JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ULINZI WA KIDIGITALI: JIFUNZE KUHUSU NYWILA (PASSWORD)

Ili kuilinda Password yako isiweze kudukuliwa unapaswa kuzingatia mambo yafuatayo;

> Usitumie Nywila (Password) moja kwenye kurasa zako zote za Mitandao ya Kijamii. Hakikisha kila mtandao unatumia Password yake

> Hakikisha Nywila yako ina jumla ya herufi/alama zisizopungua 16 au na zaidi (Mfano: M1m1$%678abc@£+#)

> Usitumie jina la ndugu, Mtoto au Mzazi wako au mfugo wako(mfano Mbwa, Paka etc), mwaka wa kuzaliwa au namba ya simu kama nywila yako. Ni rahisi Mtu kuhisi na kukufanyia udukuzi

> Usitumie maneno ya kwenye Kamusi kama nywila yako. Na usiruhusu kivinjari chako (Web browsers -Chrome, Opera, Firefox, Brave n.k) kuhifadhi nywila yako
MTU AKIOMBA RUSHWA YA NGONO ANAKUWA AMETENDA DHAMBI NGAPI?

> Anakuwa amezini, amesema uongo, ameiba, amesaliti, amepoka #HakiYaMtu

> Anakuwa amevunja #SheriaZaNchi na kumuonea mnyonge

#KemeaRushwa
ULINZI WA KIDIGITALI: JIFUNZE KUHUSU NYWILA (PASSWORD)

> Nywila dhaifu unahusisha Jina la Mmiliki wa Akaunti, mfano: henrik19. Unatumia herufi zilizo mtiririko kama vile ABCDEFG au QWERTY ambazo ziko kwenye 'Keyboard' ya Kompyuta

> Inahusisha tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa, au namba nyingine kama za kitambulisho, mtihani, bima ya afya au pasipoti

> Usihifadhi nywila yako kwa kuandika kwenye karatasi, hii itamrahisishia mdukuzi endapo ataipata karatasi hiyo

> Mambo mengine ya kuzingatia, ni kubadili nywila yako kila baada ya miezi 3
MAKONDA: ASIYE NA NAMBA WALA KITAMBULISHO CHA TAIFA AMEENDEKEZA UMBEA

- RC Paul Makonda amedai Wananchi wa Mkoa wa Dar ambao hadi jana hawakuwa na Namba wala Kitambulisho cha Taifa waliendekeza zaidi umbea kuliko kufuatilia mambo ya msingi

Zaidi, soma https://jamii.app/MakondaKitambulishoUmbea
SHERIA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA NA. 11 MWAKA 2007

- Kifungu kinaeleza, Mtu ambaye kwa udanganyifu atajifanya Afisa wa TAKUKURU au ana Ofisi na kufanya chochote kuhusiana na Kazi za Afisa huyo atakuwa ametenda Kosa

- Atawajibika kwa kupigwa faini isiyozidi Tsh. Milioni 2 au kifungo kisichozidi mwaka mwaka au vyote

#KemeaRushwa
OLE SABAYA AAGIZA KUKAMATWA WAMILIKI WA MABASI KWA KUHUJUMU MIUNDOMBINU YA RELI

> Wanadaiwa kuunda makundi ya Watu na kuharibu reli ya Dar-Moshi ili kuathiri usafiri huo

> Waliotakiwa kuripoti Polisi ni Clemence Mbowe na Rodrick Uronu

Zaidi, soma https://jamii.app/SabayaUhujumuReli
WAZIRI MKUU AZUIA SUKARI KUAGIZWA KUTOKA NJE YA NCHI

- Kassim Majaliwa amezuia hadi sukari inayozalishwa na Kiwanda cha Zanzibar kilichopo Mahonda iishe

- Amesema, haiwezekani kiwanda hicho kinachozalisha tani 6,000 kwa mwaka kikakosa wateja

Zaidi, soma https://jamii.app/SukariKutojaNjeMarufuku
KENYA: WATANO WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUTAKA KUFANYA SHAMBULIO LA KIGAIDI

> Ni wanawake wawili na wanaume watatu, Raia wa Marekani, Kenya na Somalia

> Walitaka kushambulia Klabu moja iliyopo Barabara ya Kiambu

Zaidi, soma - https://jamii.app/UgaidiPolisiNairobi
SERIKALI KUTUMIA BUSARA KATIKA UFUNGAJI WA LAINI ZISIZOSAJILIWA

- Itawasaidia walioshindwa kusajili kwa kukosa Kitambulisho cha Taifa au Namba licha ya kuanza mchakato

- Imesema, wale wenye vitambulisho na hawajasajili, laini zao zitafungwa

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikaliHekimaKufungaLaini
TANGA: POLISI WAZUIA MSAFARA WA PROF. LIPUMBA

