JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
IRAN YAWAKAMATA WALIOITUNGUA KIMAKOSA NDEGE YA UKRAINE

> Tangazo limetolewa baada ya Rais Hassan Rouhani kutaka iundwe Mahakama Maalum kushughulikia mkasa huo

> Msemaji wa Mahakama, hakubainisha idadi ya watu waliotiwa mbaroni kuhusiana na mkasa huo

Soma https://jamii.app/UkrainePlaneShootArrest
MAMBO MUHIMU YA KUFANYA UNAPOHITAJI MSAIDIZI WA KUKULELEA MTOTO

> Fanya mahojiano na msaidizi kabla ya kumpokea. Endesha mafunzo kwa msaidizi ili kumjengea uwezo zaidi. Fuatilia maisha yake ili kujua historia yake

> Awe na umri wa miaka 18 na kuendelea. Malipo ya msaidizi yasiwe madogo sana. Jenga mahusiano mazuri na msaidizi. Zingatia elimu/ufahamu wa msaidizi

Some https://jamii.app/MsaidiziKuleaMtoto
#JFMalezi
WATU WENGI HUFARIKI KUTOKANA NA DAWA BANDIA ZILIZOSAMBAA AFRIKA

> Dawa hizo mara nyingi huwa zimeisha muda wake wa matumizi au ziko chini ya kiwango, au dawa za kughushi

> Kati ya asilimia 30 hadi 60 ya dawa bandia zinatoka China na India

Soma https://jamii.app/DeathFakeMedicines
IJUE SHERIA YA MTOTO TANZANIA

> Haki za Mtoto kwa Mujibu wa Sheria (2009) ni pamoja na Haki ya kuishi, Haki ya kupumzika, Haki ya kuheshimiwa na kuthaminiwa, Haki ya kutokubaguliwa, Haki ya kuishi na wazazi wake na Haki ya kupata huduma bora za elimu, malazi, matibabu kwa ajili ya ustawi wake

> Haki ya kushiriki michezo na shughuli za kiutamaduni,Haki ya kunufaika na kutumia kwa uangalifu mali za wazazi wake, Haki ya kutoa maoni, kusikilizwa na kutoa maamuzi na Haki ya kutoajiriwa katika ajira zenye madhara

Zaidi, soma - https://jamii.app/SheriaHakiMtoto
#JFSheria
KENYA: MTOTO WA MIAKA 11 ASHTAKIWA KWA MAUAJI YA KAKA YAKE

> Mtoto huyo wa darasa la tano anashikiliwa na Polisi baada ya kumchoma kisu kaka yake

> Mahakama imeamuru arudishwe mahabusu ya watoto hadi upelelezi utakapokamilika

Soma - https://jamii.app/MtotoMauajiKaka
KATAVI: MTAALAM WA KUCHEZA NA NYOKA AFARIKI KWA KUNG'ATWA NA NYOKA

> James Pascal aling'atwa akiwa ktk harakati za kumkamata na kumuweka nyoka kwenye mfuko

> Hali yake ilikuwa mbaya hivyo kupelekwa Hospitali, alifariki akiwa anapatiwa matibabu

Soma https://jamii.app/KifoMtaalamNyoka
DODOMA: MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ZAACHA WATU 1000 BILA MAKAZI

> Nyumba 237 zimebomolewa na mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani Bahi

> Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuepuka kupita kwenye mito ambayo imefurika

Soma - https://jamii.app/MadharaMvuaDom
BARAZA LA WAWAKILISHI KUPIGA KURA YA KUPELEKA MASHITAKA DHIDI YA TRUMP

> Baraza la Wawakilishi linatarajiwa kupiga kura leo kuhusu kupeleka mashitaka dhidi ya Rais Donald Trump mbele ya Bunge la Seneti ikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya kuanza kwa kesi ya kumuondoa Rais huyo madarakani

> Trump anakabiliwa na mashtaka ya Matumizi Mabaya ya Madaraka na kuzuia Bunge kufanya shughuli zake

Soma - https://jamii.app/SenateTrumpImpeachment
FAIDA ZA KUOGA MAJI YA MOTO WALAU MARA 3 KWA WIKI

> Maji ya moto hutuliza mwili na husababisha joto la mwili kuongezeka na hivyo kupelekea kupata usingizi haraka

> Tafiti zinaonyesha mtu mwenye Shinikizo la Damu la Kupanda, akioga maji ya moto husaidia kushusha kwasababu huunguza baadhi ya mafuta yaliyopo mwilini

> Maji ya moto hufungua matundu yaliyopo kwenye ngozi na kusaidia kuondoa uchafu na mafuta yaliyoganda kwenye ngozi na kukupa ngozi laini na safi

Tembelea - https://jamii.app/FaidaKuogaMajiMoto
#JFAfya
MBOWE AMSHANGAA SELASINI KUJIUZULU NAFASI YA MNADHIMU WA UPINZANI BUNGENI

> Mbowe amesema sababu zilizotolewa hazina mashiko

> Ameuliza, kama hakupewa barua ya uteuzi imekuwaje aandike barua ya kujiuzulu?

