JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
PAPA FRANCIS AOMBA RADHI KWA KUMPIGA KIBAO MUUMINI

- Alimpiga kibao Mwanamke aliyemvuta mkono kwa nguvu wakati akisalimia watu kwenye Usiku wa Mwaka Mpya

- Amesema, "Tunapoteza uvumilivu muda mwingine. Naomba radhi kwa mfano mbaya nilioutoa"

Zaidi, soma https://jamii.app/RadhiPapaKibaoMwanamke
MBEYA: JENEZA LATELEKEZWA SOKONI LIKIWA JUU YA MEZA MBELE YA DUKA MOJA

- Wananchi wamepigwa na bumbuwazi baada ya kukuta Jeneza hilo asubuhi ya Mwaka Mpya

- Baadhi ya walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa jeneza hilo lilikuwa limetumika

Zaidi, soma https://jamii.app/JenezaSokoniMbeya
SHINYANGA: ASKARI WA JESHI LA POLISI AKATWA UUME NA MKEWE KWA TUHUMA ZA USALITI WA NDOA

> Jeshi la Polisi linamshikilia, Frola Adam (23), kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumkata uume mume wake, anayefahamika kwa jina la Kazimiri

Soma > https://jamii.app/AskariAkatwaUume

#JFLeo
MBEYA: MBARONI AKIWA NA MIHURU 56 YA KUGHUSHI YA IDARA ZA SERIKALI

- Abraham Obedi (55) amekamatwa na mihuri hiyo ya Idara za Serikali na Ofisi Binafsi

- Baadhi ya mihuri ni ya Afisa biashara wa Halmashauri, Access Bank-Mbeya na TRA-Mbeya

Zaidi, soma https://jamii.app/MbaroniMihuriKughushi
YANGA YAMTEUA ABEID MZIBA KUWA KAIMU MENEJA WA TIMU

- Imemteua Mchezaji huyo wa zamani wa klabu hiyo kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dismas Ten

- Dismas alisimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa kina kuhusu sakata la Wachezaji wa klabu hiyo kuvaa jezi feki
INDONESIA: WATU 21 WAFARIKI KWA MAFURIKO HUKU MVUA KUBWA ZAIDI ZIKITABIRIWA

- Zaidi ya watu 62,000 wameondolewa katika Mji Mkuu, Jakarta baada ya kutokea mafuriko

- Serikali imetahadharisha kuwa mvua hizo zinaweza kuendelea hadi Januari 07

Zaidi, soma https://jamii.app/MafurikoJakartaMwakaMpya2020
KISUTU, DAR: JAMHURI YAPINGA KABENDERA KUMUAGA MAMA YAKE

> Jamhuri kupitia Mawakili wake imepinga maombi yaliyowasilishwa na Wakili wa Erick Kabendera kutaka Mahakama kumruhusu kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mama yake

Zaidi, soma > https://jamii.app/KabenderaMazikoMamaye
ISRAEL: NETANYAHU AOMBA KINGA DHIDI YA MASHTAKA YAKE YA RUSHWA

- Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, anayekabiliwa na mashtaka ya ufisadi ametoa ombi hilo kwa Bunge

- Hatua hiyo huenda ikachelewesha kesi na kumuweka madarakani hadi uchaguzi ujao

Zaidi, soma https://jamii.app/NatanyahuAombaKinga
ORODHA YA MATAJIRI DUNIANI: JEFF BEZOS BADO ANAONGOZA KWA UTAJIRI

- Kwa mujibu wa Bloomberg Billionaire Index, Mwanzilishi wa Kampuni ya Amazon, Jeff Bezos anaongoza kwa utajiri

- Ni tofauti na ilivyotarajiwa kuwa atapoteza nafasi hiyo baada ya kupeana talaka na mkewe
MWANZA: ACHANWA TUMBO KWA KUHOJI MATUMIZI YA FEDHA ALIYOACHA NYUMBANI

- Ni Benedictor Gogogo (48) anayesema alimuachia mkewe Tsh. 10,000

- Amesema alichanwa akiwa amelala baada ya kumpiga kofi mkewe aliyemjibu vibaya kuhusu matumizi yake

Zaidi, soma https://jamii.app/MkeAmtoaMumeUtumbo
KENYA: WATATU WAFARIKI BAADA YA AL-SHABAAB KUTEKA BASI

- Kamishna wa Polisi wa Kaunti ya Lamu amesema Washambuliaji hao wamewaua watu hao na kuwajeruhi wengine watatu katika eneo la Nyongoro kwenye barabara ya Lamu-Garsen

Zaidi, soma https://jamii.app/AlShabaabAttackBus-KE
NJOMBE: MBARONI KWA KUMPIGA NA KUMSABABISHIA KIFO MKEWE

- Josephat Mtega (24) anashikiliwa kwa tuhuma za kumsababishia kifo mkewe kutokana na majeraha ya kipigo

- Angelina Sanga (24) anadaiwa kupigwa vibaya na Josephat baada ya kugombana

Zaidi, soma https://jamii.app/MbaroniKifoMkewe
MAREKANI YAMUUA KIONGOZI WA VIKOSI VYA QUDS VYA JESHI LA IRAN

- Jenerali Qasem Soleimani ameuawa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Baghdad

- Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Javad Zarif amesema hatua hiyo ni hatari na uchokozi wa Kishenzi

Zaidi, soma https://jamii.app/KiongoziQudsAuawa
TABORA: POLISI KUANZA MSAKO WA WANAOTAKA KUJINYONGA

- Kamanda wa Polisi mkoani humo, Barnabas Mwakalukwa amesema kufuatia matukio ya watu wawili kujinyonga, mwaka huu wataanza msako kuwabaini wanaotaka kujinyonga na kuwapeleka Mahakamani

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiKusakaWanaotakaKujinyonga
MAREKANI YAWATAKA WANANCHI WAKE KUONDOKA IRAQ

- Ubalozi wa Marekani nchini Iraq umewataka Raia wake wanaoishi nchini humo kuondoka mapema iwezekanavyo

- Ni kutokana na kuongezaka kwa vurugu ambapo Ubalozi huo pia umezingirwa na Waandamanaji

Zaidi, soma https://jamii.app/MarekaniRaiaKuondokaIraq
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
LUDACRIS NA FAMILIA YAKE WAPATA URAIA WA GABON

- Mwanamuziki wa Marekani, Christopher Brian Bridges maarufu Ludacris, sasa ana uraia wa Gabon na atakuwa na uraia wa nchi mbili

- Ludacris, Mkewe, Eudoxie Mbouguiengue na familia yake walipatiwa Uraia huo Januari 02, 2020
KAGERA: BABA WA KAMBO AMUUA MTOTO WA MIAKA MITATU

- Leonard Kishenya (36), amemuua mtoto wake wa kambo Caren Crispine (3) kwa kumkata na panga

- Anatuhumiwa kufanya hivyo baada ya kuzuka ugomvi kati yake na mke wake, Domina Andrew (30)

Zaidi, soma https://jamii.app/BabaKamboAmuuaMtoto
TUNDURU: SHEREHE WANAZOFANYIWA DARASA LA SABA ILI WAKAOLEWE, ZAPIGWA MARUFUKU

> DC wa Tunduru, Julius Mtatiro ameiambia JamiiForums sherehe hizo huhusisha Wazazi kushona sare na kuwapokea kwa maandamano Wanafunzi baada ya kumaliza mitihani

Soma > https://jamii.app/MtatiroVsWazaziTunduru