JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: GAVANA MIKE SONKO AACHIWA KWA DHAMANA

- Gavana huyo wa Nairobi ameachiwa kwa dhamana ya pesa taslimu Ksh. Milioni 15 au bondi ya Ksh. Milioni 30

- Pia, anatakiwa kutokwenda ofisini na akitaka vitu vyake atasindikizwa na Wapelelezi

Zaidi, soma https://jamii.app/SonkoAachiwaDhamana
SHINYANGA: MABINTI WAOGESHWA DAWA KUVUTIA WANAUME. SERIKALI YAOMBWA KUZUIA

- Wasichana wa miaka kati ya 10 na 15 hupelekwa kuogeshwa dawa hiyo maarufu kama ‘Samba’

- Wadau wadai vitendo hivyo vinachochea Mimba za Utotoni na maambukizi ya UKIMWI

Zaidi, soma https://jamii.app/DawaKuvutiaWanaume
CPJ: KWA MWAKA 2019 HADI KUFIKIA DESEMBA 01, TAKRIBAN WANAHABARI 250 WAMEFUNGWA

- Ni kupitia ripoti yake ya mwaka 2019

- Ripoti inaonyesha China imefunga Wanahabari 48, Uturuki 47, Saudi Arabia 26, Misri 26, Eritrea 16, Vietnam 12 na Iran 11

- Erick Kabendera wa Tanzania aingia katika orodha

Soma > https://jamii.app/Wanahabari250Wafungwa2019
YANGA YAVUNJA MKATABA NA JUMA BALINYA

- Klabu ya Yanga imevunia mkataba na Mshambuliaji wake Raia wa Uganda, Juma Balinya kuanzia leo

- Hata hivyo, haijasema sababu za uamuzi huo dhidi ya Mchezaji huyo aliyekuwa Mfungaji Bora katika Ligi ya Uganda kabla ya kujiunga nao
MICHEZO: Klabu ya Napoli imemtangaza aliyekuwa Kocha wa AC Milan, Gennaro Gattuso kuwa Kocha wa timu hiyo akichukua nafasi ya Carlo Ancelotti

- Gattuso alijiuzulu kuifundisha AC Milan baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu kushiriki Michuano ya Klabu Bigwa Ulaya msimu huu
SIMBA SC YAMTANGAZA KOCHA WAKE MPYA

- Imemtambulisha Raia wa Ubelgiji, Sven Vandenbroeck kuchukua nafasi ya Patrick Aussems aliyefukuzwa

- Vandenbroeck amewahi kuifundisha Timu ya Taifa ya Zambia na kushinda Ubingwa wa AFCON akiwa Kocha Msaidizi wa Cameroon mwaka 2017
NJOMBE: SIKU MOJA BAADA YA KUPEWA MSAMAHA WA RAIS AKAMATWA KWA WIZI

- Mussa Msola maarufu Hitler aliyekuwa miongoni mwa Wafungwa 5,533 waliopewa Msamaha wa Rais, Siku ya Uhuru, ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuvunja Nyumba ya Kulala Wageni

Zaidi, soma https://jamii.app/MfungwaMsamahaRaisMbaroni
TUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUJINUFAISHA

> Mitandao ya Kijamii kama Facebook na Instagram, ukiitumia kwa mlengo chanya inaweza kukutajirisha kwasababu inatumiwa na watu wengi sana na imegeuza Dunia kuwa Kijiji kimoja kwani hukukutanisha na watu kiurahisi

> Inakuza watu kiakili kwani kuna kurasa nyingi nzuri zenye mafundisho tofauti ikiwemo ndoa, uchumi, biashara, mahusiano, na familia na inaweza kukusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika maisha

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/SocialMediaUse
NDEGE YA JESHI ILIYOPOTEA CHILE: MABAKI YAKE YAPATIKANA

- Mabaki yanayoaminika ni ya ndege ya Kijeshi iliyotoweka Jumatatu yamepatikana katika Mkondo Bahari wa Drake ikiwa ni takriban Kilometa 30 kutoka eneo ndege hiyo ilipopoteza mawasiliano

Zaidi, soma https://jamii.app/MabakiNdegeChile
KENYA: MABASI YA MODERN COAST YAGONGANA. WATU 7 WAFARIKI, 60 WAJERUHIWA

- Yamegongana usiku wa kuamkia leo katika eneo la Salama kwenye Barabara Kuu ya Mombasa-Nairobi

