JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
PEP GUARDIOLA: KAMWE SIWEZI KUFUNDISHA MANCHESTER UNITED NA REAL MADRID

> Kocha huyo wa Manchester City amesema bora aende likizo ya kufundisha soka kuliko kukubali kuifundisha Man UTD

> Je, unadhani nini kimepelekea kauli hii ya Pep?

Soma > https://jamii.app/GuardiolaVsManUtd

#JFSports
TETEMEKO LA 6.5 LAIKUMBA PUERTO RICO NA KUATHIRI MAKAZI NA HUDUMA ZA KIJAMII

> Tetemeko hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, likiwa ni kubwa zaidi katika matetemeko ambayo yamepiga maeneo ya Amerika siku za hivi karibuni

> Limefuatana na lingine lenye ukubwa wa 5.8 ambalo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatatu

Soma - https://jamii.app/EarthquakesPuertoRico
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KISUTU: KESI YA TITO MAGOTI YAPIGWA TENA KALENDA

- Kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi imeahirishwa hadi Januari 21 baada ya Jamhuri kudai upelelezi haujakamilika

- Upande wa Utetezi umetoa rai kwa Jamhuri kutokamata Watu kabla haijapeleleza

Soma https://jamii.app/KesiMagotiKalenda
NJIA 6 ZA KUPATA MATOKEO CHANYA KUTOKA KWA MTOTO

> Njia zinazoweza kumuwezesha mzazi/mlezi kupata matokeo mazuri katika kumkuza na kumuendeleza mtoto wake kijamii, kiafya, kielimu au kitabia ni hizi zifuatazo:

> Kumrubuni mtoto wako. Kupongeza mtoto wako. Kuadhibu mtoto wako. Kumtishia mtoto wako. Kumfundisha mtoto wako. Kuwa mfano kwa mtoto wako

> Njia za kuleta matokeo chanya kwa watoto zipo nyingi na kila moja inafanya vizuri katika hali tofautitofauti, hakuna hata njia moja kati ya hizo nilizozieleza hapo juu ambayo inaweza kuingia katika kila hali kwenye maisha ya mtoto

SOMA: https://jamii.app/MatokeoChanyaMtoto
#JFMalezi
UJUMBE WA LEO KUTOKA TAKUKURU: Mtumishi yeyote akiwa ni muumini wa Rushwa hafai kuwa Mtumishi wa Umma. Jukumu la kupambana na Rushwa ni la kila mmoja wetu.

#KemeaRushwa
BASATA YAMFUTIA USAJILI DUDU BAYA

- Godfrey Tumaini maarufu 'Dudu Baya' amefungiwa kujishughulisha na shughuli zozote za sanaa kuanzia leo

- Dudu Baya aligoma kwenda BASATA jana alikoitwa kuhojiwa juu ya video zake zenye maneno yasiyo na maadili

Zaidi, soma https://jamii.app/BasataUsajiliDudubaya
MIGUNA MIGUNA ASHINDWA KURUDI KENYA, AZUIWA BERLIN

> Tahadhari ilitolewa asiondoke Uwanja wa Berlin kuelekea JKIA Kenya au nchi yoyote Afrika

> Zuio hili linakuja baada ya Mahakama ya Juu kuagiza Serikali kumruhusu Miguna kurejea nchini humo

Zaidi, soma - https://jamii.app/MigunaAzuiwaAirportGRM
IRAN: WATU ZAIDI YA 35 WAFARIKI KWENYE TUKIO LA KUAGA MWILI WA JENERALI SOLEIMAN

> Waombolezaji zaidi ya 35 wamepoteza maisha huku wengine takriban 200 wakijeruhiwa kutokana na msongamano wa mamilioni ya watu waliojitokeza mjini Kerman kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jenerali Qasem Soleimani aliyeuawa na Marekani

> Kifo chake kimeleta mvutano mkubwa kati ya Marekani na Iran huku Iran ikitishia kulipiza kisasi

Soma - https://jamii.app/DeathsSoleimanMemorial
DODOMA: MWANACHUO ANASWA NA TAKUKURU AKIJARIBU KUHONGA AONGEZEWE UFAULU

