JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MASHIRIKA YA NDEGE YAZUIA NDEGE ZAKE KUPITA ANGA LA IRAN NA IRAQ

- Ni Mashirika ya Malaysia, Poland, Taiwan (EVA Air), Uholanzi, Ufaransa, China, Korea, Australia (Qantas), Singapore, Ujerumani (Lufthansa) na Shirika la Kimataifa la Swiss

Zaidi, soma https://jamii.app/MashirikaNdegeIran
MAFUTA GHAFI YAPANDA BEI

> Gharama za Mafuta Ghafi zimepanda kwa 1.4% kwa dola 69.21 za Marekani kwa pipa moja

> Gharama za mafuta zimepanda baada ya Kambi mbili za Majeshi ya Marekani nchini Iraq kushambuliwa na makombora

Zaidi, soma https://jamii.app/OilPriceRise
IRAN: SHAMBULIO LETU KWA MAREKANI NI ‘KOFI LA USO’ KWAKE

- Imesisitiza kuwa Kitendo cha Kijeshi (kushambulia Kambi za Jeshi) walichochukua dhidi ya Marekani hakitoshi

- Imesema kilicho cha muhimu ni kutokomeza kabisa uwepo wa Marekani katika eneo hilo

Zaidi, soma https://jamii.app/IranShambuliKambiUSA
TRUMP: HAKUNA MWANAJESHI WETU ALIYEUAWA AU KUJERUHIWA

- Baada ya shambulio la Iran, Rais Trump amesema kumetokea uharibifu kidogo tu kwenye Kambi hizo

- Aidha, amesema Iran inaonekana kusitisha kutaka kulipa kisasi, ambacho ni kitu kizuri

Zaidi, soma https://jamii.app/TrumpAjibuShambulioIran
MREMA AITAKA SERIKALI IMLIPE BILIONI 2 KAMA FIDIA

- Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema ameitaka Serikali kumlipa Tsh. Bilioni 2 kama fidia ya kesi alizowahi kusingiziwa chini ya Serikali ya Awamu ya Tatu ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

Zaidi, soma https://jamii.app/MremaAtakaFidia
UKATILI WA KINGONO IRINGA: WATOTO 404 WAATHIRIKA MWAKA 2019

> Kwa kipindi cha Januari mpaka Novemba 2019, Mkoa wa Iringa umekuwa na matukio takriban 404 ya vitendo ya ukatili wa kingono kwa watoto

> Serikali imezitaka Kamati za Malezi Nchi nzima kutoa taarifa za vitendo hivyo na sio kumalizana kifamilia na watuhumiwa

Soma - https://jamii.app/RipotiUkatiliWatoto2019
RIPOTI: MAKADIRIO YA UKUAJI WA UCHUMI WA DUNIA NI 2.5% MWAKA 2020

> Benki ya Dunia imesema, ukuaji wa Uchumi wa Dunia kwa 2020 unakadiriwa kufikia 2.5% ikilinganishwa na asilimia 2.4 ya 2019

> Ukuaji ktk masoko yanayoibuka na nchi zinazoendelea unatarajiwa kufikia 4.1% kutoka 3.5% ya mwaka 2019

Soma - https://jamii.app/WorldEconomicGrowth
👍1
YANGA YATANGAZA KOCHA MPYA KUTOKA UBELGIJI

- Imemtangaza Luc Eymael atakayekuja kukinoa kikosi hicho kilicho chini ya Kocha wa Muda, Charles Mkwasa

- Luc amewahi kufundisha timu za As Vita, AFC Leopard, Rayon Sports, Al Nasr, Al-Merrikh, Polokwane na Black Leopard
BAADHI YA MAMBO YA KUYAJUMUISHA KATIKA MALENGO YAKO YA KUMLEA MTOTO

> Tenga muda wa faragha na watoto wako. Iwapo unao watoto zaidi ya mmoja, fanya kila uwezalo kupata muda na kila mmoja ili akueleze mipango aliyonayo na wewe umshauri

> Azimia kutomlinganisha mtoto wako na watoto wa wengine. Watoto huzaliwa na vipaji na karama tofauti hivyo usishawishike kutaka mtoto wako afanane na wa majirani

> Mfundishe mwanao stadi moja mwaka huu. Zipo stadi kadhaa muhimu katika maisha ikiwamo kupika, kufua, kutunza bustani, usimamizi wa fedha na kadhalika

Tembelea - https://jamii.app/MalengoKuleaMtoto
DRC: 6000 WAFARIKI KWA UGONJWA WA SURUA

- Hali hiyo imefanya kuwa, kati ya majanga makubwa ya milipuko mabaya zaidi ya magonjwa yanayoambukiza kutokea Duniani

