JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KIRUSI KUTOKA CHINA CHAHOFIWA KUSAMBAA DUNIANI

- Mamlaka za Afya Duniani kote zina wasiwasi kuwa Kirusi kiitwacho Corona kinaweza kusambaa Duniani kote

- Hadi sasa watu watatu wamefariki na wengine wanne wamethibitishwa kuwa na kirusi hicho

Zaidi, soma - https://jamii.app/KirusiCoronaChina
ULINZI WA KIDIGITALI: Je, unajua kama simu yako haina Password (Nywila), unaweza kulipa faini ya milioni 5, kifungo cha mwaka 1 jela au vyote kwa pamoja?

> Kanuni za Maudhui ya Mtandao Kifungu cha 10(2), kila Mtu analazimika kuweka Nywila kwenye kifaa chake (Simu)

> Adhabu kwa kosa hili imeelezwa katika kipengele cha 18 na cha mwisho katika Kanuni hizo zilizosainiwa mwaka 2018

Soma > https://jamii.app/UlazimaNywila
MFAHAMU ANAYESHIKILIA REKODI YA KUCHA NDEFU DUNIANI

> Ayana Williams anashikilia Rekodi Hii baada ya kukaa miaka 23 bila kukata kucha zake na kucha yake ndefu zaidi ina urefu wa Sentimita 68

> Hata kuvua nguo yake ni kazi ngumu kutokana na urefu wa kucha zake, amekiri hilo

Zaidi, soma https://jamii.app/KuchaNdefu
IRAN YABADILI MAWAZO YA KUTUMA 'BLACK BOX' UKRAINE

- Awali, ilisema itatuma ili Maafisa wa Marekani, Canada na Ufaransa wakafanyie kazi

- Siku moja baadaye, imesema bado haijaamua kutuma na sasa wanajaribu kupata Data zilizomo ndani

Zaidi, soma https://jamii.app/IranUkraine-BlackBox
DODOMA: MABASI YAPIGWA MARUFUKU KURUHUSU ABIRIA KUJISAIDIA HOVYO

> Hairuhusiwi kujisaidia sehemu isiyo Rasmi na Faini ya kosa hilo ni 200,000 au kifungo cha miezi 6 au vyote kwa pamoja

> Kitendo hicho kimetajwa kuchangia kuchafua mazingira

Zaidi, soma - https://jamii.app/MabasiUsafiMazingira
AFISA ELIMU MBARONI KWA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA ZA MADAWATI

> Stephano Ndabazi anatuhumiwa kuiba Tsh. 24,334,920 Aprili, mwaka 2016

> Alitenda kosa hilo akiwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mpwayungu Wilaya ya Chamwino, Mkoani Dodoma

Zaidi, soma zaidi https://jamii.app/AfisaWizi
SERIKALI KUJENGA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA ZIWA WILAYANI CHATO

> Sababu za kujenga hospitali hiyo ni kuwa, tafiti zinaonesha kuna wagonjwa wengi Kanda ya Ziwa, pia Mikoa ya Kanda ya Ziwa ina watu zaidi milioni 15

Zaidi, soma zaidi https://jamii.app/NeemaChato
EDINSON CAVANI AWASILISHA MAOMBI YA UHAMISHO

- Mkurugenzi wa Michezo wa Paris Saint-Germain, Leonardo amesema Mshambuliaji huyo ameomba kuondoka mwezi huu

- Cavani (33), anahusishwa kutakiwa katika klabu za Atletico Madrid, Manchester United na Tottenham Hotspurs
MAHAKAMA YAWATAKA WADHAMINI WAMPELEKE LISSU KABLA HAIJATOA MAAMUZI MENGINE

> Wakili wa Serikali, amesema jukumu la mdhamini ni kuhakikisha mshtakiwa anafika Mahakamani

> Mdhamini alisema wameandika barua kwa Freeman Mbowe ili Lissu arejee

Zaidi, soma https://jamii.app/WadhaminiLissu
KATIBA: UTEUZI WA NAIBU SPIKA BUNGENI

> Ibara ya 85-(1): Kutakuwa na Naibu Spika ambaye atachaguliwa na wajumbe kutoka miongoni mwa Wabunge

> (2) Waziri, Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine itakayotajwa na Sheria ya Bunge hataweza kuwa Naibu wa Spika

