JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MICHEZO: Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amechaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Vyama na Vilabu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)
-
Uchaguzi huo umefanyika leo katika Hoteli ya Silver Springs, Uganda na Karia ataliongoza Baraza hilo kwa kipindi cha miaka 4
SINGIDA: HAKIMU MBARONI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

- Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mtinko, Bernard Kasanda (38) anatuhumiwa kupokea rushwa ya Tsh. 250,000

- Pia, alikutwa na visu 5 anavyodhaniwa kutumia kujihami wakati akipata maslahi hayo haramu

Zaidi, soma https://jamii.app/HakimuMbaroniRushwa-SNG
Donald Trump amekuwa Rais wa tatu katika historia ya Marekani kupigiwa kura ya matumizi mabaya ya madaraka

- Hatua hiyo inampeleka moja kwa moja katika kesi dhidi yake itakayoamua ikiwa atabakia madarakani au la, uamuzi utakaotolewa na Baraza la ‘Senate’

Zaidi, soma https://jamii.app/TrumpImpeached
UCHAGUZI CHADEMA: MBOWE ACHAGULIWA KWA KISHINDO KUWA MWENYEKITI

> Freeman A. Mbowe ametangazwa kushinda nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa kwa awamu nyingine baada ya kuibuka na kura 886 sawa na 93.5% dhidi ya Cecil Mwambe aliyepata kura 59 sawa na 6.2%

> Kura 3 zimeharibika

Soma > https://jamii.app/MboweTena
MWANZA: MAJI WILAYA YA MISUNGWI YALALAMIKIWA KUWA MACHAFU

> Inadaiwa kuwa, maji yanayotoka kwenye mabomba ni machafu na hayafai kwa matumizi ya Binadamu kwani yanatoka Ziwani moja kwa moja na kisha kusambazwa kwa Wananchi bila kutibiwa

> Wananchi wadai kuna ucheleweshwaji wa kuunganishwa na Mtandao wa Maji japo wamelipa gharama zote kama inavyohitajika

Soma - https://jamii.app/UchafuMajiMisungwi
WAKENYA 4 WADAIWA KUTEKWA NA WANAMGAMBO WA AL-SHABAAB

> Wakandarasi waliokuwa wakifanya ujenzi wa barabara kati ya Riba na Konton, Kaunti ya Wajir wanadaiwa kutekwa na kundi la watu wanaoshukiwa kuwa Wanamgambo wa Kikundi Kigaidi cha Al-Shabaab

> Kamishna Msaidizi wa Kaunti amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana jioni

Soma - https://jamii.app/KenyansKidnappedAlShabaab
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
RONALDO APIGA 'BONGE LA GOLI' KUIPA USHINDI JUVENTUS

- Mshambuliaji Cristiano Ronaldo jana amefunga goli la kichwa lililozua gumzo katika mitandao ya kijamii

- Wakati akifunga goli hilo, Wataalamu wanasema aliruka urefu wa Mita 2.56 huku akikaa hewani kwa sekunde 1.5
VATICAN: PAPA AONDOA USIRI JUU YA KASHFA ZA UDHALILISHAJI WA KINGONO

- Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis ameuondoa usiri juu ya kashfa za udhalilishaji wa kingono kwa kufuta kanuni inayozuia kufichuliwa na kuchunguzwa kwa uhalifu huo

Zaidi, soma https://jamii.app/Papa-UsiriKesiUdhalilishaji
LIVERPOOL YATHIBITISHA KUMSAJILI TAKUMI MINAMINO

- Imethibitisha kumsajili Kiungo huyo Mshambuliaji (24), Raia wa Japan, kutoka Klabu ya Red Bull Salzburg ya Austria kwa Paundi Milioni 7.25 (Tsh. 21,893,401,752)

- Liverpool itasubiri hadi Januari 01 litakapofunguliwa dirisha la usajili kumuandikisha mchezaji huyo
FAIDA ZA MZAZI NA MTOTO KUSOMA VITABU PAMOJA

> Watafiti wanadai kuna faida lukuki kwa mzazi na mtoto wanaposoma vitabu pamoja. Mzazi kumsomea mtoto kitabu humjenga mtoto kiakili na kuelewa misamiati ya lugha haraka na pia huimarisha mahusiano ya mtoto na mzazi

> Utamaduni wa kusoma vitabu unamfanya mtoto awe na uwezo wa kujiamini na kuwa mdadisi katika jamii, humfanya mtoto kuwa mbunifu na kupata maarifa mengi yatakayomsaidia kimaendeleo