- Kwa Tanzania hali iko tofauti kwa kuwa watoto hupatiwa chanjo ya surua wakiwa na umri mdogo

Zaidi, soma https://jamii.app/PolioDeathRateDRC
USIANZISHE BIASHARA YA MTAJI MKUBWA KWASABABU TU UNA FEDHA NYINGI

> Mdau katika Jukwaa la Biashara ndani ya JamiiForums.com anasema, kuna Kanuni Tatu za Msingi ambazo anaziamini zinafaa katika uwekezaji

> Anashauri kuwekeza kiasi ambacho uko tayari kupoteza iwapo hasara itatokea, wekeza kwa watu na sio vitu na wekeza katika kile unachokipenda na kukiamini na sio vutio la faida kubwa

> Anasema, kanuni hizi ni muhimu sana kwani unapozifuata kuna uwezekano mkubwa sana wa kufanikiwa katika biashara

Tembelea - https://jamii.app/BiasharaKubwaVsMtajiMkubwa
MURANG'A, KENYA: AWAUA WANAYE BAADA YA KUGOMBANA NA MUMEWE

- Esther Wambui (25), amewaua Watoto wake wawili wa Kike hapo jana huko Kimwiriini katika Kijiji cha Gatanga

- Aliwanywesha sumu watoto hao kabla na yeye kujaribu kujiua kwa simu hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/WomanPoisonsDaughters
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kumetokea vurugu katika Kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji hilo, kwenye kikao maalum cha kujadili na kuamua hatma ya Meya wa Jiji la Dar, Isaya Mwita

- Chanzo cha vurugu ni kusainiwa kwa mahudhurio na Mjumbe ambaye hayupo ndani ya ukumbi wa mkutano

Zaidi, soma https://jamii.app/VuruguBarazaMadiwaniDar
MAREKANI YAZUIA MALI ZA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SUDAN KUSINI

> Wizara ya Fedha imezuia mali za Taban Deng Gai (69) nchini Marekani na imepiga marufuku Raia wake kushirikiana na Taban

> Anatuhumiwa kwa ukiukaji wa Haki za Binadamu na kuhusika na kifo cha Wakili Samuel Dong Luak na Mpinzani Aggrey Idry

Zaidi, soma - https://jamii.app/USBlacklistsTabanDeng
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE KWA MWAKA 2019 YATANGAZWA

- Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde, ametangaza matokeo hayo leo

- Pia, matokeo ya Upimaji ya Kidato cha Pili na matokeo ya Maarifa (QT) yatangazwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MatokeoKidato42019
MABASI YANAYOSAFIRISHA VIFURUSHI BILA LESENI YA TCRA YAPEWA ONYO

> Naibu Waziri Nditiye ataka mabasi kufuata taratibu zilizowekwa na Mamlaka

> Ametoa wito kwa Shirika la Posta kuboresha huduma zao ili mizigo isafirishwe na Shirika hilo

Zaidi, soma - https://jamii.app/UkaguziBasiVifurushi
MKAKATI WA TAIFA DHIDI YA RUSHWA NA MPANGO WA UTEKELEZAJI(2017-2022)

> Umelenga kuimarisha na kuwezesha umma kushiriki katika kudai Haki & Uwajibikaji wa Serikali

> Mazingira wezeshi yatawekwa kuhakikisha ushiriki kamilifu wa Wananchi ktk Mapambano dhidi ya Rushwa

#KemeaRushwa
POLISI: TANZANIA IPO SALAMA DHIDI YA VITENDO VYA UGAIDI

> Polisi imewataka Raia wa Kigeni na watalii kuendelea na shughuli zao kama kawaida

> Wamesema kuwa ulinzi unaendelea kuimarishwa nchini kote

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiUsalamaTZUgaidi
ALIYESAFIRI KWA NJIA HARAMU MWILI WAKE WAKUTWA KWENYE GURUDUMU LA NDEGE

> Mwili ulipatikana asubuhi ya Jumatano, Januari 8, karibu na Mji wa Paris, ikitokea Abidjan

> Wengi wanaamini kwamba kijana huyo alikufa kutokana na kukosa hewa au baridi

Zaidi, aoma https://jamii.app/MwiliTairiNdege-UFR
IRAN: NDEGE ILIYOUA WATU 176 ILIKUWA IKIUNGUA KABLA YA KUDONDOKA

- Wachunguzi wamedai wafanyakazi hawakufanya mawasiliano ya redio kuomba msaada

- Pia, sanduku zote mbili ambazo zina data na mawasiliano ya kutoka kwenye ndege zimepatikana

Zaidi, soma https://jamii.app/UchunguziNdegeUkraine-IRN