JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
NDEGE YA TANZANIA ILIYOKUWA IKISHIKILIWA CANADA YAANZA SAFARI

- Ndege mpya, Bombardier Q400 iliyokuwa ikishikiliwa kutokana na madai ya Mkulima, Hermanus Steyn imeanza safari kuja Tanzania

- Ndege hiyo inatarajiwa kuwasili Disemba 14, 2019 na itapokelewa jijini Mwanza
TUHUMA ZA RUSHWA YA NGONO SEKTA YA AFYA: TAARIFA ZAIDI ZINAHITAJIKA

> Kumekuwa na tuhuma ambazo zimekuwa zikisambaa kwenye Mtandao wa JamiiForums zikielekezwa kwa Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya

> Vyombo vya Dola vimeziona tuhuma hizo (katika JF) na Mamlaka zinahitaji wenye taarifa za kina zinazoweza kuwasaidia wachunguzi wazilete taarifa hizo zikiwa detailed (hata kama kuna viambatanisho zaidi) ili wahusika/watuhumiwa wachukuliwe hatua stahiki

> Tuma Barua Pepe sensitive@jamiiforums.com au uwasiliane na Waziri wa Afya (Ummy Mwalimu) kwa DM Twitter (@umwalimu) au Instagram (@ummymwalimu)

Soma https://jamii.app/RushwaYaNgonoMbeya
JAPAN: WAZEE WATUMIA 'EXOSKELETONS' ILI WACHELEWE KUSTAAFU

- Wanavaa vifaa hivyo ili kuendana na mahitaji ya kazi na kukaa kwenye kazi kwa muda mrefu

- Vifaa hivyo vinawaongezea nguvu vikiwasaidia kukimbia haraka na kubeba vitu nzito

Zaidi, soma https://jamii.app/ExoskeletonJapan
HALIMA MDEE ASHINDA UENYEKITI WA BAWACHA

- Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA)

- Hawa Mwaifunga ni Makamu Mwenyekiti Bara na Sharifa Suleiman Suleiman ni Makamu Mwenyekiti Zanzibar

Zaidi, soma https://jamii.app/UchaguziBawacha2019
UINGEREZA: BORIS JOHNSON ASHINDA UCHAGUZI, AAHIDI KUKAMILISHA MCHAKATO WA 'BREXIT' JANUARI 31, 2020

- Chama cha Conservatives kimepata viti 364 vya Wabunge wakati Labour kikipata 203, SNP 48, Liberal Democrats 11 na DUP 8

Soma => https://jamii.app/BorisAshinda

#UKElection #JFLeo
UCHAGUZI MKUU ALGERIA: ABDELMADJID TEBBOUNE ACHAGULIWA KUWA RAIS

- Abdelmadjid Tebboune ameshinda kiti hicho kwa kupata asilimia 58.1% ya kura zote

- Alikuwa Waziri Mkuu(Mei 2017-Agosti 2017), Waziri wa Makazi (2001 - 2002 na 2012 - 2017).

Soma > https://jamii.app/TebbouneAshindaUrais
MBEYA: MHANDISI WA MRADI WA MAJI MBARONI KWA KULA BILIONI 3 ZA MRADI

- Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa ameamuru kuwekwa mahabusu Mhandisi Alistides Kanyomo

- Pia, Mhandisi huyo amedai kujenga ofisi ya muda ya mabati kwa Tsh. Milioni 100

Zaidi, soma https://jamii.app/MhandisiMbaroniFedha
UHURU WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA RASIMU YA KATIBA CHINI YA TUME YA JAJI WARIOBA

- Ibara ya 31 -(1) Kila mtu ana haki na uhuru wa kutafuta na kupata habari kupitia Vyombo vya Habari na njia nyingine za upashanaji wa habari bila kujali mipaka ya nchi

- (2) Vyombo vya Habari vitakuwa huru na vitakuwa na haki ya kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa wanazozipata na kuanzisha

- Serikali na Taasisi zake, Asasi za Kiraia na Watu Binafsi watakuwa na wajibu wa kutoa habari juu ya utekelezaji wa kazi zao

- #Katiba ya sasa haijaainisha jambo hili

Soma > https://jamii.app/UhuruHabariKatibaMpya
RASIMU YA KATIBA CHINI YA TUME YA JAJI WARIOBA: HAKI YA WAPIGA KURA KUMWAJIBISHA MBUNGE WAO

- Ibara ya 129 -(1): Wananchi wanahaki ya kumuondoa Mbunge wao madarakani, kama; (a) ataunga mkono sera ambazo zinaenda kinyume na maslahi ya wapiga kura au Taifa

- (b) Atashindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero za wapiga kura wake