- Siku moja kabla basi jingine la Modern Coast liligongana na basi la Tahmeed

Zaidi, soma https://jamii.app/Ajali-7Wafariki62Wajeruhiwa
RAIS MAGUFULI: NDEGE YA TANZANIA ILIYOKUWA IKISHIKILIWA NCHINI CANADA IMEACHIWA

- Ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imeshikiliwa nchini Canada imeachiliwa

- Rais Magufuli amesema siku ya kuwasili nchini itatangazwa

Soma > https://jamii.app/NdegeCanadaHuru
INATES, NIGER: WANAJESHI 73 WAUAWA KAMBINI MWAO

- Wengine 12 wamejeruhiwa huku idadi kubwa ya Walioshambulia kambi hiyo wakiuawa

- Hakuna aliyejinadi kuhusika na shambulio hilo ila Boko Haram na Dola Ya Kiislam wapo katika maeneo hayo

Zaidi, soma https://jamii.app/Wanajeshi73Wauawa-NGR
DAR: WATANZANIA 19 WALIOZAMIA AFRIKA KUSINI WAHUKUMIWA

- Mahakama ya Kisutu imewahukumu miezi miwili jela na kulipa faini ya Tsh. 50,000 kila mmoja

- Watu hao walikamatwa na kushtakiwa baada ya kurudishwa nchini Desemba 02, 2019

Zaidi, soma https://jamii.app/WazamiajiWahukumiwaTZ
KATIBU MKUU WA CHAMA CHA KIJAMII (CCK) MBARONI

- TAKUKURU inamshikilia Renatus Muabhi kwa kujifanya Mtumishi wa Taasisi hiyo

- Pia, anadaiwa kuomba rushwa ya Tsh. Milioni 50 kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Bharya Engineering & Contracting

Zaidi, soma https://jamii.app/KatibuCCKMbaroni
MZEE PINDA ATAMANI RAIS MAGUFULI ANGEONGEZA WALAU MIAKA 5 BAADA YA 10 KUISHA

- Amesema angetamani hilo litokee lakini kwa kuwa Katiba ipo 'tight' kidogo ni ngumu

- Pia, amesema anajua Rais atakataa huku akimuomba asaidie kutafuta mrithi bora

Zaidi, soma https://jamii.app/MizengoUraisMagufuli
HISTORIA: MFAHAMU FREDDIE MERCURY - GWIJI WA MUZIKI ALIYEZALIWA NA KUKULIA ZANZIBAR, ULAYA WANAJIVUNIA

> Alizaliwa Septemba 5, 1946 Zanzibar kwenye ulimwengu wa burudani jina lake linatambulika kwa utunzi, uimbaji na uzalishaji wa vibao vya muziki

> Alifariki kwa UKIMWI mwaka 1991

Soma ~ https://jamii.app/FreddieMercury
MOROGORO: GARI LA KWENYE MSAFARA WA IGP SIRRO LAGONGA MTOTO, AFARIKI

- Jackline Samwel (9), amefariki baada ya kugongwa na gari lililokuwa katika msafara wa IGP Simon Sirro

- Amegongwa wakati akivuka barabara baada ya kutoka kununua maji

Zaidi, soma https://jamii.app/MsafaraSirroWaua
1
TAASISI 58 ZATOA GAWIO KWA SERIKALI BAADA YA KUPEWA SIKU 60

- Taasisi 58 ambazo zilikuwa hazijatoa gawio kwa Serikali zimetoa jumla ya Tsh. Bilioni 12.12

- Ni kati ya Kampuni na Taasisi 187 zilizopewa siku 60 na Rais Magufuli kutoa gawio

Zaidi, soma https://jamii.app/GawioKampuni58
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ALGERIA: ASILIMIA 20 YA WAPIGA KURA WAJITOKEZA KUPIGA KURA

- Watu wote wenye uwezo wa kupiga kura katika Uchaguzi huo Mkuu ni Milioni 24

- Wananchi wamejitokeza katika Mitaa ya Mji Mkuu wa nchi hiyo, Algiers kupinga Uchaguzi huo unaoendelea

Zaidi, soma https://jamii.app/UchaguziAlgeria
KENYA: MBARONI AKIDAIWA KUMUUA MUMEWE

- Mercy Rita Wanjiru (21) anadaiwa kumchoma kisu kifuani Kevin Kuria (23), alipojaribu kumzuia asiondoke nyumbani

- Inaelezwa kuwa, Mercy alitaka kuondoka kutokana na ugomvi usioisha baina yake na Kevin

Zaidi, soma https://jamii.app/MbaroniKuuaMume-KE