JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SERIKALI YAUTAKA UONGOZI WA UDSM KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI WA WANAFUNZI

> Ni viongozi wa Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Dar, walioipa Serikali saa 72 kulipa mikopo ya wanafunzi vinginevyo wataandamana

> Waziri wa Elimu asema tamko lilitolewa kinyume cha utaratibu wa kutoa malalamiko na ni utovu wa nidhamu wa kiwango cha juu

Soma - https://jamii.app/DARUSOKuadhibiwaSerikali
UCHUNGUZI DHIDI YA TRUMP: ALALAMIKA KUNYIMWA HAKI YA KUWASILISHA USHAHIDI

> Rais Donald Trump ameandika barua kwa Spika Nancy Pelosi, akimtuhumu kutangaza vita ya wazi dhidi ya Demokrasia ya Marekani

> Trump anakabiliwa na kura ya uchunguzi itakayopigwa leo

Soma - https://jamii.app/TrumpSlamsIllegalCoup
UTAFITI: WANAWAKE WEUSI HATARINI KUPATA SARATANI YA MATITI KUTOKANA NA DAWA ZA NYWELE

> Wanawake wanaotumia bidhaa hizo maarufu kama 'Relaxer' huongeza nafasi zao za kupata Saratani ya Matiti kwa hadi 60%

> Kulingana na utafiti huo, kuna tofauti za hatari kulingana na rangi ya muhusika ambapo wanawake weusi wanakabiliwa na hatari kubwa (45%) kupata Saratani

Soma - https://jamii.app/RelaxersBreastCancer
MADAI YA MIKOPO: RAIS WA WANAFUNZI UDSM ASIMAMISHWA MASOMO KWA MUDA USIOJULIKANA

> Aliyesimamishwa ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO), Hamis Musa Hamis

> Waziri wa Elimu alikipa Chuo hicho saa 24 kuwachukulia hatua wanafunzi waliotoa tamko kinyume cha utaratibu
Baadhi ya maneno ya Rais Magufuli wakati akizindua Jengo la Ofisi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Jengo la Mahakama ya Wilaya, Wilayani Chato katika Mkoa wa Geita
KISARAWE: MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT MBARONI KWA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI

> Mchungaji Shauri Steven anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi wa Darasa 5

> Sababu imetajwa kuwa tamaa za mwili ambapo alimlaghai kwa madai ya kumfanyia Huduma ya Maombi

Soma - https://jamii.app/MchMbaroniMimbaMwanfz
WAKENYA: MTI WA KRISMASI WA UWANJA WA NDEGE JOMO KENYATTA NI 'KITUKO'

- Mti huo umerembwa kwa mapambo ya Krimasi huku chini kukiwa na maboksi ya zawadi

- Wakenya Mitandaoni hawakuweza kuficha hisia zao huku wakilinganisha mti huo na mingine

Soma https://jamii.app/MtiKrismasiJKIA-Kenya
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ERICK KABENDERA KULA KRISMASI NA MWAKA MPYA RUMANDE

- Jamhuri imeeleza kuwa upelelezi bado haujakamilika

- Wakili wa Kabendera amesema bado wanaendelea kuzungumza na DPP kuhusu barua ya kukiri makosa

- Kesi kusikilizwa tena Januari 2, 2020

Zaidi, soma https://jamii.app/KesiKabendera-2020
NAFASI ZA KAZI NDANI YA TAASISI YA T-MARC TANZANIA

- Shirika hilo linalofanya kazi kuboresha Afya ya Umma na kukuza Maendeleo ya Jamii limetangaza nafasi 10 za kazi

- Sales Representatives (6), Accountant, Business Development Manager, Procurement Specialist na Marketing Manager

Zaidi, soma https://jamii.app/NafasiKaziT-Marc
MAMBO YA KUYAZINGATIA PINDI UTOAPO ADHABU KWA MTOTO WAKO

> Adhabu iendane na kosa: Endapo hautozingatia kosa na adhabu utatengeneza mazingira ya mtoto kutojengwa bali kubomolewa

> Epuka adhabu za kikatili kwa watoto: Kuadhibu sio kukomoa, adhabu lengo lake ni lazima liwe kumfundisha mtoto na sio kumuumiza

> Adhabu isitolewe kwa mtoto ambaye hajawahi kuelezwa lolote juu ya kosa alilolifanya: Mambo mengi sio makosa kwa watoto mpaka pale watakapoelezwa kuwa ni makosa

Zaidi, soma - https://jamii.app/MsingiAdhabuMtoto
UGANDA: AMSHUSHIA KIPIGO MKEWE KWA KUCHINJA JOGOO WA KRISMASI SIKU 10 KABLA YA SIKUKUU

- Mwanaume (50) katika Wilaya ya Budaka amemjeruhi vibaya Mke wake baada ya Mwanamke huyo kumchinja Jogoo aliyetakiwa kufanywa kitoweo siku ya Krismasi

Zaidi, soma https://jamii.app/AshambuliaMkwe-JogooKrismasi
ZIFAHAMU PESA 8 ZENYE NGUVU AFRIKA

> (1) Dinari ya Libya: Hii ndio pesa yenye nguvu zaidi Afrika ukiangalia thamani yake dhidi ya dola ya Marekani na nguvu yake ya kununua (Purchasing Power) ambapo Dola 1 = 1.38 Dinari za Libya

> (2) Dinari ya Tunisia: Hii ni pesa ya pili kwa Afrika ambayo dola 1 = 3.05 Tunisian Dinari. (3) Cedis ya Ghana: Ghana ni nchi pekee ya Afrika Magharibi ambayo ipo kwenye 8 Bora ya nchi zenye pesa yenye nguvu Afrika (Dola 1 = 5.50 Ghana Cedis)

Kuzifahamu zingine, soma - https://jamii.app/StrongCurrenciesAfrica
RAIS AWAONYA WANAOJENGA MABONDENI, AWATAKA WASIILAUMU SERIKALI

> Rais John Magufuli amewataka wananchi kujihadhari kwa kutojenga nyumba kwenye maeneo ambayo kuna Mkondo wa Maji

> Akitoa mifano ya maeneo ambayo wananchi wamejenga mabondeni, amewataka kuchukua tahadhari wanapojenga nyumba zao ili wasije wakailaumu Serikali baadaye

Soma - https://jamii.app/MagufuliUjenziBondeni