- (c) Ataacha kuishi au kuhamisha makazi yake kutoka eneo la Jimbo la Uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi

Soma > https://jamii.app/WabungeVsWapigaKura
MZEE MAKAMBA, KINANA NA MEMBE WATAITWA CCM KUHOJIWA

- Halmashauri Kuu ya CCM imewaita Wanachama hao katika Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa ya CCM

- Wameitwa kujibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili kwa mujibu wa Katiba ya Chama hicho

Zaidi, soma https://jamii.app/KinanaMakambaMembe
MAMA WA ERICK KABENDERA AMUOMBEA MWANAYE MSAMAHA

- Verdiana Mjwahuzi (81) amemuomba Rais Magufuli amsamehe Erick anayemsaidia katika matibabu

- Amesema, "Nilipomuona mwanangu sikujua kama ni yeye, amekonda na ana nywele nyingi kama mwehu.“

Zaidi, soma https://jamii.app/MamaKabenderaMsamahaRais
MPYA: Kamati ya Mahakama imepitisha Makala zinazohusu kumuondoa Rais Donald Trump Madarakani

- Wiki ijayo Makala hizo zitawasilishwa kwa Wawakilishi wa vyama ili wazipigiwe kura

Zaidi, soma https://jamii.app/TrumpImpeachmentApproved
BODI ZA MAZAO NCHINI KUUNGANISHWA NA KUBAKIZA BODI 3

- Ambazo ni Bodi ya Mazao ya Kimkakati kama Kahawa, Pamba, Mkonge, Tumbaku, Pareto, Korosho na Mchikichi

- Bodi ya Mazao ya Nafaka, Mbogamboga na Matunda na Bodi ya tatu itakuwa ya Sukari

Zaidi, soma https://jamii.app/Bodi3Mazao
MWANACHAMA MKONGWE WA YANGA MZEE AKILIMALI AFARIKI

- Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amefariki leo alfajiri

- Amefariki katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani

Zaidi, soma https://jamii.app/MzeeAkilimaliAfariki
UN: SHERIA MPYA YA URAIA NCHINI INDIA NI YA KIBAGUZI

- UN imesema sheria hiyo ina misingi ya kibaguzi kwa kuwa inawatenga Waislam

- Sheria hiyo inaongeza mchakato wa Uraia kwa makundi ya walio wachache waliokimbia kutoka nchi kama Pakistani

Zaidi, soma https://jamii.app/UNSheriaUraiaInabagua
OMAR AL BASHIR AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA

- Rais huyo wa zamani wa Sudan amekutwa na hatia katika makosa ya Rushwa na Utakatishaji Fedha

- Pia, anakabiliwa na makosa ya Mauaji ya Kimbari na Uhalifu wa Kivita katika Mahakama ya ICC
DAR: MKURUGENZI WA JAMIIFORUMS ATUNUKIWA CHETI CHA UZALENDO

- Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo ametunukiwa cheti hicho na Mtandao wa Madeni na Maendeleo Tanzania

- Maxence ni miongoni mwa watanzania wachache waliotambuliwa leo kwa mchango wao katika kutetea Haki za Binadamu nchini
MLIMBWENDE WA JAMAICA ASHINDA TAJI LA MLIMBWENDE WA DUNIA 2019

- Toni-Ann Singh (23) ametwaa taji hilo ikiwa ni mara ya 4 kwa Jamaica kushinda

- Mshindi wa 2 ni Ophely Mezino (Ufaransa) na wa 3 ni Suman Rao (India)

- Sylivia Sebastian aliiwakilisha Tanzania

Zaidi, soma https://jamii.app/MissWorld2019
NDEGE MOJA YA ATCL KUWASILI MWAKANI NA MBILI KUWASLI JUNI NA JULAI 2021

- Bombardier Q400 itawasili Mwezi Juni 2020 na Air-Bus 220-300(mbili), moja itawasili mwezi Juni na nyingine mwezi Julai 2021

- Aidha, Serikali imeweka wazi mpango wake wa kutaka kununua ndege ya mizigo

Zaidi, soma https://jamii.app/Ndege3Mpya2020
AFYA: UNAVIJUA VIASHIRIA VYA MTU ALIYEFARIKI?

- Kumekuwa na hoja kwamba baadhi ya watu hudhaniwa wamefariki kabla hata hawajafikwa na mauti hivyo yawezekana wapo wanaozikwa (kimakosa) wakiwa hai

- Wataalamu wanaeleza kuwa Ubongo ndio kiashiria kikubwa cha mtu kufariki na sio kusimama kwa mapigo ya moyo pekee yake

Jifunze zaidi kuwa kusoma > https://jamii.app/ViashiriaKifo