JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UGANDA: JELA MIAKA 13 KWA KUMNAJISI NA KUMPA MIMBA MWANAE WA MIAKA 12

> Hii ni baada ya Mtuhimiwa kukiri makosa yake kwa Jaji

> Kuongea na Jaji ni hiyari kama ilivyoidhinishwa kwa muda Tanzania kuongea na DPP kuhusu Makosa ya Uhujumu Uchumi

Soma https://jamii.app/MimbaMwanaeUmri12
#JFLeo
LESOTHO: WAZIRI MKUU ATANGAZA KUJIUZULU KUFUATIA TUHUMA ZA MAUAJI YA ALIYEKUWA MKEWE

> Thomas Thabane hajasema sababu za kujiuzulu na hajazungumzia tuhuma zinazomkabili

> Mkewe mpya, Maesaiah Thabane anatafutwa na Polisi kwa mahojiano

Soma - https://jamii.app/WaziriKujiuzuluLesotho
BASHIRU AANZA ZIARA MKOANI KIGOMA

> Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally ameanza Ziara ya Siku Tatu

> Aidha, barua ya Polisi yenye Kumbukumbu Namba KIG/A.24/60/VOL.1/114 ilimzuia Zitto Kabwe kufanya Mkutano wa Hadhara Jimboni mwake

Soma https://jamii.app/BahiruKigomaZitto
BARRICK KUPUNGUZA WAFANYAKAZI 110 NORTH MARA

> Itafanya hivyo ili kumudu gharama za uendeshaji

> Mchakato huo utazingatia Sheria zote za Nchi kuhakikisha kila anayeguswa anapata Stahiki zake

Soma https://jamii.app/BarrickKupunguza
MTANZANIA APATA MABILIONI KWA KUUZA MFUMO WA KUNUNUA GESI KADRI UNAVYOTUMIA

> Andron Mendes ameiuzia Kampuni ya Uingereza, 'Circle Gas' mfumo huo kwa Tsh. bilioni 57.6

> Mradi huo umeshaunganisha Wakazi zaidi ya 1430 wa Dar es Salaam

Soma https://jamii.app/MtanzaniaGesiBilioni
HAKI YA MWANAMKE KUTAFUTA ELIMU

- Chama cha Wanasheria wa Kike Zanzibar (ZAFELA) kimeandaa jarida la 'Haki za Mwanamke kwa Mujibu wa Qur'an na Sunnah za Mtume (S.A.W)'

- Kimesema Uislamu umetoa umuhimu Mwanaume au Mwanamke kutafuta elimu

Zaidi, soma https://jamii.app/UsawaElimuDiniKiislamu
TANZANIA vs RWANDA: UTEUZI WA WAZIRI MKUU

#KatibaTanzania, Ibara-51 (2): Mapema iwezekanavyo, ndani ya siku 14 baada ya kushika madaraka, Rais atamteua Waziri Mkuu

#KatibaRwanda, Ibara-116: Waziri Mkuu anateuliwa na Rais ndani ya siku 15 baada ya Rais kushika madaraka

#Katiba
IRAN: NCHI ZILIZOPOTEZA RAIA KATIKA AJALI YA NDEGE ZADAI FIDIA

> Nchi hizo ni Canada, Uingereza, Ukraine, Sweden, Uholanzi na Afghanistan

> Mataifa hayo yameitaka Iran kuwajibika, kuanzisha uchunguzi na kulipa fidia

Soma - https://jamii.app/FidiaAjaliIran
TANZANIA vs RWANDA: KAZI ZA WAZIRI MKUU

#KatibaTanzania, Ibara-52 (3): Atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa mambo ambayo Rais ataagiza yatekelezwe

#KatibaRwanda, Ibara-119: Kuongoza Utendaji wa Serikali kulingana na miongozo ya Rais na kuhakiki utekelezaji wa Sheria

#Katiba
KENYA: RADI YAUA WANAFUNZI WATATU NA KUJERUHI WENGINE 53

> Ni baada ya radi kupiga katika Chumba cha Darasa walichokuwa wanatumia

> Waliojeruhiwa wamepelekwa Hospitali kwa ajili ya matibabu

Soma - https://jamii.app/RadiVifoKenya
NJOMBE: VIFO VYA WAJAWAZITO NA WATOTO VYAPUNGUA

> Vifo vya kina mama vimepungua toka 250 hadi 94 na vya watoto vimepungua toka 51 hadi 2

> Pia, kuboresha huduma za VVU Mkoa utaongeza Vituo toka 112 hadi 130

> Dkt. Ndugulile ametoa pongezi

Soma - https://jamii.app/VifoWajawazitoIringa
RUKWA: WANAFUNZI KUPIGA KURA ZA SIRI KUWAFICHUA WALIMU WENYE MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA WANAFUNZI

> Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amesema, kumekuwa na ongezeko la Walimu wa kiume katika Shule za Msingi na Sekondari kujihusisha katika mapenzi na wanafunzi na kuwasababishia ujauzito

> Takwimu kwa kipindi cha 2017 hadi 2019 ni mimba 722 zimeripotiwa kati ya hizo, 171 walikuwa Shule za Msingi na 551 walikuwa Sekondari

Soma - https://jamii.app/KuraWanafunziWakware
DANGOTE AONGOZA KWA UTAJIRI AFRIKA, MO DEWJI ASHIKA NAFASI YA 16

> Ripoti ya Forbes 2020 imemtaja Dangote kuwa tajiri namba moja
Afrika

> Utajiri wa Mo washuka kwa Trilioni 3.69. Ameshuka nafasi mbili ikilinganishwa na Ripoti ya 2019

