JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KATIBA: JAMHURI YA MUUNGANO
-
#KatibaTz - 3.-(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya Kidemokrasia na ya Kjamaa, yenye kufuata mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa
-
2 (1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na sehemu ya Bahari inayopakana nayo
-
Rasimu ya Jaji Warioba: 1 (1) Jamhuri ya Muungano ni Shirikisho lenye mamlaka kamili iliyotokana na Muungano wa Nchi 2
-
(2) Ni Shirikisho la Kidemokrasia linalofuata mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa, usawa wa Binadamu, kujitegemea, utawala wa Sheria na kuheshimu Haki za Binadamu
MICHEZO: Mchezaji wa Chelsea, Victor Moses amejiunga Inter Milan kwa mkopo ambapo anaenda kuungana na Kocha wa Zamani wa Chelsea, Antonio Conte

- Anakuwa mchezaji wa hivi karibuni kujiunga Inter akitokea Ligi Kuu England baada ya Romelu Lukaku, Ashley Young na Alexis Sanchez
SABABU ZA MIKOA KUFANYA/KUTOFANYA VIZURI KATIKA MITIHANI DARASA LA SABA

> Nafasi hafifu ya wazazi kuwahamasisha watoto, Umbali mrefu kwenda shuleni

> Changamoto ya kimenejimenti na kukosa hamasa na mbinu za ziada katika kuimarisha ufundishaji

Zaidi, soma https://jamii.app/HakiElimuSababu
ULINZI WA KIDIGITALI: JINSI YA KUJUA KAMA TOVUTI ULIYOTEMBELEA NI SALAMA

> Hakikisha tovuti uliyoingia inaanza na HTTPS badala ya HTTP

> HTTPS ni 'Hypertext Transfer Protocol Secure' neno la msingi hapo ni Secure ikimaanisha usalama

> Tazama mfano pichani
ULINZI WA KIDIGITALI: JINSI YA KUJUA KAMA TOVUTI ULIYOTEMBELEA NI SALAMA

> Tovuti hiyo itakuwa imeambatanisha Sera ya Faragha (Privacy Policy) kwa ajili ya watembeleaji

> Sera ya Faragha hueleza ni taarifa gani za mtembeleaji zitakusanywa na zitatumikaje
SYRIA: WANAJESHI 40 WAUAWA NA WAASI

> Waasi walitumia milipuko ya kutegwa ndani ya magari na silaha nzito nzito katika mashambulizi hayo

> Jeshi la Serikali limepeleka Vikosi vya Msaada katika jimbo hilo

Zaidi, soma zaidi https://jamii.app/SyriaWanajeshi
MBINGA, RUVUMA: KIJANA HUNYWA MAJI LITA 100 KWA SAA MBILI, TANGU APIGWE NA RADI

> Erick Msuha ana matatizo ya kiafya tangu apigwe na radi mwaka 1993 hivyo anatakiwa kufanyiwa Upasuaji

> Baba wa Kijana huyo ameomba msaada kutoka kwa Wasamaria wema kwani wameuza kila walichokuwa nacho kumsaidia bila mafanikio

Zaidi, soma zaidi https://jamii.app/MajiLita
RIPOTI: TANZANIA YAZIZIDI KENYA NA UGANDA KATIKA KUTOKOMEZA RUSHWA

> Tanzania imepata alama 37 kati ya alama 100 kwa Viashiria vya Kutokomeza Rushwa Duniani

> Kenya na Uganda zimepata alama 28. Nyingine ni Somalia (9), Sudan Kusini (12) na Rwanda (53)

Zaidi, soma - https://jamii.app/RipotiRushwaTZ
MWAKYEMBE: 2021 MWISHO WA WANAHABARI WASIO NA ELIMU KUANZIA STASHAHADA

- Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema, Desemba mwaka 2021 ndio mwisho kwa mujibu wa Sheria ya Huduma ya habari ya Mwaka 2016

Zaidi, soma https://jamii.app/ElimuWanahabari
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM) ambaye pia ni Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema hayo leo wakati akiongoza Kikao cha Viongozi na Watendaji wa Chama na Jumuiya zake za Mikoa na Wilaya
DAR: WATANZANIA 30 WALIOZAMIA AFRIKA KUSINI WAHUKUMIWA

> Watuhumiwa hao walirudishwa nchini na kufikishwa Mahakama ya Kisutu

> 16 wahukumiwa miezi 6 jela au faini ya Tsh. 300,000. Wengine 14 wamehukumiwa miezi 18 jela au faini ya Tsh. 50,000

Zaidi, soma - https://jamii.app/WazamiajiAfrikaKusini
TAFITI: WANAWAKE WALIOZIDI UMRI WAUME ZAO HURIDHIKA NA KUFURAHIA ZAIDI MAHUSIANO YAO

