JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KIGOMA: MGANGA WA KIENYEJI AFUNGWA MAISHA KWA KUBAKA

- Mahakama ya Wilaya Kigoma imemhukumu mganga wa kienyeji, Venas Edward (48), mkazi wa Ujiji kutumikia kifungo hicho kwa kosa la kumnajisi mtoto wa kike wa miaka 8 aliyepelekewa amtibu

Soma https://jamii.app/MgangaJelaKulawiti-KGM
TCRA KUANZA MSAKO WA WALE WANAOWASAJILIA WENZAO LAINI ZA SIMU

> Pia, uhakiki huo utawahusu wale waliosajili laini zao kwa kutumia kitambulisho tofauti ambapo wote watachukuliwa hatua za kisheria

> Imesema, kundi la kwanza waliozimiwa laini zao ni watu 656,091 ambao wana vitambulisho vya Taifa au Namba lakini hawajasajili laini zao

Soma - https://jamii.app/MsakoUsajiliLaini
MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOSAFIRI NA GARI LAKO UMBALI MREFU

> Kagua hali na ubora wa magurudumu, mafuta lainishi (oil) na kiasi cha maji na kagua utendajikazi wa injini, breki, kiongeza mwendo (accelerator), usukani, taa, honi, viashiria (indicators)

> Hakikisha kabla ya safari unapata muda wa kutosha wa kupumzika ili kuepusha kusinzia barabarani

> Hakikisha unabeba vitu muhimu kama Chakula na vinywaji, kisanduku cha huduma ya kwanza, vifaa vya msingi vya matengenezo ya gari kama vile jeki, spana, tochi

Fahamu zaidi - https://jamii.app/DrivingLongDistance
#JFMagari
MICHEZO: Klabu ya TP Mazembe imetangaza kumrejesha nyota wake Raia wa Tanzania, Thomas Ulimwengu (27) kwa Mkataba wa miaka miwili na anatarajiwa kutua Lubumbashi Jumatano, Januari 29
-
Kati ya mwaka 2017 na 2018, alikuwa Sweden kwenye Timu Athletic Football Club Eskilstuna na Bosnian Club FK Sloboda Tuzla ambapo alikuwa akijaribu kutimiza ndoto zake za kupata Klabu Bora Zaidi Ulaya
RWANDA: WATOTO WA MITAANI WANATESWA KWENYE VITUO VYA KUBADILI TABIA

> Sheria ya mwaka 2017 inaeleza kutakuwa na kituo cha kubadili tabia watoto. Taarifa inasema, watoto waliokamatwa wanaendelea kupokea mateso katika kituo hicho

Soma https://jamii.app/RwandaKutesaWatoto
MAAFA YA MVUA: WATU 3 WAPOTEZA MAISHA

> Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimesababisha maafa ikiwemo watu 3 kupoteza maisha na watu zaidi ya 661 kukosa makazi katika Mikoa ya Lindi na Iringa

> Barabara inayounganisha Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Wilaya ya Iringa katika eneo la Tungamalenga imekatika

Soma - https://jamii.app/MaafaMvuaLindiIringa
MTU ANAYEDHANIWA KUWA NA VIRUSI VYA CORONA ANAPATIKANA KENYA

- Inaelezwa, mtu anayedhaniwa kuwa na #CoronaVirus anachunguzwa ktk Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta

- Aliwekwa chini ya uangalizi alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa JKIA

Soma https://jamii.app/KenyaMgonjwaCorona
#JFLeo #nCoV2019
MAAFISA WA TRA MBARONI KWA KUDAI RUSHWA YA TSH. MILIONI MOJA

> Emmanuel Ernest na Vincet Hassan, walimkamata mzigo wa 'Alminium' wenye risiti ya EFD ya tarehe ya nyuma

> Wakamdai aliyeuza mzigo awape hela ili wasichukue hatua za kisheria

Soma https://jamii.app/TRAKizimbani
JWTZ KUJENGA UWANJA WA MPIRA WA TSH. BILION 4.7 MANISPAA YA KINONDONI

> Luteni Kanali wa JWTZ amesema, ujenzi unaonyesha kukamilika kwa miezi nane lakini wao kama jeshi wataukamilisha kwa miezi sita. Wapo tayari kufanya kazi usiku na mchana

Soma https://jamii.app/JWTZUwanja
DAWA YA VVU KUTUMIKA KWA WAGONJWA WA #CORONA

> Mkurugenzi wa Idara ya Afya wa Jiji la Beijing, China amesema, wanatumia dawa za wagonjwa wa VVU za Lopinavir na Ritonavir kusaidia wagonjwa wa homa iliyozuka ya #CoronaVirus

> Mpaka sasa hakuna tiba ya ugonjwa huo huku Marekani ikisema iko maabara kutengeneza chanjo yake

Soma - https://jamii.app/ARVUseCoronaVictims
WANAOTUHUMIWA KUMUUA DKT. MVUNGI WADAI HAWANA IMANI NA HAKIMU

> Ni washtakiwa ktk kesi ya mauaji ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi, wamemkataa Hakimu Mwandamizi ktk Mahakama ya Kisutu, Vicky Mwaikambo

