JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ISRAEL: NETANYAHU AUTAKA ULIMWENGU KUIPINGA ICC

> Israel si Wanachama wa ICC, imesema mahakama hiyo haina mamlaka ya kuchunguza uhalifu wa kivita wa jeshi la Israel

> Amemsifu Rais Trump kwa kuikosoa ICC na kuwataka wengine kufanya hivyo

Zaidi, soma https://jamii.app/NetanyahuICC
MAREKANI: AREJESHA TSH. MILIONI 98 ALIZOPATA KWENYE BIDHAA YA MTUMBA

> Howard Kirby amewashangaza wengi baada ya kukuta dola 43,000 zimefichwa katika kochi la mtumba alilonunua, na akamtafuta mmiliki wa mwanzo wa kochi hilo na kumrudishia

Zaidi, soma https://jamii.app/ArejeshaPesa
FAO: NZIGE WASIPODHIBITIWA WATASAMBAA ZAIDI NA KUONGEZEKA MARA 500

- Imesema, nzige walioivamia Ethiopia, Kenya na Somalia ni wimbi kubwa kuwahi kushuhudiwa

- Yadokeza, wasipodhibitiwa wanaweza kusambaa katika nchi nyingine za Afrika Mashariki

Soma > https://jamii.app/NzigeOnyoFAO
MAREKANI: KOBE BRYANT AFARIKI

Mchezaji maarufu wa Zamani wa Mpira wa Kikapu kwenye Ligi ya NBA, Kobe Bryant (41) amefariki katika ajali ya Helikopta iliyotokea leo huko California

Helkopta hiyo imeanguka baada ya kuwaka moto angani na watu wote (5) waliokuwemo wamefariki

Zaidi, soma https://jamii.app/KobeBryantAfariki
MAAMBUKIZI YA KIRUSI CORONA KUONGEZEKA KWA KASI

> Mpaka sasa watu zaidi ya 2,000 wameshaambukizwa duniani na watu 56 wameshapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo

> Kirusi hiki kimeenea katika miji mingine ikiwemo Beijing na Shanghai, Marekani, Thailand, Korea Kusini, Japan, Australia, Ufaransa, na Canada

Soma - https://jamii.app/CoronaVirusOutbreak
NACSAP III: NJIA ZA NAMNA RUSHWA INAVYOWEZA KUJIDHIHIRISHA

- Rushwa katika Mifumo ya Utawala: Hii inatokana na Watumishi wa Umma na Mawakala wao kudai rushwa wakati wa kutoa huduma za bure kwa Wananchi

- Rushwa Kabambe (Kubwa): Aina hii ya Rushwa imebainishwa kuhusisha Viongozi wa Ngazi za juu Serikalini wenye Mamlaka ya kutoa maamuzi kupitia Sera na Mikataba

#KemeaRushwa
SERIKALI: ZOEZI LA KUZUIA MIKUTANO ISIYOFUATA SHERIA LIKO PALEPALE

> Imesema muda wa siasa ukifika Serikali itaruhusu mikutano hiyo yenye lengo la kutoa nafasi kwa wanasiasa kuzungumza na wananchi na kueleza kwa wananchi walichokifanya kwa muda waliopewa baada ya kuchaguliwa ktk nafasi mbalimbali

Soma - https://jamii.app/EndelezoZuioMikutano
LESOTHO: WAZIRI MKUU NA MKEWE WAKABILIWA NA TUHUMA ZA MAUAJI

> Thomas Thabane pamoja na mkewe, Maesaiah Thabane wanatakiwa kuhojiwa kuhusiana na mauaji yaliyotokea mwaka 2017 ya Mke wa kwanza wa Thabane, Lipolelo Thabane(58)

> Lipolelo aliuawa siku 2 kabla ya Thabane kuapishwa kuwa Waziri Mkuu kwa kupigwa risasi sehemu mbalimbali za mwili wake

Soma - https://jamii.app/PMWifeMurderExWife
KENYA: MWANAMKE AFARIKI BAADA YA KURUKA KUTOKA KWENYE GARI LA WAGONJWA

> Naiso Leslie (26) alifanya maamuzi hayo baada ya kuona hali ya mtoto wake ikizidi kuwa mbaya wakiwa njiani kuelekea katika Hospitali ya Rufaa ya Kajiado

Soma zaidi https://jamii.app/KenyaGariKifo
#CORONA: CHINA KUJENGA HOSPITALI KWA SIKU 6