- Msafara wa Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba umezuliwa na Polisi Wilayani Mkinga

- Polisi hao wamedai hawana Taarifa za Msafara wa Lipumba aliyeenda Mkoani humo kwa Ziara ya Kikazi

Zaidi, soma https://jamii.app/TangaZiaraLipumba
YEMEN: WANAJESHI 83 WAUAWA NA 148 KUJERUHIWA

> Mashambulizi hayo yanafuatia miezi kadhaa ya utulivu kiasi

> Yemen inakabiliwa na vita kati ya Waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran, na Majeshi ya Serikali

Zaidi, soma https://jamii.app/YemenWanajeshi
KIRUSI KUTOKA CHINA CHAHOFIWA KUSAMBAA DUNIANI

- Mamlaka za Afya Duniani kote zina wasiwasi kuwa Kirusi kiitwacho Corona kinaweza kusambaa Duniani kote

- Hadi sasa watu watatu wamefariki na wengine wanne wamethibitishwa kuwa na kirusi hicho

Zaidi, soma - https://jamii.app/KirusiCoronaChina
ULINZI WA KIDIGITALI: Je, unajua kama simu yako haina Password (Nywila), unaweza kulipa faini ya milioni 5, kifungo cha mwaka 1 jela au vyote kwa pamoja?

> Kanuni za Maudhui ya Mtandao Kifungu cha 10(2), kila Mtu analazimika kuweka Nywila kwenye kifaa chake (Simu)

> Adhabu kwa kosa hili imeelezwa katika kipengele cha 18 na cha mwisho katika Kanuni hizo zilizosainiwa mwaka 2018

Soma > https://jamii.app/UlazimaNywila
MFAHAMU ANAYESHIKILIA REKODI YA KUCHA NDEFU DUNIANI

> Ayana Williams anashikilia Rekodi Hii baada ya kukaa miaka 23 bila kukata kucha zake na kucha yake ndefu zaidi ina urefu wa Sentimita 68

> Hata kuvua nguo yake ni kazi ngumu kutokana na urefu wa kucha zake, amekiri hilo

Zaidi, soma https://jamii.app/KuchaNdefu
IRAN YABADILI MAWAZO YA KUTUMA 'BLACK BOX' UKRAINE

- Awali, ilisema itatuma ili Maafisa wa Marekani, Canada na Ufaransa wakafanyie kazi

- Siku moja baadaye, imesema bado haijaamua kutuma na sasa wanajaribu kupata Data zilizomo ndani

Zaidi, soma https://jamii.app/IranUkraine-BlackBox
DODOMA: MABASI YAPIGWA MARUFUKU KURUHUSU ABIRIA KUJISAIDIA HOVYO

> Hairuhusiwi kujisaidia sehemu isiyo Rasmi na Faini ya kosa hilo ni 200,000 au kifungo cha miezi 6 au vyote kwa pamoja

> Kitendo hicho kimetajwa kuchangia kuchafua mazingira

Zaidi, soma - https://jamii.app/MabasiUsafiMazingira
AFISA ELIMU MBARONI KWA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA ZA MADAWATI

> Stephano Ndabazi anatuhumiwa kuiba Tsh. 24,334,920 Aprili, mwaka 2016

> Alitenda kosa hilo akiwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mpwayungu Wilaya ya Chamwino, Mkoani Dodoma

Zaidi, soma zaidi https://jamii.app/AfisaWizi
SERIKALI KUJENGA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA ZIWA WILAYANI CHATO

> Sababu za kujenga hospitali hiyo ni kuwa, tafiti zinaonesha kuna wagonjwa wengi Kanda ya Ziwa, pia Mikoa ya Kanda ya Ziwa ina watu zaidi milioni 15

Zaidi, soma zaidi https://jamii.app/NeemaChato
EDINSON CAVANI AWASILISHA MAOMBI YA UHAMISHO

- Mkurugenzi wa Michezo wa Paris Saint-Germain, Leonardo amesema Mshambuliaji huyo ameomba kuondoka mwezi huu

- Cavani (33), anahusishwa kutakiwa katika klabu za Atletico Madrid, Manchester United na Tottenham Hotspurs
MAHAKAMA YAWATAKA WADHAMINI WAMPELEKE LISSU KABLA HAIJATOA MAAMUZI MENGINE

> Wakili wa Serikali, amesema jukumu la mdhamini ni kuhakikisha mshtakiwa anafika Mahakamani

> Mdhamini alisema wameandika barua kwa Freeman Mbowe ili Lissu arejee

Zaidi, soma https://jamii.app/WadhaminiLissu