#Katiba
KILIMO CHA MAPARACHICHI CHAMFANYA KIJANA MWENYE ELIMU YA DARASA LA SABA KUSHIKA MAMILIONI

> Steven Mlimbila ameajiri zaidi ya vijana 40

> Mwaka jana alikuwa Mkulima Bora katika maonyesho ya Nanenane kwa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini

> Mafanikio yake kiuchumi yamekuwa gumzo kwa vijana wengi wakiwamo Madereva Bodaboda ambao wamedhamiria kuingia shambani

Zaidi, tembelea https://jamii.app/MaparachichiKilimo
MALAYSIA KURUDISHA MAKONTENA 110 YA TAKA KATIKA NCHI HUSIKA

> Waziri Yeo Bee Yin amesema wanaotaka kuifanya nchi hiyo dampo waendelee kuota

> Nchi hiyo ipo katika harakati za kuachana na matumizi ya plastiki ili kutunza mazingira

Zaidi, soma - https://jamii.app/TakaMazingiraMalaysia
MWANZA: WATUMISHI WA TANESA WANYANG'ANYWA MAJENGO

- TAKUKURU imechukua majengo 4 yenye thamani ya Tsh. milioni 420 yaliyojengwa na Uholanzi na kukabidhiwa Serikali

- Imesema, baada ya mradi kuisha Watumishi walijimilikisha kinyemela majengo hayo

Zaidi, soma https://jamii.app/TAKUKURU-MajengoTANESA
ZAIDI YA WATOTO MILIONI 3 HAWAHUDHURII MASOMO KUTOKANA NA UGUMU WA MAISHA

> Sudan imeorodheshwa kama mojawapo ya mataifa masikini zaidi duniani

> Watoto hawawezi kuendelea na masomo kutokana na hali ngumu ya maisha

Zaidi, soma https://jamii.app/SudanAjiraWatoto
ELIMU KATIBA: SEKRETARIATI YA BUNGE

- Ibara ya 88.-(1) inasema Kutakuwa na Sekretariati ya Bunge itakayokuwa na nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali kwa idadi atakayoagiza Rais

- (2) Sekretariati ya Bunge itakuwa na watumishi kwa idadi na ngazi za utumishi itakavyoamuliwa mara kwa mara na Tume ya Utumishi inayohusika baada ya kushauriana na Katibu wa Bunge
IRAQ: KIONGOZI WA ISLAMIC STATE AKAMATWA

> Abu Abdul Bari amekamatwa na kubebwa na Lori kutokana na uzito wake wa kilo 250. Iraq imethibitisha kukamatwa kwa Kiongozi huyo

> Bari ni Mufti wa Kundi la IS na Mtaalamu wa Sheria za Dini

Zaidi, soma zaidi https://jamii.app/KiongoziIS
ULINZI WA KIDIGITALI: JINSI YA KUWA SALAMA UNAPOKUWA MTANDAONI

> Usifungue Link au Email kutoka kwa mtu usiyemfahamu

> Wadukuzi huambatanisha na jumbe za kuvutia. Endapo utafungua kiunganishi hicho unamruhusu mdukuzi aingilie mawasiliano yako

> Tumia Password (Nywila) iliyo Bora Zaidi

Soma > https://jamii.app/SafeBrowsing
JamiiForums kupitia Jukwaa lake la Ajira na Tenda linakupa nafasi mdau wetu kuweza kupata nafasi mbalimbali za Kazi iwe ni Serikali, katika Mashirika ya Ndani au hata ya Kimataifa

- Kujua nafasi mbalimbali za Kazi na Tenda zilizotangazwa Nchini au Nchi za Nje kwa ajili ya Raia wa Tanzania, tembelea Jukwaa hilo, fungua https://jamii.app/JukwaaTendaAjira
RSF YATAKA UCHUNGUZI WA KINA KUHUSU MAUAJI YA WAANDISHI 3

> REPORTERS WITHOUT BORDERS (RSF) yadai uhakiki wa ushahidi uliotolewa katika uchunguzi wa mwanzo

> Waandishi watatu wa Urusi waliuawa na watu wasiojulikana Jamhuri ya Afrika ya Kati

Zaidi, soma https://jamii.app/RSFWaandishi
MICHEZO: Klabu ya Aston Villa @AVFCOfficial ya nchini England yatangaza rasmi kumsajili Mbwana Samatta kutoka Klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji

> Samatta amesaini kandarasi kuitumikia Klabu hiyo kwa muda wa miaka 4 na nusu

#JFSports #KaribuSamatta