JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS WA BURUNDI KUPATA TSH. BILIONI 1.15 AKISTAAFU

> Bunge limepitisha Sheria inatakayompa Rais kitita cha Tsh. Bilioni 1.15 atakapostaafu

> Na Rais akistaafu atachukuliwa kwa Hadhi ya Makamu wa Rais kwa kipindi cha miaka 7

Zaidi, soma https://jamii.app/BurundiNkurunzinza
KANGI LUGOLA ANG’OLEWA KWENYE NAFASI YA UWAZIRI

- Lugola, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, amesema Rais ndiye aliyemteua na sasa ameona ampumzishe

- Asema, ni jambo la faraja na hatua nzuri inayolenga kujenga safu ya Serikali ya Awamu ya 5

Zaidi, soma https://jamii.app/LugolaAondolewaUwaziri
ANGOLA: MWANAMKE TAJIRI ZAIDI AFRIKA AFUNGULIWA MASHTAKA YA ULAGHAI

> Isabel dos Santos anashtakiwa kwa ulaghai, ufujaji fedha, usimamizi mbaya wa Ofisi, kughushi stakabadhi pamoja na uhalifu mwingine wa kiuchumi

> Isabel dos Santos pia ni mtoto wa aliyewahikuwa Rais wa Angola (mwaka 1979-2017), Jose Eduardo dos Santos

Zaidi, soma - https://jamii.app/IsabelUlaghaiAngola
UGANDA: RAIA WA SUDAN AKAMATWA NA KARATASI ZINAZOBADILIKA NA KUWA DOLA BANDIA

> Duach Toang alikamatwa wakati anavuka mpaka wa Malaba, akitokea nchini Kenya

> Makaratasi hayo yanabadilika kuwa Dola bandia yanapomwagiwa kemikali

Zaidi, soma - https://jamii.app/DolaBandia-UG
WAMAREKANI WATATU WAFARIKI KATIKA HARAKATI ZA KUZIMA MOTO AUSTRALIA

> Ni baada ya ndege yao kuanguka wakati wanasaidia kuzima moto

> Waliofariki tangu kuanza kwa moto huo Septemba 2019 wamefikia 38

Zaidi, soma - https://jamii.app/AjaliVifo-AUS
RAIS MAGUFULI AMEFANYA UTEUZI WA MABALOZI WATATU

- Amewateua Meja Jenerali Jacob Kingu, Kamishina Jenerali wa Magereza Faustine Kasike na Dkt. John Steven Simbachawene

- Mabalozi hao wataapishwa na vituo vyao vya kazi vitatangazwa baadaye
ULINZI WA KIDIGITALI: JINSI YA KUJUA KAMA TOVUTI ULIYOTEMBELEA NI SALAMA

> Angalia kama tovuti uliyoifungua au kuitembelea ina alama ya kufuli kwenye 'URL' yake. Alama hii hutokea kabla ya 'link' iliyofungua ukurasa huo

> Tazama mfano pichani

#UlinziWaKidigitali
KAMISHNA WA JESHI LA ZIMAMOTO ANG'OLEWA

- Rais Magufuli ametengua Uteuzi wa Kamishna Jenerali Thobias Andengenye na nafasi yake itajazwa hapo baadaye

- Mapema leo, Rais alisema Kamishna huyo amehusika kusaini mkataba wa 'ajabu' wa thamani ya takriban Tsh. Trilioni 1.042
KATIBA: JAMHURI YA MUUNGANO
-
#KatibaTz - 3.-(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya Kidemokrasia na ya Kjamaa, yenye kufuata mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa
-
2 (1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na sehemu ya Bahari inayopakana nayo
-
Rasimu ya Jaji Warioba: 1 (1) Jamhuri ya Muungano ni Shirikisho lenye mamlaka kamili iliyotokana na Muungano wa Nchi 2
-
(2) Ni Shirikisho la Kidemokrasia linalofuata mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa, usawa wa Binadamu, kujitegemea, utawala wa Sheria na kuheshimu Haki za Binadamu
MICHEZO: Mchezaji wa Chelsea, Victor Moses amejiunga Inter Milan kwa mkopo ambapo anaenda kuungana na Kocha wa Zamani wa Chelsea, Antonio Conte