Soma https://jamii.app/MvungiHakimu
SPIKA WASTAAFU KUKABIDHIWA MAJOHO YAO WALIOYATUMIA BUNGENI

> Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema maspika watakaokabidhiwa majoho hayo ni Pius Msekwa, Samuel Sitta (Mke wake, Margareth Sitta atapokea kwa niaba) na Anne Makinda

Soma https://jamii.app/SpikaWastaafuJoho
WANAODAHILI WANAFUNZI WANAOTAKA KUSOMA NJE YA NCHI WATAKIWA KUJISAJILI TCU

> TCU imetoa miezi 3 wajisajili waweze kutambulika

> Kuendesha Uwakala bila Usajili ni kinyume cha Kanuni ya 47 (1) (d) na (f) ya Kanuni za Vyuo Vikuu za Mwaka 2013

Soma https://jamii.app/MawakalaVyuoNje
ULINZI WA KIDIGITALI: UTAJUAJE KAMA SIMU YAKO 'ANDROID' IMEINGILIWA NA 'VIRUS'?

> Simu yako inapofanya kazi taratibu kupita kawaida ni dalili moja wapo ya simu yako kuwa imeathiriwa na virusi. Kila Mtu anatarajia simu yake nifanye kazi sawa sawa na kwa haraka

> Simu yako inaposimamisha utendaji (Stucking) mara kwa mara ni dalili nyingine ya kuonesha kuwa simu yako imeingiliwa na virusi.

> Betri ya Simu kuisha kwa haraka hata bila ya simu kufanya kazi kwa muda mrefu. Virusi kuendelea kufanya kazi bila ya ruhusa ya mmiliki wa simu. Hii inasabanisha betri kuwa na kazi kubwa na kuisha haraka

> Kila ukifungua 'Browser' yako unakutana na matangazo mengi ya biashara hata ambayo hakuwahi kufuatilia. Virusi vinaweza kutumika kifanya matangazo ya biashara

> Simu kuwa na Application ambazo hujawahi kuzipakua (Download) ni dalili nyingine kuwa simu yako imeingiliwa na virusi

> Simu kuwa na matumizi makubwa ya Vifurushi vya Intaneti, pia ni dalili ya simu kuwa na virusi. Watu wengi hulalamika Vifurushi kuisha bila ya kutumika sawasawa, wakati mwingine ni kwasababu ya virusi
BENKI YA DUNIA YACHELEWESHA TENA KUTOA MKOPO WA ZAIDI YA TSH. TRILIONI 1 (USD 500m) KWA TANZANIA

> Benki hiyo imeahirisha mchakato wa Kupiga Kura ya 'Ndiyo au Hapana' ili kuikopesha Tanzania mkopo wa masharti nafuu kwa ajili ya kufadhili Elimu

Soma https://jamii.app/BenkiYaDunia
INTER MILAN YAMSAJILI CHRISTIAN ERIKSEN KUTOKA TOTTENHAM

- Mchezaji huyo amesaini Kandarasi inayoisha Juni 2024 kwa ada ya £17.5m na inaaminika atalipwa £6.5m kwa msimu

- Anaenda kuungana na Romelu Lukaku, Alexis Sanchez, Victor Moses na Ashley Young waliotoka Ligi Kuu England
#KatibaTanzania, Ibara ya 11: Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu unaofaa wa kufanikisha utekelezaji wa Haki ya mtu kufanya kazi, kujipatia elimu

- Bila kuathiri Haki hizo, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi kwa jasho lake

#JFLeo #IjueKatiba
UGANDA: WATU WAWILI WAFARIKA BAADA YA NDEGE YA JESHI KUANGUKA

> Watu wawili wamethibitishwa kufa baada ya Ndege ya Jeshi AF 302 iliyokuwa kwenye mafunzo kuanguka katika Mji wa Gomba

Soma https://jamii.app/WafarikiAjaliNdege
ULINZI WA KIDIGITALI: JINSI YA KUONDOA 'VIRUS' KWENYE SIMU YA ANDROID

> 1. Ondoa 'Application' usiyoitambua katika simu yako: Kama simu yako ina 'Application' ambayo huitambui tafadhali iondoe yawezekana imeletwa na kirusi au yenyewe ni kirusi

> Tumia 'Antivirus' kuondoa virusi kwenye simu yako: zipo Antivirus nyingi sana lakini unashauriwa kutumia Antivirus zifuatazo;

Kaspersky, Avast, Norton na AVG. Tafuta moja kati ya hizo kwenye Play Store kisha itumie kujisafisha simu yako. Tumia Antivirus moja usiweke mbili

> 3. 'Reset Factory' kwenye simu yako: kabla kutumia njia hii, hakikisha umehifadhi taarifa zako (picha, nyimbo na vitu vingine) kwa lugha rahisi Hakikisha umefanya backup ya taarifa zako. Reset Factory kwa hatua zifuatazo;

Settings > System > Advanced > Reset options > Erase all data. Utaondoka kila takataka kwenye simu yako na itaanza upya kama simu mpya

> Endelea kujilinda: kila ukitaka kupakua application mpya hakikisha umeipata Playstore au kwenye chanzo kingine cha kuaminika. Hakikisha umeujua undani wa App husika kabla ya kupakua