Tembelea - https://jamii.app/MzaziMtotoKusomaVitabu
#JFMahusiano
SINGIDA: IDADI YA WANAFUNZI WANAOPATA MIMBA SHULENI YAPUNGUA

> Wanafunzi wanaopata mimba katika Shule za Msingi na Sekondari imepungua kwa asilimia 66.66 kutoka mimba 54 mwaka 2018 hadi mimba 18, Novemba 30, 2019

> Kati ya idadi hiyo, wasichana wa Shule za Sekondari ni 15 na 3 ni kutoka Shule za Msingi

Soma - https://jamii.app/PunguzoMimbaMashuleni
ZANZIBAR: WANAUME WATOA TALAKA KWA NJIA YA SMS, ELIMU YA NDOA YAHITAJIKA ZAIDI

> Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi amewataka wanandoa watarajiwa kuepuka talaka za kiholela ambazo athari zake ni kubwa katika jamii ikiwamo kutelekezwa kwa familia na watoto kutaabika

> Amesema kwa kiasi kikubwa watu wanaingia katika ndoa bila ya kupata elimu juu ya ndoa na familia

Zaidi, soma https://jamii.app/TalakaSmsZbar
CHINA YAMUONDOA MESUT OZIL KWENYE TOLEO LAKE LA MCHEZO WA VIDEO

- Kiungo huyo wa Arsenal ameondolewa kwenye mchezo wa video wa Pro Evolution Soccer (PES) 2020 toleo la China

- Ni baada ya kuikosoa China kwa kuwatesa Waislamu jamii ya #Uighur

Zaidi, soma https://jamii.app/OzilMchezoVideoChina
CECAFA: TANZANIA BARA YASHINDWA KUTWAA NAFASI YA TATU

- Timu ya Taifa ya Tanzania Bara #KilimanjaroStars imefungwa goli 2-1 na timu Taifa ya Kenya #HarambeeStars katika mchezo wa kutafuta Mshindi wa Tatu

- Mchezo unaofuata ni wa fainali kati ya timu za Uganda na Eritrea
INDIA: WAANDAMANAJI 100 WAKAMATWA WAKIPINGA MUSWADA WA KIBAGUZI

> Mandamano hayo yanapinga Muswada wa kuwapatia hifadhi ya kisiasa Wakimbizi waliokabiliwa na mateso katika nchi wanazotoka, huku ukiwabagua waumini wa Dini ya Kiislam

> Aidha, Mahakama imetangaza kuahirisha kusikiliza kesi ya madai kuhusiana na Muswada huo hadi Januari 2020

Soma - https://jamii.app/RiotsMuslimsBill
MADEREVA WA UBER NA BOLT KUFUNGUA KESI DHIDI YA KAMPUNI HIZO

> Chama cha Madereva wa Usafirishaji kwa Njia ya Mtandao (TODA) kimetoa siku 7 (kabla ya kufungua kesi) kukutana na wamiliki wa Uber na Bolt (Taxify) ili kujadiliana baada ya kuibuka kwa madai kuwa wamiliki hao wanachukua asilimia kubwa katika kila safari

Soma - https://jamii.app/MgogoroMaderevaUberTaxify
MIRADI 159 YA MAJI IMEKAMILIKA LAKINI HAITOI MAJI

- Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza kuchukuliwa hatua kwa Wakandarasi wote waliotekeleza miradi 159 nchini ambayo imekamilika ila haitoi maji au inayochukua muda mrefu kumalizika

Zaidi, soma https://jamii.app/Miradi159Maji
MAHAKAMA YASISITIZA KUMTAKA LISSU

- Mahakama ya Kisutu imesisitiza kumtaka Mahakamani Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uchochezi

- Lissu kupitia Mdhamini wake amesema bado anahofia usalama wake

- Kesi itatajwa tena Januari 20, 2020

Zaidi, soma https://jamii.app/MahakamaYamtakaLissu
TRUMP AWASHAMBULIA WABUNGE WALIOMPIGIA KURA YA KUONDOLEWA MADARAKANI

> Muda mfupi baada ya Baraza la Wawakilishi la Marekani kupitisha uamuzi wa kumshitaki Rais Donald Trump, mwenyewe ameitisha mkutano wa hadhara kuwashambulia vikali wajumbe wa Democrat waliopiga kura hiyo

> Wajumbe 230 waliidhinisha mashitaka hayo dhidi ya 197 waliopinga

Soma - https://jamii.app/TrumpTalksImpeachment