> TAKUKURU inatarajia kumfikisha Mahakamani James Kwangulija, mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa Shahada ya Kwanza ya Ualimu Chuo Kikuu cha St. John na wenzake sita kwa kutoa hongo ya Tsh. 900,000 kwa Msimamizi wa Mitihani

> James ametenda makosa hayo Kinyume cha Kifungu cha 15 (1)b cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sura ya 329, Marejeo ya 2018

Zaidi Soma https://jamii.app/MwanachuoMbaroniRushwa
Baadhi ya maoni ya Wananchi waliyoyatoa katika Mitandao ya Kijamii kupitia kurasa za JamiiForums baada ya Hospitali ya Mloganzila kujibu tuhuma za kulalamikiwa kuwa kumekuwa kukitokea vifo vingi katika Hospitali hiyo

- Katika majibu yake, Hospitali hiyo ilisema vifo vya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo vimepungua kutoka asilimia 14.9 iliyokuwepo katika kipindi cha Julai - Septemba 2018 hadi asilimia 10.4 kipindi kama hicho 2019
MWANZA: WATU 7 MBARONI KWA KUJIFANYA MAAFISA USALAMA WA IKULU

- Wamekuwa wakiwatapeli Wananchi na baadhi ya Watumishi wa Serikali kwa kujifanya wako katika kazi maalum

- Walikuwa wakitumia gari walilodai ni sehemu ya Msafara wa Viongozi Wakuu

Zaidi, soma https://jamii.app/Matapeli7Mbaroni-MWZ
MICHEZO: Dkt Jonas Tiboroha, Meneja wa Simon Msuva, mchezaji wa Taifa Stars, amesema Msuva amejiunga na klabu ya Benfica ya Ureno kwa mkataba wa miaka 3 akitokea klabu ya Difaâ El Jadida

- Amesema ataanza kuitumikia Benfica Julai 2020 na sasa anaenda kwa mkopo katika klabu ya Panathinaikos ya Ugiriki
SADIO MANE ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA 2019

- Mchezaji huyo wa Senegal na Liverpool ameshinda tuzo hiyo dhidi ya Mohamed Salah (Liverpool, Misri) na Riyad Mahrez (Manchester City, Algeria)

- Anakuwa Msenegal wa pili kushinda tuzo hiyo baada ya El Hadji Diouf
VITA RASMI? IRAN YASHAMBULIA KAMBI ZA JESHI LA MAREKANI

> Imerusha makombora zaidi ya 10 ikilenga Majengo ya Marekani yaliyopo Kaskazini mwa Iraq zikiwemo Kambi za Ain al-Asad na Ebil

> Yaonya kufanya mashambulio zaidi iwapo Marekani itafanya shambulio jipya

> Trump asema kukicha (kwa muda wa Marekani) atatoa kauli rasmi

Soma https://jamii.app/IranShambuliKambiUSA
BREAKING: A Boeing 737 plane carrying 180 passengers and crew has crashed shortly after takeoff from Imam Khomeini Airport in Tehran

> The Ukranian Airlines plane crashed due to technical difficulties, according to ISNA

#PlaneCrash
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
IRAN: NDEGE YA UKRAINE ILIYOKUWA NA WATU 180 YAANGUKA

- Ndege hiyo imeanguka karibu na Mji wa Tehran dakika 3 baada ya kuruka ikitokea Uwanja wa Khomeini

- Hakuna taarifa zozote za majeruhi au vifo ila inaonesha hakuna mtu yeyote aliyepona

Zaidi, soma https://jamii.app/NdegeUkraineYaangukaIran
FAHAMU KUHUSU KIDOLE TUMBO (APPENDIX), DALILI ZAKE NA MATIBABU

> Kidole Tumbo hupatikana katika utumbo mkubwa na urefu wake ni kama kidole cha mwisho cha mkono. Huifadhi michanga au uchafu mdogomdogo kutoka kwenye chakula

> Dalili kuu ni maumivu ya tumbo kwenye kichembe au kitovu ambayo huongezeka kadiri muda unavyosogea na huambatana na kutapika, kushindwa kutembea na homa

> Kama ukichelewa kutibiwa, Appendix inaweza kuoza, kupasuka na kueneza uchafu ndani ya tumbo na damu na hivyo kusababisha kifo

Fahamu zaidi - https://jamii.app/DaliliTibaAppendix
#JFAfya