Soma - https://jamii.app/ForbesUtajiriAfrika
HOJA: VIFAA VYA KIELETRONIKI VIMEWAPOTEZEA WATOTO UWEZO WA KUANDIKA VIZURI

> Mdau kutoka JamiiForums.com anasema, matumizi ya Kopyuta, Simujanja, 'Tablets' na vifaa kama hivyo yamepunguza uwezo wa vijana na watoto kuwa na mwandiko mzuri au hata kujua kuandika kwa mkono

> Anashauri Mtoto wako akifika miaka 2, mnunulie mkasi wa plastiki, akiweza kushika mkasi na kuutumia hatopata shida kushika kalamu

> Akifika miaka 3.5 - 4 anza kumpa maneno ya kurudia kuandika akianza na jina lake na mahali anapoishi

Tembelea - https://jamii.app/GadgetsEffectsChildren
#JFMalezi
FAHAMU KUHUSU TIBA YA KUWEKEWA BETRI KWENYE MOYO

> Betri ya Moyo ambayo kitabibu huitwa ‘Pacemaker’ ni kifaa kilichobuniwa ili kumsaidia mtu ambaye Moyo wake unashindwa kuzalisha nguvu ya kusukuma damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili

> Inaelezwa kuwa, binadamu wa kwanza kunufaika nacho, aliwekewa kifaa hicho mwaka 1960 na tangu kuanzishwa kwa huduma hii, watu zaidi ya milioni 3 duniani huwekewa kifaa hicho kila mwaka

> Miongoni mwa watu maarufu waliopandikizwa mashine hiyo ni Kocha aliyewahi kuifundisha Manchester United ya Uingereza, Sir Alex Ferguson aliyewekewa kifaa hicho mwaka 2003

Fahamu zaidi - https://jamii.app/KnowledgePacemaker
#JFAfya
USAJILI WA LAINI ZA SIMU: WADAU WAHOJI MAMBO KADHAA

- Mdau wa JamiiForums anahoji uko wapi umakini wa zoezi hilo ikiwa kuna vijana wanaopita mtaani wakisajili laini wanaoweza kutumiwa vibaya

- Kwa kuwa Mtu anaweza kusajili laini 5 za mtandao mmoja anahoji itakuwaje Mtu akisajili laini tofauti na kumpa ndugu yake?

Zaidi, tembelea https://jamii.app/MaoniUsajiliLaini
ESWATINI: KESI YA KWANZA YA UBAKAJI NDANI YA NDOA

> Nhlanhla Dlamini ni wa kwanza kushtakiwa kwa ubakaji kwa kufanya tendo la ndoa na mkewe bila ya idhini yake

> Ni kwa kutumia Sheria ya Makosa ya Kijinsia na Vurugu za Nyumbani ya mwaka 2018

Soma https://jamii.app/KesiNdoaUbakaji
ULINZI WA KIDIGITALI: Jamii Forums inatoa Elimu ya Mtandaoni kuhusu Ulinzi na Usalama wa Vifaa na Mifumo ya Kidigitali kutokana uwepo wa matukio ya kila siku yanayohusisha mashambulizi na kuingiliwa kwa Vifaa vya Kidigitali na Mifumo yake

> Hii ni kutokana na Maendeleo ya Teknolojia kubadili namna ya uendeshaji wa mambo katika jamii, matumizi ya Vifaa vya Kidigitali na Mtandao wa Intaneti yameongezeka kwa kasi

> Hata hivyo, ziko hatari kadha wa kadha zinazowanyemelea watumiaji wa Mifumo ya Kidigitali

> Baadhi ya hatari hizo ni pamoja na shambulizi la Nywila, shambulizi la Barua Pepe, shambulizi la 'DDoS', shambulizi la Virusi, Udukuzi, Wizi wa Fedha n.k
ULINZI WA KIDIGITALI: Ulinzi huu unahusisha elimu ya kulinda vifaa(simu, kompyuta n.k), mifumo na utambulisho wa Mtu dhidi ya kuingiliwa na Mtu asiyehitajika

Elimu ya Ulinzi wa Kidigitali husaidia sana kutunza faragha ya mtumiaji

> Swali la kujiuliza: Je, unazijua njia unazoweza kuzitumia kujilinda dhidi ya Mashambulizi ya Kimtandao?

> Baadhi ya njia hizo ni kuweka nywila(Password) kwenye vifaa vyako, hakikisha vifaa vyako vyako pamoja na Mifumo yake na Programu Tumishi (Application) ziko katika sasa 'Updated'

> Nyingine ni kuhakikisha unatumia Programu zilizothibishwa kuwa ni salama, hakikisha unatumia 'Anti-Virus' iliyoidhinishwa, epuka kufungua Kiunganishi (Link) usichokitambua

> Fanya 'Setting' za Kiusalama kwenye Barua Pepe, Simu na Kompyuta yako
ULINZI WA KIDIGITALI: JIFUNZE KUHUSU NYWILA (PASSWORD)

> Nywila ni mfano wa Ufunguo wa Kidigitali unaotumika kufungua milango ya akaunti na taarifa zilizohifadhiwa katika Mifumo na Programu za Kidigitali

> Nywila hupaswa kuwa Siri ya Mmliki au Wamiliki kwasababu nywila ni ulinzi namba 1 wa taarifa na faragha za Mtumiaji wa Vifaa na Mifumo ya Kidigitali

> Nywila ina umuhimu mkubwa lakini inapaswa kutengenezwa vizuri ili isiwe rahisi Kudhaniwa, Kuhisiwa na Kukisiwa

> Nywila Bora huundwa kwa kutumia, Herufi Kubwa na Ndogo, Namba, na Alama na ni lazima Iwe Ndefu (herufi 16) na ya Kipekee