho Mahakamani baada ya muda huo kupita

> Bilionea Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi mwaka 2013

Zaidi, soma https://jamii.app/MsuyaMaridhiano
ARV'S ZACHANGIA KUPUNGUA KWA KASI YA SARATANI YA NGOZI (KAPOSI)

> Virusi vinavyosababisha UKIMWI wanapoingia mwilini, husababisha kushuka kwa kinga ya mwili, ambapo ngozi nayo huathirika na kusababisha Saratani, lakini baada ya mgonjwa kuanza kutumia dawa imesaidia kupunguza Saratani hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/ARVSarataniNgozi
FAHAMU MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUJIAJIRI

> Jenga nidhamu: Huwezi ukawa mjasiriamali ambaye huheshimu hata muda wako wa kazi

> Tambua jamii inahitaji nini: Ni lazima uwe na uwezo wa kujua mazingira uliyopo yanahitaji kitu gani ndipo utaweza kuja na utatuzi wake

> Fanya bidii kuliko wengine: Tambua kuwa kila mtu anaweza kuwa mjasiriamali, lakini tofauti huja katika bidii wanayoweka katika shughuli waliyochagua

Zaidi, soma https://jamii.app/MsingiKujiajiri
MWENDELEZO: Zaidi ya Watu 4000 Wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi wameathirika na mafuriko kufuatia mvua inayoendelea kunyesha na Watu 10 wamethibitika kufariki hadi sasa

- Zaidi ya Watu 1000 wameokolewa kutoka kwenye mafuriko na wanahifadhiwa katika Shule ya Msingi Kipindimbi ambayo imefungwa kwa muda
BILIONI 5.9 ZATUMIKA KUBORESHA UPATIKANAJI WA ELIMU KWA WANAFUNZI WENYE UHITAJI MAALUMU

> Zimenunua na kusambaza Vifaa vya Elimu Saidizi katika Shule za Msingi na Sekondari

> Pia, imejenga shule inayoweza kuhudumia watu 640 wenye Mahitaji maalumu

Zaidi, soma https://jamii.app/ICTShuleni