JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MHAMIAJI AJIKATA KOO BAADA YA KUKATALIWA KUINGIA MAREKANI

> Raia huyo kutoka Mexico amejiua mita kadhaa kutoka Daraja la Kimataifa la Pharr – Reynosa, Texas

> Maafisa wa eneo hilo wamesema, mtu huyo bado hajatambulika hadi sasa

Zaidi, soma https://jamii.app/MhamiajiAjikataKoo-MXC
MAREKANI YASEMA IKO TAYARI KUFANYA MAZUNGUMZO NA IRAN

> Iko tayari kujadiliana bila masharti baada ya uhasama uliozuka baina yao

> Katika barua yake kwa Umoja wa Mataifa ilijitetea kuwa, ilimuua Qasem Soleimani kama hatua ya kujilinda

Zaidi, soma https://jamii.app/MarekaniMazungumzoIran
NETFLIX KUIFUTA FILAMU INAYOONYESHA YESU KAMA SHOGA

- Uamuzi ulifikiwa ktk kujibu ombi la Shirika la Katoliki lililosema filamu hiyo imeumiza heshima yao

- Uamuzi huo wa Mahakama ni halali hadi Mahakama nyingine itoe amri nyingine tofauti na hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/NetflixFilamuYesu
TETESI: YOUNG AKATAA MKATABA. MAN UTD YAJIONDOA KUMUWANIA ERIKSEN

- Nahodha wa Manchester United, Ashley Young anadaiwa kukataa mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo huku akihusishwa kuhamia Inter Milan

- Pia, Man. Utd inadaiwa kufutilia mbali mpango wake wa kutaka kumsajili Kiungo wa Tottenham, Christian Eriksen huku mchezaji huyo naye akihusishwa na Inter Milan
ARUSHA: MWALIMU MBARONI KWA KUMUOMBA MWANAFUNZI RUSHWA YA NGONO

- Ni William Mollel anayefundisha Kidato cha 5 na 6 shule ya Sekondari Embarway

- Inadawia, alikuwa akimnyanyasa Mwanafunzi huyo na kumuambia ili awe na amani, washiriki ngono

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuEmbarwayMbaroni
TANZIA: Mwandishi Nguli wa Kazi za Fasihi ya Kiswahili Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki leo baada ya kuugua kwa muda mrefu

> Atakumbukwa kwa kazi zake kama Rosa Mistika, Uwanja wa Fujo, Kaptula la Marx, Nagona na Mzingile na jinsi alivyotetea Mashairi ya Kisasa

Soma - https://jamii.app/RIPProfKezilahabi
#JFLeo
MPYA: Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau amesema taarifa zao za kiintelijensia zinaonyesha kuwa Ndege iliyoanguka juzi nchini Iran na kuua watu 176 wakiwemo raia 63 wa Canada ilitunguliwa na Iran

> Rais Trump pia amedai ana wasiwasi na chanzo cha ajali hiyo
KENYA: WAZAZI WADAIWA KUMUUA MWALIMU KUTOKANA NA MATOKEO MABAYA YA SHULE

> Wambua Mwangangi na Chris Kyalo Muli wamekamatwa kwa tuhuma za kumshambulia kwa panga Daisy Mbathe, Mwalimu wa shule ya Msingi Ndooni baada ya shule yake kutoa matokeo mabaya katika Mtihani wa Kitaifa wa KCPE kwa mwaka 2019

Soma - https://jamii.app/KifoMwlMatokeoMabaya
BUNGE LA MAREKANI LAPIGA KURA KUZUIA VITA NA IRAN

> Bunge la Wawakilishi limepitisha azimio linalolenga kumzuia Rais Donald Trump kupigana vita na Iran kwa kupitisha azimio hilo kwa kura 224 dhidi ya 194

> Azimio hilo linalenga kuipa Kongresi kutoa kibali cha shambulio lolote dhidi ya Iran, pale tu patakapokuwa na shambulio la ghafla dhidi ya Marekani

Soma - https://jamii.app/CongressVoteUSWarIran
#JFLeo
JANGILI MBARONI KWA KUMUUA ASKARI WA WANYAMAPORI

> Jeshi la Polisi Mkoani Kagera linamshikilia Alfred Kamugisha kwa tuhuma za kumuua kwa kumchoma mkuki Askari wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Matundu Masunga na kufanya vitendo vya ujangili ndani ya Hifadhi Mpya ya Rumanyika

> Tukio hilo lilitokea wakati Askari wa TANAPA walipokwenda kumkamata Alfred

Soma - https://jamii.app/JangiliMauajiAskariHifadhi
JE, WANANCHI WANAWEZA KUMKAMATA MWIZI AU MHALIFU NA KUMWADHIBU?

