JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DODOMA: WATU SITA WAFARIKI KATIKA AJALI

- Ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kisasa imehusisha gari aina ya Toyota Coaster na lori

- Kamanda wa Polisi Dodoma, Gilles Muroto amesema Watu wengine 12 wamejeruhiwa

Zaidi, soma https://jamii.app/AjaliDes2019-DOM
DKT. BASHIRU ALLY AWASHANGAA WANAOPENDA ‘KAZI NA BATA’

- Amewataka Wananchi kupuuza kauli hiyo akidai itachangia kuzorotesha uchumi wa Taifa

- Amedai inadhalilisha Wanawake ambao wakati wote wamekuwa wakifanya kazi kusomesha watoto wao

Zaidi, soma https://jamii.app/BashiruAshangaaKaziBata
KENYA: POLISI ADAIWA KUMUUA ALIYEKATAA KUMPA RUSHWA

- Afisa wa Polisi amekamatwa akituhumiwa kumuua kwa kumpiga risasi dereva wa gari aina ya Probox baada ya dereva huyo kukataa kumpa rushwa katika tukio lililotokea katika Kaunti ya Narok

Zaidi, soma https://jamii.app/CopKilledMan-KE
WASAIDIZI WA MNYIKA WAKAMATWA. CHADEMA NA POLISI WATOFAUTIANA MAELEZO

- Waliokamatwa na kuachiwa ni Msaidizi wa John Mnyika, Abdulkarim Muro na dereva, Said Haidan

- CHADEMA na Polisi wametofautiana kuhusu eneo na sababu za Watu hao kukamatwa

Zaidi, soma https://jamii.app/WasaidiziMnyikaWakamatwa
HUKUMU YA KIFO INAWEZA KUBADILISHWA KWA MWANAMKE MJAMZITO

> Mjamzito akihukumiwa kifo, Mahakama itachunguza na ikijiridhisha basi adhabu itakayotolewa itakuwa ni kifungo cha maisha jela badala ya kifo

Kifungu 26 cha Kanuni ya Adhabu

Soma > https://jamii.app/HukumuKifo

#JFSheria
SUDAN: MAAFISA USALAMA 29 WAHUKUMIWA KIFO KWA KUMUUA MWALIMU

- Ahmad al-Khair (36) alifariki akishikiliwa na Maafisa hao baada ya kukamatwa wakati wa maandamano ya kumtoa Omar al-Bashir madarakani

- Mahakama iligundua kuwa alipigwa na kuteswa

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiHukumuKifo-SDN
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
RAIS MAGUFULI AZURU KISIWA CHA RUBONDO

- Rais Magufuli akiwa safarini kuelekea Kisiwa cha Rubondo leo asubuhi. Rubondo ni moja ya Hifadhi za Taifa 22 zilizopo hapa nchini

- Itakumbukwa kuwa ndege moja ya ATCL ina jina la Hifadhi hiyo iliyopo katika Ziwa Victoria
TETESI ZA SOKA ZA USAJILI IKIWA BADO SAA CHACHE DIRISHA KUFUNGULIWA

- Inadaiwa Everton inaongoza katika mbio za kumsajili Mchezaji wa Real Madrid, James Rodriguez huku Manchester United ikidaiwa kutaka kumsajili Mshambuliaji wa Everton, Dominic Calvert-Lewin

- Liverpool inadaiwa kuwa kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa Sevilla, Diego Carlos huku Chelsea ikielezwa kuzungumza na RB Leipzig ili kuangalia uwezekano wa kumsajili Mshambuliaji, Timo Werner
RAIS MAGUFULI: KIGWANGALLA NA PROF. MKENDA MALIZENI TOFAUTI ZENU. VINGINEVYO NAWATENGUA

> Ametoa siku 5 na kama watashindwa kufanya hivyo atatengua teuzi zao. Dkt. Hamis Kigwangalla ni Waziri wa Maliasili na Prof. Mkenda akiwa Katibu Mkuu

> Akiwa katika Hifadhi ya Rubondo amesema Katibu Mkuu hataki kumheshimu Waziri na Waziri hataki kwenda pamoja na Katibu Mkuu

> Rais Magufuli amesema anawatazama taratibu. Hawezi kuwa na watendaji aliowateua halafu kila siku wanagombana na mambo ndani ya Wizara hayaendi.

Soma > https://jamii.app/KigwangallaVsMkenda
VIETNAM: WAZIRI WA ZAMANI AFUNGWA MAISHA KWA MAKOSA YA RUSHWA

- Son Bac Nguyen amefungwa maisha huku aliyekuwa Naibu wake, Tuan Quoc Tran akihukumiwa kifungo cha miaka 14 kwa makosa ya rushwa yaliyoisababishia Serikali hasara ya USD Milioni 3

Zaidi, soma https://jamii.app/WaziriAfungwaMaisha-Vietnam
MTANDAO WA SIMU WA MTN WASHUTUMIWA KUFADHILI MAGAIDI

- Inadaiwa kutoa rushwa kwa Al-Qaeda na Taliban ili isitoe pesa nyingi za kulinda mitambo yao Afghanistan

- Fedha hizo zinadaiwa kutumika kwenye mashumbulio kati ya mwaka 2009 hadi 2017

Zaidi, soma https://jamii.app/MTNShutumaUgaidi
KOREA KUSINI: WAZIRI WA ZAMANI ASHTAKIWA KWA MAKOSA YA RUSHWA

- Waziri wa zamani wa Sheria, Cho Kuk ameshtakiwa kwa makosa 11 yakiwemo ya rushwa, uzuiaji wa Biashara na kughushi na madai mengine yanayohusiana na kashfa dhidi ya familia yake

Zaidi, soma https://jamii.app/WaziriAshutumiwaRushwa-SK
WAYNE ROONEY ASAJILIWA RASMI KUWA MCHEZAJI WA DERBY COUNTY

- Rooney (34) amejiunga rasmi na Derby County kwa mkataba wa miezi 18 hadi majira ya joto mwaka 2021

- Pia, atakuwa akijifunza mbinu za Ukocha kutoka kwa Kocha wa Rams, Phillip Cocu
SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MAWAKILI NJE YA OFISI ZA NIDA

- Imesema haiwatambui wanaojiita Mawakili na kuwatoza Wananchi Tsh. 10,000 kama ada ya nyaraka mbadala ya Cheti cha Kuzaliwa

- Imesema kila ofisi ya NIDA itakuwa na Mawakili wa Serikali

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikaliMawakiliNIDA