JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MTWARA: WAZAZI WALIOGOMA KUPELEKA WATOTO SHULE KUSAKWA

> Wanafunzi 20,400 walitakiwa kujiunga Kidato cha Kwanza lakini 75% hawajaripoti Shule

> Mkuu wa Mkoa amesema, Wazazi waliogoma kupeleka watoto shuleni watachukuliwa hatua za kisheria

Zaidi, soma - https://jamii.app/WazaziElimuMtwara
NEW YORK: JIJI LILILOVUNJA REKODI YA KUWA NA MABILIONEA WENGI

> Lilikuwa Jiji lililokuwa na mabilionea 82, kwa takwimu za mwaka 2017 zilizotolewa na Forbes

> Idadi hiyo imeliweka jiji hilo katika Kitabu cha Guinness cha 2019

Zaidi, soma https://jamii.app/BilioneaMji
BURKINA FASO: BENDERA ZITAPEPEA NUSU MLINGOTI BAADA YA WATU 36 KUUAWA

> Kundi la Magaidi wenye silaha walivamia Vijiji vya Nagraogo na Alamou na kuua watu 36

> Serikali imetangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa kuanzia Januari 22

Zaidi, soma https://jamii.app/MagaidiShambulio
ULINZI WA KIDIGITALI: Je, wajua kuwa ukipiga picha kwa kutumia Kamera ya Simu yako hurekodi na mahali ulipo?

> Geo-tagging: hufanya Kamera yako kuambatanisha sehemu (location) uliyopiga picha wakati ukifanya zoezi hilo

> Hufanya hivi bila ya wewe kujua na inaweza kuwa hatari kwani picha yako itatoa taarifa ya sehemu ulipo kwa watu wenye nia ovu

Kwa elimu zaidi, soma > https://jamii.app/Geo-tagging
ARUSHA: WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA UWINDAJI YA GREEN MILES MBARONI

- Waliokamatwa ni Lazaro Lembrise, Moses Sikange, Mohamed Bembe na Hassan Mahonza

- Wanadaiwa kukaidi agizo la Serikali na kuendelea na kazi katika kitalu walichotakiwa kuondoka

Zaidi, soma https://jamii.app/WafanyakaziGreenMilesMbaroni
MUSEVENI: ILIKUWA MAKOSA MATAIFA YA AFRIKA KUTOISAIDIA LIBYA

- Amesema, Afrika ina uwezo wa kuzuia Mataifa ya Magharibi kuvamia Afrika kiholela

- Ameongeza, ilikuwa makosa Mataifa ya Magharibi kuvamia Libya bila ya Afrika kuzuia kitendo hicho

Zaidi, soma https://jamii.app/Museveni-MataifaMagh
SERIKALI: HATUJAPOKEA WARAKA WOWOTE WA KIDPLOMASIA KUTOKA MAREKANI

- Imesema, haijapokea waraka wowote kuwa Raia wake huenda wakawekewa vikwazo kwenda Marekani

- Imesema, yanayoendelea ni maneno ya mtandaoni na hawawezi kuzungumzia maneno hayo

Zaidi, soma https://jamii.app/TanzaniaWarakaVikwazoUSA
KATIBA YA TANZANIA NA KENYA KUHUSU RAIS KUSHINDWA KUMUDU MAJUKUMU YAKE
-
#KatibaTz Ibara ya 37.-(2) inasema Endapo Baraza la Mawaziri litaona Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au akili, laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji Mkuu athibitishe kwamba Rais hawezi kumudu kazi zake
-
#KatibaKe Ibara ya 144.(1) inasema Mjumbe wa Bunge, akiungwa mkono na robo ya Wabunge wote, anaweza kushinikiza kufanyika kwa uchunguzi wa hali ya kimwili au kiakili ya Rais katika kufanya majukumu yake
-
Hoja hiyo ikiungwa mkono na wajumbe wengi, Spika wa Bunge atatakiwa kumjulisha Jaji Mkuu kuhusu azimio hilo ndani ya siku 2 na ataunda bodi ya matabibu itakayochunguza suala hilo
MEXICO: WATU 95 HUUAWA KILA SIKU

> Mitandao ya Wauzaji wa Madawa ya Kulevya nchini Mexico imekua ikilaumiwa kwa vifo hivyo

> Kufuatia mauaji hayo, Wanaharakati wametoa wito wa kufanyika kwa Matembezi ya Amani Januari 23, 2020

Zaidi, soma https://jamii.app/KufaKilaSiku
JamiiForums kupitia Jukwaa lake la Ajira na Tenda linakupa nafasi mdau wetu kuweza kupata nafasi mbalimbali za Kazi iwe ni Serikali, katika Mashirika ya Ndani au hata ya Kimataifa

- Kujua nafasi mbalimbali za Kazi na Tenda zilizotangazwa Nchini au Nchi za Nje kwa ajili ya Raia wa Tanzania, tembelea Jukwaa hilo, fungua https://jamii.app/JukwaaTendaAjira
JAFO AAHIDI KUWATAJA WAKURUGENZI WAVIVU WANAOSHINDWA KUKUSANYA MAPATO IPASAVYO

> Amesema ameshindwa kuzivumilia Halmashauri zinazotekeleza majukumu kinyume na miongozo ya Serikali

> Amebainisha kuwa kuna Halmashauri zinadaiwa madeni makubwa

Zaidi, soma https://jamii.app/JafoWakurugenzi
ULINZI WA KIDIGITALI: JINSI YA KUONDOA GEO-TAGGING KWENYE SIMU YAKO (ANDROID)

- Nenda kwenye Application ya Kamera > Settings, shuka hadi sehemu ya Geo tags > bofya 'Disable'

- Zima Location, au tumia App ya Geobyebye

Zaidi, soma > https://jamii.app/Geo-tagging
MWANAFUNZI ANAYEDAIWA KUONESHA TATIZO LA MAJI UDOM MBARONI

- Ni Mugaya Tungu anayesoma mwaka wa 2 katika Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)

- Wenzake wanadai walienda Kituoni alikopelekwa wakaambiwa amepewa dhamana ila wamemtafuta na hawajampata bado

Zaidi, soma https://jamii.app/MwanfunziUDOMMbaroni
CHINA: USAFIRI WA UMMA WASITISHWA ILI KUEPUSHA VIRUSI VYA CORONA KUSAMBAA ZAIDI

> Wakazi wa Wuhan wameagizwa wasitoke nje ya Mji. Huduma za usafiri zimesitishwa kuanzia leo

> Virusi hivyo pia vimeripotiwa Korea Kusini, Marekani na Thailand

Zaidi, soma - https://jamii.app/CoronaVirusChina
PWANI: MCHUNGAJI ASHTAKIWA KWA KUMCHOMA MOTO MWANAYE

> Mch. Japhes Manwa anatuhumiwa kumchoma moto mikononi na mgongoni mwanaye wa miaka 7 ambaye ni mlemavu

> Inadaiwa Mchungaji amefanya hivyo kwasababu hampendi mtoto huyo

Zaidi, soma - https://jamii.app/UkatiliPwani
Lengo Kuu la Mkakati huo ni Kupunguza Rushwa Nchini kwa kutumia mbinu za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa kuweka mkazo katika Sekta zenye Mazingira shawishi ya Rushwa

- Mkakati huu utajikita katika kushughulikia Sekta za Manunuzi ya Umma, Ukusanyajiwa Mapato, Uvunaji na Matumizi ya Maliasili, Madini, Nishati, Mafuta na Gesi, Utawala, Vyombo vya Utoaji wa Haki na Shughuli za Vyama vya Siasa

#KemeaRushwa
TAKUKURU YAOKOA TSH. BILIONI 4 KWENYE USHIRIKA

> Vyama vilivyofanyiwa ukaguzi ni 4,413 na kugundua viashiria vya ubadhirifu na rushwa ya Tsh. bilioni 124

> Kati ya Vyama vya Ushirika 11,410 vilivyosajiliwa, Vyama 2,103 havijulikani vilipo

Zaidi, soma https://jamii.app/TakukuruUshirika
POLISI WAKANA KUMKAMATA MWANAFUNZI ANAYEDAIWA KUPIGA PICHA ZA UKOSEFU WA MAJI UDOM

- Kamanda wa Polisi Gilles Muroto amesema hana taarifa za kukamatwa kwa Mugaya Tungu

- Makamu wa Chuo, ameomba radhi kutokana na tatizo la maji chuoni hapo

Soma https://jamii.app/MwanfunziUDOMMbaroni
#JFLeo
KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI AJIUZULU

- Rais Magufuli amesema Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu amemuandikia barua ya kujiuzulu na amemkubalia

- Rais ameyasema hayo akiwa anazindua Nyumba za Askari Magereza zilizopo Ukonga Jijini Dar

Zaidi, soma https://jamii.app/UzinduziJengoMagereza
Baadhi ya maneno aliyoyasema Rais Magufuli leo Januari 23 wakati wa Uzinduzi wa Nyumba za Maafisa na Maaskari wa Jeshi la Magereza zilizopo Ukonga Jijini Dar

Zaidi, soma https://jamii.app/UzinduziJengoMagereza