- Mji wa #Wuhan unajenga hospitali inayotarajiwa kuanza kutumika Februari 3 ikiwa na vitanda vya Wagonjwa 1000

- Ili kusaidia kutibu #coronavirus ambapo Watu 3000 wameathirika na 80 kufa

Soma https://jamii.app/CoronaHospSiku6
#JFLeo #nCoV2019
UPELELEZI KESI YA KABENDERA UNAENDELEA. KUSOMWA TENA FEBRUARI 10, 2020

- Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Mwandishi Erick Kabendera imeahirishwa baada ya Jamhuri kudai upelelezi unaendelea

- Pia, Jamhuri imesema mchakato wa Mshtakiwa kukiri makosa kwa DPP unaendelea
BUNGE LAIAGIZA TAKUKURU KUKAMATA VIGOGO KWA UBADHIRIFU

> Limebaini watendaji wa NARCO na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi waliohudumu 2008 hadi 2015, walishirikiana na Kampuni ya NICOL kuwaibia Watanzania Tsh. bilioni 15

> Soma https://jamii.app/BungeWizaraTakukuru
LINDI: ZAIDI YA WATU 4,500 HAWANA MAKAZI KUFUATIA MVUA KUBWA ILIYONYESHA

> Mali zao zimesombwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku tatu mfululizo

> Uokoaji unaendelea na wanahitaji msaada wa chakula, dawa, nguo na vitu vingine muhimu

Soma https://jamii.app/MafurikoKilwaLindi
RIPOTI: CHINA NI NCHI YA 2 KWA UUZAJI WA SILAHA DUNIANI

> Ripoti ya Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani (SIPRI) imesema, China ina Makampuni 4 yanayoingiza mapato makubwa ya mauzo ya silaha

> Makampuni hayo ambayo ni pamoja na Kampuni ya kutengeneza ndege ya China (AVIC) yaliuza silaha zenye thamani ya dola Bilioni 54.1 mwaka 2017

Soma - https://jamii.app/China2UuzajiSilaha
MWENDELEZO: Haya ni majina ya wengine waliofariki katika ajali helikopta iliyowauwa Kobe Bryant na Mwanaye Gianna;

- John Altobelli, mkewe Keri na mwanaye Alyssa; Sarah Chester na Mwanaye Payton Chester; Christina Mauser na rubani Ara Zobayan

Soma https://jamii.app/KobeBryantAfariki
#JFLeo
BRAZIL: WATU 46 WAFARIKI KWA MAPOROMOKO YALIYOSABABISHWA NA MVUA KALI

> Nyumba zaidi ya 20 zimekwenda na maji na watu 28 hawajulikani walipo

> Siku tatu za maombolezo zimetangazwa katika Jimbo la Minas Gerais na katika Miji mingine 47

Soma https://jamii.app/MvuaKaliBrazil
FAHAMU NJIA BORA ZITAKAZOKUFANYA UFANIKIWE KATIKA MAISHA YAKO

> Weka Malengo: Malengo ni dira inayokuonyesha unahitaji kutimiza nini. Huwezi kufanikiwa wala kushidwa kama hujui unahitaji nini

> Tengeneza mpango mkakati wa kutimiza malengo yako: Mpango mkakati ni njia na mbinu mbalimbali utakazozitumia kutimiza malengo uliyonayo

> Kuwa na nidhamu ya kukamilisha malengo na ratiba uliyojiwekea. Fuata mipango na mikakati yote uliyojiwekea katika kutimiza malengo yako

Tembelea - https://jamii.app/NjiaKufanikiwaMaisha
#JFMaisha
IRAN: WATU 135 WANUSURIKA KUFA BAADA YA NDEGE YAO KUANGUKA BARABARANI

> Ndege hiyo aina ya Caspian 6936 ilitarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mahshahr

> Ndege kama hiyo ilianguka mwaka 2009 katika mji wa Qazvin kusababisha vifo 168

Soma https://jamii.app/NdegeYaangukaIran
IKULU: Rais Magufuli awaapisha Mawaziri wawili na Mabalozi watatu aliowateua hivi karibuni

- Mabalozi hao wataiwakilisha Tanzania katika vituo vya Geneva-Uswisi, Tokyo-Japan na New York-Umoja wa Mataifa

Fuatalia https://jamii.app/UapishoIkuluJan27-20
#JFLeo