JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TAKUKURU YAOKOA TSH. BILIONI 4 KWENYE USHIRIKA

> Vyama vilivyofanyiwa ukaguzi ni 4,413 na kugundua viashiria vya ubadhirifu na rushwa ya Tsh. bilioni 124

> Kati ya Vyama vya Ushirika 11,410 vilivyosajiliwa, Vyama 2,103 havijulikani vilipo

Zaidi, soma https://jamii.app/TakukuruUshirika
POLISI WAKANA KUMKAMATA MWANAFUNZI ANAYEDAIWA KUPIGA PICHA ZA UKOSEFU WA MAJI UDOM

- Kamanda wa Polisi Gilles Muroto amesema hana taarifa za kukamatwa kwa Mugaya Tungu

- Makamu wa Chuo, ameomba radhi kutokana na tatizo la maji chuoni hapo

Soma https://jamii.app/MwanfunziUDOMMbaroni
#JFLeo
KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI AJIUZULU

- Rais Magufuli amesema Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu amemuandikia barua ya kujiuzulu na amemkubalia

- Rais ameyasema hayo akiwa anazindua Nyumba za Askari Magereza zilizopo Ukonga Jijini Dar

Zaidi, soma https://jamii.app/UzinduziJengoMagereza
Baadhi ya maneno aliyoyasema Rais Magufuli leo Januari 23 wakati wa Uzinduzi wa Nyumba za Maafisa na Maaskari wa Jeshi la Magereza zilizopo Ukonga Jijini Dar

Zaidi, soma https://jamii.app/UzinduziJengoMagereza
RAIS WA BURUNDI KUPATA TSH. BILIONI 1.15 AKISTAAFU

> Bunge limepitisha Sheria inatakayompa Rais kitita cha Tsh. Bilioni 1.15 atakapostaafu

> Na Rais akistaafu atachukuliwa kwa Hadhi ya Makamu wa Rais kwa kipindi cha miaka 7

Zaidi, soma https://jamii.app/BurundiNkurunzinza
KANGI LUGOLA ANG’OLEWA KWENYE NAFASI YA UWAZIRI

- Lugola, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, amesema Rais ndiye aliyemteua na sasa ameona ampumzishe

- Asema, ni jambo la faraja na hatua nzuri inayolenga kujenga safu ya Serikali ya Awamu ya 5

Zaidi, soma https://jamii.app/LugolaAondolewaUwaziri
ANGOLA: MWANAMKE TAJIRI ZAIDI AFRIKA AFUNGULIWA MASHTAKA YA ULAGHAI

> Isabel dos Santos anashtakiwa kwa ulaghai, ufujaji fedha, usimamizi mbaya wa Ofisi, kughushi stakabadhi pamoja na uhalifu mwingine wa kiuchumi

> Isabel dos Santos pia ni mtoto wa aliyewahikuwa Rais wa Angola (mwaka 1979-2017), Jose Eduardo dos Santos

Zaidi, soma - https://jamii.app/IsabelUlaghaiAngola
UGANDA: RAIA WA SUDAN AKAMATWA NA KARATASI ZINAZOBADILIKA NA KUWA DOLA BANDIA

> Duach Toang alikamatwa wakati anavuka mpaka wa Malaba, akitokea nchini Kenya

> Makaratasi hayo yanabadilika kuwa Dola bandia yanapomwagiwa kemikali

Zaidi, soma - https://jamii.app/DolaBandia-UG
WAMAREKANI WATATU WAFARIKI KATIKA HARAKATI ZA KUZIMA MOTO AUSTRALIA

> Ni baada ya ndege yao kuanguka wakati wanasaidia kuzima moto

> Waliofariki tangu kuanza kwa moto huo Septemba 2019 wamefikia 38

Zaidi, soma - https://jamii.app/AjaliVifo-AUS
RAIS MAGUFULI AMEFANYA UTEUZI WA MABALOZI WATATU

- Amewateua Meja Jenerali Jacob Kingu, Kamishina Jenerali wa Magereza Faustine Kasike na Dkt. John Steven Simbachawene

- Mabalozi hao wataapishwa na vituo vyao vya kazi vitatangazwa baadaye
ULINZI WA KIDIGITALI: JINSI YA KUJUA KAMA TOVUTI ULIYOTEMBELEA NI SALAMA

> Angalia kama tovuti uliyoifungua au kuitembelea ina alama ya kufuli kwenye 'URL' yake. Alama hii hutokea kabla ya 'link' iliyofungua ukurasa huo

> Tazama mfano pichani

#UlinziWaKidigitali
KAMISHNA WA JESHI LA ZIMAMOTO ANG'OLEWA

- Rais Magufuli ametengua Uteuzi wa Kamishna Jenerali Thobias Andengenye na nafasi yake itajazwa hapo baadaye

- Mapema leo, Rais alisema Kamishna huyo amehusika kusaini mkataba wa 'ajabu' wa thamani ya takriban Tsh. Trilioni 1.042