JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MPYA: Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau amesema taarifa zao za kiintelijensia zinaonyesha kuwa Ndege iliyoanguka juzi nchini Iran na kuua watu 176 wakiwemo raia 63 wa Canada ilitunguliwa na Iran

> Rais Trump pia amedai ana wasiwasi na chanzo cha ajali hiyo
KENYA: WAZAZI WADAIWA KUMUUA MWALIMU KUTOKANA NA MATOKEO MABAYA YA SHULE

> Wambua Mwangangi na Chris Kyalo Muli wamekamatwa kwa tuhuma za kumshambulia kwa panga Daisy Mbathe, Mwalimu wa shule ya Msingi Ndooni baada ya shule yake kutoa matokeo mabaya katika Mtihani wa Kitaifa wa KCPE kwa mwaka 2019

Soma - https://jamii.app/KifoMwlMatokeoMabaya
BUNGE LA MAREKANI LAPIGA KURA KUZUIA VITA NA IRAN

> Bunge la Wawakilishi limepitisha azimio linalolenga kumzuia Rais Donald Trump kupigana vita na Iran kwa kupitisha azimio hilo kwa kura 224 dhidi ya 194

> Azimio hilo linalenga kuipa Kongresi kutoa kibali cha shambulio lolote dhidi ya Iran, pale tu patakapokuwa na shambulio la ghafla dhidi ya Marekani

Soma - https://jamii.app/CongressVoteUSWarIran
#JFLeo
JANGILI MBARONI KWA KUMUUA ASKARI WA WANYAMAPORI

> Jeshi la Polisi Mkoani Kagera linamshikilia Alfred Kamugisha kwa tuhuma za kumuua kwa kumchoma mkuki Askari wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Matundu Masunga na kufanya vitendo vya ujangili ndani ya Hifadhi Mpya ya Rumanyika

> Tukio hilo lilitokea wakati Askari wa TANAPA walipokwenda kumkamata Alfred

Soma - https://jamii.app/JangiliMauajiAskariHifadhi
JE, WANANCHI WANAWEZA KUMKAMATA MWIZI AU MHALIFU NA KUMWADHIBU?

> Hapana, kumpiga mhalifu ni kosa la jinai. Unachopaswa kufanya ni kumweka mhalifu chini ya ulinzi na kisha kumpeleka kituo cha Polisi kilichopo karibu. Hutakiwi kumpiga mhalifu au kushirikiana na kundi la watu wanaofanya hivyo

> Polisi anayeruhusu hilo au anayeungana na watu wanaofanya hivyo anaweza kukabiliwa na mashtaka ya kinidhamu au jinai

Soma - https://jamii.app/JinaiKumpigaMhalifu
KENYA: BIMA YA TAIFA KUTOGHARAMIA MATIBABU YA MKE WA PILI

> Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) umefanya mageuzi ambapo sasa utakuwa unagharamia matibabu ya mke au mume mmoja tu na watoto 5 kwa wenye ndoa zenye zaidi ya mwenza mmoja

> Mageuzi hayo yalianza kutekelezwa rasmi Januari 1, 2020

Soma - https://jamii.app/MageuziBimaAfyaKE
RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA ZANZIBAR LEO

> Anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la jengo la Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar na la Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe iliyoko Mjini Magharibi

> Pia, atafungua hoteli yenye hadhi ya Nyota 5 iitwayo Hotel Verde Azam Luxury Resort and Spa iliyoko Mtoni

Soma - https://jamii.app/ZiaraMagufuliZanzibar
KENYA: MWANASHERIA MKUU ATAKIWA KUELEZA KWANINI MIGUNA KAZUILIWA KURUDI KENYA

- Kihara Kariuki ametakiwa kufika Mahakamani kuleza kwanini maagizo ya Mahakama hayajafuatwa

- Mahakama ilitaka Serikali kumruhusu Miguna kurudi Kenya ila alizuiliwa

Soma https://jamii.app/GovntVsCourt-Miguna
ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUJIFANYA DAKTARI NA KUTIBU WANANCHI

> Ismail Onyango amekamatwa baada ya Raia wema kutoa taarifa

> Inadaiwa kuwa, alikuwa anatoa huduma bila kuwa na cheti chochote cha Taaluma ya Udaktari wala Utabibu

Soma - https://jamii.app/DktFekiAkamatwa
EMOJI ILIYOVUNJA REKODI YA KUTUMIKA SANA DUNIANI