Soma https://jamii.app/MboweKujiuzuluSelasini
MICHEZO: Man. United imeingiza kiasi cha Paundi milioni 627.1 (zaidi ya trilioni 1 za Kitanzania) msimu wa mwaka 2018/19 na kuwafanya kushika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa klabu nyuma ya Barcelona (Spain) wenye paundi milioni 741.1 wakiwa nafasi ya 1 na Real Madrid (Spain) paundi milioni 667.5 wakiwa wa 2
-
Wengine ni Man. City ambao wana paundi milioni 538 wakiwa nafasi ya 6, Liverpool iliyopo nafasi ya 7 ikijikusanyia paundi milioni 533, Tottenham Hotspur ikiwa nafasi ya 8 kwa kuingiza paundi milioni 459.3 huku Chelsea wakiwa wa 9 kwa kuingiza paundi milioni 452.2
SUDAN: JESHI LASHIKILIA MAKAO MAKUU YA WAASI JIJINI KHARTOUM

> Kiongozi wa Baraza Huru amesema hachukulii tukio hilo kama jaribio la mapinduzi

> Mkuu wa Zamani wa Usalama wa Taifa, Salah Gosh atuhumiwa kuhusika na uasi huo

Soma - https://jamii.app/JaribioUasiSudan
RIPOTI: CHINA YADAIWA KUWA NCHI HATARI KWA HAKI ZA BINADAMU

> Shirika la Human Rights Watch, limesema China inaweka mikakati ya kuidhoofisha mifumo ya kulinda Haki za Binadamu Duniani kote

> Serikali ya China inachukulia uanaharakati wa Haki za Binadamu nchini humo na Sheria za Kimataifa na Taasisi zinazotetea haki kama kitisho

Soma - https://jamii.app/UkiukwajiHakiBinadamuChina
UGANDA: MTOTO WA MIAKA 10 AMCHOMA KISU MWENZAKE KWA WIVU WA MAPENZI

> Polisi wanamsaka mtoto huyo, ambaye amekimbia na baba yake baada ya kifo cha mwenzake

> Ndugu wa marehemu walitishia kushambulia familia ya mtuhumiwa kwa kulipiza kisasi

Soma https://jamii.app/MauajiWatotoMapenzi
TANZIA: MBUNGE WA NEWALA VIJIJINI AFARIKI

> Mbunge Rashid Ajali Akbar, amekutwa amefariki katika Gesti ya Mingoyo - Mnazi Mmoja, Mkoani Lindi

> Inaelezwa kuwa yeye ndio mmiliki wa Gesti hiyo na mpaka sasa bado chanzo cha kifo chake hakijafahamika

Soma - https://jamii.app/RIPAjaliRashidNewala
#JFLeo
RAIS WA UTURUKI AMPA ONYO MBABE WA KIVITA WA LIBYA

> Rais Recep Tayyip Erdogan amesema nchi hiyo itachukua hatua endapo Jenerali Khalifa Haftar ataendelea kufanya mashambulizi dhidi ya Serikali ya Tripoli ambayo inatambulika kimataifa

Soma - https://jamii.app/RaisOnyoHaftarLibya
MALAWI: JESHI LA POLISI LASHTAKIWA KWA KUTOCHUNGUZA KESI ZA UBAKAJI DHIDI YA MAAFISA WAKE

> Baadhi ya Polisi wanadaiwa kutumia upenyo uliotokea kipindi cha maandamamo Oktoba 2019 kufanya vitendo vya ubakaji kwa wanafunzi na wanawake katika maeneno ya Msundwe, M’bwatalika na Mpingu

Soma - https://jamii.app/PoliceAccusedGenderViolence
MICHEZO: Mchezo kati ya Yanga SC na Kagera Sugar umemalizika kwa Yanga kuadhibiwa na Kagera kwa kufungwa mabao 3 kwa 0 kwenye Uwanja wa Uhuru
-
Magoli ya Kagera Sugar yamefungwa na
Mhilu 13'
Ramadhan 67'
Mwalyanzi 90'
TANZANIA YAPOKEA MSAADA KUTOKA SWEDEN ILI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU

> Tanzania imetia saini mikataba 2 ya msaada na Sweden kwa kupatiwa Tsh. Bilioni 240.95 ili kugharamia mpango wa maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) 2016/17 – 2021/2022 ikiwemo Elimu ya Msingi, Elimu Jumuishi, Elimu ya Watu Wazima na iliyo nje ya Mfumo Rasmi

Soma - https://jamii.app/MsaadaElimuSweden
DARASA LA SABA DAR KUFANYA MITIHANI KESHO, NECTA WATOA UFAFANUZI

> Kitachofanyika kesho si Mitihani ya NECTA, ni jaribio kwa walimu wa Mkoa huo baada ya kupewa mafunzo ya namna bora ya kutunga mitihani

> Lengo la mazoezi hayo ni kuhakikisha walimu wanakuwa na umahiri wa kutunga mtihani

Soma https://jamii.app/MtihaniNecta7