- Anakuwa mchezaji wa hivi karibuni kujiunga Inter akitokea Ligi Kuu England baada ya Romelu Lukaku, Ashley Young na Alexis Sanchez
SABABU ZA MIKOA KUFANYA/KUTOFANYA VIZURI KATIKA MITIHANI DARASA LA SABA

> Nafasi hafifu ya wazazi kuwahamasisha watoto, Umbali mrefu kwenda shuleni

> Changamoto ya kimenejimenti na kukosa hamasa na mbinu za ziada katika kuimarisha ufundishaji

Zaidi, soma https://jamii.app/HakiElimuSababu
ULINZI WA KIDIGITALI: JINSI YA KUJUA KAMA TOVUTI ULIYOTEMBELEA NI SALAMA

> Hakikisha tovuti uliyoingia inaanza na HTTPS badala ya HTTP

> HTTPS ni 'Hypertext Transfer Protocol Secure' neno la msingi hapo ni Secure ikimaanisha usalama

> Tazama mfano pichani
ULINZI WA KIDIGITALI: JINSI YA KUJUA KAMA TOVUTI ULIYOTEMBELEA NI SALAMA

> Tovuti hiyo itakuwa imeambatanisha Sera ya Faragha (Privacy Policy) kwa ajili ya watembeleaji

> Sera ya Faragha hueleza ni taarifa gani za mtembeleaji zitakusanywa na zitatumikaje
SYRIA: WANAJESHI 40 WAUAWA NA WAASI

> Waasi walitumia milipuko ya kutegwa ndani ya magari na silaha nzito nzito katika mashambulizi hayo

> Jeshi la Serikali limepeleka Vikosi vya Msaada katika jimbo hilo

Zaidi, soma zaidi https://jamii.app/SyriaWanajeshi
MBINGA, RUVUMA: KIJANA HUNYWA MAJI LITA 100 KWA SAA MBILI, TANGU APIGWE NA RADI

> Erick Msuha ana matatizo ya kiafya tangu apigwe na radi mwaka 1993 hivyo anatakiwa kufanyiwa Upasuaji

> Baba wa Kijana huyo ameomba msaada kutoka kwa Wasamaria wema kwani wameuza kila walichokuwa nacho kumsaidia bila mafanikio

Zaidi, soma zaidi https://jamii.app/MajiLita
RIPOTI: TANZANIA YAZIZIDI KENYA NA UGANDA KATIKA KUTOKOMEZA RUSHWA

> Tanzania imepata alama 37 kati ya alama 100 kwa Viashiria vya Kutokomeza Rushwa Duniani

> Kenya na Uganda zimepata alama 28. Nyingine ni Somalia (9), Sudan Kusini (12) na Rwanda (53)

Zaidi, soma - https://jamii.app/RipotiRushwaTZ
MWAKYEMBE: 2021 MWISHO WA WANAHABARI WASIO NA ELIMU KUANZIA STASHAHADA

- Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema, Desemba mwaka 2021 ndio mwisho kwa mujibu wa Sheria ya Huduma ya habari ya Mwaka 2016

Zaidi, soma https://jamii.app/ElimuWanahabari
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM) ambaye pia ni Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema hayo leo wakati akiongoza Kikao cha Viongozi na Watendaji wa Chama na Jumuiya zake za Mikoa na Wilaya
DAR: WATANZANIA 30 WALIOZAMIA AFRIKA KUSINI WAHUKUMIWA

> Watuhumiwa hao walirudishwa nchini na kufikishwa Mahakama ya Kisutu

> 16 wahukumiwa miezi 6 jela au faini ya Tsh. 300,000. Wengine 14 wamehukumiwa miezi 18 jela au faini ya Tsh. 50,000

Zaidi, soma - https://jamii.app/WazamiajiAfrikaKusini