> Hapana, kumpiga mhalifu ni kosa la jinai. Unachopaswa kufanya ni kumweka mhalifu chini ya ulinzi na kisha kumpeleka kituo cha Polisi kilichopo karibu. Hutakiwi kumpiga mhalifu au kushirikiana na kundi la watu wanaofanya hivyo

> Polisi anayeruhusu hilo au anayeungana na watu wanaofanya hivyo anaweza kukabiliwa na mashtaka ya kinidhamu au jinai

Soma - https://jamii.app/JinaiKumpigaMhalifu
KENYA: BIMA YA TAIFA KUTOGHARAMIA MATIBABU YA MKE WA PILI

> Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) umefanya mageuzi ambapo sasa utakuwa unagharamia matibabu ya mke au mume mmoja tu na watoto 5 kwa wenye ndoa zenye zaidi ya mwenza mmoja

> Mageuzi hayo yalianza kutekelezwa rasmi Januari 1, 2020

Soma - https://jamii.app/MageuziBimaAfyaKE
RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA ZANZIBAR LEO

> Anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la jengo la Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar na la Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe iliyoko Mjini Magharibi

> Pia, atafungua hoteli yenye hadhi ya Nyota 5 iitwayo Hotel Verde Azam Luxury Resort and Spa iliyoko Mtoni

Soma - https://jamii.app/ZiaraMagufuliZanzibar
KENYA: MWANASHERIA MKUU ATAKIWA KUELEZA KWANINI MIGUNA KAZUILIWA KURUDI KENYA

- Kihara Kariuki ametakiwa kufika Mahakamani kuleza kwanini maagizo ya Mahakama hayajafuatwa

- Mahakama ilitaka Serikali kumruhusu Miguna kurudi Kenya ila alizuiliwa

Soma https://jamii.app/GovntVsCourt-Miguna
ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUJIFANYA DAKTARI NA KUTIBU WANANCHI

> Ismail Onyango amekamatwa baada ya Raia wema kutoa taarifa

> Inadaiwa kuwa, alikuwa anatoa huduma bila kuwa na cheti chochote cha Taaluma ya Udaktari wala Utabibu

Soma - https://jamii.app/DktFekiAkamatwa
EMOJI ILIYOVUNJA REKODI YA KUTUMIKA SANA DUNIANI

> Emoji inayotumika sana ni 'Uso Wenye Machozi ya Furaha', inayofahamika kama "LOL Emoji" 😂

> Kati ya meseji milioni 427 zilizotumwa katika nchi 212, hii alama ilikuwa ni asilimia 15.4

Soma https://jamii.app/MostUsedEmoji
BADO FRANCISCO JOAQUIM HAJAPATA WA KUMSHINDA KWA UKUBWA WA KINYWA

> Kijana huyo (28), anaweza kutanua kinywa chake hadi 17CM

> Picha yake maarufu ni ile aliyoweka chupa ya Cocacola kinywani

Soma https://jamii.app/MtuMdomoMkubwa
TANZANIA INA KASI YA MTANDAO YENYE WASTANI WA 2.34 Mbps

> Nchi Tano Bora ni Singapore 60.39 Mbps, Sweden 46.00 Mbps, Denmark 43.99 MB/S, Norway 40.12 Mbps na Romania 38.60 Mbps

Soma https://jamii.app/FastestInternetCountries
CHAKULA NI KICHOCHEO CHA KUIMARISHA MAHUSIANO MAZURI YA FAMILIA

- Je, unajua kwamba familia ambazo zinakula chakula pamoja zinapata faida nyingi ikiwemo kuimarisha mawasiliano na mahusiano ya wazazi na watoto?

- Kuwapa uhuru wanafamilia wa kuchagua chakula wakitakacho ni njia mojawapo ya kuwafanya wajisikie wanawajibika na wana maamuzi katika masuala muhimu ya familia

Kujua njia nyingine, tembelea https://jamii.app/ChakulaKuimarishaMahusiano