> Emoji inayotumika sana ni 'Uso Wenye Machozi ya Furaha', inayofahamika kama "LOL Emoji" 😂

> Kati ya meseji milioni 427 zilizotumwa katika nchi 212, hii alama ilikuwa ni asilimia 15.4

Soma https://jamii.app/MostUsedEmoji
BADO FRANCISCO JOAQUIM HAJAPATA WA KUMSHINDA KWA UKUBWA WA KINYWA

> Kijana huyo (28), anaweza kutanua kinywa chake hadi 17CM

> Picha yake maarufu ni ile aliyoweka chupa ya Cocacola kinywani

Soma https://jamii.app/MtuMdomoMkubwa
TANZANIA INA KASI YA MTANDAO YENYE WASTANI WA 2.34 Mbps

> Nchi Tano Bora ni Singapore 60.39 Mbps, Sweden 46.00 Mbps, Denmark 43.99 MB/S, Norway 40.12 Mbps na Romania 38.60 Mbps

Soma https://jamii.app/FastestInternetCountries
CHAKULA NI KICHOCHEO CHA KUIMARISHA MAHUSIANO MAZURI YA FAMILIA

- Je, unajua kwamba familia ambazo zinakula chakula pamoja zinapata faida nyingi ikiwemo kuimarisha mawasiliano na mahusiano ya wazazi na watoto?

- Kuwapa uhuru wanafamilia wa kuchagua chakula wakitakacho ni njia mojawapo ya kuwafanya wajisikie wanawajibika na wana maamuzi katika masuala muhimu ya familia

Kujua njia nyingine, tembelea https://jamii.app/ChakulaKuimarishaMahusiano
SHAMBULIO KATIKA KAMBI YA JESHI NIGER LAUA WANAJESHI 25
-
Watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa Wanamgambo wa Kijihadi wameua wanajeshi 25 na kujeruhi 6 katika Kambi ya Jeshi la Niger karibu na mpaka na Mali
-
Hata hivyo, Washambuliaji 63 wanadaiwa kuuawa wakati wa mapigano hayo, ambayo yalitokea katika Mji wa Chinagodrar
TANZANIA NI YA 73 KWA PASSPORTS ZENYE NGUVU DUNIANI

> Henley Passport Index imeitaja Japan kuwa kinara wa Passport yenye nguvu, ina Nchi 191 za kutembelea bila VISA

> Afghanstan ni ya mwisho ambayo ina Nchi 26

Soma https://jamii.app/StrongPassportCountries
SONGWE: ANYWA SUMU KWA KUPATA UFAULU WA DARAJA LA 4 KIDATO CHA 4

- Michael Aroni (20) amekunywa sumu kufuatia kupata ufaulu wa Daraja la IV la alama 26

- Alitarajia kupata ufaulu wa Daraja la Kwanza katika matokeo hayo yalitolewa jana

Zaidi, soma https://jamii.app/MatokeoIVAnywaSumu
ALIYEMUINGIZA NYETI MTOTO MDOMONI KUHUKUMIWA

> Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam imepanga Januari 20, 2020 kutoa hukumu kwa Riziki Kessy

> Alitenda kosa hilo, Julai 24 mwaka 2018 maeneo ya Kimara Stop Over Dar es Salaam

Zaidi, soma https://jamii.app/HukumuNyetiMtoto
VITABU VITAKATIFU VINAKEMEA VITENDO VYA RUSHWA

- Mnamo mwezi Desemba 2019, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iliwaomba Viongozi wa Dini na Wazazi kutumia nafasi zao kutoa mafunzo ya athari ya rushwa katika jamii

- TAKUKURU wanatukumbusha kuwa Rushwa ina madhara makubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla inapaswa kukemewa kuanzia ngazi ya familia, Kanisani, Misikitini na maeneo ya Shule na Vyuo

#KemeaRushwa
RAILA ODINGA: MIGUNA HAJAZUIWA KURUDI. ANABWEKA KAMA MBWA

- Amesema aliyekuwa Msaidizi wake, Miguna Miguna hajazuiwa na yeyote kurudi Kenya

- Amesema, “Anabweka bweka huko nje kama Mbwa, si aje abweke hapa. Uhuru na Raila hawaogopi Miguna.”

Zaidi, soma https://jamii.app/RailaOdingaVsMiguna