> Furaha na kuridhika kwao hutokana na usawa wa kijinsia

> Tafiti zinaonyesha wanaozingatia usawa wa kijinsia katika mahusiano huwa na furaha zaidi

Zaidi, soma https://jamii.app/RidhikaUmri
MTINDI NI KINGA DHIDI YA MAFUA

> Ni utafiti wa Dkt. Nizami Duran, wa Chuo cha Hatay Mustafa Kemal

> Utafiti umeonyesha Mtindi huongeza kiwango cha 'Immunoglobulin' au 'Antibody' ambazo ni muhimu kwa kuzalisha kinga ya mwili dhidi ya Magonjwa ya Kuambukiza

Zaidi, soma https://jamii.app/MtindiKinga
WAZIRI KABUDI AELEZA KWA NAMNA ALIVYOTAKA KUJIUZULU

- Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi ameeleza wakati mgumu aliopitia hadi kufikia hatua ya kuandika barua ya kujiuzulu

- Ameeleza hayo katika hafla ya Utiaji saini Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Madini ya Barrick, iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Kikwete ulipo Ikulu Jijini Dar
SERIKALI YATOA TAHADHARI YA VIRUSI VYA CORONA, YASEMA HAKUNA MGONJWA TANZANIA

> Wizara ya Afya imesema imekuwa ikifuatilia mlipuko huo tangu ulipoanza

> Tahadhari imetolewa kwa wanaosafiri China, Thailand, Japan, Marekani na Korea Kusini

Zaidi, soma https://jamii.app/VirusiCoronaTZ
MOROGORO: WATATU WAFARIKI KWA KUPIGWA NA RADI

- Maua Kibamba (22), Dativa Nyego (60) na Shukuru Samnyau (28), waliungua maeneo mbalimbali baada ya kupigwa radi

- Wito kwa Wananchi kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua

Zaidi, soma https://jamii.app/RadiWatatu
JE, WAJUA?: AFRIKA NDIO BARA LENYE NCHI ZAIDI

> Kuna Nchi 54 zinazotambuliwa kama Mataifa Barani Afrika. Sudani ya Kusini ni Taifa changa, Sahara Magharibi haijatambulika UN

> Asia ni Bara linalochokua eneo kubwa kuliko Afrika, lina nchi 49

Zaidi, soma https://jamii.app/AfrikaNchi
ULINZI WA KIDIGITALI: JE, ZIPI NI 'BROWSER' SALAMA UWAPO MTANDAONI? (PART 1)

> Browser kwa lugha ya Kiswahili huitwa Kivinjari. Hii ni programu ya Kompyuta au Simu ambayo hufanya kazi ya kupangilia, kuleta na kuonesha maudhui kutoka kwenye tovuti

> Ifahamike kuwa 'Browser' ni kiungo muhimu kwa watumiaji wa #MtandaoWaIntaneti. Zifuatazo ni Browser salama zaidi;

> 1: Firefox: Utengenezaji wa kivinjari hiki umezingatia umuhimu wa Usalama na Faragha. Aidha, toleo jipya la Firefox ambalo ni Firefox Quantum limeboreshwa kwa kuwa na kasi na rahisi kutumia

> Hata hivyo, Firefox haijakamilika katika usalama ingawa inamruhusu mtumiaji kuambatanisha program za usalama

> 2: Iridium Browser: Hii imetengenezwa kwa kufanana na Chrome lakini usalama wake uko juu zaidi. Imetengenezwa kwa kuzingatia Usalama na Faragha kuliko Chrome

> 3: GNU IceCat: Hii ni program yenye urafiki na Firefox imetengenezwa na kutolewa bure na inafanya kazi ya kuulinda usalama wako. Huitaji kufanya settings za kiusalama

> 4: Tor Browser: Hili ni toleo la Firefox lililoimarishwa zaidi. Iko taratibu kiutendaji kutokana na ukweli kwamba inamuunganisha mtumiaji na 'server' kadhaa kabla ya kufikia sehemu husika
KUSIKILIZA KILIO CHA MTOTO NI SANAA KATIKA MALEZI

> Mzazi anapaswa kusikiliza kilio cha mtoto wake ili kubaini mahitaji ya mtoto huyo

> Kilio huonyesha jambo linalomkera pia ni lugha na ishara ambayo inaonyesha mchakato wa kujishikamanisha

Zaidi, soma https://jamii.app/KilioMtoto
#JFMalezi
INDONESIA: ACHOMWA SHINGONI NA SAMAKI ALIYERUKA KUTOKA MAJINI

> Muhammad Idul (16) alikumbwa na mkasa huo alipokuwa anavua samaki

> Madaktari walistaajabu kuona mkasa huo, na walihitaji wataalam watano kufanya upasuaji uliotumia saa 1

Zaidi, soma https://jamii.app/SamakiShingoni